Jinsi Moto Na Maji Vilivyoamua Hatima Ya Watuhumiwa Nchini Uingereza Katika Karne ya 17

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
FB_IMG_1637006940492.jpg

JINSI MOTO NA MAJI VILIVYOAMUA HATMA YA WATUHUMIWA NCHINI UINGEREZA KATIKA KARNE YA 17

Jinsi wakati unavyozidi kusonga ndivyo mambo mengi yanavyobadilika , maendeleo ya sayansi na teknolojia hali tuliyonayo kwa sasa si kama ilivyokuwa hapo zamani.

Sekta nyingi zinabadilika na kuboresha huduma zao kama vile sekta ya afya kwa kugundua vifaa bora zaidi kwa ajili ya kuchunguza afya ya mwili wa binadamu, pia katika sekta ya mahakama yapo mambo ambayo wanayafanya ili kuhakikisha watu wanapata haki zao kwa usahihi.

tuangalie jinsi mahakama inavyofanya kazi kwa sasa yaani kwa mfano mtu akiwa na mashtaka yanayomkabili inampasa kuwa na maelezo ya kutosha ama mashahidi ambao watamsaidia ili aonekane hana hatia.

Pia kunaweza kuwa na mashahidi ambao wakathibitisha mtu Fulani ana hatia hivyo ndivyo mahakama inavyofanya kazi yake ya kutoa haki kwa wananchi wake.

Ushahidi ukikosekana katika mahakama mtuhumiwa anaweza kuachiwa huru au akabaki mahabusu kwa ajili ya kusubiri upelelezi wa kesi yake kukamilika.

Lakini katika karne ya 13 nchini Uingereza mambo yalikuwa tofauti kidogo kwani wao katika mahakama yao mtu alikuwa akishutumiwa kwa kutenda kosa kwa mujibu wa sheria zao walikuwa na njia tatu za kuthibisha kuwa mtuhumiwa alikuwa na hatia au hakuwa na hatia.

Zipo nadharia mbalimbali zinazoonyesha chimbuko la mtindo huu wa kimahakama moja wapo inadai kuwa ilianzia nchini Liberia na inasemekana watu wa nchi hiyo walikuwa wakiipenda kwa sababu walikuwa wanaamini kuwa kupitia njia hii walipata haki zao bila kudhulumiwa.

Ipo nadharia nyingine inadai kuwa chimbuko la mtindo huu wa kimahakama ulianzia nchini Ujerumani baadhi ya makabila yalianzisha mtindo huu ikihusianishwa na kisa kinachopatikana katika kitabu kitakatifu cha hesabu 5: 11-22.

Katika sura hiyo kuna kisa cha mwanaume ambaye alikuwa akitaka kuthibitisha kupitia kuhani kuwa mkewe alikuwa yuko safi yaani hakutoka nje ya ndoa yao.

Zipo nchi nyingine ambazo zilikuwa na mtindo huu wa kimahakama kama vile
Kulikuwa na adhabu nyingi sana zilizokuwa zinatisha hata ukisikia lazima utajawa na woga , wengine walikuwa wanauliwa kinyama taratibu kwa maumivu yasiyokuwa na kipimo pia wengine walikuwa wakidhalilishwa mtaani kwa kuvaa vinyago vya Wanyama katika sura zao.

Walikuwa wakizitumia njia hizi tatu kufikia mwisho wa maamuzi ya kimahakama na kuhakikisha haki inapatikana .

Adhabu ya kwanza ilikuwa ni matumizi ya maji ya baridi ambapo mtuhumiwa aliwekwa kwenye maji hayo kwa muda kadhaa, na akionekana mtu huyo anaelea kwenye maji basi mtu huyo moja kwa moja alipatikana na hatia.

Lakini kama angezama ndani ya maji alionekana kama mtu asiyekuwa na hatia na aliachiliwa mara moja na kuwa huru.

Adhabu ya pili walitumia maji ya moto, ndani ya maji hayo walikuwa wanaweka mawe ambayo yalikuwa yakipata moto haswa.

Baada ya maji hayo kuchemka mtuhumiwa alitakiwa kuingiza mkono ndani ya maji hayo ili kutoa jiwe , hii ilikuwa ni adhabu mbaya sana kwani watu wengi walikuwa wakipata majeraha .

