Jinsi Mullar Omar wa Taleban alivyoishi karibu na kambi ya jeshi ya Marekani nchini Afghanistan

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,609
154,916
Viongozi wa Marekani na Afghanistan walikuwa wakiamini kuwa Mullar aliyeasisi kikundi cha wapiganaji cha Taliban alikimbilia na kufia Pakistan
PIC+MULLER.jpg


Kwa miaka mingi, muasisi wa kikundi cha wapiganaji cha Taliban, Mullah Omar alikuwa akiishi umbali mfupi kutoka kambi ya majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, kwa mujibu wa kitabu kipya ambacho kinatoa ushuhuda unaoonyesha udhaifu wa taifa hilo kubwa katika ujasusi.

Viongozi wa Marekani na Afghanistan wanaamini kuwa kiongozi huyo mkimbizi na aliyekuwa na jicho moja alikimbilia na baadaye kufia nchini Pakistan, lakini kitabu hicho kipya cha maisha yake kinasema Omar alikuwa akiishi maili tatu tu kutoka kambi ya Marekani ya Forward Operating katika jimbo la Zabul, ambako alifia mwaka 2013.

"Kumsaka Adui", kitabu kilichoandikwa na Mholanzi Bette Dam, kinasema kiongozi huyo wa Taliban caliishi kama mtu mpweke, akikataa kutembelewa na familia yake na akijaza daftari lake la kumbukumbu kwa kuandika lugha ya kufikirika.

Dam alitumia miaka mitano kufanya utafiti kwa ajili ya kuandika kitabu hicho na alifanya mahojiano na Jabbar Omari, ambaye alikuwa mlinzi wa Omar na ambaye alimficha na kumlinda baada ya utawala wa Taliban kuondolewa madarakani.

Mwandishi huyo alitumia miaka mingi kufanya kazi ya kuripoti nchini Afghanistan na pia aliandika kitabu kuhusu rais wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai.

Baada ya shambulio la Septemba 11, 2001 ambalo lilisababisha kuanguka kwa utawala wa Taliban, Marekani ilitangaza dau la dola 10 milioni za Kimarekani kwa mtu ambaye angetoa taarifa ambazo zingefanikisha kukamatwa kwa Omar na akaenda kujificha katika makazi yenye eneo dogo ya Qalat jijini Kabul, ameandika Dam.

Familia iliyokuwa inaishi eneo hilo haikutambulishwa kuhusu mgeni huyo wa aina yake, lakini majeshi ya Marekani nusura yamkamate mara mbili.

Wakati fulani, askari wa doria wa Marekani walikaribia makazi hayo wakati Omar na Omari wakiwa eneo hilo. Baada ya kupata ishara, wawili hao walirukia nyuma ya lundo la miti lakini wanajeshi wa Marekani walipita bila ya kuingia.

Mara ya pili, wanajeshi wa Marekani walifikia hatua ya kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo lakini hawakuweza kutambua mlango wa kuelekea kwenye chumba cha siri alimokuwa akiishi.

Omar aliamua kutembea wakati Marekani ilipoanza kujenga kambi yake eneo la Lagman mwaka 2004, ikiwa ni mita chache kutoka sehemu alimokuwa amejificha.

Baadaye alihamia kwenye jengo la pili lakini muda mfupi baadaye Marekani ilianza kujenga kambi nyingine ya Forward Operating Base Wolverine -- ambayo ilikuwa na wanajeshi 1,000, na ambako vikosi maalum vya Marekani na Uingereza vilikuwa vikiweka kambi wakati mwingine.
Aliamua kutotembea tena, anasema Dam, hata kwenda nje ilikuwa kwa nadra sana na mara nyingi alikuwa handakini wakati ndege za Marekani zikipita juu.

Ingawa alikuwa akisikiliza kipindi cha jioni cha BBC kilichokuwa kikirusha habari kwa lugha ya Pashto, hata baada ya kusikia habari za kuuawa kwa kiongozi wa al-Qaeda, Osama Bin Laden Omar alitoa maoni yake mara chache sana.

Kitabu hicho kinadai kuwa Omar alianza kuumwa mwaka 2013, hakutaka kutibiwa na daktari na akakataa kusafiri kwenda Pakistan kw amatibabu na baadaye akafariki akiwa Zabul. AFP
Jinsi Mullar Omar wa Taleban alivyoishi karibu na kambi ya jeshi
 
Ila kuna watu watiifu aisee! Au Mula alikuwa akimlipa kiasi gani huyo mlinzi wake mpaka akalipiga chini hilo deal la US$ 10m bila kumuuza?
Nalog off
 
Mulla Mohamad Omar inaaminika hakuwahi kupiga Picha katika Maisha yake yote Na ndio sababu Jeshi L Marekani halikuwahi kuweka Picha yake hadharan wakati wa kumsaka Kama ilivyofanya kwa kina Usamah Na Ayman Alzawaheer sasa hiyo Picha imepatikana wapi?
 
Ila kuna watu watiifu aisee! Au Mula alikuwa akimlipa kiasi gani huyo mlinzi wake mpaka akalipiga chini hilo deal la US$ 10m bila kumuuza?
Nalog off

Hata sie Ndugu William Lukuvi si anasema alikataa Mabilion ya Matajiri wasio waaminifu kwa Uzalendo Na uchungu wa nchi yake ?

Tusifie vya Nyumbani jamani
 
Kwakweli kati ya mla omary na george bush,ukiwapima kwenye mzani,Bush anaonekana ndo muuaji mkubwa tukiweka unafiki pembeni,haijalishi unaua mtu kwasababu gani,iwe unatumia dini,au demokrasia,it doesnt matter,
tukija kwa huyu jicho moja ,yeye kosa lake ni kukataa kumkabidhi bin laden kwa wamarekani,kwa kudai kuwa alihitaji ushahidi kwamba ladeni ndo kalipua pentangon,Bush kwa upande wake ameuwa raia,ukiacha wanajeshi wa afaghanistan,raia zaidi ya milioni moja,
sure bush hakukamata silaha mwenyewe bali alitoa order,tofauti na mla ambaye wala hakuhusika na 9/11,bali kosa lake ni kumuhifadhi laden,
hivi tuseme tuweke ushabiki pembeni nani kaua watu na kwa wingi kama bush,obama na hata Trump?kwa kisingizio cha demokrasia,tangu lini mungu,kama yupo alisharuhusu mtu kuua mwenzake kwasababu za kisiasa?
 
Son for beach haipo popote duniani isipokuwa son of bitch ndio ipo mwisho ni kwamba gaidi ni ukoo wenu mnaofuga misukule nyambafu
 
Back
Top Bottom