Jinsi michango ya Wabunge inavyotolewa Bungeni ni dhahiri kuwa hatuna Wabunge, Taifa letu halina watu makini

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Taifa ambalo lina watu makini waliopewa dhamana ya kuwakilisha wenzao kwenye chombo muhimu kama bunge wanachangia michango ya ajabu kana kwamba hawana akili za kuzaliwa.

Mbunge bila ya aibu anasimama bungeni na kudai kudai kuwa mashehe wa uamsho wamekaa muda mrefu mahabusu hivyo waachiwe kama hawana kosa. Anashindwa kupambanua kuwa suala likiwa mahakamani halitakiwi kujadiliwa bungeni maana kwa sasa mashehe wa uamsho kesi yao ipo mahakama kuu. Mbunge kama huyu anapoteza muda wake, na pesa za umma kujadili suala ambalo halitakiwi kujadiliwa.

Mbunge mwingine anasimama na kudai waliokufukuzwa kazi kwa kughushi vyeti feki walipwe mafao na stahiki zao. Bila kutumia ubongo wake kuwa walitenda jinai na kwa sababu jinai ni kosa linalohitaji adhabu basi kusamehewa kwao ni msaada mkubwa. Lakini anasimama bila aibu na kudai wanastahili kulipwa mafao yao na kulipwa stahiki zao. Hivi mbunge kama huyu anajua yupo bungeni kufanya nini?

Hii ni mifano miwili tu.
 
Ndugu yangu akili yako inafanya kazi sawasawa kweli lakini? Alichodai yule mbunge siyo kosa na ndiyo kuwatetea wananchi haswa. Kumbuka watu wale walichangia kwa jasho Lao.
Zombe alikutwa na hatia ya muaji ya wale wachimbaji wa madini wa MAHENGE Tuseme zombe hajalipwa mafao yake ya kustaafu jeshi la Polisi????
Babu seya alinajisi watoto wetu mpaka mahakama za nje zilimtia hatiani na aliachiliwa huru. Huku uraiani tumpige made????
 
Al Ustaadh Sheikh Rashid Gwajima ameamua kuwapigania Masheikh wenzake. Ngoja tusubirie matokeo sasa.
 
Back
Top Bottom