Jinsi Mkapa alivyokuwa makini hii ni moja ya barua zake za kujibu hoja dhidi ya maimam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Mkapa alivyokuwa makini hii ni moja ya barua zake za kujibu hoja dhidi ya maimam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkasoukumu, Aug 9, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  A Letter from the President of Tanzania, Hon.
  Benjamin Mkapa, in Response to Tanzanian
  Muslims' Grievances
  The President of the United The State House
  Republic of Tanzania Dar es Salaam
  17 Desemba 1999

  Ndugu Saleh Al-Miskry,
  Halmashauri Kuu ya Waislamu,
  C/o Islamic Club,
  S.L.P. 11392,
  DAR ES SALAAM

  Ndugu Al-Miskry,
  Ninakiri kupokea, kwa shukrani, barua yako ya tarehe 26 Agosti 1999, pamoja na viambatisho
  vyake. Imenichukua muda mrefu kukujibu kwa sababu mambo uliyoandika ni mazito, ya kitaifa, na
  ilinibidi niyatafakari kwa kina, niyafanyie utafiti zaidi, na nishauriane na wenzangu Serikalini kabla ya
  kuyajibu.

  Leo ninakuandikia si kwa lengo la kujibu hoja moja baada ya nyengine, au kutoa jibu kwa kila
  swali. Katiba ya Jamhuri yetu inanipa mimi, kama Rais, wasaidizi wengi. Ninaye Makamu wa Rais, na
  ninaye Waziri Mkuu. Ninaye waziri kwa kila sekta, na ninao wakuu wa mikoa na wilaya kwa kila eneo la
  nchi yetu. Nitakuwa siwatendei haki nikijibu maswali yanayowahusu wao. Ningeshauri, kama mlivyojenga
  mahusiano mazuri nami, mjenge pia mahusiano mazuri na mawaziri, wakuu wa mikoa, na kadhalika, ili
  kila jambo lisingoje mpaka lifikishwe kwa Rais.

  Nina uhakika kwa mfano, kwamba Waziri wa Elimu ana uwezo wa madaraka ya kutosha
  kushughulikia masuala ya elimu, ambayo kwangu ni muhimu sana. Akikwama atayaleta kwangu. Hiyo
  itasaidia kufanya mawasiliano nami yawe yale yanayohusu mambo ya msingi, badala ya kujadili matukio.
  Misingi hiyo itasaidia kuwaongoza watendaji wa Serikali na kuniwezesha mimi na nyinyi kuwa na vigezo
  vya kupima tunafanikiwa kiasi gani katika kuhakikisha kila mwannvhi anapata haki zake za msingi bila
  ubaguzi wowote kwa sababu za dini, dhehebu, kabila, jinsia, eneo analotoka, na kadhalika.
  Msingi wa kwanza ni utawala wa sheria. Nchi yetu lazima iendelee kutawaliwa kwa msingi wa
  sheria zilizowekwa kwa njia za demokrasia. Hivyo napata taabu kidogo raia wa nchi hii anapofikiri
  matatizo aliyo nayo yanaweza kutatuliwa nje ya mfumo wa utawala wa sheria.

  Kila mwenye kero
  akichukua msimamo huo, nchi hii itakuwa haitawaliki tena; itakuwa vurugu tupu. Kazi ya msingi ya
  Serikali yoyote ni kuhakikisha unakuwepo utawala wa sheri, ulinzi na usalama wa raia wote, wa aina na
  imani zote. Uhalali wa raia kudai haki nje ya mfumo wa utawala wa sheria unaweza ukakubalika penye
  utawala wa kikoloni, utawala wa ubaguzi wa rangi, au utawala wa kidikteta. Uhalali huo haupo hata kidog
  katika nchi huru, inayoongozwa kwa misingi ya demokrasia kama ilivyo Tanzania.
  Kwa sababu hiyo nimefadhaishwa sana na kauli za kuashiria shari za wale wanojiita "Shura ya
  Maimau Dar es Salaam". Pamoja na mbmo mengine ya uchochezei wanasema, "Waislamu hatuna moyo
  tena na Serikali ya nchi hii na vyombo vyake vyote likiwemo Bunge na Mahakama". Ninajua huu sio
  msimamo wa Waislam walio wengi, lakini matamko yasiyokuwa na kiasi kama haya yasipokanushwa, na
  wanaoyatoa wanapopewa fursa na majukwaa ya kuyasema, hiyo inawapa silaha wale wachache
  wanojaribu kupakamatope heshima na picha nzuri ya Waislamu. Mimi na ninyi tuna kazi ya kuwashihisha
  wenye hulka ya aina hiyo, lakini matamko kama haya yatafanya kazi hiyo iwe ngumu zaidi.
  Utawala wa sheria chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri. Katiba yetu imepiga marufuku ubaguzi
  wowote, kwa msingi wowote, ikiwemo dini, kabila, rangi, eneo analotoka mtu, na kadhalika. Katiba hiyo
  pia imetoa uhuru kamili, ndani ya uwigo wa sheria, wa imani za dini kustawi katika uhuru wa ibada.
  Isipokuwa kwa wale ambao hawan imani na vyombo vyote vya dola, mimi nina imani kuwa mahakama
  zetu nina uwezo na uhusu kamili wa kumpa haki hizi za msingi yule ambaye atkauwa amenyimwa kwa
  ubaguzi.

  Narudia. Haki za msingi za kila raia zimo ndani ya Sheria Mama - Katiba - ya Jamhuri yetu.
  Kama kweli upo uhsahidi kwamba baadhi ya taasisi za umma au viognozi wa umma, wamebuni mfumo
  wao wa kuhakikisha Waislamu wananyimwa haki hizo, hao wala si wa kuchukuliwa hatua za nidhamu tu,
  bali ni wa kushitakiwa mahakamani. Wasionewe haya. Tusaidianeni wahsitakiwe!

  Siwezi kushangaa iwapo kuna mtu au kiongozi mahali ambaye ndani ya moyo wake ana chuku
  dhidi ya Wakristo au dhidi ya Waislam; au ana chuki dhidi ya naume au wanawake; au ana chuku dhidi ya
  wazramo au wahaya; au chuki dhidi ya watu warefu au wafupi. Ninachosema ni kuwa katika utafiti
  niliofanya hakuna mahali popote katika Serikali hii ambapo mfumo rasmi wa kubagua au kumnyima haki
  za msingi mtu yeyote kwa msingi wowote.

  Kweli, zipo tofauti kati ya idadi ya Waislamu na wasio Waislamu katika shile, vyuo, sehemu
  mbalimbli za kazi lakni huo si ushahidi wa mfumo wa ubaguzi. Sababu zake sote unazijua - ni za kihistoria
  na za kijamii, kama ilivyo kwa tofauti kati ya idadi za watu wa kabila mbalimbali au jinsia. Ingekuwa
  tofauti hizo peke yake zinatosha kuthibitisha mfumo rasmi wa Waislamu, kwa nini tusiseme pia kuwa upo
  mfumo rasmi wa kubagua wanawake, au watu wa kabila fulani, au rangi fulani, au umbo fulani. Na ukweli
  ni kuwa si kila mahali Waislamu ni wachache. Kwa mfano nimejaribu kuhesabu ni mabalozi wangapi, tena
  kwenye zile Ofisi za ubalozi muhimu sana, ambao ni Waislamu. Naomba na ninyi mfanye hesabu hiyo.
  Lakini turudi kwenye masuala ya msingi. Si jambo zuri sana kuanza kujena utamaduni wa
  kuhesabu watu kwa misingi ya kabila zao, dini zao, rangi zao, jinsia zao, au maeneo wanayotoka. Tangu
  uhuru tumejitahidi kujenga taifa ambapo haki na heshima ya mtu inatokana na utu wake, si dini yake,
  kabila lake, jinsia yake, na kadhalika. Siko tayari kujenga mfumo wa utawala ambapo sifa ya mtu kupata
  nafasi ya shule, au nafasi ya kazi, ni dini yake. Aidha, tukishaanza na dini tutawazuiaje wengine kudai nao
  wafikiriwe kwa misingi ya dhehebu la dini, kabila, jinsia na kadhalika. Hapo tutakuwa tumefumua kabisa
  misingi ya umoja, upendo, mshikamano na kuheshimiana waliyotuachia waasisi wa Taifa letu. Naomba
  sana tusitafute dawa ya ugonjwa mdogo itakayozua magonjwa makubwa zaidi yasiyokuwa na tiba.


  Vile vile kuanzisha taasisi mpya ya kupokea na kuchunguza ubaguzi wa kidini kutazidi kuvuruga
  tu kwa vile ni kukiri kuwa kweli upo ubaguzi uliojengeka ndani ya mfumo wa utendaji Serikalini; jambo
  ambalo si kweli. Aidha, kama nilivyosema, ukianzisha taasisi ya kushughulikia ubaguzi wa kidini, uwezi
  kukataa wengine wakidai taasisi nyingine ya kushughulikia ubaguzi wa jinsia, ubaguzi wa kabila, rangi, na
  kadhalika.

  Tusijitose sana katika zoezi la kuhesabu watu kwa misingi ya dini. Tukifanya hivyo tutaimarisha,
  badala ya kujihisi kwanza kama Watanzania. Mimi nilifikiri kuwa Tanzania ilishavuka hatua hiyo.
  Naomba usirudi nyuma kwenye kutukuza udini, ukabila, au maeneo tunayotoka. Tukishajitumbukiza huko
  hatuwezi kutoka tena. Badala yake lengo letu liwe kuelekea mahali ambapo tutakuwa vipofu wa dini,
  vipofu wa rangi, vipofu wa kabila, na kadhalika. Na pia tusisahau kuwa Tanzania yetu hii ina hata
  Maaskofu wenye majina ya Ramadhani au Hussein, na wengine wengi ambao wana majina yasiyofichua
  dini zao au kabila zao.

  Jambo jingine la msingi ni kuhakikisha kuwa Tanzania kama Taifa, na kama Serikali au Chama
  chochote cha siasa, inakuwa haina dini. Kwenye hili hakuna mjadala, maana ni hali hiyo ya kutinamia
  upande wa dini yoyote ndiyo inayotupa nguvu ya kusimamia na kuhakikisha kila raia anapata haki zake za
  imani za dini na uhuru wa ibada bila hofu au wasiwasi.
  Kwa hili Serikali ni refa anayehakikisha kila upande una haki sawa, na uhuru sawa; na kuwa
  uhuru wa kuabudu au kutangaza dini kwa upande mmoja hauathiri haki ya uhuru wa ibada na kutangaza
  dini kwa upande wa pili.

  Mimi ni Rais wa watu wa dini zote, na ni Rais pia wa wale wasiokuwa na dini; ni Rais wa kabila
  zote na rangi zote, jinisa zote na hulka zote. Mimi ni Rais wa wanywa pombe na wasio wanywa pombe;
  wala nguruwe na wasiokula nguruwe. Si kazi yangu kuhukumu nani kati yao ni mwema na nani si mwema.
  Kunitaka nimkataze mmoja anachopenda ni kunitaka nifanye kazi ya kuhukumu juu ya imani za watu
  ambayo si yangu; hiy mimi naamini ni kazi ya Mwenyezi Mungu mwenyewe.

  Hiyo pia ndiyo inayonifanya nichelee kukubali haraka haraka hoja ya Tanzania kujiunga na
  Shirika la Waislam (OIC). Nadhani si sahihi kuishinikiza Serikali ikubali hoja hiyo kwa vile tu zipo nchi
  nyingine zilizojiunga. Kila nchi huangalia mazingira yake na sababu zake. Kwa vile ukijiunga unafanya
  hivyo kama Taifa zima, si kama sehemu ya Taifa, siwezi kupuuza kabisa maoni ya wale ambao si
  Waislamu. Hivyo huu si uamuzi ambao ninaweza kuufanya kwa wepesi; unahitaji mashauriano zaidi na
  pande zote na kuelimishana ili Jamii yote ya Tanzania ielewane.

  Kuhusu suala la Mwembe Chai mimi nlilifikiri tulishaelewana kuwa haitasidia sana kuunda Tume
  ya Uchunguzi, maana unajua kulichotokea. Na tunajua kuwa zile fujo, ambazo hatimaye zilihitaji nguvu
  kubwa ya dola kuzizima, hazikuwa na uhusiano na mambo ya dini kabisa. Ndio maana miongoni mwa
  waliokamatwa walikuwapo wtu ambao wala si Waislamu. Bado haja na hoja ya kuunda Tume sijaiona.
  Tulipokutana tarehe 7 Julai, mwaka huu, mojawapo ya mambo tuliyozungumzia ilikuwa umuhimu
  wa kuwa na fursa ya mzungumzo ya kudumu baina ya waumini wa dini mbalimbali, (inter-faith dialogue),
  ili mradi wahusika wawe watu waliokomaa kimawazo, wenye busara na nia njema. Hii itasaidia kujenga
  maelewano baina ya waumini wa dini zote na hivyo kupunguza hisia za kibaguzi za kila upande, na
  kujenga msingi bora zaidi wa kufurahia uhuru wa imani katika mazingira ya kupendana na kuheshimiana,
  japo tuwe na imani tofauti za dini.

   
 2. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kweli ben alikuwa anajua kujenga hoja.
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red nimependa sana Mkapa alivyowajibu mashekh.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Miafrika jamani ama kweli Ndivyo Ilivyo..
  Ebu rudieni kusoma vizuri, Mkapa anajibu hoja ya Waislaam waliposema:-
  "Waislamu hatuna moyo tena na Serikali ya nchi hii na vyombo vyake vyote likiwemo Bunge na Mahakama".

  Sasa mnachokisifia hapa ni kipi? haya sii maneno tunayoyasema watu wote kila siku au kwa sababu yalisemwa na waislaam! Ni majibu gani ya kuridhisha ama yenye kuonyesha ukomavu hapa.. mimi sioni isipokuwa siasa za udini mtupu.. rahisi kwenu kuwaona waislaam ktk hali inayowakandamiza hata nyie, mlichoka na mnaendelea kuchoka na utawala wa CCM na Mkapa?..

  Yaani mnadanganywa kirahisi na maandishi ya mtu kwa sababu tu alikuwa akijibu upande wa pili usiokuhusu wewe kama Mkristu.. Ujinga mwingine bana ndio maana JK atatawala hadi 2015 na CCM itatawala milele maanake hapa kinachofuata ni CCM kumweka mgombea Mkristu Dr. Slaa anapokonywa washabiki na umaarufu.
   
 5. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [h=2][SIZE=+3]Barua kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Wananchi wa Tanzania kuwaomba waibane Serikali juu ya kadhia ya Mwembechai[/SIZE][/h] [SIZE=+2]Utangulizi[/SIZE] Mara baada ya mauaji ya kinyama yaliyofanywa na polisi katika eneo la Mwembechai tarehe 13 Februari, 1998, Kamati yetu iliitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza ukweli wa mambo yalivyotokea. Tulifanya hivyo kwa sababu hadi wakati huo, taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa mamlaka mbalimbali za nchi zilikuwa hazielezi ukweli wote. Na kwa bahati mbaya taarifa hizo zikawa zinafikishwa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na hivyo kupotosha ukweli wa mambo. Ndio maana katika mkutano ule tuliiomba serikali yetu, ili kuondosha utata uliokuwepo, iunde tume huru ya kuchunguza tukio la Mwembechai na yale yaliyopelekea kutokea kwa tukio hilo.
  Kwa bahati mbaya hadi leo tume hiyo bado haijaundwa. Mbali ya kutoundwa kwa tume, taarifa zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini, viongozi ambao awali walidai kuujua ukweli wa mambo na hivyo kuikataa haja ya kuundwa tume, ziliendelea kuwakanganya wananchi. Kwa kipindi kisichozidi mwezi na nusu, viongozi hao waliodai kuujua ukweli wa mambo walitoa sababu nne tofauti, na zenye kupingana. Hali hiyo ilitosha kuwa ni ushahidi wa haja na umuhimu wa kuundwa tume ya kuchunguza ukweli wa tukio na hasa yale yaliyopelekea kuzuka kwake.
  Waheshimiwa wabunge, hiyo ndio hali iliyopelekea Kamati yetu kutoa waraka wa kurasa 13 ambao ulieleza kwa kina chanzo cha tukio lile na yale yaliyotokea. Waraka huo uliosainiwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Kamati yetu, ulisambazwa kwenu waheshimiwa wabunge, wanasheria, wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na taasisi mbalimbali za nchi ikiwemo inayoshughulikia usalama wa taifa letu. Tulikuleteeni waraka ule Waheshimiwa wabunge ili kukujulisheni ukweli wa mambo na hivyo kukupeni fursa ya kuuchambua ukweli wa tukio hilo kwa kupima maelezo ya pande zote.


