Jinsi Kampuni ya PAP ilivyoichukua IPTL bure na kujichotea Dola za Marekani 128M kutoka BoT

Kesi ya tanesco na iptl kuhusu ni kiasi gani cha malipo ya capacity charge na bei ya kuuziwa umeme imekwishatolewa maamuzi?

1. IPTL na TANESCO hawana kesi.
2. ESCROW ni malipo ya huduma iliyokuwa tayari TANESCO wamehudumiwa na IPTL kwa kuuziwa umeme na pesa kutunzwa kwenye akaunti hiyo ili kupisha mgogoro wa umiliki kati ya VIP na MECHMAR.
 
Nyie watu hebu acheni mambo ya kingese,yaani hamuwezi ku-comment mpaka m-quote the all thread?

Baada ya post kubandikwa kuwa kuna tetesi kwamba pesa za escrow zimetumika kumtibu mama yake zitto india na yeye kuomba milioni mia tano,mamluki wamekuja na mbinu mpya ya ku~quote post nzima ili kuifanya iwe more boring
 
Hili sakata linaendeshwa kisiasa ...... hadi sasa linapotoshwa mno ....... kuna wanasiasa wanataka kucheza na akili zetu .....kwa taarifa zao sisi si wajinga ........wakati utaongea ..........
 
Pinda apita njia ya Lowassa

- Alitetea Richmond, Pinda IPTL
- Kafulila aapa Bunge lijalo hapatoshi
06/10/2014 | Na Josephat Isango

KATIBU Mwenezi wa Chama cha NCCR Mageuzi, na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema Bunge lijalo hapatatosha kati ya yeye na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama ripoti ya ufisadi Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), haitaletwa bungeni.

Alisema ripoti ya IPTL huenda ikamfanya Waziri Pinda akapitia njia iliyomng’oa madarakani mtangulizi wake, Edward Lowassa aliyekuwa akiitetea Richmond.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za NCCR Mageuzi jijini Dar es Salaam jana, Mbunge huyo alisema kuwa nchi imetafunwa sana lakini serikali haichukui hatua na sasa imetosha.

Mbunge huyo machachari wa NCCR Mageuzi, alisema kumekuwa na kampeni ya kupotosha ukweli kuhusu ufisadi huo na kampeni hiyo inaratibiwa na baadhi ya watu waliojitoa ufahamu kutetea wizi huo.

Alisisitiza kuwa fedha zilizotolewa kwenye Akaunti ya Escrow, Dola za Kimarekani 270 milioni (zaidi ya sh 400 bilioni), zilitolewa kifisadi na ndio sababu kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mkakati wa kuzuia ripoti za uchunguzi zisijadiliwe katika Bunge lijalo.

Alitoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa ripoti hiyo inaletwa, vinginevyo atapeleka hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais mwenyewe, baada ya kushauriana na wanasheria wake, kwani anao ushahidi wa kutosha kuonesha namna Katibu Mkuu Kiongozi na vigogo wengine wa Ikulu wanavyohusika.

Aliwataka wahusika wa IPTL/PAP na Singasinga Sethi waache kupotosha watanzania kuwa wasijadili masuala ya biashara ndani ya IPTL (Merchmar, Piperlink na PAP), kwani maazimio hayo yana utata wenye maslahi ya taifa, kwani yanaambatana na kodi kwa mujibu wa Sheria ya fedha ya 2012.

Kafulila, alimlaumu Sethi kuwa hakununua IPTL bali alitumia pesa za Escrow alizopora kwa baraka za Waziri Mkuu Pinda, Waziri wa Nishati Prof. Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wa Nishati Eliakim Maswi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema, Gavana wa Benki Kuu Beno Ndulu, Mkurugenzi Tanesco Felchesmi Mramba ili kufanya asilimia 90 ya malipo ya ununuzi wa IPTL.

Tanzania Daima limeona moja ya barua ya Rugemalila aliyekuwa mmiliki wa VIP iliyopokelewa BoT Desemba 6, 2013 akikumbusha barua ya Novemba 28, 2013 akisisitiza kuwa Sethi sio mwaminifu na alikuwa hajamlipa fedha kufikia Desemba 5, 2013 wakati amekwishachukua hela za Escrow kuanzia Novemba 28, 2013 hadi Desemba 5, 2013.

Hii maana yake Sethi alitumia fedha za Escrow ambazo ni za umma kulipa dola 67.5 milioni kwa ajili ya kununua IPTL, kiasi ambacho ni karibu asilimia 90 ya malipo yote ya manunuzi hayo.

Amewataka watanzania wafahamu kwamba, pamoja na fedha hizo kuwa nyingi lakini uamuzi wake haukuwahi kujadiliwa wala kutolewa taarifa kwenye baraza la mawaziri kabla ya kutolewa, ingawa fedha hizo zimo kwenye vitabu vya hesabu za serikali (rejea taarifa ya hesabu za Tanesco ya 2011).

Aliongeza kwamba, wafahamu kwamba nchi wahisani mpaka sasa hazijachangia bajeti kusubiri utekelezaji wa ripoti za PCCB na CAG kuhusu ufisadi huo.

Kafulila, amewataka watanzania washirikiane kuikabili serikali iwajibike kwani uwajibikaji katika nchi upo hoi, ndio maana inasikitisha kwani hata leseni ya Ikulu inatumika kufanya ujangili na Waziri wa Maliasili yupo kimya na Ikulu ipo kimya.

Alisema Benki ya FBME imekuwa ikituhumiwa kufanya biashara haramu miaka sita, lakini Gavana wa BoT yupo ofisini, huku bodi ya BoT ikibaki bila kuvunjwa kwa ajili ya uwajibikaji.

Suala la pesa za Escrow limekuwa likigubikwa na utata tangu lilipoanza kuripotiwa bunge lililopita na Bunge lilituhumiwa kutumia njama mbalimbali ili kutaka kusiundwe kamati teule kuchunguza ufisadi huo mkubwa kuliko mwingine uliowahi kutokea nchini.

Baada ya kuripotiwa suala hilo, IPTL ilimfungulia Kafulila kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania ikitaka ailipe sh bilioni 310 kama fidia ya kuwachafulia jina.
Pia kampuni hiyo iliwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikitaka itoe zuio la muda kwa Kafulila asiendelee kuikashifu hadi shauri la msingi litakaposikilizwa.

Licha ya IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solution (T) Limited (PAP) na Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Harbinder Singh Seth kuwasilisha maombi ya kumfunga mdomo Kafulila, siku chache David Kafulila alijitokeza na kusema suala hilo linashughulikiwa na CAG na Takukuru kwa azimio la Bunge, hivyo haliwezi kujadiliwa mahakamani.

Katika mkutano wa jana, Kafulila aliitupia lawama ofisi ya CAG kwani iliomba siku 45 kumaliza uchunguzi wa sakata hilo lakini hadi sasa kuna siku zaidi ya 180, huku CAG akistaafu na kuliacha bila kutoa ripoti.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Pro Muhongo na Katibu Mkuu wake, Maswi, wamekuwa wakisisitiza kwamba fedha hizo zilitolewa kwa kuzingatia hukumu ya Mahakama Kuu ya Septemba 5, 2013 chini ya Jaji Utamwa.

Hukumu hiyo ya Jaji John Utamwa, ndiyo inapingwa na Kafulila na wadau wengine kuwa imetafsiriwa visivyo, kwani hakuna popote alipotaja Akaunti ya Escrow, ingawa katika muhtasari wa kikao kati ya Tanesco, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za akaunti hiyo zipewe Kampuni ya PAP (inayomilikiwa kwa asilimia 50 na Harbinder Singh na 50 Simba Trust iliyosajiliwa Australia).

Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusu gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa Tanesco.

Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari 2014, ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.

Kwa uamuzi huo, ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya Escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.
 
Acha upumbavu wako wewe. Kama huna la maana la kuandika kaa kimya.

IPTL/PAP ni kampuni makini isiyokuwa na
chembe ya kifisadi na imefika hapo baada ya kupita
hatua zote za kisheria, ikiwemo kununua hisa za VIP na
Mechmar.
IPTL/PAP wanazidi kuwaomba watanzania, wawaamini na
kuendelea kuwaamini kwa kuwa hakuna vitendo vya
ufisadi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mshauri wa Biashara wa Kimataifa wa Kujitegemeawa wa VIP, James Rugemarila ambaye pia ni Mkurugenzi wa IPTL, alisema kuwa mgogoro huo ulidumu kwa muda mrefu na kuwagharimu fedha nyingi.

Aliongeza kuwa mgogoro huo ulikuwa na tafsiri mbalimbali na kwa kuwa ulikuwa mahakamani walishindwa kutoa taarifa kwa jamii kuhofia kuingilia uhuru wa mahakama.

Rugemarila alisema kwa kuwa umeisha wameamua kuweka kila kitu wazi ili jamii ielewe na taarifa hizi zitatangazwa kwenye magazeti ya Jambo Leo, The African, Daily
News, Guardian, blogus, Channel Ten, ITV nk.

Akizungumzia zaidi kuhusu Kampuni ya Pan Africa Power Sulutions Tanzani LMT, iliyonunua hisa za VIP kwenye IPTL na kupewa kibali na VIP kuhalalisha ununuzi wa shea za Mechmar katika IPTL, alisema itawakomboa wananchi kwa kupata nishati hiyo kwa bei nafuu.

Aliongeza kuwa katika muda mfupi baada ya kampuni hiyo kuanza kazi itazalisha megawati 500 kwa bei kati ya uscents 6 na uscent 8 kwa kila unit ukilinganisha na bei za sasa zinazotozwa na makampuni ya kuzalisha umeme zilizo kati ya uscent 33 na 55 uscen kwa unit moja.

“Hii ni kampuni ya Kitanzania, ambayo ni bahati mbaya tu huyu Mkurugenzi wa PAP, Dr. Harbinder Singh Sethi amefiwa na jamaa yake ndiyo maana hayupo tutamleta mtamuona atakuja Jumatatu mtawasiliana naye, inaonesha Watanzania tunaweza,” alisema Rugemarila
 
"Makubalianohayo yalitoa haki na wajibu wa kila upande, na BOT ilihusika kuzitunza fedhahizo na kuhakikisha kwamba hazitumiki nje ya madhumuni ya kuhifadhiwa kwake,kuwekeza katika miradi inayoruhusiwa na kuziwasilisha kwa mmiliki aliyekubalikapale matakwa ya kifungu 7.7 cha makubaliano hayo yanapotekelezwa," alisema.

Alisemabenki kuu haihusiki na malumbano juu ya wamiliki wa IPTL na uhalali wa umilikiwao wa hisa za kampuni hiyo, wala haihusiki na uhalali wa madai ya wadeni wakampuni hiyo.
 
"Makubalianohayo yalitoa haki na wajibu wa kila upande, na BOT ilihusika kuzitunza fedhahizo na kuhakikisha kwamba hazitumiki nje ya madhumuni ya kuhifadhiwa kwake,kuwekeza katika miradi inayoruhusiwa na kuziwasilisha kwa mmiliki aliyekubalikapale matakwa ya kifungu 7.7 cha makubaliano hayo yanapotekelezwa," alisema.

Alisema benki kuu haihusiki na malumbano juu ya wamiliki wa IPTL na uhalali wa umilikiwao wa hisa za kampuni hiyo, wala haihusiki na uhalali wa madai ya wadeni wakampuni hiyo.

Hizi ni dalili mbaya kuwa Kafulila anataka kuyakataa matokeo
ya uchunguzi kama yatakuwa hayajalinda interest zake!

Hata jana tumemkoti alivyoeleza wasiwasi wake kuwa ripoti
inaweza isijadiliwe bungeni, mbona yeye tu anayetapatapa?

Kuna nini David Kafulila mbona ni wewe tu ndio umelivalia njuga suala hili la IPTL/ESCROW?
 
Bure? Watu wamepiga deal wewe unasema bure? Bure kaishafariki long time kitambo
 
Si ajabu umeme wa Tanesco kuwa ghali kwa kiwango cha kutisha kupita nchi zote Afrika Mashariki,wakati umeme mwingi ni wa vyanzo vya maji ,Tanesco ilitakiwa na umeme nafuu kuliko nchi zote hapa EA,lakini kwa kuwa hele nyingi inaingia kwa matapeli wa kimataifa na waoTanesco kuambulia punje hayo ndio matokeo yake,na huu utapeli unafanywa na mafisadi wa kimataifa wakisaidiwa na wanasiasa wetu kupiga dili,na si ajabu wao ndio wananufaika,wengine ndio hao wa Dowans,Richmond na wengine ndio wanaopewa mgao na ''kaka''zao kulipia mikopo ya shule wanazomiliki.Tanzania kweli ni shamba la bibi.
 
Huyo anayejiita iparamasa!?? Lazima atakuwa Mafisiem waliopo humu Jf, ili kuvuruga fikra za watanzania ama yeye mwenyewe ni mnufaika wa moja kwa moja.

Inakuwaje baada ya analysis hii inayoonyesha kila wizi na kuuweka wazi halafu Iparamasa sijui anakuja na utumbo huu tena wa nguruwe!!!

Aibu Taifa linaangamia kwa madeni, wananchi wanalipia umeme gharama kubwa na zinaliwa na akina Seth na Rugemarila, halafu unakuja na uchafu wako huo!!!

Inauma sana. Hivi Watanzania tuna laana ya nani !!!?
 
Yuko busy kuwaonea Wafanyakazi wa JKN Airport, bandari, kuendelea kukalia mabilioni ya pesa za wahanga wa tetemeko na kuhakikisha Lipumba anapewa ruzuku badala ya katibu Mkuu wa CUF, hana muda wa masuala nyeti kama hili, Lugumi, MV ufisadi etc.

Magu mwenyewe kimyaaa
 
Si ajabu umeme wa Tanesco kuwa ghali kwa kiwango cha kutisha kupita nchi zote Afrika Mashariki,wakati umeme mwingi ni wa vyanzo vya maji ,Tanesco ilitakiwa na umeme nafuu kuliko nchi zote hapa EA,lakini kwa kuwa hele nyingi inaingia kwa matapeli wa kimataifa na waoTanesco kuambulia punje hayo ndio matokeo yake,na huu utapeli unafanywa na mafisadi wa kimataifa wakisaidiwa na wanasiasa wetu kupiga dili,na si ajabu wao ndio wananufaika,wengine ndio hao wa Dowans,Richmond na wengine ndio wanaopewa mgao na ''kaka''zao kulipia mikopo ya shule wanazomiliki.Tanzania kweli ni shamba la bibi.
Lingeanzishwa shirika linguine la umeme, raia wawe na uamuzi umeme upi watumie kama yalivyo makampuni ya simu. TANESCO kuwa monopoly electric supplier kunatuumiza sisi wanyonge.
 
Back
Top Bottom