Basi mtuhumiwa akiingiza mikono ndani ya maji hayo yamoto na kuchuku jiwe, kisha ni lazima atapata jeraha la kuungua, ikitokea kidonda kikapona ndani ya siku tatu ilimaanisha mtuhumiwa hakuwa na hatia na kama kidonda kingechukua zaidi ya siku tatu kupona basi mtu huyo alihesabiwa ana hatia.

Adhabu hizo zilikuwa zinahusishwa na Mungu kwani waliamini kuwa Mungu ni mwaminifu na hawezi kumuacha mtu asiye na hatia akadhibiwa.

Pia Wakati mwingine watuhumiwa walitakiwa kuweka mikono yao katika jungu lenye maji ya moto, na inasemekana kuwa kwa wale ambao walikuwa hawana hatia mikono yao ilikuwa haiungui kwa kuwa Mungu alikuwa akiwasaidia.

Lakini kwa waliokuwa wanakutwa na hatia ni wale ambao walipokuwa wakiingiza mikono kwenye maji na kuungua.

Mtu alipobainika na hatia kulikuwa na sheria ya kulipa faini kwa kusema uongo, pia kulikuwa na adhabu ya kifo na uhamisho hii ilitegemea mtuhumiwa anashutumiwa kwa kesi gani, lakini kwa wale ambao walijijua kwamba hawana hatia hawakuwa na hofu walichagua njia hizo za kujaribiwa, kuwa waliamini Mungu atawalinda katika hayo.

Inaelezwa kuwa majaribio hayo yalikuwa yakifanyika katika kesi ambazo ni muhimu na za kijinai ambazo ushahidi wake ilikuwa ni ngumu kupatikana.

Adhabu ya kwanza ya kumtupa mtuhumiwa ndani ya maji baridi hii sanasana ilikuwa inatumika ili kuwaumbua wachawi walioko ndani ya jamii yao, kama nilivyoeleza hapo juu ikitokea mtuhumiwa ameelea juu ya maji basi huyo alichukuliwa kuwa ni mchawi na hatua dhidi yake zilichukuliwa.

Pia inaelezwa kuwa majaribio hayo yalikuwa yakifanyika kanisani kwa sababu waliamini kuwa Mungu ana uwezo wa kuangalia na kuamua kuzihirisha nani mwenye hatia na nani alikuwa hana hatia.

Kutokana na ushawishi wa watawala na viongozi wa kidini mitindo hii ya kimahakama ilifikia kikomo ambapo watawala waliamua kuwe na njia nyingine na kupata ushahidi juu ya mshtakiwa na kupendekeza adhabu nyingine badala ya kifo.

Ushawishi wa pili ulitoka kwa viongozi wa makanisa ambao walitaka kuwe na usawa na maisha ya watu yasiangamie kwa sababu ya makosa waliyoyafanya hivyo walipendekeza watu hao kupewa nafasi nyingine ili wasitende maovu tena

Kwa amri ya Papa Innocent III katika baraza lake la nne la Lateran mwaka 1215 ndipo alipoamuru makuhani wote wasitoe adhabu kama walivyokuwa wakitoa mwanzo na huo ndio ulikuwa mwisho wa mtindo wa utoaji adhabu wa mahakama nchini humo.
 
Pongezi kubwa kwa Papa na Kanisa Catholic Duniani kote kwa kuondoa njia hii mbaya kabisa ya kutambua watuhumiwa, japokuwa hata hii ya kutegemea mashaidi sio nzuri kabisa ila walau ina uhafadhal.
 
Pongezi kubwa kwa Papa na Kanisa Catholic Duniani kote kwa kuondoa njia hii mbaya kabisa ya kutambua watuhumiwa, japokuwa hata hii ya kutegemea mashaidi sio nzuri kabisa ila walau ina uhafadhal.
Kweli hii haikuwa njia nzuri sana kutumika
 
Uliposema karne ya 13 alafu ukasema huenda waliipata katika nchi ya "Liberia"

umeanza kunitia wasiwasi
 
Back
Top Bottom