  [SIZE=+2]Shukrani[/SIZE]
  Hatuna budi Waheshimiwa wabunge kutanguliza shukrani zetu kwenu na hususan Mheshimiwa Kitwana Kondo, Mheshimiwa Ibrahim Msabaha, na Mheshimiwa Spika wa Bunge aliyewaruhusu kuzungumza juu ya kadhia ya Mwembechai, na ukatili wa polisi uliowadhalilisha akina mama na uliomtia kilema kijana Chuki Athumani. Aidha Waheshimiwa wabunge tunaomba kutoa shukrani za dhati kwa mbunge na waziri, Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru pamoja na baadhi ya wabunge kwa jinsi alivyojitokeza na kumtembelea mtoto Chuki Athumani alipokuwa mahabusu Hospitali ya Muhimbili alikofungwa pingu kitandani licha ya kilema cha kupooza mwili, alichopewa na polisi waliompiga risasi.
  Waheshimiwa wabunge, Kamati yetu na wanachi wote waliolaani mauaji yaliyofanywa na polisi Mwembechai tulifarijika sana kuona Jumuiya ya wanafunzi wa taaluma ya siasa, Utawala na Sayansi ya Jamii wakishirikiana na jopo la wasomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliona umuhimu wa kukutana ili kujadili kadhia ya Mwembechai, ukatili wa polisi na uvunjwaji wa haki za binadamu ulioandamana na kadhia hiyo. Tunakiri kufarijika vilevile na juhudi za Mwislamu mmoja aitwae Abu Aziz aliyempelekea Mwanasheria Mkuu wa Serikali yetu waraka wa kurasa 53 kuhusu suala la Mwembechai. Waraka huo ambao nakala yake pia ulitumwa kwenu, ofisi ya Rais, mabalozi na kwenye taasisi na jumuiya mbalimbali nchini, ulituongezea tamaa kuwa huenda wahusika na wenye majukumu ya kusimamia haki nchini watauona ukweli wa mambo kutokana na uchambuzi wa kina uliofafanua dhulma iliyotendwa na polisi Mwembechai dhidi ya haki za raia zilizoainishwa katika katiba ya nchi yetu.
  [SIZE=+1] [/SIZE]
  [SIZE=+2]Matumizi Mabaya ya Bajeti[/SIZE]
  Waheshimiwa wabunge, wananchi tunafahamu kuwa moja ya majukumu yenu ni kuchambua na kuidhinisha kasma ya bajeti kwa ajili ya matumizi ya wizara na taasisi mbalimbali za serikali, na mnafanya kwa niaba yetu. Na kwa sababu ya idhini mliyoipata kutoka kwa wananchi, mnayo haki na wajibu wa kuhoji matumizi mabaya au yale yanayokwenda kinyume na makusudio ya idhini yenu.
  Ni dhahiri, Waheshimiwa wabunge, kuwa kitendo cha wizara ya Mambo ya Ndani kuwaacha polisi wawapige risasi raia na kuwauwa kwa makusudi ni matumizi mabaya ya idhini yenu katika kupitisha bajeti ya wizara hiyo mwaka uliopita (1997/98). Hatuamini kwamba mliipa idhini serikali kutumia kodi za wananchi kununulia risasi jeshi la polisi ili liwauwe raia kwa kuwalenga shabaha kama wanyama. Na hivyo ndivyo walivyofanya pale Mwembechai tarehe 13 Februari, 1998.
  Mbali ya mauaji hayo wizara ya Mambo ya Ndani ilitumia pesa mlizoidhinisha mwaka jana kuwalipa posho askari ili wauzingire na waugeuze msikiti wa Mwembechai kuwa ni lindo la polisi, na wakadiriki hata kuzifuja pesa za wananchi kwa kuzungukazunguka na helikopta eneo la msikiti huo. Ilizitumia pesa hizo pia kwa kuwatesa raia waliovamiwa na kukamatwa kwa nguvu pasipo na kosa lolote, wengine wakiwa wamelala majumbani kwao, bila hata kufuata taratibu za kisheria kama vile kuwa na "Arrest Warrant" au "search warrant." Wananchi zaidi ya 200 walikumbwa na ukamatwaji huo wa kinyama ndiyo maana wengi kati ya hao wameachiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kutokuwepo na shitaka la kujibu.
  Wengi wa watuhumiwa, wake kwa waume, watoto na vikongwe waliwekwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne na kupewa mateso ya kila aina. Waliwekwa katika hali mbaya na kupatwa na magonjwa, walinyimwa matibabu wanayostahili, kisha walinyanyaswa kwa matusi na masimango kinyume na haki zao za Kibinadamu.
  Waheshimiwa wabunge, mahabusu mmoja Mohamed Omari alifia mikononi mwao. Wengi wengine wametoka wakiwa katika hali mbaya kiafya. Mtoto Chuki Athumani aliendelea kufungwa pingu kiasi cha kuwa taabu kumhudumia huku akiwa katika hali mbaya kiafya baada ya kupigwa risasi na polisi.
  Familia za mahabusu hao zimeteseka pia kwa kukosa huduma na msaada wa wale ambao walikuwa wasimamizi na viongozi wa familia hizo, kutokana na kuwekwa mahabusu kinyume cha sheria.
  Ni mateso makubwa kwa binadamu kuona binadamu mwenziwe anaonewa kwa kunyimwa haki yake ya kimsingi kama Mwanadamu. Ni jambo la mateso na huzuni kubwa vile vile kwa wananchi waliohuru katika nchi yao kuona wananchi wenzao wakinyanyaswa na kudhulumiwa haki zao kama raia.

