Jinsi kikundi cha watekaji cha wasiojulikana kinavyoweza kuja kuwa na nguvu kuliko JWTz tukizembea

concordile 101

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
6,823
Reaction score
15,190
Katika miaka ya karibuni, baadhi ya matukio ya utekaji na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu yamehusishwa na kile kinachoitwa kikundi cha wasiojulikana nchini Tanzania. Ingawa taarifa zao ni za kusikika tu bila ushahidi wa wazi, mjadala kuhusu uwezekano wa kikundi hiki uongezeka na tishio la kitaifa limeanza kujitokeza. Ili kuelewa athari za uwepo huu, ni muhimu kulinganisha hali hiyo na historia ya ukuaji wa Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, kikundi ambacho kilianza kama jeshi dogo la kujitegemea na baadaye kuja kuwa nguvu kubwa iliyotikisa nchi nzima ya Sudan

Kwanza, RSF ya Sudan ilikuwa kutokana na mazingira ya udhaifu wa serikali, vita vya muda mrefu, na ukosefu wa taasisi imara za usalama. Serikali ya Sudan ilianza kuitumia RSF kama kikosi cha dharura kupambana na waasi Darfur kwa dizaini ya wasiojulikana kwa tanzania.

Hatua hii iliwapa uwezo wa kupata silaha, uhuru wa kufanya operesheni bila kuhojiwa, na baadaye uwezo wa kujitengenezea fedha kupitia biashara za dhahabu na mianya ya rushwa. Kwa miaka michache tu, kikundi kilichokuwa na jukumu dogo kiligeuka na kuwa nguvu ya kijeshi iliyoishinda hata jeshi la taifa la sudan. Hali hii ilitokana na mchanganyiko wa uzembe wa serikali, ufadhili wa serikali na kutodhibitiwa.

Kwa upande wa Tanzania, mazingira ni tofauti lakini bado yanatupa funzo muhimu. Ikiwa kikundi cha watu wasiojulikana kitakuwa kikifanya vitendo vya utekaji, vitisho au uvunjifu wa haki bila kuchukuliwa hatua madhubuti, kinaweza kuanza kupata nguvu taratibu. Hatari ya kwanza ni kupoteza hofu ya sheria. Kikundi chochote kinapojua hakitachunguzwa wala kuchukuliwa hatua, kinaweza kuongeza ukubwa wa operesheni zake. Pili, ikiwa kitapata rasilimali, fedha au uungwaji mkono kutoka kwa watu wenye maslahi binafsi, kinaweza kujijengea mtandao unaodumu.

Tofauti kubwa kati ya Tanzania na Sudan ni kwamba Tanzania ina jeshi imara, taasisi za sheria zinazofanya kazi, na historia ya utulivu kuliko nchi nyingi za Afrika Mashariki. Hivyo, uwezekano wa kikundi chochote kukua na kufikia kiwango cha RSF ni mdogo. Hata hivyo, historia ya Sudan inatoa funzo muhimu: vikundi visipoangaliwa mapema, vinaweza kukua kimya kimya mpaka vinapokuwa vigumu kudhibitika. Hata kama Tanzania ina mifumo bora, uzembe mdogo au kuruhusu mianya ya uhalifu unaweza kutengeneza tatizo la muda mrefu.

Kwa jumla, inafaa serikali na vyombo vya usalama kuchukulia kwa umakini uwepo au tetesi za vikundi visivyojulikana. Historia ya RSF inaonyesha wazi kwamba juhudi zisizo rasmi, kukosa uwazi, na kutowajibika kwa watu wenye mamlaka vinaweza kuleta athari kwa kizazi kizima. Tanzania ina nafasi nzuri ya kuzuia hali kama hiyo mapema kupitia uchunguzi, uthibiti wa silaha, usimamizi wa intelijensia, na kuwapo kwa uwajibikaji bila upendeleo.

Ombi letu kwa JW msikimbilie kulinda katiba tu ni wajibu wenu pia kuhakikisha hata hawa watu wanaoteka watu mnawadhobiti .
 
Uchambuzi wako ungelieleweka zaidi kama usingeliingiza uchawa ndani yake.

Taifa lenye jeshi imara ni lipi hilo? Hili ambalo linaruhusu raia wake wanagongwa risasi mchana wa jua kali kama digidigi wa porini na lenyewe linatoa mimacho ndiyo jeshi imara unalolizungumzia ?

Mifumo imara ya kisheria ni hii ya Mtu mmoja kuweza kufanya Uhaini huku akiwa hana hata wembe achiliambali jiwe la relini 🤣🤣 seriously?

Utawala wakisheria ni huu unaosikiliza Bi_chura anasema nini na siyo sheria zinatakaje ?

Mfumo imara wakisheria ni huu unaoruhusu kila siku watu wawe wanatekwa kama kuku ,wanapelekwa kulisikojulikana na siku watakapofikishwa mahakamani majaji wanamsikiliza mwanasiasa akitakachoamua juu ya aina ya kesi na aina ya hukumu aitakayo kwa aliyowaleta.

Muhimu chakushika nikwamba tulipo siyo salama na tayari hivyo vikosi vishakuwa na nguvu zaidi ya majeshi yote tuliyonayo.
 
Sio Kila mtu anayefikiria tofauti nawe ni chawa
 
Hadi sasa RSFTZ ina nguvu kuliko chombo chochote. Hao wengine wamebaki kupiga kelele kama raia wema na kuvujisha taarifa tu mara Dulla ndio mkuu wa kitengo, wanajeshi wametoka uganda n.k. huku wakiwa hawana nguvu ya kunyoosha hata kidole.
 
TANZANIA HATUNA JESHI TUNA KIKUNDI CHA GREEN GUARD YA CCM (UVCCM).HUWEZI UKAAGIZA JESH TOKA NJE UGANDA NA KMKM WANAUA WATU KM KUKU WA KIDERI ALAFU JESHI LETU MNAANGALIA TU
 
  • Thanks
Reactions: vnn
TANZANIA HATUNA JESHI TUNA KIKUNDI CHA GREEN GUARD YA CCM (UVCCM).HUWEZI UKAAGIZA JESH TOKA NJE UGANDA NA KMKM WANAUA WATU KM KUKU WA KIDERI ALAFU JESHI LETU MNAANGALIA TU
Hapa ndipo nilipo onankumbe tanzania hatuna jeshi
 
Katika miaka ya karibuni, baadhi ya matukio ya utekaji na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu yamehusishwa na kile kinachoitwa kikundi cha wasiojulikana nchini Tanzania. Ingawa taarifa zao ni za kusikika tu bila ushahidi wa wazi, mjadala kuhusu uwezekano wa kikundi hiki uongezeka na tishio la kitaifa limeanza kujitokeza. Ili kuelewa athari za uwepo huu, ni muhimu kulinganisha hali hiyo na historia ya ukuaji wa Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, kikundi ambacho kilianza kama jeshi dogo la kujitegemea na baadaye kuja kuwa nguvu kubwa iliyotikisa nchi nzima ya Sudan

Kwanza, RSF ya Sudan ilikua kutokana na mazingira ya udhaifu wa serikali, vita vya muda mrefu, na ukosefu wa taasisi imara za usalama. Serikali ya Sudan ilianza kuitumia RSF kama kikosi cha dharura kupambana na waasi Darfur kwa dizaini ya wasiojulikana kwa tanzania.
Hatua hii iliwapa uwezo wa kupata silaha, uhuru wa kufanya operesheni bila kuhojiwa, na baadaye uwezo wa kujitengenezea fedha kupitia biashara za dhahabu na mianya ya rushwa. Kwa miaka michache tu, kikundi kilichokuwa na jukumu dogo kiligeuka na kuwa nguvu ya kijeshi iliyoishinda hata jeshi la taifa la sudan. Hali hii ilitokana na mchanganyiko wa uzembe wa serikali, ufadhili wa serikali na kutodhibitiwa.

Kwa upande wa Tanzania, mazingira ni tofauti lakini bado yanatupa funzo muhimu. Ikiwa kikundi cha watu wasiojulikana kitakuwa kikifanya vitendo vya utekaji, vitisho au uvunjifu wa haki bila kuchukuliwa hatua madhubuti, kinaweza kuanza kupata nguvu taratibu. Hatari ya kwanza ni kupoteza hofu ya sheria. Kikundi chochote kinapojua hakitachunguzwa wala kuchukuliwa hatua, kinaweza kuongeza ukubwa wa operesheni zake. Pili, ikiwa kitapata rasilimali, fedha au uungwaji mkono kutoka kwa watu wenye maslahi binafsi, kinaweza kujijengea mtandao unaodumu.

Tofauti kubwa kati ya Tanzania na Sudan ni kwamba Tanzania ina jeshi imara, taasisi za sheria zinazofanya kazi, na historia ya utulivu kuliko nchi nyingi za Afrika Mashariki. Hivyo, uwezekano wa kikundi chochote kukua na kufikia kiwango cha RSF ni mdogo. Hata hivyo, historia ya Sudan inatoa funzo muhimu: vikundi visipoangaliwa mapema, vinaweza kukua kimya kimya mpaka vinapokuwa vigumu kudhibitika. Hata kama Tanzania ina mifumo bora, uzembe mdogo au kuruhusu mianya ya uhalifu unaweza kutengeneza tatizo la muda mrefu.

Kwa jumla, inafaa serikali na vyombo vya usalama kuchukulia kwa umakini uwepo au tetesi za vikundi visivyojulikana. Historia ya RSF inaonyesha wazi kwamba juhudi zisizo rasmi, kukosa uwazi, na kutowajibika kwa watu wenye mamlaka vinaweza kuleta athari kwa kizazi kizima. Tanzania ina nafasi nzuri ya kuzuia hali kama hiyo mapema kupitia uchunguzi, uthibiti wa silaha, usimamizi wa intelijensia, na kuwapo kwa uwajibikaji bila upendeleo.
Omni letu kwa jw msikimbilie kulinda katiba tu ni wajibu wenu pia kuhakikisha hata hawa watu wanaoteka watu mnawadhobiti .
Sasa hapo sielewi wanailinda vip hiyo katiba Na hiyo katiba inamlinda nani na kwa maslahi ya nani
 
Nchi yetu ina katiba ya hovyo sana. Katiba inayompa mtu mmoja mamlaka ya kufanya apendacho. Hii katiba tukiendelea kuikumbatia, nchi yetu itasambaratika mapema sana.
 
Na wanao ikumbatia ni wale ambao inawafurahisha
 
Hapo uliposema serikali ume_maanisha serikali gani hii hii iliyokiunda hicho kikundi ama?
 
Namaanisha serikali hii, kwa sasa wanaweza kuona kikundi kinawasaidia kwa sababu ya ukandamizaji na kutimiza matakwa yao , ila huko mbeleni kikundi kinaweza pata vyanzo vya mapato na watu wengine wenye tamaa zaidi kikaja kikawa tishio hata kwao na familia zao.
Mfano halisi ni huo wa Sudan , Leo hii jeshi la sudan halina ubavu wa kupigana na rsf kwa sababu ya kukosa mapato na vifaa vya kukabiliana
 
Katika miaka ya karibuni, baadhi ya matukio ya utekaji na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu yamehusishwa na kile kinachoitwa kikundi cha wasiojulikana nchini Tanzania. Ingawa taarifa zao ni za kusikika tu bila ushahidi wa wazi, mjadala kuhusu uwezekano wa kikundi hiki uongezeka na tishio la kitaifa limeanza kujitokeza. Ili kuelewa athari za uwepo huu, ni muhimu kulinganisha hali hiyo na historia ya ukuaji wa Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, kikundi ambacho kilianza kama jeshi dogo la kujitegemea na baadaye kuja kuwa nguvu kubwa iliyotikisa nchi nzima ya Sudan

Kwanza, RSF ya Sudan ilikuwa kutokana na mazingira ya udhaifu wa serikali, vita vya muda mrefu, na ukosefu wa taasisi imara za usalama. Serikali ya Sudan ilianza kuitumia RSF kama kikosi cha dharura kupambana na waasi Darfur kwa dizaini ya wasiojulikana kwa tanzania.

Hatua hii iliwapa uwezo wa kupata silaha, uhuru wa kufanya operesheni bila kuhojiwa, na baadaye uwezo wa kujitengenezea fedha kupitia biashara za dhahabu na mianya ya rushwa. Kwa miaka michache tu, kikundi kilichokuwa na jukumu dogo kiligeuka na kuwa nguvu ya kijeshi iliyoishinda hata jeshi la taifa la sudan. Hali hii ilitokana na mchanganyiko wa uzembe wa serikali, ufadhili wa serikali na kutodhibitiwa.

