NGolo Kante
Member
- Feb 28, 2017
- 80
- 131
Nanai anahama na nani anabali lilikuwa ni swali linalogonga vichwa vya wengi Alhamisi iliyopita ya Novemba 15 ambayo kwa mujibu wa CCM iliuwa ni siku ya mwisho kwa Wabunge na Madiwani kutoka upinzani wanaotaka kuhamia ndani ya chama hicho.
Joto lilipanda na kuwavuruga wabunge hasa baada ya Mbunge wa Temeke CUF, Abdalah Mtolea kutagaza kujiuzulu Ubunge na kuhamia CCM
Duru za Siasa zinadai kuwa Katani Katani mapema siku hiyo alionekana katika viunga vya Bunge akiwa na Mtolea jambo hilo liliwahusisha wawili hao kujiuzulu na baadaye ikatajwa kuwa Wabunge wawili James Mbatia (NCCR) na Seleman Bungara 'Bwege' (CUF) walimnasua Katani
- ''Ni kweli Katani alikuwa miongoni mwa waliotakiwa kuhama siku hiyo(Alhamis) lakini kuna Wabunge wawili walizungumza naye na kumsihi sana asihame, alikuwa njiani kuhama kama alivyofanya Mtolea Bungeni'' Alisema Mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Katani alipozungumza na Mwananchi alisema hana wazo la kuhama na hata akihama hawezi kwenda CCM waliosema anaondoka walikuwa na hoja zao
Mbatia ambaye imeelezwa kuwa alihusika kumshawishi Katani asihame, alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alisema ni kweli alizungumza na Katani kipindi ambacho tayari 'nilishatoka Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli mbali na mengine nilimwambia 'Hekima, umoja na amani inalisimamisha taifa'
Kuhusu Katani Mbatia anasema ''Ni kweli Katani aliniambia anataka afanye uamuzi mgumu kwasababu anaona kuna giza nene katika chama chake(CUF)''
Baada ya kunieleza hayo nilimweleza mambo manne ambayo ni majukumu ya Bunge tuliyofundishwa na Spika Mstaafu Pius Msekwa yanayopaswa kuzingatiwa kabla ya kufanya maamuzi
Mambo hayo ni taifa lake, jimbo lake, chama chake na dhamira yake binafsi..
Chanzo: Mwananchi