  [SIZE=+2]Kulaani na Kudhibiti Madhalimu[/SIZE]
  Waheshimiwa wabunge, tumewaandikieni barua hii kwa kuzingatia mambo mengi likiwemo hili la kuidhinisha na kusimamia matumizi ya serikali na kutetea haki za raia. Mkiwa wananchi mlio Bungeni, mnalo jukumu la kitaifa la kuona kuwa taifa letu katika masuala tuliyoyataja haliwi taifa la madhalim na wabaguzi wa haki za binadamu kwa kisingizio chochote kile kama ilivyokuwa katika nchi ya Afrika Kusini zama za utawala wa makaburu. Ndiyo maana mnapo tunga na kuzipitisha sheria mbalimbali huzingatia yale yaliyotamkwa kwenye Katiba yetu ya nchi ambayo [SIZE=-0]inalinda [/SIZE]ubinadamu wetu na kusimamia haki za raia, pasipo ubaguzi.
  Hivyo mnayo haki na uwezo wa kulaani na kudhibiti madhalim wa haki za binadamu na raia nchini.
  Hadi leo, Wizara ya Mambo ya Ndani haijawakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya Sheria wale polisi waliouwa wananchi kwa kuwapiga risasi tarehe 13/2/98 Mwembechai. Bado haijawakamata na kuwafikisha mbele ya Sheria wale waliotoa amri kwa polisi kuwauwa wananchi wale. Bado haijachukua hatua yoyote dhidi ya malamiko ya wananchi waliopata mateso wakati wakiwa mahabusu. Haijawachukulia hatua yoyote wale polisi waliompiga risasi mtoto Chuki Athumani na kumsababishia kilema cha kupooza mwili. Hawajachukua hatua yoyote ya kuchunguza kifo cha mtuhumiwa Mohamed Omari aliyefia mahabusu.

  [SIZE=+2]Maombi Yetu[/SIZE]
  Kutokana na haya, Waheshimiwa wabunge tunakuombeni:
  (i) Mchukue hatua za kulaani utendaji mbovu uliojitokeza Wizara ya Mambo ya Ndani kuhusu suala la Mwembechai kwa kushindwa hadi sasa kuchukua hatua dhidi ya wauaji na waliodhulumu haki za raia kwa kuwatesa, kuwatia kilema na kuwaweka ndani kinyume cha Sheria.
  (ii) Tunakuombeni muibane Serikali iwaondoshe watendaji wabovu katika Wizara hiyo hususan viongozi wa Wizara na watendaji wake wakuu kwa kuachia polisi wauwaji na watesaji kuwa huru hadi leo.
  (iii) Tunawaomba muibane serikali ihakikishe kuwa polisi waliouwa Mwembechai na wale waliowatesa watuhumiwa wanafikishwa mbele ya Sheria.
  (iv) Tunakuombeni Waheshimiwa wabunge muibane Serikali mpaka tume ya kuchunguza kifo cha mtuhumiwa Mohamed Omari aliyefia Mahabusu inaundwa kama taratibu za kisheria (Inquest) zinzvyotaka.
  (v) Waheshimiwa tunawaomba muiambie Serikali iunde tume huru ya kuchunguza sababu zinazopelekea Waislamu kupuuzwa na kunyimwa haki zao za kimsingi kama binadamu na raia katika nchi yao.
  Tupo tayari kushirikiana na tume hiyo kupata ukweli wote ili nchi yetu iepukane na dhulma zinazotaka kuota mizizi dhidi ya wananchi kwa misingi ya kibaguzi.
  Tunakuombeni Msiidhinishe bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya mwaka huu (1998/99) mpaka Serikali ikupeni majibu sahihi.
  Vinginevyo itakuwa mmeshirikishwa katika kuwapa nyenzo wauwaji na kuhalalisha dhulma kwa kwa raia nchini.
  Tuanakutakieni heri,
  (Abdul Sattar)
  KAIMU Katibu
  Kamati ya Kupigania Haki za
  Waislamu Tanzania. Dar es Salaam, 9 Julai, 1998.
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280
  Slaa hana washabiki bali yeye kama mwenyekiti wa CDM ana wanachama.
  Hapa tunampongeza Mkapa alivyojibu kwa umakini mapendekezo yaliyotolewa na Mashekh coz yalikua hayana mantiki. Soma vizuri barua hii ya uncle Ben.
   
 7. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ndefu. nimesoma nusu nitamalizia kesho. crdt imeisha.
   
 8. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Poleni sana ndugu zangu waislam...ss kwa bunge la ndiyooo na siyooo nadhani hakuna aliyeongelea suala hili hata kidogo! Kwani nani alikuwa waziri wa mambo ya ndani muda huo?
   
 9. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />

  Don't generalize, waliosema hawana imani na bunge ni waislam kwa maandishi.....hao wengine don't speak for them,

  Mimi vuguvugu la mageuzi limeniingia miaka ya 2000 so speak for those who felt that way @ that time, don't drag everyone else..na sio udini...nakumbuka I voted for Lipumba not bcoz he's a moslem but bcoz he was the only oppsn candidate I had faith in...so yes in the year 1998 I wasn't into it and so shouldn't be dragged into it and I think many others too
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Baadhi wanamchukia mkapa lakini mimi huyu ndiye rais bora tangu ajiweke pembeni Mt Jk Nyerere!
   
 11. w

  woyowoyo Senior Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  kweli huyu alikuwa mdini kweli kweli, yaani alipoiingiza nchi ktk mkataba wa memorandum of understanding na mabilioni mangapi yanapewa taasisi za wakristo kama ruzuku alishauriana na waislam wapi?
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wa jiji la dar wa kipindi hicho aliyetoa amri kwa FFU wagawe dozi kwa mashekh alikua ni Mukama ambaye sasa ni katibu mkuu wa CCM.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lady Plse.. read between the lines. I said we all had no confidence na serikali ya Mkapa na Bunge! Kwa hiyo waislaam wakisema ndio inaleta tofauti gani. You voted for Lipumba right, tell me why? if not for the same reason..Oooh! and I quote You had FAITH in.... not Mkapa and his Cabinet I guess!

  Nachoshindwa kuelewa hizi mada zetu ni kupoint to musllim this Muslim that as if nyie ni ma genius fulani. lakini mwisho wa siku sisi wote ni maskini na Tanzania inazidi kudidimia kiuchumi. halafu bibie I don't speak for anyone here, na kibaya zaidi kama huwezi kuona Udini then wewe una matatizo. why is it so special what Mkapa wrote against Muslims..

  Labda nirudi nyuma kidogo ktk historia.. zamani ilikuwa hakuna mabucha ya nguruwe, wakristu wakaomba wakapewa..Ni sheria kupasisha watu wa dini moja kula nguruwe ambao mimi sioni tatizo hata kidogo lakini wasiombe waislaam kwa lolote ni tatizo kwa wakristu.. it's a problem ati ina influence watu wa dini nyingine. Tanzania ni member wa Jumuiya zote za Kikristu toka Red cross, YMCA, Mabenki, na taasisi zake nchi inafurika na mashirika ya dini lakini itakuwa ubaguzi kuikubali taasisi moja ya kiislaam. It's Ok serikali kuingia Muafaka na kanisa lakini ni makosa kuingia na chombo chochote cha kiislaam bila ridhaa ya wakristu. Haya kweli ni akili.. ndio maana mnafura Mkapa alivyowajibu waislaam!.. I mean, kuwajibu waislaam? - where does it leave you!

  Udini gani zaidi wa CCM ambao mnataka tuuzungumze!..Viongozi wa CCM siku zote wamekuwa wakiwakandamiza waislaam na hili halina Ubishi. Ndio maana mwanakjiji aliwahi kuuliza toka lini CCM wamekuwa marafiki na waislaam..
   
 14. c

  chinga 1 Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i like this guy kwa kweli natamani arudi he knows what he want in life.
   
 15. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ukiwauliza leo waislamu waliotoa tamko hilo hasa kuhusu serikali, watakuambia wako nayo bega kwa bega just because rais na makamu wake ni waislamu, na rais ajaye kama atakuwa mkristo watabadili mtazamo na kuwa dissidents wa serikali-huu ni ukigeugeu wa aina hii ya waislamu na tunawajua! kuhusu barua ya Mkapa pamoja na kwamba katika uongozi wake kuna mambo mengi yalinikera-amejibu barua kwa hekima na weledi wa hali ya juu hasa ukizingatia kundi la waislamu waliomuandikia barua walitaka kumuingiza mkenge rais na wananchi kwa ujumla katika kutuaminisha eti kuna mfumo rasmi wa ubaguzi dhidi ya waislamu! walitaka tuamini kuwa serikali,bunge na mahakama wana mfumo wa kubagua waislamu which is a total lie! these people are just suffering from inferiority complex, imagine hata leo hii ambapo viongozi wa juu wa kiserikali ni waislamu lakini bado kuna malalamiko kuwa serikali ina mfumo kristo, inashangaza sana! jamani watu wenye mawazo kama haya please abandon it! you are wasting time obsessing with something that does not exist, i honestly feel pity for people with such belief=(not religious faith).
   
 16. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkapa ndiye alikuwa Mkatoliki mkubwa hapa TZ akifuatiwa na Nyerere. Kaiba hela nyingi sana, bora aende kutubu kwa wizi alioufanya kwa nchi hii.
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mijitu mingine bwana haina cha kuwaza zaidi ya udini!
   
 18. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
   
 19. Nish

  Nish JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 732
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sishangai mkapa ni mfumo kristo mbona mbwa aliyepewa jina la migration aliyeuwawa sumbawanga aliundiwa tume sembuse waislam wa mwembechai? laana zimshukie
   
 20. C

  CLEMENCY JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hii inaitwa End Of thinking Capacity (ETC). Umetumia DOMOKRASIA yako Mr. Right. Changia hoja
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...