Jinsi kesi ya Lema ilivyoibua Mapinduzi ya kisheria

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Arusha. Kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, inaendelea, lakini inaweza kuwa imejenga misingi ya utoaji haki kwa vyombo vya Serikali, mawakili na mahakama.

Lema alipata dhamana Ijumaa baada ya kukaa mahabusu kwa siku 121 kutokana na sarakasi za kisheria baada ya ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kuweka pingamizi dhidi ya dhamana yake alipofikishwa kortini kwa mara ya kwanza.

Akitoa dhamana hiyo, Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kaskazini alisema uamuzi wa Mahakama ya hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha kumpa dhamana Lema, Novemba 11 mwaka jana ulikuwa sahihi na hakukuwa na sababu za kupinga.

Alisema DPP angekuwa na haki ya kupinga dhamana iwapo mshtakiwa asingetimiza masharti ya dhamana na si vinginevyo.

Jaji huyo alizielekeza mahakama za chini kusimamia mamlaka yake bila kuyaachia na kuzitaka ziheshimu misingi ya sheria.

Alikuwa akirejea kitendo cha Hakimu Mkazi wa Arusha kuacha kuendelea na masharti ya dhamana aliyompa Lema baada ya mawakili wa Serikali kumtaarifu kwa mdomo kuwa wana nia ya kukata rufaa kupinga dhamana hiyo.

Tangu wakati huo, dhamana ya Lema ilikuwa ikitegemea sarakasi hizo za kisheria zilizotinga hadi Mahakama ya Rufaa ambayo katika uamuzi wake iliweka bayana kuwepo kwa sintofahamu.

Lakini Februari 28 wakati wa kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la dhamana lililowekwa na Serikali, Jaji Bernard Luanda, ambaye aliongoza jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, alionyesha kushangaa jinsi ofisi ya DPP ilivyoshughulikia suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuondoa rufaa siku ya uamuzi,

Jaji Luanda alisema tabia ya wanasheria wa DPP inanajisi taaluma na hivyo kuitaka ifanye kazi kwa njia ambayo haitaonea wananchi.

Pia majaji hao walitupa mapingamizi mawili yaliyokuwa yamewasilishwa na ofisi ya DPP.

Kauli ya Jaji Maghimbi na ya majaji hao ni kama zimejenga msingi wa utoaji haki kwa vyombo hivyo.

“Ofisi ya DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilipaswa kuwa ni watetezi wa haki, lakini zimebadilika na sasa zinatumika kukandamiza watu wakose haki zao,” alisema mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche.

“Leo mbunge amekaa miezi minne gerezani kwa kosa ambalo lina dhamana. Tujiulize ni Watanzania wangapi wanasota magereza kutokana na DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushindwa kusimamia sheria?”

Alisema Serikali inatumia fedha nyingi kugharamia vyakula vya wafungwa, lakini uchunguzi wa kina ukifanyika itabainika wengi wapo jela kutokana na ofisi hizo mbili kutotimiza wajibu wao.

Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Hamis Mkindi alisema kosa la kutoa lugha ya uchochezi lina dhamana, lakini kilichokuwa kinafanyika ni ukiukwaji wa sheria.

Mkindi alisema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi dhamana ni haki ya mtuhumiwa, lakini haki hiyo ilikuwa inachelewa kutokana na DPP kutumia vibaya mamlaka yake.

Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala alisema tangu kuanza kwa shauri hilo walikuwa wanatetea haki na hadhi ya mahakama ambayo alidai iliporwa na DPP.

Kibatala, ambaye pia ni mmoja wa mawakili wa Lema, alisema wanashukuru kwa uamuzi wa Jaji Maghimbi kutoa dhamana.

“Jaji aliweka wazi kwenye uamuzi wake, mahakama za chini zinatakiwa kuheshimiwa na pia kuzuia DPP kuweka mapingamizi yanayokiuka haki,” alisema.

Mara baada ya Lema kutoka nje kwa dhamana, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema:

“Mhe Lema, karibu sana uraiani. Aliyeshinikiza unyimwe dhamana alidhani anakukomoa, kumbe anazidi kukuimarisha. Hongera sana Kamanda.”

Msanii wa filamu nchini aliyejiunga na Chadema hivi karibuni, Wema Sepetu naye aliandika katika ukurasa wa Instgram akimpongeza Lema na kwenda Arusha kumtembelea.

“Kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe. Mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke,” aliandika msanii huyo.

Ofisa mmoja wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema ofisi hiyo haipaswi kunyooshewa kidole cha lawama kwa sababu mahakama ilikuwa na uwezo wa kuingilia mapema na kutoa uamuzi inayoona unafaa.

“Hawakuwa na sababu ya kukaa kimya siku zote na kuja kutoa lawama hivi sasa,” alisema ofisa huyo.
 
Ofisi ya DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilipaswa kuwa ni watetezi wa haki, lakini zimebadilika na sasa zinatumika kukandamiza watu wakose haki zao,” alisema mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche.

“Leo mbunge amekaa miezi minne gerezani kwa kosa ambalo lina dhamana. Tujiulize ni Watanzania wangapi wanasota magereza kutokana na DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushindwa kusimamia sheria?”
 
Kwa hili Lema ni shujaa......
Sijajua wahusika ambao walikuwa wanajisi sheria wamepata faida gani Lema kukaa mahabusu zaidi ya miezi ya minne.
Mhe Lema, karibu sana uraiani. Aliyeshinikiza unyimwe dhamana alidhani anakukomoa, kumbe anazidi kukuimarisha.
 
Waliopata faida ni watanzania.....kwani kesi yoyote yenye dhamana hayawezi kufanyika yale yaliyofanyika kwa Lema.
 
Ni kweli imeleta mapinduzi (precendence) lakini kwan nini High court ilishindwa kuingilia mapema (suo moto) kurekebisha (revision) dosari hiyo mapema??

Kwa ruling ya mahakama kuu, kwmb Mhe. Lema aliwekwa kizuizini kunyume cha sheria, (section 148 (5) CPA ) Kinachoweka wazi dhamana yak, Kwa abuse of law na DPP Je mhe. anaweza kumfungulia DPP kesi ya madai ya kumweka kizuidhini bila sababu za msingi (false imprisonment?)
 
Kwanza maDc na maRC waondolewe kuwa W/viti wa Kamati za mahakama Wilaya na Mikoa.

Pili mchakato wa kumpata Jaji mkuu ubadilishwe japo tuwaige wenzetu wa nchi jirani ya Kenya,

Tatu, CJ huru akishapatikana yeye ndie apandishe vyeo na teuzi mbali mbali za mahakimu na majaji. Rejea tishio la kutoteua jaji kutoka TLS iwapo (?????).

Kaimu CJ nacho ni mjadala mzito unaojitegemea.
 
Siku hili ulilolisema likiwezekana tutajenga viwanda vya kuonekana na si vya maneno.
 
hongera lema kuwa maabusu siyo kukushusha dhamana yako bali ni kukomoza ushujaa wako na dhamana yako. wapo watz ambao waliteseka kama wewe na bado wanapigania kupata mdhamana kama wwe . ukirudi bungeni mwezi wa nne kapiganie hilo....tuko pamoja na tutaendelea kuwa pamoja kulijenga jiji la arusha... karibu rais wa arusha
 
Arusha. Kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, inaendelea, lakini inaweza kuwa imejenga misingi ya utoaji haki kwa vyombo vya Serikali, mawakili na mahakama.

Lema alipata dhamana Ijumaa baada ya kukaa mahabusu kwa siku 121 kutokana na sarakasi za kisheria baada ya ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kuweka pingamizi dhidi ya dhamana yake alipofikishwa kortini kwa mara ya kwanza.

Akitoa dhamana hiyo, Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kaskazini alisema uamuzi wa Mahakama ya hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha kumpa dhamana Lema, Novemba 11 mwaka jana ulikuwa sahihi na hakukuwa na sababu za kupinga.

Alisema DPP angekuwa na haki ya kupinga dhamana iwapo mshtakiwa asingetimiza masharti ya dhamana na si vinginevyo.

Jaji huyo alizielekeza mahakama za chini kusimamia mamlaka yake bila kuyaachia na kuzitaka ziheshimu misingi ya sheria.

Alikuwa akirejea kitendo cha Hakimu Mkazi wa Arusha kuacha kuendelea na masharti ya dhamana aliyompa Lema baada ya mawakili wa Serikali kumtaarifu kwa mdomo kuwa wana nia ya kukata rufaa kupinga dhamana hiyo.

Tangu wakati huo, dhamana ya Lema ilikuwa ikitegemea sarakasi hizo za kisheria zilizotinga hadi Mahakama ya Rufaa ambayo katika uamuzi wake iliweka bayana kuwepo kwa sintofahamu.

