Jinsi Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza na Marekani yalivyozingatia mauaji kama suluhisho

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Jinsi Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza na Marekani yalivyozingatia mauaji kama suluhisho.jpg


Je mauaji yanayodhaminiwa na serikali yanaweza kutumika kama mkakati? Na mauaji kama hayo yanaweza kukubalika kweli? Serikali hazikubali hilo, lakini wanasayansi wa nyuklia wa Iran wanajua inafanyika - na sio rahisi kutofautisha mauaji kama hayo na mpango wa serikali ya Marekani kuwauawa 'washukiwa wakuu wa ugaidi'

Miaka themanini iliyopita, timu ya wauaji waliopewa mafunzo Uingereza walikuwa wakijiandaa kutekeleza ukatili huo.
Aliyekuwa akilengwa alikuwa Reinhard Heydrich, mmoja wa watu walioogopwa sana katika Utawala wa Tatu, wakati huo akitawala Czechoslovakia

Kiokosi cha oparesheni maalum cha Uingereza kilichoundwa hivi karibuni (SOE) na harakati ya wakimbizi kutoka Czechoslovakia London zote zilihitaji kufanya tendo kubwa katika harakati za kukabiliana na serikali ya Czechoslovakia.
Upangaji wa Operesheni Anthropoid, kama inavyojulikana, umeelezewa kwa kumbukumbu za zamani za siri katika Hifadhi ya Kitaifa.
Kumbukumbu hizo zinafafanua jinsi raia wawili wa Czechoslovakia waliojitolea kw ahiari walivyofundishwa huko Uingereza na kisha kuingizwa kwa parachuti nchini mwao.

Maajenti wawili wamefundishwa kuhusu njia zote za mauaji tunazojua sisi, inasoma kumbukumbu mo...jpg



Maajenti wawili wamefundishwa kuhusu njia zote za mauaji tunazojua sisi," inasoma kumbukumbu moja kutoka Januari 1942.
"Wanakusudia kutekeleza operesheni hii ikiwa kuna fursa ya kutoroka baadaye au la."

Mnamo Mei wa mwaka huo, wanaume hao walimvizia Heydrich akiwa katika gari lake aina ya Mercedes ambalo ufa wake ulikuwa wazi wakati likipiga kona .

Bunduki ya mmoja wao iligoma lakini yule mwingine alitupa bomu ndani ya gari la Heydrich. Alijaribu kuwafukuza wanaume hao lakini majeraha aliyopata siku hiyo mwishowe yalimfanya kupoteza maisha yake .

Majibu ya watawala wa Nazi yalikuwa makali. Katika kijiji cha Lidice, inayodhaniwa kuhusishwa na wauaji, wanaume 173 zaidi ya umri wa miaka 16 waliuawa, kila mwanamke alipelekwa kwenye kambi ya mateso, kila mtoto alitawanywa, kila jengo lilibomolewa .

Je mauaji ni mbinu yenye ufanisi?​

"Kwa kweli waathiriwa hao wote wa ugaidi wa Nazi hawakustahili kuteswa'
Anasema mwandishi wa biografia wa Heydrich, Robert Gerwarth. Na mrithi wa Heydrich huko Prague alikuwa mkali zaidi, anasema.
Labda inaelezea kwamba mauaji hayakutumika sana wakati wa vita, baada ya hii.

Operesheni Foxley ilikuwa kawaida - SOE iliangalia kutumia mpiga risasi kumuua Hitler, na ikakusanya ujasusi wa kina juu ya mpangilio wa nyumba yake huko Berchtesgaden. Lakini mpango huo ulighairiwa, kwa sababu ulidhaniwa kuwa haungefanikiwa lakini pia kwa sababu maafisa waliogopa ingeharibu juhudi za vita - walisema kwamba kumtafuta mtu mwingine kumrithi Hitler ungeweza kuwa wa busara zaidi na mzuri katika kupigana na Uingereza.

Hofu juu ya matokeo limekuwa jambo muhimu kila wakati linalopunguza utumiaji wa mauaji. Lakini vivutio vya mauaji kama dawa rahisi havikuondoka. Wakati wa mzozo wa Suez, Waziri Mkuu Anthony Eden aliguswa na Kanali Nasser, rais wa Misri.

"'Ninataka Nasser,' na kwa kweli alitumia neno 'kuuawa'," waziri mmoja baadaye alikumbuka Edeni akisema. MI6 iliangalia njia mbali mbali lakini fursa hiyo haikujitokeza kamwe.

Umaarufu wa vitabu vya Ian Fleming vya James Bond katika miaka 50 iliyopita umesababisha watu wengi kuamini kwamba huduma ya ujasusi ya Uingereza ina leseni ya kuua. Mnamo 2009, nilimwuliza Mkuu wa MI6 wakati huo, Sir John Scarlett, ikiwa kulikuwa na kitu kama hicho.

"Hatuna leseni ya kuua," aliniambia.
Kisha nikauliza ikiwa MI6 ilikuwa imewahi kuwa nayo. Kulikuwa na kimya kisha akasema : "Sawa, sio kwa ufahamu wangu."
Machapisho katika Jalada la Kitaifa la Uingereza yanaonyesha kwamba mauaji yalikuwa kwenye fikra za baadhi ya watu huko London wakati wa Vita Baridi.

Mnamo 1960, Whitehall alihofia Waziri Mkuu wa Congo Patrice Lumumba alikuwa karibu sana na Muungano wa Soviet i, kwa hivyo HFT Smith, afisa wa Ofisi ya Mambo ya nje ya Uingereza - na baadaye mkuu wa MI5 - alielezea mapendekezo mawili ya kumshughulikia.
Ya kwanza, ambayo Smith alisema alipendelea, ilikuwa "ile rahisi ya kuhakikisha kuondolewa kwa Lumumba kutoka eneo la tukio kwa kumuua".

Aliendelea: "Kwa kweli hii inapaswa kutatua shida hiyo, kwani, kwa kadri tunavyoweza kusema, Lumumba sio kiongozi wa harakati ambayo ndani yake warithi wenye ushawishi kama wake'.

Maoni mengine kwenye faili yanaonyesha hisia tofauti juu ya chaguo hilo, miongoni mwa maafisa wa Uingereza.
Huko Washington, maafisa walitaka kuepuka kuhusishwa Rais Eisenhower na mauaji hata wakati kila mtu alijua kuwa ndivyo alivyotaka.

Katika mkutano mmoja wa baraza la Usalama wa Kitaifa mnamo 1960, rais alisema alitaka Lumumba "aondolewe".
CIA ilipeleka mmoja wa maajenti wake kwenda Congo, akiwa amebeba dawa ya meno yenye sumu, lakini mshirika wake aliyekuwa huko tayari alitupa sumu hiyo kwenye Mto Congo.

Lumumba mwishowe aliuawa na msaada kutoka kwa Ubelgiji badala ya msaada wa Marekani au Uingereza. Lakini wakati hii na njama zingine zikifichuliwa miaka ya 1970 - dhidi ya Fidel Castro huko Cuba kati ya zingine - kulikuwa na ghasia. Rais Gerald Ford alipiga marufuku mauaji.

Huko Uingereza, jaribio la kutumia mauaji kama njia ya mkato lilibaki. Alipokuwa Katibu wa Mam...jpg


Huko Uingereza, jaribio la kutumia mauaji kama njia ya mkato lilibaki. Alipokuwa Katibu wa Mambo ya Nje mwishoni mwa miaka ya 1970, David Owen aliwauliza maafisa wake ikiwa dikteta katili wa Uganda Idi Amin anaweza kuuawa.

Anakumbuka jinsi afisa ambaye alihudumu kama ofisa wa uhusiano na MI6 alisimama na kumwambia: "Hatufanyi kitu cha aina hiyo."
"Sawa, tunapaswa kufikiria kufanya kitu kama hicho, hali ni mbaya sana," Bwana Owen alijibu.

Anasema kuwa hali ya kibinafsi ya utawala mkali wa Amin nchini Uganda ilimaanisha kuwa kuua mtu mmoja kunaweza kuokoa maisha ya watu wengi.

Kuanzia miaka ya 1970 na kuendelea, Uingereza iligubikwa na mabishano juu ya Ireland ya Kaskazini. Kulikuwa na maswali juu ya ikiwa mamlaka ya Uingereza ilishirikiana na wanamgambo au kutumia sera ya "kupiga risasi kuua" ili kukabiliana na wanachama wa IRA.
Ugaidi umefanya suala hio kuwa gumu kwa kufifisha mipaka kati ya vita na amani, wapiganaji na raia na mizozo kati ya mataifa yenyewe.

Israeli, ambayo inajiona kama iliyo katika vita vya kudumu , imewalenga maadui zake kote Mashariki ya Kati. Huduma yake ya ujasusi, Mossad, inatuhumiwa kumuua kiongozi wa Palestina huko Dubai na vile vile wanasayansi wa nyuklia huko Tehran.

Tangu 9/11, Marekani inazidi kuzungumzia juu ya "mauaji yaliyolengwa" ili kuhalalisha vitendo ambavyo huenda viliitwa mauaji.
Marufuku ya Rais Ford juu ya mauaji bado inatumika hata hivyo, ambayo inasaidia kuelezea kwanini Mwanasheria Mkuu wa Marekani wakati huo Eric Holder alitaka sana kukataa alipokuwa afisini mauaji yaliyofanywa na ndege zisizo na rubani huko Pakistan na Yemen - nchi ambazo hazina vita - zilikuwa " mauaji ".

Washington hata inadai kwamba haikukusudia kumuua Osama Bin Laden huko Abbottabad. Haki ya kisheria ya "mauaji yaliyokusudiwa" imetolewa kwa kuzidisha sababu za kufanya hivyo kwa msingi wa kujilinda. Sasa inachukuliwa kumaanisha kujikinga na shambulio linaloweza kutekelezwa , na kwa utata zaidi, kulenga kikundi chochote ambacho kinapanga shambulio, hata ikiwa haujui ni lini shambulio hilo linaweza kutekelezwa.

Hofu ambayo imetolewa na wengi kuhusu mauaji au kuwalenga watu Fulani kwa mauaji ni mjadala utakaokuwepo kwa muda hasa iwapo patazidi kutokea sababu za kutaka kuhalalisha hatua kama hizo .

Iwapo Marekani inaweza kuwaua raia wake kihalali huko Yemen ,Mbona Urusi isanye hivyo London? Wengi wanajiuliza iwapo tayari imefanya hivyo wakitaja mfano wa kupewa sumu kwa Alexander Litvinenko.

chanzo. Leseni ya kuua: Serikali zinapoamua kufanya mauaji - BBC News Swahili
 
Back
Top Bottom