Jinsi Mkwawa alivyosalitiwa na mtu aliyemuamini

Asante mkuu na barikiwa... mimi nilikua naijua lugalo hii ya Dar es Salaam sasa nilipofika Iringa mwaka 2010 nikapakuta hapo lugalo Iringa. Asante mkuu kwa uandishi maridhawa.
 
Mwendelezo..

Wajerumani walimweleza Mtaki kuwa wao wasingeweza kufanya mazungumzo yoyote na Mkwawa kwa sababu aliliaibisha taifa lao hasa kwa akitendo cha kumuua Zelewski. Wajerumani walimshawishi Mtaki akubali kuwapa siri za namna ya kumpindua Mkwawa na baada ya hapo, yeye angefanywa Chifu wa Wahehe.

Ahadi hiyo ya kufanywa Chifu wa Wahehe ilimsisimua Mtaki. Akamwaga siri zote za namna ya kumvamia Mkwawa bila kushtukiwa. Hakuishia hapo, Mtaki aliwaongoza Wajerumani kupitia njia isiyo na ulinzi ya Ifakara, Mgololo, Mufindi mpaka makao makuu ya utawala wa Mkwawa.

Njiani Wanzagila walipomuona Mtaki yupo na Wajerumani wala hawakushtuka, walijua ndiyo alikuwa anawapeleka kwa Mkwawa kwa ajili ya mazungumzo, hawakujua kuwa tayari Mtaki alikuwa ameshauza utawala wao.

Bila kutarajia, Mkwawa alishtuka Kalenga inalipuliwa na mizinga ya Wajerumani. Himaya ya Mkwawa ilidhibitiwa kila upande. Mkwawa baada ya kuona hana namna yoyote na kwa vile alikataa aibu ya kukamatwa na kuteswa na Wajerumani, aliamua kujipiga risasi iliyofumua kichwa. Hiyo ilikuwa Julai 19, 1898.

Ni Mtaki ndiye aliyemtambua Mkwawa na kuwathibitishia Wajerumani kuwa ndiye mwenyewe. Wajerumani walimkata kichwa na fuvu lake kwenda kuliweka kwenye makumbusho ya Ubersee, Bremen, Ujerumani, kabla ya Julai 9, 1954, kurejesha fuvu hilo la Mkwawa na kuhifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho la Mkwawa, Kalenga, Iringa.

Baada ya Mkwawa kuuawa, Wajerumani hawakutimiza ahadi ya kumpa Mtaki uchifu wa himaya yote ya Wahehe. Waliamini kuwa kama aliweza kumsaliti Mkwawa, basi angeweza kuwasiliti Wajerumani wakati mwingine kama angeshawishiwa.

Himaya ya Wahehe ikagawanywa mara nne, ili wawe viongozi wenye himaya ndogondogo na kufanya kazi kwa muongozo wa Wajerumani. Uhehe Kati, kiongozi wake alikuwa Lusinde Mwang’ingo, Kaskazini-Magharibi, alipewa Msengidunda Mwamgongolwa, Kaskazini-Mashariki, Msatima Mwakindole na Kusini alisimikwa Mtaki.

(Copied and pasted from facebook source; mm ni mtanzania najivunia kiswahili)
 
Bongowood yetu kutwa na maswahibu ya mapenzi...! Yaaani hawajiongezi hata kidogo.
-----
Hata hivyo nisiwalaumu sana ...kutengeneza movi bora kabisa ya Mkwawa dhidi ya wajerumani inahitaji ela nyingi sana.

Asante sana Mleta mada.
... wakati ya mapenzi ni chumba chenye kitanda na ka-tv show imeisha! Kutengeneza movie lenye akili sio lelemama.
 
Mwendelezo..

Wajerumani walimweleza Mtaki kuwa wao wasingeweza kufanya mazungumzo yoyote na Mkwawa kwa sababu aliliaibisha taifa lao hasa kwa akitendo cha kumuua Zelewski. Wajerumani walimshawishi Mtaki akubali kuwapa siri za namna ya kumpindua Mkwawa na baada ya hapo, yeye angefanywa Chifu wa Wahehe.

Ahadi hiyo ya kufanywa Chifu wa Wahehe ilimsisimua Mtaki. Akamwaga siri zote za namna ya kumvamia Mkwawa bila kushtukiwa. Hakuishia hapo, Mtaki aliwaongoza Wajerumani kupitia njia isiyo na ulinzi ya Ifakara, Mgololo, Mufindi mpaka makao makuu ya utawala wa Mkwawa.

Njiani Wanzagila walipomuona Mtaki yupo na Wajerumani wala hawakushtuka, walijua ndiyo alikuwa anawapeleka kwa Mkwawa kwa ajili ya mazungumzo, hawakujua kuwa tayari Mtaki alikuwa ameshauza utawala wao.

Bila kutarajia, Mkwawa alishtuka Kalenga inalipuliwa na mizinga ya Wajerumani. Himaya ya Mkwawa ilidhibitiwa kila upande. Mkwawa baada ya kuona hana namna yoyote na kwa vile alikataa aibu ya kukamatwa na kuteswa na Wajerumani, aliamua kujipiga risasi iliyofumua kichwa. Hiyo ilikuwa Julai 19, 1898.

Ni Mtaki ndiye aliyemtambua Mkwawa na kuwathibitishia Wajerumani kuwa ndiye mwenyewe. Wajerumani walimkata kichwa na fuvu lake kwenda kuliweka kwenye makumbusho ya Ubersee, Bremen, Ujerumani, kabla ya Julai 9, 1954, kurejesha fuvu hilo la Mkwawa na kuhifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho la Mkwawa, Kalenga, Iringa.

Baada ya Mkwawa kuuawa, Wajerumani hawakutimiza ahadi ya kumpa Mtaki uchifu wa himaya yote ya Wahehe. Waliamini kuwa kama aliweza kumsaliti Mkwawa, basi angeweza kuwasiliti Wajerumani wakati mwingine kama angeshawishiwa.

Himaya ya Wahehe ikagawanywa mara nne, ili wawe viongozi wenye himaya ndogondogo na kufanya kazi kwa muongozo wa Wajerumani. Uhehe Kati, kiongozi wake alikuwa Lusinde Mwang’ingo, Kaskazini-Magharibi, alipewa Msengidunda Mwamgongolwa, Kaskazini-Mashariki, Msatima Mwakindole na Kusini alisimikwa Mtaki.

(Copied and pasted from facebook source; mm ni mtanzania najivunia kiswahili)
Mnyamwezi mtu m-bad sana.
 
Hii story ni nzuri sana aisee asante kwa kuchukua muda wako kutufahamisha tusio yajua hongera sana wewe ni mwandishi hodari

Asante mkuu...nimesoma "Mtaki Mwanyenza" nikakumbuka "Kapele" ambaye naye alipewa hadhi ya uchifu mdogo kama mtaki. Kapele naye alikuwa Mnyamwezi, aliyepelekwa ufipani kwa chifu Milanzi wa wafipa baada ya wakoloni - waarabu kisha wajerumani kukumbana na upinzani mkali. Hasa wajerumani walipokuta Wafipa tayari wanatengeneza magobole.

Falme hizi mbili za wafipa na wahehe zilikuwa tishio kwa Chifu Isike wa Tabora, na hata chifu Milambo wa Urambo-Tabora Magharibi alimchukia sana Isike kwa kuwa kibaraka wa wakoloni. Ukizingatia kuwa Mirambo alikuwa chotara wa muha na mbungu. hakuwa pure mnyamwezi.

Isike alikuwa anatumia trick hiyo ya kuwapeleka vibaraka wake katika himaya ngumu kwake na kwa wajerumani, na hata kuwatoa wanawake binti zake na jamaa zake wakaolewa na machifu hao, na hata kuwashawishi waachane na dini zao za asili waembrace dini za wakoloni, hasa dini yake mpya aliyokuwa ameshaipokea kutoka kwa waarabu. trick ambayo alifanikiwa sana kwa mkwawa.
 
Kwa nini wajerumani walichukua fuvu la Mwawa
as signature proof kwa chancellor kuwa wamemuua mpinzani wao. hata hivyo zamani hata wakati wa utawala wa warumi ilikuwa hivyo. Na asipofanywa hivyo anachukuliwa mateka anapelekwa kwao.

Bila shaka Mkwawa asingejiua, wangemteka wakampeleka ujerumani akawa mfungwa wa kudumu huko.
 
Asante mkuu...nimesoma "Mtaki Mwanyenza" nikakumbuka "Kapele" ambaye naye alipewa hadhi ya uchifu mdogo kama mtaki. Kapele naye alikuwa Mnyamwezi, aliyepelekwa ufipani kwa chifu Milanzi wa wafipa baada ya wakoloni - waarabu kisha wajerumani kukumbana na upinzani mkali. Hasa wajerumani walipokuta Wafipa tayari wanatengeneza magobole.

Falme hizi mbili za wafipa na wahehe zilikuwa tishio kwa Chifu Isike wa Tabora, na hata chifu Milambo wa Urambo-Tabora Magharibi alimchukia sana Isike kwa kuwa kibaraka wa wakoloni. Ukizingatia kuwa Mirambo alikuwa chotara wa muha na mbungu. hakuwa pure mnyamwezi.

Isike alikuwa anatumia trick hiyo ya kuwapeleka vibaraka wake katika himaya ngumu kwake na kwa wajerumani, na hata kuwatoa wanawake binti zake na jamaa zake wakaolewa na machifu hao, na hata kuwashawishi waachane na dini zao za asili waembrace dini za wakoloni, hasa dini yake mpya aliyokuwa ameshaipokea kutoka kwa waarabu. trick ambayo alifanikiwa sana kwa mkwawa.
Nimepata kitu kipya hapa
 
Kizazi hiki what went wrong tuko na vijana laini laini sana dah. Kulikua na wanaume enzi hizo.
 
Mzee Mohammed said njoo huku,kuna mtu anapotosha historia ya sheikh mkwawa!
Wise...
Mbona historia hiyo imekaa vyema kapotosha kitu gani?

Wewe ndiyo mpotoshaji.
Mkwawa hakupata kuwa Sheikh katika maisha yake yote.

Mkwawa alisilimu na kuwa Muislam na aliyemsilimisha ni Abushiri bin Salim Al Harith wa Pangani.

Jina alilochagua baada ya kuingia Uislam ni Abdallah.

Ukifika Mkwawa Museum Kalenga utakuta kumbukumbu nyingi za Mkwawa pamoja na barua alizokuwa akiandika kwa hati za Kiarabu kwani alijifunza kusoma na kuandika.
 
Kwa nini aliitwa Mkwawa? Hilo linatokana na jina lake “Mkwavinyika” ambalo lilifupishwa na kutamkwa “Mkwava” lakini baadaye watu wakaona ni rahisi zaidi kuita “Mkwawa”
Kuna ukoo Iringa unaitwa Mbeva ikimaanisha panya, sasa wanaiga hii ya Mkwava na wao wanaitwa Mbewa, sasa mdogo mdogo hata vanu yenye maana ya watu itakuwa wanu etc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom