Jinsi gani vita ya kwanza (WW1) na (WW2) zinatuasa kuwa hatuko mbali na WW3

bernard10

JF-Expert Member
Apr 2, 2021
410
731
Karne ya 20 imeshuhudia Vita kubwa kabisa zilizotawaliwa na uharibifu mkubwa kuwahii kutokea katika historia ya dunia Huku takribani mamilioni ya watu na Mali zikiangamia kwakiasi kikubwa njaa, maradhi na anguko la uchumi.

HISTORIA NI MWALIMU MZURI.

Kuna msemo huwa unasemwa kwamba historia Inatabia yakujirudia jambo ambalo Ni kweli Lina mantiki tukitazama kwa makini sababu za Vita kuu mbili zilozotikisa dunia Karne ya 20 mwaka1914-18 na 1939-45.

JE, SABABU GANI ZILIZOSABABISHA VITA YA (WW1) ZILIJIRUDIA (WW2) NA ZINAWEZA KUSABABISHA (Vita ya 3 (ww3).

1.Political & military alliances(miungano ya kisiasa /kijeshi)
Kuanzia mwishoni mwa karne ya 19 dunia ilitawaliwa na miungano ya kijeshi miongoni mwa nchi zenye maslai yanayoshabiana VON BISMARK chancellor wa UJERUMANI ndye anayesemekana kuwa mwanadiplomasia mwenye ushawishi zaidi 19C akiwa ndye msingi na mwanzilishi wa miungano hi lengo likiwa Ni kumtenganisha Ufaransa na dunia baada ya kuchukua majimbo yake ya Alsance & Lorraine Huku yeye akipata washirika. Bismarck alifanikiwa kuunda kwa mara ya Kwanza League of three emperors Kati yake (PRUSSIA) Austria na Russia. Ambapo baadae ulivunjika na mwanzoni mwa karne ya 20 ukaundwa triple alliance (German, Austria-Hungary & Italy) ambao ukaja kupata upinzani wa triple entente (Ufaransa, Urusi & Uingereza) hivyo kupelekea ww1.

Vita ya pili vivyo hivyo kukawa na Axis powers(Nazi ya GERMAN FASCISM ITALY, JAPAN Kama major Powers n.k) na Allied powers (U.K, RUSSIA (SOVIET REPUBLIC,) FRANCE, BELGIUM na baadae USA n.k.

Kwa Sasa muungano mkubwa wa kijeshi uliopo Ni NATO pekee ikiwa na ushirika na nchi Kama Taiwan, Japan, S.Korea, Islael n.k Huku nchi Kama Urusi, China, zikitazamiwa kuanzisha muungano wao ambao Kama upo ila sio rasmi(officials) zikiungwa mkono na nchi Kama Iran, N.Korea, n.k Huku upinzani wakimaslai, uchumi , historia siasa n.k ukiwa mkubwa.

2.Kushindwa kwa taasisi za kimataifa kutatua migogoro yakiuchumi kisiasa kihistoria n.k. kwakutawaliwa na migongano ya kimaslai baina ya nchi wanachama upendeleo na unafki (double standards).

Kabla ya Vita ya Kwanza ya dunia taasisi kubwa zilikuwepo kana international court of arbitration (ICT), lengo likiwa kusuruhisha migongano baina ya mataifa makubwa hasa kuhusu makoloni waliyoyatwaliwa Afrika na sehemu nyingine duniani. Taasisi hizi zilishindwa kutatua migogoro wa eneo la Balkan hivyo kupelekea chuki na visasi vulivyozaa Vita ya 1 ya dunia baada ya kutokea kwa mauaji ya Arch Duke Francis Ferdinand.

Vita ya pili pia ilitokea baada ya madhaifu ya league of Nations kushindwa kutimiza majukumu yake Huku mataifa YENYE nguvu kila moja akivutia kwake maslai yake binafsi pia kushindwa kuzuia NAZISM NA FASCISM kupata nguvu ambayo ilikuja kuwa moja ya sababu za Vita hii

Kwa Sasa umoja wa mataifa(UN) Ni Kama unashindwa kutimiza majukumu yake either kwakukosa nguvu kamili dhidi ya mataifa makubwa Kama China, US au Urusi au kuwepo kwa mvutano wakimaslai baina ya mataifa makubwa yanayoshikiria umoja huu.

3.Uvamizi wa kijeshi baina ya nchi na nchi(Foreign invasion).
Vita ya Kwanza ya dunia ilitokea baada tu ya Austria Hungary kuivamia Serbia Huku ikisaidiwa na Ujerumani hivyo Urusi Kama rafiki mkubwa wa Serbia hakusita kutia mguu dhen Ufaransa, Uingereza na Belgium wakafuata na baadae Italy.

Vita ya pili kwa upande mwingine ilichajizwa na Uvamizi was Ujerumani nchini Poland na baadae ubelgiji na Ufaransa Jambo ambalo lilipelekea Vita ya 2 ya dunia.

Kwa miaka ya hivi karibuni Uvamizi wa nchi na nchi umeanza kwa Kasi mfano mwaka 2008 Urusi alipoivamia Georgia ,Marekani akivamia Iraq NATO wakiivamia Libya 2011 Huku hivi karibuni Uvamizi mkubwa kabisa tangu Vita ya 2 ya dunia ukifanywa na Urusi dhidi ya UKRAINE na dalili zikionesha China akijipanga kuivamia Taiwan ambayo in mslai makubwa na USA Iran ikiwa katika mzozo mkubwa na Islael hivyo kuibua matishio ya ujio wa WW3.

4. Ushindani wa kijeshi (utengenezaji siraha /majeshi) militarism & arm race;
Kabla ya Vita ya Kwanza ya dunia shughuli za uimarishaji /utengenezaji siraha nzito ulishamiri barani ulaya Asia( Japan) America (USA). Mwanzoni mwa karne ya 20 kwa mfano ushindani Kati ya Ujerumani na Uingereza katika jeshi la majini (NAVAL arms) ulishamiri Huku Ufaransa na nchi nyingine zikiimarisha majeshi yao hivyo kupelea sintofahamu iliyochangia kutokea kwa Vita ya kwanza ya dunia.

Baada ya Vita ya 1 kuisha UJERUMANI Kama aggressor yaani msababishi wa Vita alipewa adhabu moja ikiwa kupunguza idadi ya jeshi na siraha zake kwa KIASI kikubwa.

Hii ilikuja kuwa tofauti baada ya Hitler kuchukua madaraka Huku moja ya Sera yake Ni kulifanya jeshi la Ujerumani kuwa na nguvu zaidi duniani. Kitendo hicho kilifungua ukurasa mpya wa kuibuka Vita ya 2 yadunia mnamo mwaka 1939.

Kwa Sasa mataifa YENYE nguvu ya kijeshi hasa YENYE siraha za nuclear yamekuwa yakitunishiana misuri tangu kuisha kwa Vita ya 2 ya dunia Huku Urusi akiongoza kuwa na siraha nyingi zaidi za nuclear Marekani akimfuata na nchi nyingine Kama India, UK , Ujerumani N.Korea , Iran n.k hivyo kuchochea Zaidi ukaribu wa Vita ya 3 ya dunia.

Kwakumalizia Vita ya 3 ya dunia Kama itatokea
Dunia itakabiriwa na uharibifu mkubwa zaidi kuwahi kusababishwa na binadamu hii nikutokana na uwezo mkubwa wa siraha za nuclear katika kufanya uharibifu na maangamizi rejea mwaka 1945 Hiroshima na Nagasaki Huku hi leo ikiwa imepita takribani miaka 77 jinsi gani Teknolojia ya utengenezaji wa siraha hizo umekuwa zaidi na Zaidi.

Let's together pray for peace in the world.
 
Hii vita hii inaagenda muhimu sana, ukicheck huko ujerumani ilikuwa huwezi kununua kitu chochote kama hajachanjwa. Na tangu hii vita ianze sijasikia takwimu za covid 19 kwa haya mataifa makubwa. So sidhani kama ni ww3 hii
 
Hii vita hii inaagenda muhimu sana, ukicheck huko ujerumani ilikuwa huwezi kununua kitu chochote kama hajachanjwa. Na tangu hii vita ianze sijasikia takwimu za covid 19 kwa haya mataifa makubwa. So sidhani kama ni ww3 hii
Vita ipo njian kutokana na mfurulizo wa matukio yanayoweza kukaribisha ww3 sijui mwaka gani ila naona haiko mbali Sana mkuu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom