Jinsi Mamlaka ya Maji Dodoma (DUWASA) wanavyohujumu juhudi za serikali za kuzuia kuenea kwa Corona jijini Dodoma

Li Hong

New Member
May 27, 2020
1
0
Serikali katika juhudi za kupambana na Corona ilitoa maelekezo kwamba watu wawe wananawa mikono na kutumia sanitizers. Hili suala la kunawa Mikono ndio njia rahisi na yenye matokeo chanya. Kwa mantiki hiyo, wizara ya maji ni wizara muhimu sana katika kuzuia kuenea kwa maambukizi ya Corona, na hivyo haikupaswa kabisa kuruhusu kukatika kwa maji hovyohovyo bila mpangilio wala taarifa.

Kama ni lazima kukata maji kwasababu za kiufundi, ilipaswa wizara husika kupitia vitengo vyake vya mamlaka ya maji watoe taarifa mapema ili watu watunze maji ya kutumia. Lakini cha kushangaza mamlaka ya maji Dodoma (DUWASA) wamekuwa na tabia ya kukata maji bila kutoa taarifa, hasa tangu corona ilipoanza, kwa sababu ambazo hazieleweki na haziwekwi wazi, hususan maeneo ya Nzuguni Dodoma. Sasa hii inatafsirika kama hujuma kwa serikali na Watanzania, kuendelea kusababisha uenezaji wa corona hapa Dodoma na bila hata mamlaka husika na za juu yake kuona kuwa hilo ni tatizo.

Sasa watu wanajiuliza, hivi mamlaka za serikali Dodoma, kuanzia mkurugenzi, mkuu wa wilaya, wizara, wanashindwaje kuliona hili na kulichukulia hatua?

Tatizo hili limedum kwa zaidi ya miezi 3 sasa ambapo maji yanakuwa yanakatikaki rejareja, ghafla, bila taarifa yoyote.hii imesababisha watu kushindwa kunawa mikono ipasavyo ili kuzuia korona na pengine kwa sehemu kubwa imesababisha kuenea kwa maambukizi ya vkorona hapa Dodoma kwa wagonjwa waliothibitishwa.

Serikali inashindwaje kuchukua hatua?
 
Back
Top Bottom