Jinsi mkutano wa Dr.Slaa ulivyochanganya polisi na wahuni wa CCM..na dili kuharibika.

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Wiki hii watu watakuwa wamechanganyikiwa ,kucheka na kushangazwa na kinachotokea ktk kipindi hiki.CCM wamedhamini na coordinate matukio maalumu kwa ajili ya kumkwamisha Dr.Slaa au hata kumdhuru ktk kivuli cha wafuasi wa Zitto.

CCM walijisahau na kutangaza kuwa wafuasi wa Zitto wamepiga marufuku Dr.Slaa kwenda.Dr.Slaa kwa kujua kuwa shetani siku zote ana tumia vitisho na mifano fulani ya kutisha ili kukatisha mipango ya watu.Ila hiyo ikaiubua tena hatari kwa CCM kutuhumiwa na kuwajibishwa baada ya matukio ya aina fulani ya kigaidi Arusha,na sehemu nyingine nchini.Game likaanza kuwa ugly na linalowapa CCM majukumu kuliko nafasi ya kufanikisha nia hiyo.

CCM pia walikuwa wanakabiliwa na shinikizo lingine la kuwalinda hao washabiki, wafuasi wa ZITO in collabo with CCM.CCM walijua kuwa hao jamaa wangeshikwa na makamanda+red brigade hao jamaa wangaamizwa au kupata kichapo ambacho kingepelea kuumbuliwa kwa kukutwa na kadi za CCM km kitambulisho mara polisi wakiwakamata ili kusort wa CCM na wachadema (Masalia), na wanaobaki wawaambiwe wakiri na kufanyiwa show nyinginyingi.Hapo ndipo Polisi wakapewa role

Sasa balaa likaja kuwa gumu kuliko uwezo wa CCM na Polisi,Polisi walisindwa cheza timing ,ya kuwaachia jamaa wafanye show yao ,halafu kabla ya reaction ya makamanda basi polisi wawashike na kuwaokoa.Sasa hali iliharibiwa sana na Dr.Slaa kwa kuwakaribisha..polisi wakashindwa wachezesha show ,ili wawakamate na kuwatenganisha ili wawapate wale watakaotumika kutangaza kuwa ni wanachadema wanaopinga hiyo hali.Halafu akina Kova wapande na kutangaza huku wakimwambia dr.Slaa ni hatari kwa hivyo ni bora wakatatue matatizo ya ndani ili kuepusha vurugu.

CDm wamekujwa unpredictable na hivyo polisi kw autendaji wa robot hawakupercieve hilo na mwisho wakaishia kufanya show ya kusaidia CDM kushika na kuwaabisha wahuni ktk Whuni days.

Hiyo ndiyo hali halisi ya polisi walioshngaza watuktk issue ya Zitto-Kigoma na Ziara ya Dr.Slaa.

3511736_orig.jpg

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kushirikiana na wananchi, wakimdhibiti mmoja wa vijana waliofanya fujo katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika katika kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo mkoani Kigoma. (Picha na Joseph Senga)

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa jana alitibua mkakati wa kuvuruga mkutano wake uliofanywa na vijana watano kwa kutumia jina la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, baada ya kuwakaribisha wasogee mbele ya jukwaa ili awasikie vizuri. Kabla ya hapo, Dk. Slaa alifanya kitendo kilichowashangaza wengi mkutanoni, wakiwemo askari, baada ya kuwataka polisi waache mara moja kuchana mabango ya vijana hao na wasiendelee kuwazuia kujitokeza mbele ya mkutano wake uliofanyika jana mjini Kakonko.

"Polisi wangu nawaomba sana msiendelee kuchana mabango ya hao vijana wala msihangaike nao kuwazuia wasije hapa, tena ningependa kuwaona, waacheni wasogee hapa mbele ya watu wote.

"Chama hiki ni cha kidemokrasia, wala wasiwapatie taabu. Tunajua kuwa hayo yapo," alisema Dk. Slaa.

Vijana hao walionekana wakitoa mabango yao mifukoni mara tu baada ya msafara wa Dk. Slaa kuwasili eneo la mkutano ambapo kiongozi huyo alifungua dirisha na akiwaonyesha ishara ya kuwaita eneo la mkutano, huku akiwataka wasikae mbali na hayo madukuduku yao ili waende kupata majibu kama wana maswali.

