Jinsi mende alivyotaka kunitoa uhai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi mende alivyotaka kunitoa uhai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Sep 29, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wandugu uhai wa mtu ni kitu cha thamani sana na cha kulindwa kwa sababu sisi wanadamu tuko so fragile dakika moja tu mtu anakuwa sio hai tena. Katika ofisi nayofanya kazi ina mende wengi kupita maelezo famigation inafanyika kila mwezi lakini baada ya siku wanaibuka tena.

  Jana wakati narejea nyumbani kuilaki familia yangu ambayo haijaniona tangu kukuche nilipatwa na kisa cha ajabu sana. Nikiwa kwenye mataa ya salender bridge nilisikia muwasho maeneo ya paja la kulia, sikushtuka sana baada ya dakika chache nikasikia kitu chenye kama kinatoboa maeneo ya bailolojia nilishutuka sana kutokana na eneo lenyewe lilivyo nyeti badala ya kushika break nikakanyaga mafuta zaidi na kuacha njia. Sikuumia ila ule mshtuko ulikuwa mkubwa moyoni.

  Watu waliokuja na polisi waliishia kutabasamu na kucheka kwa sababu walinikuta nimeng'ang'ania bailojia kwa mikono miwili huku jasho linanitoka. Kwa kifupi ndio hivyo nikafanikiwa kumtoa mende alikuwa mkubwa sn. Kama kulikuwa na bonde kubwa pale nilikopata ile thoruba ningezama kwenye bonde au mto na mngesikia ndg yenu nipo MOI.

  Kwa wale wanaoishi ofisi kama yangu kabla ya kutoka ofisini ingia rest room toa suruale kung'uta kwa nguvu zote kujiweka salama. Au funga suruale kwa chini na rababendi ili wadudu wasipenyeze.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  pole sana mzee ni vema ukawa unatumia dawa ya mbu ya kuspry kama doom au rungu badala ya kujipulizia parfume.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  Pole sana mzee.
  Lakini pia Daraja la Salenda lina mauzauza yake.
  Si ndio hapohapo watu wanapoota manyoya?
   
 4. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole maskini, dah najaribu kuvuta picha haiji...
  Hiyo ofisi yenu nayo balaa
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni ofisi ya serikali au binafsi? Nahisi ni ya serikali japo sina uhakika.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mukubwa lets cut the chase..Imarisha usafi wa makazi yako bana.
   
 7. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu, tatizo la office zetu nyingi ni chafu sana, utakuta boss kachukua sofa iliyochakaa nyumbani na kuileta officen basi hapo ndipo kasheshe linaanzia mende kunguni hadi panya wanakuwa wanajiifadhi uko bila wasi wasi na isitoshe hakuna mtu wakufanya usafi yaani ni hatari tupu....

  Hizi office za waindi taaabu tupu.
   
 8. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mshikaji, unatuchek tu watu wa sumbawanga wakati na nyie wa mjini mnaamini ushirikina.
  Hapo salenda lazima pana zindiko kali sana.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kuna jamaangu mmoja akiona mende tu, basi ni balaa...anatapika hujawahi ona!
  Mkuu, pole sana, maana hapo ungeweza kupata accident mbaya sana!
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha mzee mende aliingiaje kunako?
  Ukifika job huwa unavua suruali kwanza ndo unaanza kazi?
  Dah pole mkuu hahahaha bora ulikuwa alone ungekuwa na wife angekuelewa vingine angejua umetoka kumega
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Haya maofisi yetu yamezeeka sana na kutokana na watu kulipwa mshahara mdogo wanakuja na vyakula vyao kama mihogo ya kuchemsha na mikate kama mlo wa mchana/lunch ikimwagika ofisini inasababisha mende kupata mlo na kuzaliana zaidi. Poverty is very expensive
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, pole sana. Lakini nakushauri wahi kwa Dr Sheikh yahya Hussein ukapate maneno maana huyo mende si bure, lazima alitumwa huyo... yaani maeneo yote ya kukaa yeye anakimbilia huko! Si bure
   
 13. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakuu sio kitu ya utani ni kweli kabisa, tena katika ofisi nyingi za serikali ni mambo ya kawaida kabisa..

  Hata panya wapo tuu katika hizi ofisi !!!!
   
 14. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  dah kweli we PHD nimecheka mpaka bas.......!!!!!!
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  bila kusahau
  panadol or aspirin kwa maumivu baada ya kumuondoa mende .pole sana ni la kawaida sema tu akukutaarifu anakupitia leo
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  dalili ya kwanza ni kwamba huvai chupi wewe,
  ishu ya pili ni kwamba hizo furmigation ni gelesha tu kwani wanakuja na povu la sabuni na wanaweka dawa kiduchu kiasi cha kuwalevya wadudu ionekane wanahangaikia kifo lakini hakuna kitu.

  Ishu ya tatu ni kwamba next time hakikisha umefunga seat-belt while you drive. huwezi jua kuwa nilikuona unavyohangaika na kuparamia kale kamsingi. pole sana
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280

  umenifurahisha unapouliza gongo tandale ,bila kuuliza hiyo ni ya sirikali ....
   
 18. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Pole ndugu... Lol!
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hamna kitu ..mkono wa mtu tu huo mkuu..1
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mtani umenichekesha sana...eti sivai kofuli...ngoja siku yatakukuta .....
   
Loading...