Jinsi kugeuza celing fan kuwa wind generator -inawezekana?

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,409
9,183
Hivi majuzi ceiling fan limekorofisha ,out of curiosity nimelifungua kwa lengo la kujua tatizo. Nilibaini coil zimeungua kabisa(jumla ya coil 28 ie miviringo miwili kila mviringo coil 14). Kwa sababu Uwezo wa kulikarabati mdogo nimenunua jengine. Swali langu ambalo nalielekeza hasa to electrical technicians/engineers ni hili- je upo uwezekano wa kuconvert 14 pole ceiling motor to alternator kwa madhumuni ya kuzalisha umeme wa upepo?
 
Inawezekana mkuu!!

Watu wengi hatufahamu kuwa ALTONATORS Ndio pekee zinaweza kufua umeme hata tanesco wana hiyo sema i think ni kubwa kiasi kwamba inafua umeme wa mkubwa.

Altonators haziwezi kujizungusha zenyewe kufua umeme,lazima kuwe na External Power kama Maji ya mtera, Upepo Au Joto mvuke pressure etc.
Na huwa zinaukubwa tofauti wa kuzalisha umeme.

So kuhusu Fan kuzalisha umeme ukiunganisha na hicho kifaa, unaweza pata umeme ila Challenge ni Je! utatumia External power gani? kuzungusha hio fan?

kama utalitegesha hewani upate upepo then itawezekana.
kama ulimaanisha utumie Fan linalozungushwa na umeme wa tanesco ndio lizungushe hiyo altonator duh! itawezekana pia ila ni sawa na kutumia Nyundo kuua Mende yaani utapoteza nguvu nyingi kuzalisha nguvu kidogo.

hapo vipi?!
 
Back
Top Bottom