2879970_orig.jpg

Akihutubia mkutano huo wa pili katika Uwanja wa Mwenge mjini Kakonko, akiwa ametokea kijiji cha Muhange, kata ya Muhange, ambako alifanya mkutano wake wa kwanza, Dk. Slaa alianza kwa kuwataka vijana hao wasogee mbele ya jukwaa ili wamsikie naye ayaone mabango yao yameandika nini.

"Vijana wangu hebu sogeeni hapa mbele kabisa ya jukwaa mkae hapa, kaeni hapa niwaone na nisome mlichoandika maana huko sioni mabango yenu yameandikwa nini," alisema Dk. Slaa huku vijana hao wakitii amri hiyo.

"Najua watu wengi mlishangaa nilipowazuia wale polisi wangu wasiendelee kuwazuia hawa wasije hapa mkutanoni na wasichane mabango yao.

"Haya mambo tulijua kuwa yangelikuwepo. Hayatusumbui kabisa. Naomba wananchi wangu kama mlivyoshangilia muwasikitikie tu hawa vijana maana hawajui wanachokifanya. Hebu ngoja niwaulize vijana wangu."

3885008_orig.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Community Center mjini Kibondo.

Dk. Slaa alianza kuwauliza vijana hao masuala kuhusu CHADEMA, ambapo alitaka kujua kama wanaifahamu katiba ya chama chao, nao walijibu mmoja mmoja kuwa hawajui, kisha akawauliza kadi za chama, wakajibu pia mmojammoja kuwa hawana, akawahoji tena kila mmoja aseme anatokea tawi gani.

Wakasema hawajui matawi yao, kisha akawauliza kama walikuwa wanawajua viongozi wa matawi yao, wakajibu walikuwa hawamjui kiongozi wao hata mmoja.

Kisha mmoja wao akasikika akisema, "Mimi ni mtoto wa mwenezi mstaafu wa CCM, sijui hayo mambo."

"Vijana wangu ni wazi hamjui mnachokifanya. Mnatumika tu, ndiyo maana nilitaka mje hapa karibu yangu, maana najua hamjui kitu mnastahili kuhurumiwa na kusikitikiwa! "Haya nikiwaambia hawa askari hapa wakawapime kiwango cha pombe mlicholewa leo mchana nani kati yenu atasalimika hapa?

"Wote! Kila mmoja hapa anaweza kuona mlivyolewa! "Askari mnaweza kuwapima hawa…aah! Haya! Hamna vifaa…bahati yenu; wanasema hawana vifaa," alisema Dk. Slaa huku vijana hao mmojammoja akianza kuondoka jukwaani wakikunja mabango yao, huku wananchi wakiwazomea kwa nguvu, wakiwaita ombaomba.
Picture
Baada ya kuondoka mbele ya jukwaa, vijana hao waligawanyika ambapo watatu waliondoka kabisa eneo la mkutano na kuwaacha wenzao wawili wakiwa wamekunja mabango yao.

Mabango hayo ambayo yalionekana kuandikwa kwa hati moja ya mwandiko, yalisomeka hivi: "Tanzania, Kigoma, Kakonko bila Zitto haiwezekani; Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe wote wajiuzulu mara moja; Hatuko tayari kusikiliza lolote bila Zitto."

7334002_orig.jpg

Baada ya vijana hao kuondoka kwa kunyongea, Dk. Slaa akishangiliwa na umati wa watu, aliendelea kuhutubia ambapo alisema ziara yake mkoani Kigoma haina uhusiano na masuala ya tuhuma za utovu wa nidhamu na uvunjwaji wa misingi ya chama hicho yanayoendelea ndani ya chama hicho, akisema kuwa ziara hiyo ilipangwa tangu Julai mwaka huu.

Alizidi kueleza kuwa ziara hiyo iliahirishwa mara tatu kutokana na majukumu ya kichama aliyokuwa akiyapata ndani na nje ya nchi, lakini akaendelea kupata msisitizo kutoka kwa viongozi hasa wa wilaya za Kasulu na Kibondo, kutokana na manyanyaso ambayo wananchi wanayapata kutoka kwa viongozi wa serikali na vyombo vya dola.

"Nimewauliza vijana wale masuala ambayo mwana CHADEMA yeyote anapaswa kuyafahamu na kuyajua, mambo yote yanayoendesha CHADEMA yamo ndani ya kitabu hiki. Kitabu cha katiba kina sehemu ya maadili, kanuni, itifaki pia tunayo miongozo ya chama. Si Mbowe, si Dk. Slaa, wala Mzee Mtei muasisi wa chama anaweza kuwa juu ya kitabu hiki.

"Ni kama ilivyo kwa Muislamu safi hawezi kuwa juu ya Korani au Mkristo hawezi kuwa juu ya Biblia. Hakuna! Ndugu zangu chama hiki kimekuwa kikubwa mno, si chama cha mtu yeyote yule, hakiendeshwi kwa kauli ya Mbowe, Slaa wala mtu mwingine. Hakuna aliye juu ya katiba hii. Kama kuna mtu hayuko tayari!"

via Tanzania daima

4153033_orig.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akipokea kadi ya uanachama, kutoka kwa liyekuwa Mwenyekiti Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM, Sevelino Damian, ambaye amehemia Chadema, wakati wa mktano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
 
Na bado watachanganyikiwa zaidi kesho. Maandamano hayazuii watawala kuendelea na ratiba zao. Chamsingi wanaoandamana wajulikane na waseme wanataka nini? Bilashaka Dr. Slaa atawajibu.
 
Chama cha kilaghai chadema kilishakufa mtahangaika sana na huyu marehemu chadema.
 
Hiki chama cha mafisadi tutakizikaje mkuu embu tuanze plan b
I think there is some thing to do here
Haiwezekani watu wanakufa njaa huduma mbovu alafu bado wanatuletea bla bla hapa
Hela walizompa Zitto zingetosha hata kujenga shule moja huko Kigoma
Ufisadi unaofanywa na hawa maccm ni mkubwa
Kwanza tuanze maandamano ya kukataa bei za umeme kupandishwa

Ivi wananchi wanajua kuna kodi tena kubwa zinazokatwa kwenye simu bila ridhaa ya wananchi
Hivi ndo vitu vya kuandamana
Tunawasubiri CDM watusaidie maana ndo kimbilio lilobaki
RIP maccm
 
ccm wanahangaika kuwafanyia mabaya cdm,kwa hilo wameshindwa na cdm wanazidi kupasua mawimbi,ccm waendelee kuuwa tembo.
 
Mbinu na mikakati ya kishetani ya CCM hazikuanza leo: aliekuwa msajili wa vyama vya siasa aliwahi kumtisha kamanda Lema eti asiende Arumeru kufanya kampeni kuwa atauawa! leo yuko wapi kile kibabu? Mwigulu amewahi kupeleka timu ya SImba iramba kijijini ili Slaa asipate wasikilizaji ! Kila mwenye kutaka kuhoji uhalali wa BAKWATA kumiliki mali za waislam kwa niaba ya CCM lazima watamdhuru! ... Majambia waliyosingiziwa CUF yako wapi? kuna wachagga wangapi Iringa, Tunduma, Mwanza, Kigoma, Singida, Dar es Saalam, Arusha waliowachagua wachagga wenzao? Siasa za ukabila na Udini ni sehemu ya mikakati ya mbinu chafu za CCM zisizokubalika kamwe... CCM watueleze sisi wananchi wenye kukabiliwa na hali ngumu ya maisha RASILIMALI zetu kwanini zinawanufaisha wageni? kwanini Tembo wanaangamizwa? kwanini Kodi inatuumiza? kwanin Huduma muhimu za kijamii hazipatikani ilhali sisi ni matajiri wakubwa katika sayari hii Dunia?...
 
Hiki chama cha mafisadi tutakizikaje mkuu embu tuanze plan b
I think there is some thing to do here
Haiwezekani watu wanakufa njaa huduma mbovu alafu bado wanatuletea bla bla hapa
Hela walizompa Zitto zingetosha hata kujenga shule moja huko Kigoma
Ufisadi unaofanywa na hawa maccm ni mkubwa
Kwanza tuanze maandamano ya kukataa bei za umeme kupandishwa

Ivi wananchi wanajua kuna kodi tena kubwa zinazokatwa kwenye simu bila ridhaa ya wananchi
Hivi ndo vitu vya kuandamana
Tunawasubiri CDM watusaidie maana ndo kimbilio lilobaki
RIP maccm

Haha..hao jamaa si wachawi..wachawi wapo tayarai kuangamiza kilakitu ili tuu wafanikisho kupata ushindi ktk kuloga .
 
hao jamaa muwakaribishe mbele halafu muwazunguke..wakija kwa shari wajue hadi polisi wawasaidie itakuwa issue.Wakija kwa amani basi waondoke kwa amani.
 
Chama cha kilaghai chadema kilishakufa mtahangaika sana na huyu marehemu chadema.

Kwani wewe hili ndio shairi pekee ulilomezeshwa na kiongozi wenu lumumba? kila siku wasema hivohivo huku unaumizwa moyo na ukweli uliopo? CHADEMA itawaliza vijana mnaoongozwa na uti wa mgongo badala ya ubongo
 
3511736_orig.jpg

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kushirikiana na wananchi, wakimdhibiti mmoja wa vijana waliofanya fujo katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika katika kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo mkoani Kigoma. (Picha na Joseph Senga)

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa jana alitibua mkakati wa kuvuruga mkutano wake uliofanywa na vijana watano kwa kutumia jina la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, baada ya kuwakaribisha wasogee mbele ya jukwaa ili awasikie vizuri. Kabla ya hapo, Dk. Slaa alifanya kitendo kilichowashangaza wengi mkutanoni, wakiwemo askari, baada ya kuwataka polisi waache mara moja kuchana mabango ya vijana hao na wasiendelee kuwazuia kujitokeza mbele ya mkutano wake uliofanyika jana mjini Kakonko.

“Polisi wangu nawaomba sana msiendelee kuchana mabango ya hao vijana wala msihangaike nao kuwazuia wasije hapa, tena ningependa kuwaona, waacheni wasogee hapa mbele ya watu wote.

“Chama hiki ni cha kidemokrasia, wala wasiwapatie taabu. Tunajua kuwa hayo yapo,” alisema Dk. Slaa.

Vijana hao walionekana wakitoa mabango yao mifukoni mara tu baada ya msafara wa Dk. Slaa kuwasili eneo la mkutano ambapo kiongozi huyo alifungua dirisha na akiwaonyesha ishara ya kuwaita eneo la mkutano, huku akiwataka wasikae mbali na hayo madukuduku yao ili waende kupata majibu kama wana maswali.

2879970_orig.jpg

Akihutubia mkutano huo wa pili katika Uwanja wa Mwenge mjini Kakonko, akiwa ametokea kijiji cha Muhange, kata ya Muhange, ambako alifanya mkutano wake wa kwanza, Dk. Slaa alianza kwa kuwataka vijana hao wasogee mbele ya jukwaa ili wamsikie naye ayaone mabango yao yameandika nini.

“Vijana wangu hebu sogeeni hapa mbele kabisa ya jukwaa mkae hapa, kaeni hapa niwaone na nisome mlichoandika maana huko sioni mabango yenu yameandikwa nini,” alisema Dk. Slaa huku vijana hao wakitii amri hiyo.

“Najua watu wengi mlishangaa nilipowazuia wale polisi wangu wasiendelee kuwazuia hawa wasije hapa mkutanoni na wasichane mabango yao.

“Haya mambo tulijua kuwa yangelikuwepo. Hayatusumbui kabisa. Naomba wananchi wangu kama mlivyoshangilia muwasikitikie tu hawa vijana maana hawajui wanachokifanya. Hebu ngoja niwaulize vijana wangu.”

3885008_orig.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Community Center mjini Kibondo.

Dk. Slaa alianza kuwauliza vijana hao masuala kuhusu CHADEMA, ambapo alitaka kujua kama wanaifahamu katiba ya chama chao, nao walijibu mmoja mmoja kuwa hawajui, kisha akawauliza kadi za chama, wakajibu pia mmojammoja kuwa hawana, akawahoji tena kila mmoja aseme anatokea tawi gani.

Wakasema hawajui matawi yao, kisha akawauliza kama walikuwa wanawajua viongozi wa matawi yao, wakajibu walikuwa hawamjui kiongozi wao hata mmoja.

Kisha mmoja wao akasikika akisema, “Mimi ni mtoto wa mwenezi mstaafu wa CCM, sijui hayo mambo.”

“Vijana wangu ni wazi hamjui mnachokifanya. Mnatumika tu, ndiyo maana nilitaka mje hapa karibu yangu, maana najua hamjui kitu mnastahili kuhurumiwa na kusikitikiwa! “Haya nikiwaambia hawa askari hapa wakawapime kiwango cha pombe mlicholewa leo mchana nani kati yenu atasalimika hapa?

“Wote! Kila mmoja hapa anaweza kuona mlivyolewa! “Askari mnaweza kuwapima hawa…aah! Haya! Hamna vifaa…bahati yenu; wanasema hawana vifaa,” alisema Dk. Slaa huku vijana hao mmojammoja akianza kuondoka jukwaani wakikunja mabango yao, huku wananchi wakiwazomea kwa nguvu, wakiwaita ombaomba.
Picture
Baada ya kuondoka mbele ya jukwaa, vijana hao waligawanyika ambapo watatu waliondoka kabisa eneo la mkutano na kuwaacha wenzao wawili wakiwa wamekunja mabango yao.

Mabango hayo ambayo yalionekana kuandikwa kwa hati moja ya mwandiko, yalisomeka hivi: “Tanzania, Kigoma, Kakonko bila Zitto haiwezekani; Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe wote wajiuzulu mara moja; Hatuko tayari kusikiliza lolote bila Zitto.”

7334002_orig.jpg

Baada ya vijana hao kuondoka kwa kunyongea, Dk. Slaa akishangiliwa na umati wa watu, aliendelea kuhutubia ambapo alisema ziara yake mkoani Kigoma haina uhusiano na masuala ya tuhuma za utovu wa nidhamu na uvunjwaji wa misingi ya chama hicho yanayoendelea ndani ya chama hicho, akisema kuwa ziara hiyo ilipangwa tangu Julai mwaka huu.

Alizidi kueleza kuwa ziara hiyo iliahirishwa mara tatu kutokana na majukumu ya kichama aliyokuwa akiyapata ndani na nje ya nchi, lakini akaendelea kupata msisitizo kutoka kwa viongozi hasa wa wilaya za Kasulu na Kibondo, kutokana na manyanyaso ambayo wananchi wanayapata kutoka kwa viongozi wa serikali na vyombo vya dola.

“Nimewauliza vijana wale masuala ambayo mwana CHADEMA yeyote anapaswa kuyafahamu na kuyajua, mambo yote yanayoendesha CHADEMA yamo ndani ya kitabu hiki. Kitabu cha katiba kina sehemu ya maadili, kanuni, itifaki pia tunayo miongozo ya chama. Si Mbowe, si Dk. Slaa, wala Mzee Mtei muasisi wa chama anaweza kuwa juu ya kitabu hiki.

“Ni kama ilivyo kwa Muislamu safi hawezi kuwa juu ya Korani au Mkristo hawezi kuwa juu ya Biblia. Hakuna! Ndugu zangu chama hiki kimekuwa kikubwa mno, si chama cha mtu yeyote yule, hakiendeshwi kwa kauli ya Mbowe, Slaa wala mtu mwingine. Hakuna aliye juu ya katiba hii. Kama kuna mtu hayuko tayari!”

via Tanzania daima

4153033_orig.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akipokea kadi ya uanachama, kutoka kwa liyekuwa Mwenyekiti Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM, Sevelino Damian, ambaye amehemia Chadema, wakati wa mktano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
 
Magamba wamechanganyikiwa baada ya kugundua mwaka huu unamalizika bila CHADEMA kusambaratika kinyume na alivyowatabiria Wassira!
 
Back
Top Bottom