Jinsi Mhasibu alivyotafuna Mamilioni ya Jiji la Arusha na Kutokomea Gizani

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
581
1,000
Mhasibu wa halmashauri ya jiji la Arusha, Charles Jacob anasakwa na Mwajiri wake na ametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kabla ya kumpiga pingu kwa madai ya kutafuna kiasi cha sh,milioni 84 fedha za makusanyo ya kila mwezi kuanzia Machi, 2019 katika mizani wa mazao ya chakula.

Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea Mizani ya mazao iliyopo kwa Morombo ,jijini hapa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,Dkt Maulid Madeni amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, 2019 imekuwa ikiingiza Sh milioni 2.8 kwa siku lakini mhasibu hiyo amekuwa akiwasilisha kwenye akaunti ya halmashauri kiasi cha sh,110,000 tu kwa siku huku fedha zingine zikiishia mfukoni mwake.

Mhasibu huyo pamoja na wasimamizi wa mizani hiyo,Thobias Julius na Agness Loishiye ambao wanashikiliwa polisi ,wanadaiwa kusababisha upotevu huo wa fedha na kuisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo.

Madeni amewakamata na kuwaweka ndani wafanyakazi hao na kuagiza Jacob ambaye hakuwepo kazini kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi na kwamba hadi sasa hapatikani nyumbani kwake hata Simu yake ya mkononi haipatikani.

Kwa mujibu wa dkt .Madeni kituo hicho cha kukusanya ushuru hakifanyi vyema na kusababisha fedha nyingi kuishia mikononi mwa wakusanyaji na mhasibu huyo.

“Nilifuatilia muda mrefu ukusanyaji wa mapato nikagundua kuna ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na mhasibu huyo ndio maana leo hajaja hapa.”

“Nitahakikisha wahasibu wote wenye tabia kama hii nawatia pingi siwezi kukubali fedha za rais Magufuli zichezewe hivi ni bora unichezee Mimi "Alibaimisha Dkt Madeni

Aliongeza kuwa wakati anaanza Kazi aliikuta halmashauri hiyo kama Shamba la bibi kila mtu anajichotea fedha anavyotaka.

" Kwa mfano masoko mbalimbali ya Jiji yalikuwa yakiingiza makusanyo ya shilingi milioni 10 kwa mwezi lakini sasa yanaingiza sh,milioni 60 kwa mwezi kwa kila soko" Amesema Madeni
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,730
2,000
Atashikwa kalio sikumoja wemwache tu, pamoja na ukali wa Lema na madiwani wake hela inapigwa tu,
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,477
2,000
"siwezi kukubali pesa za Magufuli zichezewe hivi bora unichezee mimi" hahahahahaha uwiiii.
Pesa za hazina, ....pesa za serikali, ....pesa za halmashauri au za jpm!?
Maendeleo hayana chama na uzalendo hauna chama pia.
 
Coin

Member
Sep 4, 2013
10
45
Mkurungenzi alikuwa wapi muda wote mhasibu akitafuna pesa.miaka yote jamaa ankusanya kila gari 20000 kila siku zaidi ya magari 100 kwa siku
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,529
2,000
Alipokuwa anafuatilia kwa mda mrefu Ulaji huo akawa kimya tu

Kweli nchi ya ajabu sana hii yaani unaona kabisa hela zinapigwa umeuchuna tu halafu baada ya miezi ndio unamtafuta
 
infinix

JF-Expert Member
Sep 6, 2018
2,097
2,000
Alipokuwa anafuatilia kwa mda mrefu Ulaji huo akawa kimya tu

Kweli nchi ya ajabu sana hii yaani unaona kabisa hela zinapigwa umeuchuna tu halafu baada ya miezi ndio unamtafuta
Huyu mluguru kweli ni bwege,kwanza hajui hizo fedha ni za uma,anajua ni za Magufuli.
Pili,leo unagundua wizi kisha unasikilizia.....kamata kwanza,weka ndani mengine yatajulikana mbele ya safari.

Anafananisha Arusha na Matombo,Bunduki,sijui Mgeta
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,462
2,000
Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea Mizani ya mazao iliyopo kwa Morombo ,jijini hapa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,Dkt Maulid Madeni amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, 2019 imekuwa ikiingiza Sh milioni 2.8 kwa siku lakini mhasibu hiyo amekuwa akiwasilisha kwenye akaunti ya halmashauri kiasi cha sh,110,000 tu kwa siku huku fedha zingine zikiishia mfukoni mwake

Na huyo Mkurugenzi atumbuliwe, alikuwa wapi kuyajua hayo yote kwa miezi mingi namna hiyo
 
Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,653
2,000
“Nitahakikisha wahasibu wote wenye tabia kama hii nawatia pingi siwezi kukubali fedha za rais Magufuli zichezewe hivi ni bora unichezee Mimi "Alibaimisha Dkt Madeni"

Hivi kwanini mtu unajidhalilisha kiasi hiki ? Achezewe yeye ? Anataka achezewe wapi ?

Hizo pesa ni za Magufuli au kodi za walalahoi wa nchi ?

Hiyo Ph.D aliyonayo ni ya nini huyu ?

Ndio wale walio okotwa Jalalani ?

Ghaiii mmezidi sasa mpaka mnatia kinyaa.
 
ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
12,501
2,000
Mhasibu wa halmashauri ya jiji la Arusha, Charles Jacob anasakwa na Mwajiri wake na ametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kabla ya kumpiga pingu kwa madai ya kutafuna kiasi cha sh,milioni 84 fedha za makusanyo ya kila mwezi kuanzia Machi, 2019 katika mizani wa mazao ya chakula.

Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea Mizani ya mazao iliyopo kwa Morombo ,jijini hapa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,Dkt Maulid Madeni amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, 2019 imekuwa ikiingiza Sh milioni 2.8 kwa siku lakini mhasibu hiyo amekuwa akiwasilisha kwenye akaunti ya halmashauri kiasi cha sh,110,000 tu kwa siku huku fedha zingine zikiishia mfukoni mwake.

Mhasibu huyo pamoja na wasimamizi wa mizani hiyo,Thobias Julius na Agness Loishiye ambao wanashikiliwa polisi ,wanadaiwa kusababisha upotevu huo wa fedha na kuisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo.

Madeni amewakamata na kuwaweka ndani wafanyakazi hao na kuagiza Jacob ambaye hakuwepo kazini kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi na kwamba hadi sasa hapatikani nyumbani kwake hata Simu yake ya mkononi haipatikani.

Kwa mujibu wa dkt .Madeni kituo hicho cha kukusanya ushuru hakifanyi vyema na kusababisha fedha nyingi kuishia mikononi mwa wakusanyaji na mhasibu huyo.

“Nilifuatilia muda mrefu ukusanyaji wa mapato nikagundua kuna ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na mhasibu huyo ndio maana leo hajaja hapa.”

“Nitahakikisha wahasibu wote wenye tabia kama hii nawatia pingi siwezi kukubali fedha za rais Magufuli zichezewe hivi ni bora unichezee Mimi "Alibaimisha Dkt Madeni

Aliongeza kuwa wakati anaanza Kazi aliikuta halmashauri hiyo kama Shamba la bibi kila mtu anajichotea fedha anavyotaka.

" Kwa mfano masoko mbalimbali ya Jiji yalikuwa yakiingiza makusanyo ya shilingi milioni 10 kwa mwezi lakini sasa yanaingiza sh,milioni 60 kwa mwezi kwa kila soko" Amesema Madeni
We mkurugenzi bila kuiba ulitaka akale wapi
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,523
2,000
DED kachanganyikiwa, fedha za Umma anasema fedha za Rais, eti bora umchezee yeye kuliko kuchezea fedha za Rais

Magu anatisha hatareee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom