Jinsi Kabaila (Noble man) alivopata watu makini & kuwaajiri na tuna nini chakujifunza katika biashara zetu

Hypolite

JF-Expert Member
Jul 6, 2017
226
459
Hapajawahi duniani kua na biashara iliyofanikiwa ila ni watu waliofanikiwa wanaoiendesha biashara~Nahau ya Uchina

Hawa watu waliofanikiwa wanaoifanya biashara ifanikiwe ndio wakoje!?Nawapata wapi!?

Moja ya sehemu ngumu sana katika biashara au unapoanzisha biashara ni kupata rasilimali watu utakaofanya nao kazi.

Mtu mmoja peke ake ni ngumu kuweza kutengeneza biashara yeny thamani kubwa lazima Upate leverage,LEVERAGE-Muda wa watu wengine, pesa za watu wengine, Nguvu za watu wengine, kuhustle tu/kuchapa kazi peke yako tu katk umimi hakukufanyi uwe na biashara yeny thaman kubwa bali leverage.

Mtu mmoja alinambia kilichompeleka chuoni ni vitu viwili tu
1.Kubwa kuliko vyote ni kupata watu sahihi atakaofanya nao kazi kama jinsi waanzilishi wa kampuni ya Facebook Mark, Dustin&Saverin walivyokutana chuo cha Harvard nakuanzisha Fb, Brian Chesky&Joe Gebbia walivyokutana chuo cha RISD nakuanzisha AirBnB

2.Kusoma ambapo alisema sio big deal ila kupata watu sahihi wakufanya nao kazi

Kupata watu waliosahihi ili ufanye nao kazi si jambo jepesi sku ya interview kila mtu hutia huruma kutaka kua ni mmoja watakaoajiriwa, moyo wa mtu una siri kubwa una tabia yakufisha au wasawahili husema moyo ni kichaka ndio maana tunaona hata katk serikali kuna fukuza ajiri mwingine fukuza yule weka huyu fukuza tena yule weka huyu,
Kuajiri ni kozi kabisa Vyuoni mtu anaisomea kwa miaka kadhaa Elimu ya rasilimali watu(Human Resource, HR)

Hii Elimu aliitoa Yesu miaka 2000 iliyopita ipo katika biblia katk Fundisho la mfano(parable)
jinsi KABAILA(Tajiri/....enye mamlaka/Noble man) alivyoajiri/ alivopata watu sahihi wakufanya nae kazi.

Habari hii uisome kwa umakini si kwa ukawaida ulivyozoea kuisikia utajikuta umetoka na Elimu ya Human Resource na utaweza kujua namna yakupata watu waliosahihi

"Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.

Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi, Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.

Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda.

basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang'anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.Wakamwambia,Bwana, anayo mafungu kumi.Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang'anywa hata alicho nacho"(Luka19:12-26)

Summary of the parable in relation to the subject matter

Lengo la kabaila katika Hyo habari lilikua ni lipi??
Lengo halikuwa katika kuwaajiri wamanage nakuzizalisha zile fedha ktk biashara sku zote, lengo lakudumu lilikua ni kuwafanya wawe WATAWALA katika ile miji aliyokua anaenda kuipata, biashara ilikuwa ni kipimo cha uwezo wa kila mmoja wao ili aje awape majukumu ya utawala kwa kadri ya uwezo wakuzalisha faida kwa kila mmoja ktk fedha walizokabidhiwa kuzizungusha kweny biashara zipate kuzaa.

Alitambua biashara ina frustration kama jinsi uongozi ulivyo, na uwezo wa kuzimudu frustrations na kadhia za biashara ndivyo watakavyoweza mudu kuongoza miji ile, mweny uwezo wakuzalisha kingi ana uwezo mkubwa wakuhimili kadhia hivo atapewa miji yakutosha.

Hii inanikumbusha rafiki yangu na mwalimu wangu mmoja aliyefanikiwa nilipomuapproach kumuomba kiasi cha 5Million zakufanyia biashara miaka kadhaa nyuma baada yakumaliza form four mwaka 2016, alichonambia mtu hakupi pesa kwa sababu anakufahamu au ni rafiki yako na yeyote afanyavo hivo ni mpumbavu wa wapumbavu, mtu anakupa kwa sababu anaona wazi unauwezo wakuihandle 5Million hivo anza n kidogo ulichonacho katk kile unachotaka kufany then njoo na proof of stake bwana nilianza hapa nimefika hapa.

Tunaona yule wa kwanza alipoleta proof of stake yakuzalisha mafungu kumi alipewa miji kumi na yule wa mafungu 5 alipewa miji 5 kuitawala

Kukosa kazi kwa mweny KUJIONA(Ego):Mwenye kujiona tunaona earning report yake ilivyo alichukua fedha nakuifunga ktk leso nakuifadhi tu sababu amezieleza kama; yule kabaila huvuna bila kupanda hichi ndicho vijana wengi haswa wakitanzania Graduates kinachowaumiza mtu anamaliza degree yake ana full of egos kwa sababu ya High grades zake alizopata kweny mfumo uliomuaminisha kua yeye ni best of the best hivo haitaji kuanza chini huku akikua pole pole pole, ajira hamna hataki kufanya petit jobs zitakazoweza hata chochote lakini anataka kwenda kuingia kweny biashara ya MTU akamess up on someone else's business balance sheet na muda mwingine hata kumchukia boss nakuona Kama anamnyonya hapo haoni frustrations behind boss alizopitia mpaka kuifikisha hapo biashara/kampuni ikaweza hata kumwajiri Nchi za wenzetu kama Marekani hua wana mfumo wakuwafanyisha wanafunzi community works za kawaida kabisa na wanapeleka report ya hizo community works hii inasaidia kwa kiasi kuondoa ego na watu kutochagua kazi.

Kwa nini matajiri wanazidi kutajirika na maskini wanazidi kua maskini wakutupwa
Tunaona yule mweny Ego alinyang'anywa hats kile kidogo alichonacho akaongezewa mweny alichozalisha kingi, leo hii hata dunia hii matajiri wote wanyang'anywe walichonacho wote tugawiwe sawa tuanze 1 nakuhakikishia baada ya muda fulani tu kile kilichopo kwa maskini kitaanza kurudi kwao ndio hivo ndio ubepari unavyo fanya kazi.

Ndivo watu walipoanza kutupa lawama za huyo mweny kingi kwa kumwambia kabaila mbona anacho tayari ndivyo hata sasa dunia utakuta walichonacho wanachukiwa vibaya bila sababu.

Kwa kiasi kweny article above nimejibu swali hili hivo nami ningependa kujifunza kwako khusu

Hapajawahi duniani kua na biashara iliyofanikiwa ila ni watu waliofanikiwa wanaoiendesha biashara~Nahau ya uchina
Cheki hizi statement utajua nini wachina walimaanisha kusema watu waliofanikiwa wanaoiendesha biashara.

Unabiashara yakuuza soda ila kila ukijiskia kiu wafungua jokofu wanywa soda

Unauza vocha huna critical reason yakuunga kifurushi ila unataka tu kupost na kucheki vichekesho whatsap status.

Matendo hayo yanadhihirisha wazi kua hujaipa biashara uhai ikajitenga nawe ikaishi yenyewe kama yenyewe ndivyo watu waliofanikiwa walivyo wamezipa biashara uhai inajitegemea na akitaka fanya expenditure anaiuliza biashara kama itamruhus au itamwambia hapana umeniwithdraw sana niache nijikusanye kidogo.

Hawa watu waliofanikiwa ndio wakoje?? Nawapataje!? Let us engage kweny comments tujifunze zaidi
 
Ccm wao formula ya biashara wanayoitumia ni kufukuza matajiri na kuwateka then wanalalamika kuwa biashara zimedorora.Wakati mwingine wanapandisha kodi kienyeji ili kuwakomoa wafanyabiashra

Nduli Idd Amin Dadah wa Uganda baada ya kumpindua Milliton Obote aliwafukuza Wahindi wote na maduka yao akawagawia Waganda baada ya muda mfupi Waganda walifilisika wote!


Kwa marabya kwanza umeandika madini hatari!😍😍! Achana naye huyo hajielewi
 
Hahahha...unataka kuudhi watu hapa wewe!...hehehe!biashara ni uchawiiii walofanikiwa wote wanatumia ndumba na wana misiri mizito mizito
Mkuu "Imani ni bayana ya mambo yasionekana tena ni hakika ya mambo yatarajiwayo".

Kwa maana hiyo hizo n imani tu na Kila mtu anaamini kivyake.
 
Ccm wao formula ya biashara wanayoitumia ni kufukuza matajiri na kuwateka then wanalalamika kuwa biashara zimedorora.Wakati mwingine wanapandisha kodi kienyeji ili kuwakomoa wafanyabiashra

Nduli Idd Amin Dadah wa Uganda baada ya kumpindua Milliton Obote aliwafukuza Wahindi wote na maduka yao akawagawia Waganda baada ya muda mfupi Waganda walifilisika wote!
Hahaha nimependa hapo akawafukuza wahindi biashara za wahindi akawapa waganda baada ya muda wakafiliska

Hakika mkuu in the long run money goes in the hands to where it is supposed to be, unampa mtu biashara huku mindset yake still haijawa liberated kufit The business mindset lazima hela ya biashara ichomeke tu!
 
Back
Top Bottom