Lakini Februari 28 wakati wa kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la dhamana lililowekwa na Serikali, Jaji Bernard Luanda, ambaye aliongoza jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, alionyesha kushangaa jinsi ofisi ya DPP ilivyoshughulikia suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuondoa rufaa siku ya uamuzi,

Jaji Luanda alisema tabia ya wanasheria wa DPP inanajisi taaluma na hivyo kuitaka ifanye kazi kwa njia ambayo haitaonea wananchi.

Pia majaji hao walitupa mapingamizi mawili yaliyokuwa yamewasilishwa na ofisi ya DPP.

Kauli ya Jaji Maghimbi na ya majaji hao ni kama zimejenga msingi wa utoaji haki kwa vyombo hivyo.

“Ofisi ya DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilipaswa kuwa ni watetezi wa haki, lakini zimebadilika na sasa zinatumika kukandamiza watu wakose haki zao,” alisema mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche.

“Leo mbunge amekaa miezi minne gerezani kwa kosa ambalo lina dhamana. Tujiulize ni Watanzania wangapi wanasota magereza kutokana na DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushindwa kusimamia sheria?”

Alisema Serikali inatumia fedha nyingi kugharamia vyakula vya wafungwa, lakini uchunguzi wa kina ukifanyika itabainika wengi wapo jela kutokana na ofisi hizo mbili kutotimiza wajibu wao.

Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Hamis Mkindi alisema kosa la kutoa lugha ya uchochezi lina dhamana, lakini kilichokuwa kinafanyika ni ukiukwaji wa sheria.

Mkindi alisema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi dhamana ni haki ya mtuhumiwa, lakini haki hiyo ilikuwa inachelewa kutokana na DPP kutumia vibaya mamlaka yake.

Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala alisema tangu kuanza kwa shauri hilo walikuwa wanatetea haki na hadhi ya mahakama ambayo alidai iliporwa na DPP.

Kibatala, ambaye pia ni mmoja wa mawakili wa Lema, alisema wanashukuru kwa uamuzi wa Jaji Maghimbi kutoa dhamana.

“Jaji aliweka wazi kwenye uamuzi wake, mahakama za chini zinatakiwa kuheshimiwa na pia kuzuia DPP kuweka mapingamizi yanayokiuka haki,” alisema.

Mara baada ya Lema kutoka nje kwa dhamana, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema:

“Mhe Lema, karibu sana uraiani. Aliyeshinikiza unyimwe dhamana alidhani anakukomoa, kumbe anazidi kukuimarisha. Hongera sana Kamanda.”

Msanii wa filamu nchini aliyejiunga na Chadema hivi karibuni, Wema Sepetu naye aliandika katika ukurasa wa Instgram akimpongeza Lema na kwenda Arusha kumtembelea.

“Kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe. Mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke,” aliandika msanii huyo.

Ofisa mmoja wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema ofisi hiyo haipaswi kunyooshewa kidole cha lawama kwa sababu mahakama ilikuwa na uwezo wa kuingilia mapema na kutoa uamuzi inayoona unafaa.

“Hawakuwa na sababu ya kukaa kimya siku zote na kuja kutoa lawama hivi sasa,” alisema ofisa huyo.
Hivi mi nauliza kwa Mahakama kutomtendea haki mtuhumiwa ambaye anastahili dhamana . . . JE HAKUNA JINSI YA WANASHERIA KUFUNGUA MASHTAKA JUU YA MAHAKAMA ISHTAKIWE AU IRUDISHE FIDIA KWA KUMWONEA MTEJA WAO ambayo ni haki yake kisheria mtuhumiwa kuipata kutokana na kosa lake kuruhusu kupewa Dhamana. . ? ?
 
SHERIA KUU KULIKO ZOTE INASEMA YOU ARE INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY. MAANA YAKE KILA MSHITAKIWA NI HURU HADI AHUKUMIWE. WATETEZI WA HAKI MSAIDIENU SCORPION AACHIWE. NA MBOWE. NA MAMA WA MENO YA NDOVU. WANANYIMWA HAKI YAO KIKATIBA.
 
Umeandika vizuri, ila umekosea kuja kumuweka wema sepetu kwenye maelezo yako...

Hafai kukaa line moja na intellectuals....
 
Back
Top Bottom