Kwa upande wa Tanzania, mazingira ni tofauti lakini bado yanatupa funzo muhimu. Ikiwa kikundi cha watu wasiojulikana kitakuwa kikifanya vitendo vya utekaji, vitisho au uvunjifu wa haki bila kuchukuliwa hatua madhubuti, kinaweza kuanza kupata nguvu taratibu. Hatari ya kwanza ni kupoteza hofu ya sheria. Kikundi chochote kinapojua hakitachunguzwa wala kuchukuliwa hatua, kinaweza kuongeza ukubwa wa operesheni zake. Pili, ikiwa kitapata rasilimali, fedha au uungwaji mkono kutoka kwa watu wenye maslahi binafsi, kinaweza kujijengea mtandao unaodumu.

Tofauti kubwa kati ya Tanzania na Sudan ni kwamba Tanzania ina jeshi imara, taasisi za sheria zinazofanya kazi, na historia ya utulivu kuliko nchi nyingi za Afrika Mashariki. Hivyo, uwezekano wa kikundi chochote kukua na kufikia kiwango cha RSF ni mdogo. Hata hivyo, historia ya Sudan inatoa funzo muhimu: vikundi visipoangaliwa mapema, vinaweza kukua kimya kimya mpaka vinapokuwa vigumu kudhibitika. Hata kama Tanzania ina mifumo bora, uzembe mdogo au kuruhusu mianya ya uhalifu unaweza kutengeneza tatizo la muda mrefu.

Kwa jumla, inafaa serikali na vyombo vya usalama kuchukulia kwa umakini uwepo au tetesi za vikundi visivyojulikana. Historia ya RSF inaonyesha wazi kwamba juhudi zisizo rasmi, kukosa uwazi, na kutowajibika kwa watu wenye mamlaka vinaweza kuleta athari kwa kizazi kizima. Tanzania ina nafasi nzuri ya kuzuia hali kama hiyo mapema kupitia uchunguzi, uthibiti wa silaha, usimamizi wa intelijensia, na kuwapo kwa uwajibikaji bila upendeleo.

Ombi letu kwa JW msikimbilie kulinda katiba tu ni wajibu wenu pia kuhakikisha hata hawa watu wanaoteka watu mnawadhobiti .
Tatizo lenu hamfuatilii. Ile sheria ya usalama wa taifa iliyopelekwa bungeni moja ya kifungu ilitoa ruhusa kwa TISS kuwa na vitengo vya siri ambavyo vinapewa mamlaka kufanya hayo matukio. Hii miswaada huwa inaandikwa kwa lugha ngumu ya kisheria ambayo wabunge wa aina ya baba levo hatawakiachiwa kusoma kifungu wiki nzima hawawezi kuelewa kilichoandikwa, ndio maana watu wa aina ya Tundu Lissu watawala hawawataki bungeni. Kuna mazingira JWTZ hawawezi kufanya chochote kwa sababu hivyo vikundi vya watu wasiojulikana vinafanya huo uhuni kisheria
 
TANZANIA HATUNA JESHI TUNA KIKUNDI CHA GREEN GUARD YA CCM (UVCCM).HUWEZI UKAAGIZA JESH TOKA NJE UGANDA NA KMKM WANAUA WATU KM KUKU WA KIDERI ALAFU JESHI LETU MNAANGALIA TU
Kuna police militarization imefanyika Tanzania. Polisi wamepewa mafunzo na dhana za kivita kama wanajeshi. Wanasiasa wamelipa nguvu zaidi polisi ili kujilinda endapo jeshi likihasi.

Uliona mwenyewe maandamano ya juzi polisi waliingia mtaani kudhibiti raia na silaha za kivita, hata ukamataji wa siku hizi raia anafuatwa na silaha nzito ni tofauti na zamani wakati polisi wanatumia uniform za kaki

Yale mauaji yaliyokua yanafanywa na polisi endapo jeshi lingeingilia ingekua vita kali sana baina ya jeshi na polisi. Usifikiri jeshi lingewadhibiti polisi kirahisi rahisi tu, and obviously jeshi kingeshindwa tu hiyo vita kwa sababu silaha za polisi zilikua loaded wakati za wanajeshi hazikua na risasi zile. Mafwele sio mjinga kujitamba amekamata wanajeshi, anaongea yale kwa sababu anajua kwa sasa wanajeshi hawana nguvu kuzidi polisi
 
Back
Top Bottom