Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Msishangilie sana huyo siyo Khumbu.

FB_IMG_1614545061794.jpg
 
Inaendelea

Maisha ya kujitahidi kumtoa Khumbu kichwani yaliendelea. Haikuwa jambo rahisi ila kwa kiasi flani nilifanikiwa maana nilianza kujiona mtu mpya. Nilianza kufurahia maisha na huyu mwanamke wangu wa Bloemfontein huku nikiendelea kuwasiliana na Amina pamoja na huyu wa Sinza. Huyu wa Bloemfontein tulianza kupanga mipango mingi tu ya kimaisha. Alikuwa anaishi township moja inaitwa Tabanju. Tulianza mtindo wa kila siku ya Ijumaa nikitoka kazini tunaenda kukaa kwao mpaka Jumapili jioni ndio tunarudi town nyumbani kwangu. Siku za weekend nilikuwa siendi kazini hivyo weekend nzima tulikuwa tunashinda kwao.

Kama mnakumbuka nimesema huko nyuma kuwa niliajiriwa huku nikiwa bado sijagraduate. Niliendelea kufanya kazi huku mara kwa mara naenda Durban kwa ajili ya tests na assignments zingine. Hatimae nilifanya mtihani wa mwisho wa lile somo moja lililobaki, na 06 September 2012 ilikuwa graduation yangu.

Siku ya graduation nilienda Durban kwa ajili ya hiyo shughuli. Nilipata wazo la kumjulisha Khumbu aje kwenye hii siku muhimu kwangu lakini nilipofikiria kuwa rafiki yangu Sandile na Pontsho wasingenielewa kama ningemwalika huyu mwanamke hilo wazo niliamua kuachana nalo japo nilitamani Khumbu awepo. Sandile na Pontsho nilikuwa nimewajulisha siku ya graduation na waliomba gharama za sherehe ziwe juu yao. Gharama za Joho na suti waliniambia wala nisihofu. Sandile alinipa zawadi ya shati moja zuri sana.

Nilifika Durban siku moja kabla ya graduation. Kesho yake asubuhi nikakutana na Sandile campus ili anipatie joho na suti niweze kutinga kabla ya shughuli ya graduation haijaanza. Nikapiga hiyo suti na kutupia joho kwa juu. Kati ya siku muhimu katika maisha yangu ni hiyo siku nilipovaa hilo joho. Niliona hiyo ilikuwa ishara ya milango ya mafanikio kuanza kufunguka. Nilihisi ndoto yangu ya muda mrefu imetimia. Bongo niliishia form three, niliona kama naota kumaliza elimu ya chuo tena kwenye nchi kama South Africa, niliinua mikono juu na kusema “Asante Mungu”.

Mimi na Sandile tukaanza kuelekea kwenye ukumbi wa graduation nikiwa nimejawa furaha kuu. Nikiwa nawaza sasa nimeingia kwenye ulimwengu wa opportunities. Tukiwa tunaelekea ukumbini tukakutana na rafiki yangu mwingine akiwa na demu wake nao wamekuja kwenye graduation yangu. Kwa kweli nilijiona kama mfalme. Kuzungukwa na watu wanaokupenda na wanaofurahia mafanikio yako ni hisia nzuri sana.

Mgeni rasmi alikuwa mtu maarufu sana kwa South Africa ambaye nisingependa nimtaje. Alitoa speech moja nzuri sana iliyotufanya magraduate wote tuone anything is possible, you can be anything you want. Hapo nikawa napiga picha jinsi maisha yangu yatakavyobadirika, nikawa nafikiria kuwa na mwanamke mrembo, nyumba nzuri ya kuishi kwenye suburb, maisha ya kutoka kila weekend na kwenda kula bata nikiwa na mke wangu mrembo ambaye atanielewa na kufurahia maisha kama tupo peponi. Nikawa najiona naingia boardroom nikiwa kama CEO wa kampuni kubwa, nimepiga suti naendesha mkutano nikiwa nimezungukwa na wafanyakazi.

Ulipigwa wimbo wa taifa wa South Africa, baada ya wimbo ndio shughuli za graduation zikaanza. Mgeni rasmi alikuwa anataja jina la graduate na kwenda mbele kushikana mkono, kupiga picha na kukabidhiwa cheti. Jina la graduate likitajwa ndugu zake wanashangilia na kupiga vigelegele akiwa anaenda kupokea cheti. Hatimae jina langu likatajwa, yalisikika makelele hayo hata sikujua yametoka wapi. Nilitaka kuangalia ni wakina nani hao wanaonishangilia maana nilijua kuna watu wanne tu ndio wamekuja kunipa company ambao ni Sandile, Pontsho, rafiki yangu na demu wake. Ule ukumbi umejengwa kama uwanja wa mpira. Juu wanakaa wageni waalikwa hivyo graduate mnakuwa mmekaa chini, kwa hiyo ukitaka kuwaona wageni waalikwa inabidi utazame juu. Niliposikia yale makelele ya kunishangilia niliona noma kuanza kuangalia juu ilihali naelekea kwa mgeni rasmi kwenda kuchukua cheti na kupiga picha. Nilitamani sana kugeuza shingo niangalie ni watu gani hao wanaonishangilia ila haikuwa rahisi hivyo niliendelea kubaki na shauku yangu mpaka pale shughuli itakapoisha maana watu walikuwa wamejaa hasa, ukumbi ulikuwa umefurika. Huko parking magari yalikuwa yamejaa hadi sehemu ya kupaki ikawa haitoshi. Magari mengine yakawa yamepaki hadi barabarani. Nakumbuka tulipotoka tuliikuta gari moja iliyokuwa imepakiwa barabarani imedondokewa na mti, kioo chote cha mbele kimemwagika na mti umeenda kujikita kwenye siti za mbele. Huyo mweye gari nadhani alilaani sana siku hiyo.

Baada ya hotuba ya mgeni rasmi na shughuli ya graduation kuisha nikawa natoka nje kwenda kukutana na hao wageni wangu waalikwa kwa ajili ya kile walichoniandalia. To my surprise nikamkuta Khumbu yupo pamoja na akina Sandile. Ile kutoka tu nje ghafla namuona Khumbu akinikimbilia na kuja kunivalisha shada la maua. Sikutegemee kumuona Khumbu siku hiyo, na niliamini hajui kama leo ni siku ya graduation yangu na hajui kama nipo Durban. Hapo hapo nikaanza kutokwa na machozi. Sijui yalikuwa ni machozi ya furaha au machozi ya hisia za mapenzi, sielewi. Kulikuwa na watu kama sita hivi. Alikuwa ameongezeka Khumbu na mke wa Sandile. Basi kila mtu ananipa hongera huku Sandile akawa ananipiga picha kwa camera yake ile ya kazi.

Baada ya zoezi la kukumbatiana na kupongezana tukawa tunaelekea parking kwa ajili ya kuondoka na kwenda kupata chakula cha pamoja nilichoandaliwa. Niliingia kwenye gari ya Sandile, Khumbu na wengine wakatumia magari yao. Tulienda mgahawa mmoja unaitwa Nandos, haukuwa mbali sana na pale chuoni. Njia nzima nilikuwa najiuliuza Khumbu kafikaje hapa, nani kamwambia leo ni graduation yangu?

Itaendelea
P1 sana Mkuu
 
Back
Top Bottom