Jinsi kampuni ya Sauli Luxury Bus ilivyofanikiwa katika biashara ya usafirishaji

1. Usichokijua kuhusu sauli ni kuwa saul hakuanza na gari mbili alianza na gari 3, benzi moja na scninia mbili..

2. Huyo jamaa an hela chafu anaweza shusha hata gari 10 izo Scania isipokuwa anakwepa kukutana na kesi ya utakatishaji. Kwa gari izo izo tatu alizonunua alipewa kesi ya utakatishaji fedha, kakaa ndani zaid ya miezi 8 mpka rais alivyosema watakatishaji fedha watoke kwa kulipa fidia ndo alitoka.
Umetuchanganyia habari Mkuu ishu aliyokaa ndani inahusu madini waliyomuuzia mteja wa nje ya nchi hapa tupo kwenye magari hilo swala tuliache maana kwenye hiyo kesi yupo mshkaji mmoja wa Arusha nafamiana nae alikuwepo...
 
Kampuni inamiaka miwili unasifia ni sawa usifie ndoa yako kua umetimiza miaka miwili,wakti hiyo biashara inachangamoto sana pia kuondoa basi likiwa na abiria 10 ni jambo la kawaida.
Yani unaenda bila faida ili ratiba ya gari isiharibike
Jinsi sauli alivyosasa haitotokea atoke na abiria 10 labda aanze kubweteka,ile gari iwe masika au kiangazi zinazotoka dar zipo full,zinazotoka mbeya zipo full.Na sasa hivi anatoa gari mbili mbili kwa pamoja na zote zipo full
 
Dar mbeya sauli ni 44,000/=.na tiketi zinaisha mapema .gari zingine zote nauli ni elfu arobain hadi thelathini na tano....pia kilichomsaidia sauli ni kuwapata madereva wazuri yule mwinuka na mwanyilu
 
Umetuchanganyia habari Mkuu ishu aliyokaa ndani inahusu madini waliyomuuzia mteja wa nje ya nchi hapa tupo kwenye magari hilo swala tuliache maana kwenye hiyo kesi yupo mshkaji mmoja wa Arusha nafamiana nae alikuwepo...
Asante kwa kusahihisha ndugu maana waTanzania kwa kuzusha hawajambo ndugu....
 

Sauli ni kampuni ya bus za kusafirisha abiria kutoka Mbeya kuja Dar na Dar kwenda Mbeya, kampuni hii ina takriban miaka miwili toka ianze kazi rasmi katika ardhi ya Tanzania.

Katika miaka miwili hiyo kumekuwepo na changamoto mbalimbali lakini kikubwa ni haijawahi kupata ajali.

Mmiliki wa hii kampuni anaweza kua ni mfano mzuri wa kuigwa kwani ameweza kutonesha wengi biashara ni kitu ambacho huanzia mbali sana.

Miaka zaidi ya saba nyuma njia ya Nyanda juu Kusini Dar - Iringa - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga na Songea kampuni kutoka China ya NEW FORCE na GOLDEN DEER walifanya mapinduzi makubwa sana kwa kuweza kuteka masoko haya na kua na abiria wa uhakika.

Mwaka 2018 SAULI ilianza kazi rasmi kukiwa na bus mbili tu moja inaanzia Dar kwenda Mbeya na nyingine inaanzia Mbeya kurudi Dar na kwa nauli ya 44,000 ambayo mpinzani wake wa karibu New Force na Golden Deer kwa nauli hii ya 44,000 aliweza kwenda Dar mpaka Tunduma.

Mwanzo hua mgumu sana lakini Sauli alikuja na itikadi zake za kufanya abiria wachague gari lake waache kupanda ya mpinzani

Kwanza aliweza kujali muda kitu ambacho kilifanya apendwe sana na kuanza kua na jina ingali ana gari mbili tu

Alitumia mbinu ya SCANIA pamoja na BENZ ni gari za luxury na bora kuliko gari za michina kitu ambacho pia ni kweli hivo pia iliweza khmuongezea credit ya biashara yake

Kampuni hii ya SAULI iliweza kupata jina na umaarufu katika kipindi kichache sana hivo kupelekea kuongeza bus zingine mbili aina na kufanya kua na total fleet ya bus 4 ambazo tatu ni Scania Gemilang na moja ni Mercedes Benz

Mzee huyu mwenye kampuni ameweza kutufundisha kuamini kwa kile tunachoona kinafaa kutokubali kuyumbishwa na kumuangalia mpinzani wako kwa jicho la karibu ili kujua wapi pa kumuovertake katika biashara

Niljua SAULI S.H Amon kumbe Sauli wa Madini? Watu wanaofanya Biashara ya Madini kaa nao MBALI Sana.
 
Back
Top Bottom