Jinsi makanjanja ya magazeti/tv/redio yanavowapa raha Wanayanga

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Jun 12, 2021
1,061
2,475
Amini usiamini hiki ni kile kipindi ambacho makanjanja ya redio/tv na magazeti huwa yanawawapa raha za kufa mtu wana jangwani, raha huongezeka pia pale MITAMBO YA MAGOLI inaposhuka airport na kupokelewa kwa mbwembwe na misafara ya magari hadi mitaa ya twiga na jangwani

Kuna hali ya furaha sana baada ya makanjanja kadhaaa kudai Yussuph manji amevunja mkataba wa konde boy toka simba unaoisha 2024 na hiyo ni baada ya hapo siku za nyuma yanga kufanikiwa "kuwavuta jangwani wachezaji kama ,manula,chama,mkude,kapombe,zimbwe"

Kipindi hiki ama kwa hakika mwana yanga yoyote anatakiwa akitumie vizuri kwani ifikapo september kunakuwa na transition kidogo ni kipindi cha lawama,kuwaita wachezaji maduka,kufukuza makocha na kumtupia lawama Wallace karia kwa kusababisha MITAMBO YA MAGOLI ishindwe kufunga

Ikumbukwe pia TFF na Wallace karia watakuwa responsible kwa team hiyo ya yanga kufanya vibaya katika round ya awali michezo ya Caf mwezi wa 9 mwaka huu



hatariii.PNG
 
Huyo Fiston hakabiki kirahisi😀
jamaa ni hatari sana naskikia Gomes amemtaka sema thamani yake ni kubwa sana simba hawezi kuimudu, unakumbuka wakati yikpe anakuja makanjanja yaliandika "makipa watayarishe gloves za chuma"kwamba mashuti ya mdogo wake drogba ni hatari
 
Mbumbumbu wanaumiaaaa
inauma sana kaka jinsi utopolo wanabyovunja benki za watu pale simba na kuwang'oa chama,manula,kapombe,zimbwe,luis ni hatari sana
inauma zaidi pale mitambo ya magoli inapofanyiw ahujuma na karia na tff ishindwe kufunga magoli
 
Back
Top Bottom