Jinsi maamuzi mabovu yalivyoifilisi benki ndani ya saa 48, wateja waliomba kutoa dola bilioni 42 kwa siku moja(Mara mbili ya bajeti ya Tanzania)

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Silicon Valley Bank inayosifika kuwa muhimu kwa kampuni za kiteknolojia hasa zinazoanza na kukua imedondokea pua na kuwa benki ya pili kubwa nchini Marekani kudondoka tangu kumaliza kwa mdororo wa uchumi wa mwaka 2008.

Mdororo wa 2008 ulianzia nchini Marekani baada ya mabenki mengi kuporomoka kutokana na kuporomoka soko la nyumba ambazo sehemu kubwa zilitokana na mikopo ya mabenki iliyopelekea sheria kali kutungwa kudhibiti sekta ya fedha Marekani. Anguko hili linahisiwa kutengeneza sheria nyingine.

Nini kimetokea
Mwaka 2022 benki ilianza kupata hasara baada ya ukuaji wa 250% miaka mitatu nyuma. Sekta ya teknolojia ilipungua kasi ilhali sehemu kubwa ya madeni ya benki hiyo yalikuwa kwenye sekta hiyo ya teknolojia.

Menejiment ya Bank ikaamua kuuza hati fungani zenye thamani ya dola bilioni 21 kwa hasara ya dola bilioni 1.8 na kuibua maswali kuhusu uwezo wake na ufanisi wake. Labda walilenga kuwahakikishia wawekezaji kwamba wana mtaji imara lakini hali hiyo ilipokelewa tofauti.

Watu na makampuni wakaanza kutoa fedha zao kwenye benki na ndani ya saa 48 benki ikapata upungufu wa mtaji kuweza kujiendesha kulingana na sheria za Marekani. Ijumaa asubuhi wateja walitoa maombi ya kutoa dola bilioni 42(Zingatia bajeti ya Tanzania ya 22/23 ni dola bilioni 18) na benki ikashindwa kukidhi maombi hayo.

Punde wathibiti wa Califonia walifika kwenye benki hiyo na kuifunga huku ikiwekwa chini ya uangalizi wa FDIC ikimaanisha benki hiyo iko mbioni kufilisiwa ili kuwalipa wateja wake.

=====

UPDATES - March 13

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WATEJA PESA ZIKO SALAMA

Serikali ya Marekani imesema wateja wa Benki iliyofungwa ya Silicon Valley wataweza kuzifikia pesa zao zote kuanzia leo Jumatatu, ikisisitiza haitatumia pesa za walipa kodi kuinusuru kama ilivyokuwa mdororo wa 2008. Serikali imesema inachukua maamuzi ya haraka na yenye ufanisi kulinda uchumi wa Marekani kwa kuongeza uaminifu wa umma kwenye mfumo wa kibenki.

Mfumo wa kibenki wa Marekani unabaki imara kwenye msingi imara sehemu kubwa kwasababu ya mageuzi makubwa baada ya mdororo wa kiuchumi wa 2008 ambapo taratibu zilianzishwa kulinda sekta ya mabenki.

Masaa machache kabla ya taarifa hiyo, waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen alisema hawatafanya 'bailout' kwa benki hiyo. Baada ya kuanguka kwa Lehman Brothers mwaka 2008 wadhibiti waliyataka mabenki kuwa na mtaji wa ziada kukabiliana na matatizo pindi yakitokea.
 
Hizi mada watanzania wengi hawataki kuzielewa na kujifunza na kila mtu analalamima eti maisha ni magumu
Mimi huwa sielewi ile Economic Depression ya 2008 ilitokea vipi nilisoma tu kuwa inahusiana na mortgage loans kuwa nyingi ila mpaka kuleta ugumu wa maisha mechanism sikuielewa.
Little explanation on that nitashukuru.
Concerning bad loans given by banks my mind is empty on that.
 
Afadhali umeuliza hili, maana kati ya economic crisis huwa siielewi ni hii ya 2007/2008.
 
Mimi huwa sielewi ile Economic Depression ya 2008 ilitokea vipi nilisoma tu kuwa inahusiana na mortgage loans kuwa nyingi ila mpaka kuleta ugumu wa maisha mechanism sikuielewa.
Little explanation on that nitashukuru.
Concerning bad loans given by banks my mind is empty on that.
Benki zilikua zinatoa mikopo ya nyumba kwa masharti nafuu kiasi hata wasio na sifa wakapata,kuurudisha ikawa shughuli,benki zikapoteza uwezo wa kifedha,zikahitaji kupigwa jeki,waliokopeshwa nyumba wakaporwa na kuwa homeless baada ya kushindwa kulipa,lakini wenye mabenki makubwa hawakupata hasara walivuta mpunga, serikali ndiyo iliyoliwa
 
Benki kubwa hazikupata hasara kivipi? Zilivuta mpunga kutoka wapi?
 
Benki zilikua zinatoa mikopo ya nyumba kwa masharti nafuu kiasi hata wasio na sifa wakapata,kuurudisha ikawa shughuli,benki zikapoteza uwezo wa kifedha,zikahitaji kupigwa jeki,waliokopeshwa nyumba wakaporwa na kuwa homeless baada ya kushindwa kulipa,lakini wenye mabenki makubwa hawakupata hasara walivuta mpunga, serikali ndiyo iliyoliwa
Ahaa yaani ile ukishindwa kulipa mkopo wa nyumba wahuni wanachukua nyumba kulipia mkopo in the long run homelessness everywhere. Mkuu ebu elezea ile USD 200 billion ya rais Bush ilinufaishaje mabenki makubwa mpaka useme serikali ilipigwa. Pia elezea kuhusu Troubled Asset Reformation Plan(TARP).
 
Mimi huwa sielewi ile Economic Depression ya 2008 ilitokea vipi nilisoma tu kuwa inahusiana na mortgage loans kuwa nyingi ila mpaka kuleta ugumu wa maisha mechanism sikuielewa.
Little explanation on that nitashukuru.
Concerning bad loans given by banks my mind is empty on that.
Benki zilikuwa zinatoa mikopo ya nyumba kwa masharti nafuu kiasi hata wasio na sifa wakapata, kuurudisha ikawa shughuli, benki zikapoteza uwezo wa kifedha, zikahitaji kupigwa jeki, waliokopeshwa nyumba wakaporwa na kuwa homeless baada
 
Ahaa yaani ile ukishindwa kulipa mkopo wa nyumba wahuni wanachukua nyumba kulipia mkopo in the long run homelessness everywhere. Mkuu ebu elezea ile USD 200 billion ya rais Bush ilinufaishaje mabenki makubwa mpaka useme serikali ilipigwa. Pia elezea kuhusu Troubled Asset Reformation Plan(TARP).
Siwezi kwenda deep, Ila niliiona documentary aljazeera ndiyo nikapata picha, walifungwa dagaa, mapapa yakabaki yakafungua biashara mpya, itafute hiyo documentary
 
Tok
nki kubwa hazikupata hasara kivipi? Zilivuta mpunga kutoka wapi?
Toka serikalini,Kuna jina walikua wakiita ule msaada wa kifedha
 
Benki zilikua zinatoa mikopo ya nyumba kwa masharti nafuu kiasi hata wasio na sifa wakapata,kuurudisha ikawa shughuli,benki zikapoteza uwezo wa kifedha,zikahitaji kupigwa jeki,waliokopeshwa nyumba wakaporwa na kuwa homeless baada ya kushindwa kulipa,lakini wenye mabenki makubwa hawakupata hasara walivuta mpunga, serikali ndiyo iliyoliwa
Tafsiri ya inside job, kwa nini bank kubwa hazikuathirika?
Movies kama vile LA big shot, inside job zinajaribu kuelezea kwa hint kilichotokea
 
Hizi mada watanzania wengi hawataki kuzielewa na kujifunza na kila mtu analalamima eti maisha ni magumu
Hapo ukilaumu watz unatuonea hivi mada ni zito sana kwetu. Hatujui mambo hayo

Sisi tuambie diamond amepata demu mpya nasi tutajadili in/out
Au
Uteuzi umefanyika kwa mtu tunamjua basi tutamchambua.
 
Ngoma ilianzia kwa Lehman brothers, ikasambaa USA Kisha worldwide
Lehman ilikua inamilikiwa na wayahudi.
Conspiracy theories zinaanzia huko kua ile 2008 economic crisis was planned
 
Ngoma ilianzia kwa Lehman brothers, ikasambaa USA Kisha worldwide
Lehman ilikua inamilikiwa na wayahudi.
Conspiracy theories zinaanzia huko kua ile 2008 economic crisis was planned
Hebu wekeni hizo documentary links hapa au ka kuna kitabu muweke hapa tukasome wenyewe. Tukiwaomba mfafanue vizuri mnakuja na stori mnatuacha kwa suspense.
 
Mimi huwa sielewi ile Economic Depression ya 2008 ilitokea vipi nilisoma tu kuwa inahusiana na mortgage loans kuwa nyingi ila mpaka kuleta ugumu wa maisha mechanism sikuielewa.
Little explanation on that nitashukuru.
Concerning bad loans given by banks my mind is empty on that.

Tatizo lilianzia mwaka 2003, Rais wa wakati huo, George Bush alisain 'American dream' iliyojumuisha ndoto ya kila Mmarekani awe na nyumba. Masharti yalilegezwa na watu wengi walikopesheka, nyumba nyingi zikajengwa(Biashara ya makazi ililipa sana watu wakawekeza zaidi) na watu kununua kwa mkopo.

Mwaka 2007/08 watu wengi wakashindwa kuendelea kulipa hii mikopo kwa sababu ilitolewa kwa sera kuliko kupima uwezo wao wa kulipa. Kwa kawaida ukishindwa kulipa benki hurudi sokoni na kuuza ili kufidia deni. Wafilisi wakaenda sokoni kwa pamoja, nyumba zikawa nyingi sana sokoni na kawaida vitu vikizidi kuliko uhitaji huwa vinashuka bei, Marekani ikashuhudia anguko kali la bei kwenye sekta ya nyumba na bado zikawa haziuziki kwa urahisi.

Hii ikaleta 'panic' na soko la nyumba likafeli rasmi, kumbuka mzunguko mkubwa wa pesa umeshikiliwa na sekta ya makazi. Mabenki na 'hedge funds' vikaathirika pakubwa. Mwaka 2008 Lehman brothers akadondoka ikiwa ni anguko kubwa zaidi kwenye sekta ya fedha Marekani.

Nchi zilizoendelea mabenki ni muhimu sana kwenye uchumi, kuyumba kwao kukapelekea sekta nyingi kukwama. Watu wakaacha kufanya manunuzi wakilinda walichonacho na wengine wakashindwa kukopa ili kufanya manunuzi. Uzalishaji ukapungua na ajira zikapotea. Mzunguko wa mchakato huu ukapelekea mdororo wa uchumi ukiwa mkubwa zaidi baada ya mdororo uliosababishwa na vita kuu ya pili ya dunia.

Imani yangu umepata mwanga kilichotokea.
 
Back
Top Bottom