Jinsi Katiba Mpya itakavyorahisisha kuitoa CCM Madarakani

Last KING Ontuzu

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
587
783
Nawasalimu kwa jina la Muungano wa Tanzania.kitu
Ninachoona kinaendelea nchini kwa sasa ni harakati za wapinzani Kutaka KATIBA mpya,ni harakati za kupaza sauti kufanya makongamano ya katiba na makongamano kufanyika nchi nzima.

Tumeona leo mwenyekiti wa CDM jijini Mwanza amekamatwa na polisi ambao walizunguka Hotel ambayo walitaka kufanyia kongamano la katiba mpya.

Mchakato huo sio mpya na tayari uliwahi kugharimu mabioni ya pesa miaka 6 nyuma.

Swali la kujiuliza ni kwanini serikali inaona hatari sana kuruhusu mchakato huo kukamilika?Nini kipo nyuma ya pazia?

Je chama tawala kinachounda serikali kinafaidikaje na katiba iliyopo mpaka kupata kigugumizi kuruhusu mchakato huo.

Kwa haraharaka naona huenda kweli mchakato wa katiba mpya unaweza kuitoa madarakani CCM .

Kama ndio ukweli je, ni kwa mambo gani hasa yanayoweza kusaidia kuitoa ccm madarakani kupitia mchakato wa katiba mpya ? Au ni uoga tuu wa SSH na dawati lake la kiufundi?
Kwenu wachambuzi.
 
Moja kati ya mambo yatakayofelisha katiba mpya ni kuiegemeza kwenye siasa,kwamba katiba mpya itasaidia kuindoa CCM madarakani ili chama kingine kishike madaraka,hapo kupata katiba mpya patachimbika.
 
Acheni mambo ya kitoto, watanzania hawataki katiba mpya kwa ajili ya siasa! Tunahitaji katiba mpya kwa ajili dira mpya ya nchi yetu!

Hata kama CCM ikikaaa madarakani miaka mia, hilo siyo tatizo kwa Watanzania na ndo maana wanaendelea kuichagua kila uchaguzi unapokuja!

Tunahitaji katiba mpya itakayoleta usawa na haki kwa watanzania wote!
 
Moja kati ya mambo yatakayofelisha katiba mpya ni kuiegemeza kwenye siasa,kwamba katiba mpya itasaidia kuindoa CCM madarakani ili chama kingine kishike madaraka,hapo kupata katiba mpya patachimbika.
Chadema,CCM au wananchi ama nani anafelisha suala hilo kwa kulihusisha na siasa?
 
Back
Top Bottom