Jinsi Lowassa alivyojichomeka sherehe za RC Ifakara na kumchefua kardinali Pengo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Lowassa alivyojichomeka sherehe za RC Ifakara na kumchefua kardinali Pengo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Apr 1, 2012.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Gazeti la kiongozi linalomilikiwa na kanisa katoliki leo limeeleza kinaga ubaga jinsi lowasaa alivyojialika kwenye sherehe za kumsimika Askofu libena wa jimbo jipya la ifakara.

  Akitoa maelezo mhashamu askofu mkuu Pengo alisema, kiprotokali alikaribishwa mkuu wa mkoa wa morogoro ili amkaribishe mzee mwinyi kutoa neno la shukrani, lakini kwa mshangao mkubwa wakashangaa kumwona anamwalika kwanza lowasa kutoa hotuba ambayo haikutarajiwa kwani lowasa hakualikwa na kuwa alihudhuria kama muumini mwingine.

  Kanisa katoliki limeeleza kufedheshwa na kitendo hicho cha RC bendera kupachika akina Lowassa kwenye shughuli zake bila utaratibu huo kuwekwa na kanisa.gazeti hilo kwenye ukurasa wa pili limeendelea kuandika kuwa "RC achafua sherehe za kanisa Morogoro".

  Wakati huo huo kardinali ameshauri wanahabari kuwa macho na habari wanazoziita kuwa ni matamko ya kanisa katoliki. Ili tamko liwe limetolewa na kanisa ni lazima litolewe na rais wa baraza la maaskofu ambaye atakuwa tayari ameshauriwa na au kukubaliana na TEC. Amekanusha matamshi kama vile kikwete ni chaguo la mungu liliwahi kutolewa na mojawapo ya maaskofu hayakuwa matamko ya kanisa bali ya askofu binafsi labda kwa ukaribu wake na kikwete.

  ======
   
 2. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  EL anaaibisha!!
  RC huyo amelikoroga,lakini pongez ziende kwa RC kwa kuamua kumuumbua huyu fisad El.
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mbona waandishi waliokuwa huko hawajaandika habari? Mbona kwenye TV zetu hawakuonyesha hayo? Au ndio yale matatizo aliyosema JK juzi? Kama ni kweli, hii ni aibu na kashfa kwa vyombo vyetu vya habari maana walikuwapo waandishi makini huko. Na hata hii Kiongozi ni kwa kuwa ni gazeti la kanisa na wameona wajisafishe na mafisadi, kwa kuwa watu sasa wanasema kanisa Katoliki linachukia mafisadi lakini linapenda fedha zao, kumbe sivyo bali ni kuingiliwa kama alivyofanya RC Bendera.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona hapo kuna mchanganyiko tena? Makala inasema ili liwe tamko la kanisa lazima litolewe na rais wa baraza, kwa maana nyingine ni kwamba hayo ya kusema kwamba EL alijipenyeza basi si tamko la Kanisa bali Tamko la Muadhama Polycarp Kafdinali Pengo binafsi kwa.kuwa Pengo si Rais wa Baraza.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Fisadi anataka kuwa Rais
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kanisa liache ubabaishaji. Taarifa za lowasa kualikwa zilitolewa siku nyingi kabla na kweli ikawa hivyo!
   
 7. N

  Ndole JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu RC naye sijui anataka kujipendekeza.......Hivi kanisa halijakoma kuwaalika wanasiasa kwenye shughuli zao? hawajakoma baada ya ****** kuwaambia ni wauzaji wa unga?
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna taarifa kwamba ratiba ya EL kualikwa makanisani imejaa hadi Septemba.
   
 9. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Tutashuhudia mengi kabla ya 2015. Wanasiasa wanaona njia bora ya kukubalika ni kujipenyeza kwenye makanisa na misikiti. Mwaka 2015 hatutadanganyika hata waseme mwana ccm yoyote ni chaguo la Mungu
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Acheni uongo nyie viunbe wa Mungu mbona tabia zenu zinakuwa za kikwere; Lowassa atahudhuriaje sherehe hizo kama muumini mwingine wakati yeye sio mkatoliki?
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lowassa ni chaguo la Mungu.
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mgosi Bendela amesoma alama za nyakati, hataki kupata aibu kama Mashishanga alivyomkataa Kikwete then Jamaa akawa Rais!:eek:
   
 13. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kiongozi linamilikiwa chini ya TEC
   
 14. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Mkanganyiko upo wapi mkuu? Pengo amesema Luwasa alijialika. Hakuna mahali ilipoandikwa Kanisa limesema Luwasa alijialika. Sasa wewe ulitaka iweje?
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  Mimi ni Mkatoliki, kutokana na heshima kwa dhehebu langu sio busara kuujadili humu usafi wa Kanisa Katoliki ila kutaka kumtenga EL kwa kisingizio si msafi hakina mashiko. Kwani Masiya alikuja kwa ajili ya waliopotea na wasio wakamilifu. Nimebahatika kufika mpaka Rome na kuishuhudia lile dungu la dhahabu pale juu kwenye ule mduara, si wengi wanajua hìlo dungu lilitoka wapi na lilipatikanaje mpaka kufika hapo!. Sio wengi wanawajua the realy funders wa Vatican!. EL anauchafu gani wa kuwa despised na Kanisa Katoliki!. Tatizo la kanisa letu, the right men ni kwao ni Wakatoliki tuu kama alivyokuwa Julius, akaja Beninyamini na sasa wanampigia chapuo Berinado au Wilibodi!. Kwa vile EL ni Mlutheri, huyo kwao sio!.
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Basi kama haya ni ya kweli maujania yake yatakuwa yamekwisha kabisa. hongera Pengo
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kanisa katoliki na hasa Pengo wajifunze kutokana na hii blunder. Hiyo shughuli ilikuwa ya kanisa na sio ya mkuu wa mkoa. Kwanini wasi-take control ya shughuli yao badala yake kumwachia mwanasiasa? (Mkuu wa mkoa na harufu nzito ya siasa).

  Kanisa lingeweza kuandaa list ya watoa salamu, na kumuita mtu mmoja mmoja kama walivyopanga atoe salamu. Hakuna ulazima wa kupanga 'matofali' ili kumuita mtu, kwa maneno mengine hakukuwa na ulazima wa kanisa kumuita mkuu wa mkoa ili huyo mkuu wa mkoa amkaribishe Mwinyi!!! Hizi ni protocol za kisiasa, kanisa liko huru kufuata protocol zake kwenye shughuli yao.

  Kwa kifupi sikubaliani na maelezo ya Pengo, Kanisa katoliki lina intelligensia ya hali ya juu, wangetaka kujua Lowassa anafuata nini Ifakara wangejua, lakini either hawakufanya au walifanya na kuweka mambo kabatini. Na Lowassa hajanzaa kuongea kwenye shughuli za kanisa katoliki leo, alikuwa Mwanza,hivyo Ifakara ni mwendelezo tu.

  Pengo akubali kanisa limeingia doa, and it is up to him kama kiongozi wa kanisa nchini Tanzania kutafuta 'jiki' vinginevyo waumini wengi wamefadhaika na huu mchezo wa harambee. Kanisa limeegemea mno hela! Jukumu la kuhubiri Injili linafifia. Na hii inatokea under Pengo's watch!
   
 18. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Pasco kama kawaida yako unamtetea sana EL.
   
 19. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Naona jina hapo chini Luwasa anafuatilia thread hii
   
 20. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Hivi lowassa hakomi tu??
   
Loading...