Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
1589085901859.png

JINSI YA KUEPUKA KUNUKA MDOMO
Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.

Kile unakula kina affect hewa unayotoa iwe mdomoni au sehemu nyingine. Na baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.

Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90 ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

NINI HUSABABISHA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI

Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula). Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na medications Kuvuta sigara, kunywa kahawa.

JINSI YA KUTAMBUA KWAMBA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI

Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).
Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.

Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

JINSI YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)

Kula vyakula vyenye afya na pia kula vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri. Kusafisha meno mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, unashauriwa kutumia tongue cleaner kusafisha ulimi. Tumia chewing gum ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya. Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku. Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa.

Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.

Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.
---

JINSI YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI!

WATU wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.

Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:

KUPIGA MSWAKI

Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.

Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.

KUNYWA MAJI MENGI

Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).

Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.

Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.

Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka au 'chewing gum' yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria. Mwisho, hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.
---
Katika maisha ya kila siku inawezekana umewahi kukutana na mtu ambaye ukiwa karibu naye kimazungumzo, utagundua anatoa harufu mbaya mdomoni.

Kwa kawaida mdomo na pua hutoa pumzi nje ambayo huwa na harufu asilia ambayo haiwezi kumkera mtu mwingine, lakini mara nyingine hali hiyo inaweza kujitokeza kwa mtu kutoa pumzi yenye harufu mbaya.

Pengine watu wa karibu au wanaokutana na mwathirika wa hali hii, wanaweza wakadhani mtu huyo ni mchafu mwenye na tabia ya kutopiga mswaki au kutosafisha kinywa chake vizuri.

Wengi hawajui kuwa mtu huyo anaweza kuwa na tatizo linalojulikana kitabibu kwa jina la halitosis, ambalo maana yake ni kutoa pumzi ama mdomoni au puani.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kukumbana na kunyanyapaliwa na wanajamii wanaomzunguka kiasi cha kuweza kumsababishia matatizo ya kisaikolojia.

Mwathirika anaweza kupata na tatizo la hofu iliyopitiliza anapokuwa katika jamii; anaweza akajinyofoa kutoka katika jamii na kujitenga na baadaye anaweza kupata sonona.

Ugonjwa wa halitosis

Karibu asilimia 20 ya watu duniani wanakumbwa na ugonjwa huu na hivyo kukimbilia kwa wataalamu wa afya ya kinywa.

Hufika kwa wataalamu hawa wakidhani wana magonjwa ya kinywa ikiwamo mashimo katika meno, kulika kwa meno, kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi.

Ukweli ni kuwa si wagonjwa wote wenye kutoa pumzi yenye harufu mbaya wana tatizo halisi la halitosis, kati ya asilimia tano hadi 72 wanaofika katika huduma za afya hugundulika kuwa hawana tatizo hili moja kwa moja.

Tatizo la kutoa pumzi yenye harufu mbaya ambalo ndiyo ugonjwa halisi, linasababishwa na uwapo wa mrundikano wa bakteria katika uvungu wa fizi na nyuma ya ulimi karibu na koo.

Kinywa kwa ujumla, kikijumuisha meno, fizi, ulimi na vifuko vya mate kinaweza kuwa ni maficho mazuri kwa mamia ya bakteria. Ndiyo maana inaaminika tatizo la harufu mbaya mdomoni ni kinywa chenyewe.

Kinywani pekee kuna karibu jamii 600 za bakteria ambao huambatana na mabaki ya vyakula tunayokula kila siku. Kuwapo kwa protini ya kwenye mate na protini ya vyakula tunavyokula na uvunjwaji wa mabaki yake na bakteria waliopo mdomoni, ni chanzo cha kuwapo kwa harufu mbaya.

Mabaki ya protini mdomoni ambayo huvunjwavunjwa na bakteria na kuwa tindikali ya amino na hapo baadaye inapovunjwa, hutoa gesi yenye harufu mbaya.

Mfano mzuri ni pale protini ijulikanayo kama methionine na cysteine inapovunjwavunjwa kinywani na hivyo kutoa gesi yenye harufu mbaya ijulikanayo kama Hydrogen sulphide.

Mara nyingi harufu ya kinywa inaweza kuwa nzito zaidi baada ya mtu kuamka. Hii ni kwa sababu wakati wa kulala mdomoni kunakuwa na kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni.

Bakteria waliopo mdomoni ni wale wasiohitaji uwepo wa hewa ya oksijeni hivyo kipindi cha usiku tukiwa tumelalala, ndipo huvunjavunja mabaki ya chakula ambayo huambatana na kutolewa gesi zenye harufu mbaya.

Vilevile harufu ya kinywa inaweza kubadilikabadilika kutokana na vyakula tunavyokula ikiwamo vitunguu maji, vitunguu swaumu, hiliki, tangawizi na pia uvutaji sigara na unywaji wa pombe.

Hivyo siyo mara zote kupumua harufu isiyo ya kawaida ni ugonjwa; mara nyingine inakuwa ni tatizo la muda tu lililochangiwa na vyakula na matumizi mengine ya vitu.

Asilimia 10 zilizobaki, mara nyingi husababishwa na matatizo mengine ikiwamo magonjwa ya kooni, puani, shambulizi za nyufa za mifupa iliyopo usoni, magonjwa ya mfumo wa chakula, magonjwa katika mapafu, magonjwa ya masikioni na madhara ya ugonjwa sugu wa mafindofindo.

Vilevile kuwapo kwa majipu ya fizi au meno, vidonda mdomoni au michubuko, vidonda vya kooni na maambukizi ya virusi vya herpes simplex na HPV. Mara chache pia tatizo hili linaweza kuchangiwa na magonjwa ya ini ikiwamo kuharibika kwa ini na majipu katika ini.

Mara nyingine wanaoshtakia tatizo hili hubainika kuwa na tatizo la usafi wa kinywa. Na wanaposhauriwa kuboresha usafi wa kinywa kwa kutumia dawa za meno, au kusukutua na dawa maalumu za kusafisha kinywa nyuma ya ulimi, tatizo huisha haraka.

Tiba ya ugonjwa

Uchunguzi wa tatizo hili huanzia kwa mhusika mwenyewe kueleza historia ya tatizo, kisha wataalamu wa kinywa au daktari wa kawaida humchunguza kwa kumfanyia majaribio na vipimo kadhaa.

Baada ya wataalamu wa afya kubaini ugonjwa ndipo ushauri na matibabu huanza. Kama chanzo cha harufu mbaya ni maradhi ambayo si ya kinywani wataalam watakupa matibabu ya kutibu chanzo hicho.

Kama chanzo cha kutoa pumzi yenye harufu mbaya ni kinywa, wahudumu wa afya watamwelekeza mgonjwa mambo mbalimbali kama ifuatavyo;

- Kupiga mswaki katika ulimi mara mbili kwa siku kwa kutumia mswaki laini, kifaa kama kijiko kwa ajili ya kukwangua uso wa ulimi. Pia kutumia dawa yenye kiambata cha kuua bakteria.

- Ulaji wa kifungua kinywa chenye afya ikiwamo kula matunda na mboga za majani yenye nyuzi nyuzi, husaidia kusafisha kinywa eneo la nyuma ya ulimi wakati wa kumezwa.

- Utafunaji wa bazoka unasaidia kuufanya mdomo usiwe mkavu na hewa ya oksijeni kuingia kinywani kwa wingi. Pia utafunaji wa bazoka unaweza kusaidia kutiririka kwa mate kwa wingi yanayosaidia kusafisha kinywa na kuua vimelea vya maradhi. Mdomo ukiwa mkavu na hautafuni chochote huchangia kujiimarisha kwa bakteria

- Kusukutua kwa maji mengi ikiwezekana ya vuguvugu kila mara baada ya kula chakula na kabla ya kwenda kulala. Unaweza pia kutumia dawa maalumu za kusukutulia kinywa zenye dawa ya kuulia vimelea.

- Jaribu kuboresha usafi wa kinywa kwa kuusafisha ulimi. Safisha meno kwa mswaki kila unapomaliza kula chakula, ondoa mabaki ya chakula yaliyojibana katika meno na fizi na safisha na sukutua kinywa chako kwa dawa maalumu kabla ya kulala.

- Unaweza kutumia vitu asilia kama majani ya minti na karafuu, kama njia ya kupunguza kupumua hewa yenye harufu mbaya.

- Ni vyema kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa kila baada ya miezi sita, ili kuweza kubaini magonjwa mbalimbali ya kinywa mapema.
---
Tatizo hilo kitaalamu linaitwa Halitosis na husabababishwa na sababu nyingi zinazoambatana si tu na meno bali pia ufizi. Ikumbukwe pia kuwa upigaji mswaki unaweza kuchangia kwa namna moja au nyingine.

Kwa ushauri wa haraka nikngekushauri utumie dawa aina ya sensodyne, piga mswaki kila unapomaliza kula, tumia mouth wash ikibidi. Kuna kitu kama nyuzi maalumu kinaitwa dental floss hiki ni kizuri sana kwani kinapenya kati ya meno ambapo mswaki hauwezi kuingia. Kama utafanikiwa kupata(bei rahisi tu) tumia kila mara kuondoa vyakula kati ya meno.

Angalia aina ya mswaki unaotumia kama ni hard brush au soft. Hard inaweza kuwa inaumiza ufizi na soft yaweza kuwa haifanyi kazi kama inavyotarajiwa. Kwa mantiki hii ni mganga wa meno anaweza kukupa jibu sahihi la tatizo lako.

Wakati ukisubiri kumuona unaweza kutumia buble gum(zisizo na sukari) kuondoa harufu hiyo.

Hata hivyo ni muhimu sana umuone daktari wa meno kwani anaweza kujua undani na ukubwa wa tatizo.

1592036579450.png

What is Bad Breath?
In one old mythological tale, when a young woman pleased three spirits who lived in a pool of water they bestowed favors upon her. One of these favors was sweet breath, so we know that bad breath has been a problem for quite some time!

Today it's still one of the banes of our existence-- embarrassing rich and poor, young and old alike. Fortunately, we understand a bit more about it now than we did hundreds of years ago, and know a few tricks to help with this most unfortunate difficulty.

Bad Breath
Bad Breath or Halitosis can be a serious source of embarrassment and shame. Some people with bad breath aren't even aware there's a problem. However, you no longer have to let it handicap or affect your social life. Please browse through our site to learn how to treat Bad Breath.

We explain what causes bad breath as well as the solutions to treating bad breath (halitosis). We sell a large range of products to help treat and get rid of the bacteria and horrible taste in your mouth.

Maintaining good oral health is essential to reducing bad breath. Nearly all bad breath originates from the mouth, mostly from the surface of the tongue, below the gum line, between the teeth and other hard to reach areas. Bad breath is not contagious and you cannot catch it from someone else.

Follow these simple steps to help treat bad breath:

* Brush and floss using a chlorine dioxide toothpaste (avoid toothpaste containing sodium laryl sulphate)
* Use an oral mouthwash containing chlorine dioxide (gargle as well)
* Use of a tongue scraper to remove any white coating as far back as you can.
* Regular professional cleanings.
* Drink lots of water!

Causes of Bad Breath
Bad breath is not contagious and you cannot catch it from someone else. Also, chronic bad breath (Halitosis) does not come from the stomach. The only stomach odor that someone smells occurs when you burp.

Certain foods like garlic and spicy foods once absorbed into the body can release odor through the lungs when you breathe. This food odor is transitory and should not be confused with bad breath.

Air flow though the nose of someone with bad breath does not have an offensive odor, only air flow through the mouth. Because our sense of smell has the ability to adjust to odor most people with halitosis are not aware of their bad breath.

Nearly all bad breath originates from the mouth, mostly from the surface of the tongue, below the gum line, between the teeth and other hard to reach areas.

The mouth is normally inhabited by bacteria and the balance between the different kinds of bacteria determines the quality of your breath. The odor causing bacteria are anaerobic which means they cannot live in the presence of oxygen.

These anaerobic bacteria inhabit the surface of the tongue by residing between the papillae of the tongue which is oxygen deficient i.e. they live "within" the tongue. These bacteria cannot be removed completely with a tongue scraper and will recolonize the mouth following antibody therapy.

These naturally occurring bacteria feed on proteins (oral debris) and produce volatile sulfur compounds (VSC) as a by-product of metabolism causing the malodor of bad breath.

Everyone has some level of VSC in their mouth, but it is at a low level that cannot be detected by the nose. When these levels of VSC gets high it becomes detectable as bad breath.

Halitosis is rarely associated with certain medical conditions - e.g.: diabetes. If the onset is sudden, grows noticeably worse over a short period of time and is associated with fever, see a doctor.

Q: What causes Bad Breath Odor (Excessive Volatile Sulfur Compounds)?

Anything that decreases the flow of saliva or stimulates the growth of anaerobic bacteria.

Saliva irrigates the mouth, stimulates swallowing thereby flushing away debris. Morning breath occurs due to decreased salivary flow during sleep. As saliva contains oxygen, the dryer your mouth and the thicker your saliva, the less the washing action and the lower the oxygen level creating a more anaerobic environment for bacteria to produce sulfur compounds.

This oral stagnation is more pronounced in mouth breathers and those who snore. Alcohol and even certain mouthwashes containing alcohol can dry the oral tissues causing bacteria to profilerate. Certain medications for high blood pressure, antihistamines and depression can decrease saliva flow. Dehydration and stress also reduces the flow of saliva.

These anaerobic bacteria breakdown proteins as the start to digestion, and produce these sulfur compounds as a by-product. These proteins come from oral cellular debris (poor oral hygiene), dead bacteria, saliva, food debris, mucous, post nasal drip and phlegm.

Certain conditions cause these bacteria to produce these VSC at an unusually rapid rate. Types of foods may include dairy products especially if you are lactose intolerant and certain foods high in protein. Numerous antibiotics or sulfa-drugs upset the balance of bacterial flora causing some to proliferate and others to perish.

An important factor in bacterial growth is the pH of the mouth. Bacteria reproduce faster in a more acid environment. Coffee and acidic foods increase acidity. Hormonal changes have even been implicated with bad breath.

During menstruation, estrogen causes sloughing of body lining tissue including that of the mouth. This gives additional nutrition for anaerobic bacteria. Then their is the luck of the draw....your genetics.

We all have a different tongue morphology. The more fissured the tongue, the greater the anaerobic environment and the higher the level of VSC.

Steps to test for Bad Breath?

Q: How to test if you have Bad Breath

1. Let it dry for a few seconds and then smell. If you notice an odor, you have a breath disorder.

2. Place dental floss between your back teeth and then smell the floss.

3. While looking at the mirror, grab the tip of your tongue with a Kleenex and pull it out as far you can. If you see that the very back of your tongue is whitish in color, it may be a sign that you have bad breath.

4. Ask the opinion of someone you can trust. Check your breath several times daily because your breath changes throughout the day.

5. Professional use of a Halimeter will measures the concentration of volatile sulfur compounds (VSC) in the mouth.


Bad Breath Treatment Cure Bad Breath

Q: What is the truth about mouthwashes, breath mints and breath capsules?

Approximately millions of people suffer from halitosis, otherwise known as chronic bad breath. They cover up the odor and do nothing to treat the cause of bad breath.

Each year over a billion dollars is spent on over-the-counter products that do not eliminate bad breath but merely mask it for only a few hours. Some even make the problem worse. Alcohol based mouthwash dries out the oral tissue and can worsen the condition.

Q: I used the chlorine dioxide mouthwash and I have a strong metallic taste in my mouth. Coffee tastes lousy, even water tastes lousy. I have stopped using the product. Will this taste go away?

Yes, it will eventually go away. If you're switching back and forth between different products, you will definitely notice a strange taste. During the first 14-21 days of brushing and rinsing with TheraBreath almost everybody notices a difference in taste.

Then your taste buds will acclimate. This is because most people have highly acidic oral environments. TheraBreath is a base which neutralizes these excess acids. This causes a strange taste at first while your mouth normalizes.

When you switch back and forth your oral environment gets confused and never gets a chance to acclimate - this is why you could be experiencing a difference in taste.

In addition, to help speed up this process you can also try sprinkling a little baking soda on your toothbrush along with your toothpaste. This may help neutralize any excess acids.

Q: How do you cure Bad Breath?

As the anaerobic bacteria which cause bad breath reside within the tongue itself it is impossible to remove these bacteria completely by brushing or using a tongue scraper alone. Scraping the surface of the tongue may remove excessive VSC (a whitish film) that have surfaced to the top of of the tongue.

Although bad breath is not necessarily an oral hygiene problem, it is important to brush and floss to maintain oral health. Maintain regular professional cleanings especially if you suffer from Periodontal Disease (gum disease).

Broken down diseased tissue is bacterial nutrition. It is important to know that most toothpaste contains sodium laryl sulphate which is used as a foaming agent. This is actually a detergent which dries out the mouth even more.

To effectively treat bad breath, the level of anaerobic bacteria and the amount of VSC produced needs to be reduced and or neutralized.

Q: What products reduce anaerobic bacteria and neutralize bad breath?

As ph is important, the product used needs to have a neutral or slightly basic ph. As the bacteria thrive in an anaerobic climate, the incorporation of an oxygenating complex would be advantageous.

An oxidizing agent is needed to neutralize the volatile sulphur compounds from the active sulfite to an inactive odorless, tasteless sulfate form. The active ingredient is chlorine dioxide. Chlorine dioxide besides neutralizing vsc is also an antimicrobial agent.
Bad Breath Summary:

* Brush and floss using a chlorine dioxide toothpaste (avoid toothpaste containing sodium laryl sulphate)

* Use an oral mouthwash containing chlorine dioxide (gargle as well)

* Use of a tongue scraper to remove any white coating as far back as you can.

* Regular professional cleanings.

* Drink lots of water!!

Products currently available which claim to neutralize vsc include Breath Remedy, BreathRx, CloSys11, Oxyfresh, Profresh and Therabreath

These products do not foam like regular toothpaste and do not contain minty flavoring agents. They are bland tasting and some may even find it unpleasant tasting, but they do appear to work. Profresh is the only product that contains the active form of chlorine dioxide.

The others contain a stabilized form of chlorine dioxide which needs an acidic environment to break down to the active form. Some question their efficacy, while others indicate that Profresh is overkill.

Oxyfresh is the only one that contains sodium laryl sulphate(a foaming agent-like regular toothpaste) which some say may dry out the mouth. There is inadequate research at this time to indicate any product superiority and dentist recommends that you try the different products until you find the one that works best for you.

Good Luck

1592036755422.png

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
Polee! I feel it.

Hakikisha unasugua ulimi vizuri na si meno tu. Ulimi unachangia sehem kubwa kuwa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ziko dawa za kinywa nzuri..ntakupa jina lake badaye.

Pia
Baada ya kula tu na kusukutua kinywa unaweza kutumia limao, yan unakamua unakunywa namanisha unakamua hlf unakunywa..kama unasukutua hiv, au kulamba kwa ulimi pia.

Limao linasaidia kuua bacteria hao. Unaeza tumia limao baada ya muda fulani. Ukiulizwa kwanini unatumia limao unaeza sema ni kwa ajili ya kuzuia gesi tumboni kila wakati au tumbo lisikuume baada ya kula.

Wengine wanatumia tangawizi kutafuna kipande kidogo tu nayo inasadia. Ni chungu kiasi ili dawa nzuri tu unaposukutua nayo kinywani. Unaeza tafuna pia baada ya muda fulani.
Zote njia unaweza tumia hata usiku kabla hujalala na asubuhi kupiga mswaki unatumia pia
---
Nilikuwa na hii shida nikiwa sekondari ila shida yangu nikajua ipo sehemu gani.

1. Kama una tabia ya kutafuna vinyama ndani ya kinywa acha, mimi baada ya kuacha niliona mabadiliko makubwa.

2. Piga mswaki kwa dawa ambazo ni herbal. Unaponunua dawa ya meno itazame mwisho kabisa ina alama ipi? Je ni red, blue or green? Tumia saana green maana hiyo natural, red ni chemical na blue ni natural+chemical. Nitaweka picha ya hizi alama.

3. Jizoeze kupiga mswaki kila ulalapo na uamkapo, ata kama ni mchana wewe piga.

4. Kuna maji flani ya kusukutua ktk kinywa, supermarkets wanauza, uwe unatumia mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Tatizo lako ni dogo tu kijana.

Jitahidi unapopiga mswaki uwe unasugua ulimi kwa sababu chakula huwa kinaangukia na kuburuzwa hapo wakati wote wa kula,unaposahau kuukosha ulimi na ikawa ni suala la muda mrefu basi mabaki ya chakula yanagandana baadae hutoa harufu.

Sugua ulimi wako kwa mswaki usiokuwa mgumu sana kuepusha michubuko na vidonda ulimini.

Jambo lingine jitahidi kupiga mswaki kila baada ya kula chakula na usiweke kipaumbele sana kupiga mswaki wakati wa kuamka na kulala,bali kipaumbele iwe kila unapokula chakula cha ratiba yako upige mswaki na iwe ndio tabia yako hiyo.

Tatu tafuta dawa inaitwa sensodyne bei ni kuanzia 12000 hii dawa nzuri sana kwa mambo ya kinywani uwe unatumia hiyo kama dawa yako ya maisha japo bei kubwa,kama huwezi tafuta dawa zingine za meno nzuri.

Pia unapopiga mswaki piga juu chini juu chini,na sio ile kushoto kulia kushoto kulia.

Piga katika kila engo.

Vuta picha unapopiga mswaki basi mswaki wako uwe unaishia katika nafasi baina ya jino na jino(hapa ngumu kuelewa,ni kama ile juu chini)
---
Ngoja na mm nikupe eperience yangu.

Mkuu harufu mbaya itaondoka kwako ukijitahidi usafi wa kinywa chako.

Mi nakushauri unapopiga nswaki zingatia haya:

1.Usitumie mswaki wako zaidi ya miezi2.

2.Sugua vizuri meno yako pande zote za kinywa pamoja na ulimi wako.

3.Weka dawa ya meno mara mbili na ya kutosha pia hapa namaanisha kuwa unaweka dawa mara ya kwanza unasugua meno yako vizuri na ulimi kisha unatema na kusukutua,kisha unaweka dawa tena unasugua tena meno na ulimi vizuri ila povu da dawa usiteme liache kwa muda hata wa dk5 mpaka 8 huku kama unalisukutua ndani baada ya hapo ndo uliteme na kupitisha mswaki kisha usukutue na maji.

4.Sababu ww una tatizo waweza piga ht mara tatu kwa awamu moja ya usafi wa kinywa.

5.Kama una meno yenye matobo usiruhusu mabaki ya vyakula hayakai kwa muda mrefu baada ya kula so piga mswaki kila mara baada ya kula ili kuyaondoa mabaki kinywani.

NB.Hapa tumechangia tukiassume tatizo linasababishwa na kinywa ila niliwahi kusikia kuna wwngine tatizo huwa linatoka ktk njia ya chakula yaani kuanzia hapo kwa msosi tunapomezea kwenda ndani huko so km utaona njia zote za kusafisha kinywa zimedunda basi nenda hospitali waeleze wakucheck na hilo pia.

Pole sana mkuu naimagine unayopitia kwenye mahusiano yako na dada zetu walivyo na nyodo.

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Pole sana kw hiyo hali.

Kwanza hakikisha unaenda kusafisha kinywa walau mara mbili kwa mwaka(Kuna tabaka huwa linaganda kati ya meno ambayo yanakuwa ni malimbikizo ya vyakula mwisho huganda na kuwa vigumu,hivi huchangia sana harufu mbaya mdomoni hivyo inatakiwa vikasafishwe.yaan kati ya jino na jino ibaki fizi tu.unaweza angalia hapa meno ya mbele kwa ndani uone kama hizo calculi hazipo.

Pili hakikisha baada ya kula unafanya flossing,tafuta flossing thread zinapatikana pharmacy ukishamaliza kula unapitisha uzi huu kati ya meno kwa kinywa kizima.

Lakini pia tumia miswaki mizuri na uhakikishe unapiga mswaki kila kona ya kinywa chako bila kusahau ulimi.

Kila la kheri.

NB kusafisha kinywa kwa dentist ni muhimu mno kama hatua ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Rejea kwenye title husika hapo juu

Habari zenu wana jf
Leo nimeona kuna tija ya kujulishana tips mbalimbali za kuweka kinywa kiwe safi ili kuepuka harufu mbaya

Kutosafisha kinywa vizuri
Kwa kawaida unatakiwa kusukutua kinywa chako angalau mara mbili kwa siku - asubuhi na usiku kabla ya kulala. Wakati wa kusafisha kinywa, hakikisha umesugua vizuri ulimi. Meno na fizi havina tatizo sana, bali ulimi ndio sehemu kubwa ambapo bakteria wanajijenga. Vilevile, ni ulimi unaosababisha kinywa kunuka. Ni vizuri kama utasafisha vizuri ulimi ili kuondoa harufu.

Ni vizuri kufahamu kuwa mswaki unatakiwa kubadilishwa kila baada ya muda - angalau kila mwezi. Usitumie mswaki kwa muda mrefu, maana hauwezi kusafisha kinywa chako kwa ufasaha kama inavyotakiwa maana wengine wanatumia mswaki kwa mwaka na zaidi. Je utaacha kunuka kinywa?

Kutokula chakula vizuri
Harufu ya kinywa inaashiria kutokula chakula na kinywaji kwa muda mrefu. Kuwa na njaa husababisha mdomo kuwa mkavu. Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa hupotea mara tu baada ya kula chakula kizuri na mdomo ukiwa una mate ya kutosha. Acha kutumia vyakula na vinywaji vinavyoongeza harufu kali mdomoni na kukupunguzia maji mwilini – mfano pombe, viungo kama kitunguu maji au kitunguu saumu.

Kinywa kikavu
Bakteria hushamiri kwenye kinywa kikavu. Kama hupendi kunywa maji mengi na kinywa chako kinakuwa kikavu mara nyingi basi jua kuwa kunuka kinywa kwako ni jambo la kawaida.

Jinsi ya kutatua tatizo

Hakikisha mdomo haukauki

Kwa kawaida mdomo mkavu hutoa harufu mbaya. Hii ndio sababu kuwa kinywa chako kinanuka sana asubuhi sababu mdomo wako unatengeneza mate machache sana ukiwa umelala. Mate ni adui wa harufu mbaya mdomoni siyo tu sababu inaondoa bakteria na masalia ya chakula, bali mate yana vimengenyo vinavyoua na kuzuia kuzaliana kwa vijidudu kwenye kinywa. Ili kuzuia kunuka, jaribu kufanya haya

Kunywa maji mengi ili kuondoa masalia ya chakula na bakteriaTafuna bazoka, sababu bazoka inasababisha mdomo kuwa na mate mengi. Kuwa makini katika kuchagua bazoka zisizo na sukari. Sukari ni adui mkubwa wa kinywa chenye afya.

Piga mswaki kabla ya kulala
Kupiga mswaki ni muhimu, lakini wengi tunasahau kuwa mswaki ni lazima kupiga angalau mara mbili kwa siku haswa usiku naasubuhi. Kupiga mswaki asubuhi ni muhimu ili kuondoa uchafu uliojijenga usiku kucha na hivyo harufu mbaya - lakini siku nzima mdomo unatengeneza mate na kuwa laini. Hii ni tofauti na usiku. Usiku mdomo hubaki mkavu na mate kidogo, hivyo kuwa rahisi kwa vijidudu kuzaliana na kuharibu mazingira ya mdomoni kwako. Hivyo, ni afya zaidi kupiga mswaki usiku ili kuzuia kushamiri bakteria waharibifu wanaosababishwa na masalia ya bakteria kwenye kinywa chako. Njia hii itasaidia kuzuia bakteria kuharibu meno na fizi, hivyo kutokuwa na harufu mbaya ya masalia wakati ukiamka.

Kula ndizi au apple
Ndizi au apple husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini ni kwa muda mfupi sana. Ukiwa unahisi mdomo unanuka na unahitaji njia ya haraka, tafuta ndizi au apple, na hapo utakuwa umetatua tatizo kwa muda.

Kula Tango
Maji ya tango yana kemikali zinazozuia kukua kwa bakteria kwenye kinywa. Baada ya mlo mzuri wenye viungo vyenye harufu kali, kata kipande kidogo cha tango, kigandishe kwenye ukuta wa juu wa mdomo wako kwa sekunde 30 huku ukikandamiza na ulimi. Zoezi hili litasaidia kuua bakteria na kuacha kinywa chako kikiwa na afya na harufu nzuri.

Jenga Tabia ya Kupia Mabusu (Kissing)
Ni ukweli kuwa ukifanya kitu chochote kinachosababisha kutoa mate basi unazuia kunuka kinywa. Kissing ni mojawapo ya njia mbadala za kuzuia harufu mbaya mdomoni. Kiss mara nyingi uwezavyo ili kufanya mdomo wako uwe na mate mengi, na hivyo kuzuia kunuka kinywa.

Harufu ikizidi, kamuone daktari
Je harufu yako ya kinywa ni ugonjwa? Basi kamuone daktari. Wakati mwengine harufu ya kinywa hutokana na kuwa na matatizo mwilini na huwezi kuondoa kwa kutumia njia tulizozieleza hapo juu.

View attachment 334469
---
Harufu mbaya(halitosis) mdomoninini chanzo chake nini?

Kinywa au mdomo wa mwanadamu ni sehemu mhimu sana kwa kazi mbalimbali ikiwemo

1. Kuongea

2. Kula

3. Kucheka na kuimba

Kinywa cha mwanadamu kinaweza patwa na shida mbali mbali endapo hakita tunzwa vizuri ikiwemo kuto fanya usafi wa kinywa vizuri kwa kupiga mswaki wenye dawa ya meno yenye flourides

Harufu mbaya mdomoni husababishwa na ugonjwa uuitwa periodontitis ,huu ni ugonjwa ambao hutokana na uchafu utokanao na mabaki ya chakula kwenye meno ambayo huungana na na bacterial baadaye kutengeneza vitu vigumu na kuganda kwenye meno ambavyo havitoki kirahisi kwa kupiga mswaki, mwishowe kupelekea harufu mbaya sana kinywani,kulegea meno na kutoka pia kutoa damu wakati wa kupiga mswaki,pia meno kubadilika rangi kutoka nyeupe kuwa njano ugonjwa huu ni moja wapo ya sababu za kutoa harufu mbaya ila zipo sababu nyingine pia endapo kama hutakuwa na ugonjwa huu nazo hupelekea kutoa harufu mbaya mdomoni ,tutazungumzia siku nyingine.

TIBA,
kuondoa matabaka hayo kwa vifaa naalumu ,hii hufanywa hospital na dactari tiba inaitwa scalling and root planing

Kufanya usafi wa kinywa na meno angalau mara mbili kwa siku hasa usiku usilale bila kupiga mswaki na dawa ya meno yenye flourides

Tumia dawa ya kusukutua iitwayo rinsing drug kama listerine mouth wash na sonetic na hexidine na betadine sln 2%
next time tutazungumzia kwanini meno yana tobaka na nini kifanyike.

Imeandaliwa na
DR L MBOBOYU
0762291006
EKENYWA SPECIALIZED HOSPITAL MAGOMENI MWEMBE CHAI,DSM
---
Kinywa kutoa harufu mbaya huweza kuwa kero kwako binafsi au kwa watu wanaokuzunguka.

Yapo matibabu aina mbalimbali dhidi ya kinywa kutoa harufu mbaya, ikiwepo pamoja na pipi, bigijii na dawa za kusafisha meno

Dawa hizi huweza kuwa zinafanya kazi au kutomsaidia mtu. Jambo la msingi ni kufahamu nini kisababishi na kuanza matibau ya

Kisababishi.

Dalili
Darufu ya kinywa hutofautiana kutokana na nini kilichosababisha, kuna baadhi ya watu huhofu saa kuhusu harufu ya kinywa ingawa wana harufi kidogo inayotoka, na kuna wengine wanavinywa vinavyotoa harufu mbaya bila wao kujitambua. Siku zote muulize jirani yako endapo kinywa chako kinatoa harufu au la.

Visababishi
Kuna visababishi mbalimbali vinavyoweza kupelekea kinywa kutoa harufu mbaya, mara niyngi huwa chakula, Tania na hali ya kiafya ya mtu.

Chakula
Vyakula jamii ya vitunguu, tangawizi, na viungo vingi vya chakula endapo vitamengenywa na bakteria katika kinywa huleta harufu mbaya ya kinywa. Vyakula jamii ya nyama pia endapo vitaliwa na kubaki katika kinywa huoza nakusababisha harufu mbaya kutoka kinywani

Kutofanya usafi wa kinywa
Kama husafishi kinywa kwa dawa ya mswaki na kuchukutua mdomo mara baada ya kula haswa wakati wa jioni, utapata harufu mbaya mdomoni kutokana na vyakula hivyo vinavyobaki kinywani kuoza na kutoa harufu.

Vyakula mara nyingi vikibaki kinywani hutengeneza ukuta kuzunguka meno na ulimi na kuta hizi ni chakula kizuri kwa bakteria waliopo mdodomoni. Bakteria wanapokula kuta hii husababisha kuzalisha kwa tindikali na harufu mbaya mdomoni.

Midomo kukauka
Mate husaidia kuosha mdomo dhidi ya mabaki ya chakua na harufu, endapo mtu ana midomo iliyokauka kwa kukosa unyevu wake atapata harufu mbaya kinywani. Midomo kukauka hutokea sana wakati wa usiku kama asili ya maumbile ya binadamu na hivyo mtu kuamka na harufu mbaya kinywani wakati wa asubuhi. Tatizo la harufu mbaya kinywaji huzidi endapo mtu amelala kinywa kikiwa wazi.

Baadhi ya dawa
Dawa zinazokausha mate husababisha kinywa kutoa harufu kama yalivyo maelezo ya hapo juu. Baadhi ya dwa pia huwa na kemikali ambazo zikivunywa kinywani au tumboni husababisha mtu kuwa na harufu mbaya kinywani.

Maambukizi ya kinywa
Mtu akiwa na maambukizi kinywani huweza kutoa harufu mbaya. Maambukizi haya yanaweza kuwa kwenye vidonda vinavyotokana na upasuaji, kutolea jino, kuoza kwa meno au magonjwa mengine ya kinywa na meno.

Magonjwa mengine ya kinywa, koo na pua kama tonsil n,k
Saratani, magonjwa ya kimetabliki na tatizo la kiungulia huweza kusabaisha kinywa kutoa harufu kali, watoto wadogo wanaweza kutoa harufu kali kinywani kutokana na vipande vya chakula kubaki kinywani.

Mara nyingi mtu anaweza kuimarisha afya ya kinywa chake kwa kuzingatia usafi wa kinywa
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII:
- Namna ya kuondoa harufu mbaya mdomoni kwa kutumia baking soda - Tofauti
 
Tatizo la harufu mbaya mdomoni

Chanzo cha harufu mbaya mdomoni

Harufu mbaya mdomoni inachagizwa na mambo kadhaa ikiwamo tabia zetu za kila siku na maradhi ya meno.Wakati mwingine jambo hili laweza kukufanya ushindwe kujiamini wakati wa kuzungumza na watu.

Lakini pia laweza kuwafanya wanaokuzunguka wakushushe thamani wakidhani wewe ni mchafu...na kumbe una maradhi.

Tatizo la kunuka mdomo linawapata baadhi ya watu, ambao hata wakipiga mswaki, lakini bado ananuka mdomo hata pale anapotumia vitu vya kuufanya mdomo unukie vizuri kama ‘Chewing gum’ pipi hususan pipi-kifua na hata Big G bado mtu mwenye tatizo hilo ataendelea kuwa na harufu mbaya.

Wanasayansi wamekiri kwamba ni vigumu sana mtu kufahamu kuwa ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea lakini ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine.

Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini na pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.

Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama ‘Halimeter’, ‘Gas’ ‘Chromatography ‘na ‘BANA Test.

Daktari wa Kinywa wa Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, Gillberth Lema anasema:“Magonjwa ya kinywa yanasababishwa na mabaki ya chakula kwa kuwa mwili wa binadamu una vijidudu aina ya bacteria ambao kwa kitaalamu huitwa ‘normal flora’.

Wadudu hao mara wanapokula hutoa tindikali ambayo husababisha magonjwa ya fizi na kinywa.

attachment.php

Dk. Lema akimtibu mgonjwa wa meno katika kliniki yake.

Vitu vyenye sukari ikiwemo sukari ya kawaida pia huchochea tatizo hili, lakini mpangilio wa meno katika kinywa huhifadhi mabaki na kuleta harufu mbaya,”

Anaeleza kuwa tatizo hili pia huchangiwa na vijidudu vya ‘bacteria’ wanaojificha kati ya jino na jino na wengine kama ana jino lililotoboka vijidudu hivi hutumia nafasi ya kujificha humo.

Lakini wale ambao wana tabia ya kulala mdomo wazi, tabaka la juu la ngozi ya mdomo huoza na kutoa harufu mbaya.

Unywaji Pombe:

Unywaji wa pombe husababisha kiwango cha kabohaidreti kubaki mdomoni na kuoza hivyo kusababisha magonjwa ya fizi.

Chanzo kingine kikuu cha harufu mbaya ya kinywa ni pale ambapo chakula kingi kinabaki mdomoni hasa hasa nyama.

Utumiaji wa chakula chochote kitakachokaa ndani ya mfumo wa usagaji wa chakula kwa muda mrefu kitaanza kuoza, na siku zote nyama inapooza huanza kutoa harufu mbaya ( kunuka ).

Kwa hiyo hiki nacho ni chanzo kikubwa cha harufu mbaya ya kinywa.

Chanzo:Mwananchi

Jinsi ya kujikinga na kuondoa harufu mbaya mdomoni

Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii.

Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.

Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:

Kupiga mswaki

attachment.php


Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.

Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo.

Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.

Kunywa maji mengi

attachment.php


Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo.

Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani.

Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu.

Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.

Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.

Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka au ‘chewing gum‘ yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.

Mwisho, hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.

Chanzo:GPL
 
XP,

This is a great piece of info. I wish people knew where they stand and how embarrassing is it to have bad breath. But one thing which surprises me (according to my observation), halitosis seems to involve more men than women??

Most of people ambao wananuka midomo, hawajijui kama wananuka midomo. Na wanakuwa waongeaji sana.
 
Nenda Mansoor daya pharmacy pale IPS waaulizie watakupa dawa nzuri sana mimi siikumbuki kwa jina maana best yangu alikuwa na tatizo hilo hilo alipoelekezwa hapo akanunua mpasa sasa nakwambia hata asipopiga mswaki hanuki mdomo.
 
Nashkuru pastor. Ila nikusumbue kidogo. Hebu nielekeze zaidi jinsi ya kufika hapo phamacy, na-assume ni hapahapa Dar.

Mwisho kabisa; Kwa hiyo jamaa ako ali2mia mara 1 au ni ki2 cha ku2mia once in a life tyme.

Thanx in advance!
 
Tripo9 Ni hapo hapo Dar ukifika Samora mnara wa Askari kama unatokea Posta Mpya Jengo lipo upande wa kushoto hapo hapo around about ukifika hapo sema shida yako kuna dokta mmoja sikumbuki jina Muhindi atakuuliza maswali inakuwaje kisha kama ipo atakupa kama imeisha atakwambia njoo kesho wanachanganya hapo hapo.

Na jamaa alipona kwa Wiki mbili tu kisha hata leo akiamka asubuhi asipopiga mswaki sawa tu kwani hapo zamani alikuwa anapiga mara tano hata sita kwani anaweka mswaki kwenye gari lake.

Pole sana ukipotea sema, kwani hapa natafuta namba ya huyo dr. alitupaga sasa nikipata naweka hapa, ok
.
 
Ndugu, go see a dentist, you probably have gum disease. Also you need to floss, it's one of the best prevention for dental diseases. Most of us just brush our teeth but, flossing is very important too, at leas once a day and the best time is at night before you go to bed after brushing your teeth....word is flossing increases longevity.
 
Dawa ya kutibu Mdomo kutowa Harufu mbaya

1.Tangawizi ya unga fresh
2.Pilipili manga ya unga
3.chumvi.

Vyote fanya kiasi uchanganyishe viwe pamoja tena utafanya wewe mwenyewe kiasi tia katika chupa uwe kila mara unasugulia kwa kidole au unaweza ukanunua msuaki ukauweka kwa kupigia hiyo tangawizi jaribu na inshallah m/mungu atakusaidia ok hata ikiwa meno yako yanatoka damu hii dawa inasaidia.
 
Rafiki yangu alinieleza kuwa kinywa chake huwa kinatoa harufu licha ya kupiga mswaki kwa whitedent kila asubuhi na jioni anapoenda kulala; hii hali inamkela sana hasa akiwa na dem wake ndani 6 x 6 demu huwa anaangalia pembeni kwa kukwepa harufu.
Karibuni
 
rafiki yangu alinieleza kuwa kinywa chake huwa kinatoa harufu licha ya kupiga mswaki kwa whitedent kila asubuhi na jioni anapoenda kulala; hii hali inamkela sana hasa akiwa na dem wake ndani 6 x 6 demu huwa anaangalia pembeni kwa kukwepa harufu.
Karibuni

Mwambie atumie quality toothbrush na toothpaste, asukutue meno in a circular motions,asugue ulimi haswa kwani ndio huwa chanzo cha harufu. Pia narecomend atumie listerine mouthwash twice a day after brushing.

Hope it will help. Ani update akiona changes au la ili nimpe mbinu zingine.
 
Rafiki yangu alinieleza kuwa kinywa chake huwa kinatoa harufu licha ya kupiga mswaki kwa whitedent kila asubuhi na jioni anapoenda kulala; hii hali inamkela sana hasa akiwa na dem wake ndani 6 x 6 demu huwa anaangalia pembeni kwa kukwepa harufu.
Karibuni

Kichwa Ngumu,

Wewe ni mlalamishi, unapenda kulonga tu,
Kila siku unakuja na tatizo kwa JF doctor halafu ukishakupewa ushauri unapotea bila ya kurudi na kutoa feedback!!

Ok, umepata ushauri hapo juu, mwambie rafiki yako autumie huo, halafu akutaarifu mafanikio yake! Pia tunakutegemea urudi hapa utoe feedback. Huenda ukawasaidia na wengine wenye tatizo ambalo lilitolewa ushauri.
 
Tatizo hilo kitaalamu linaitwa Halitosis na husabababishwa na sababu nyingi zinazoambatana si tu na meno bali pia ufizi. Ikumbukwe pia kuwa upigaji mswaki unaweza kuchangia kwa namna moja au nyingine.

Kwa ushauri wa haraka nikngekushauri utumie dawa aina ya sensodyne, piga mswaki kila unapomaliza kula, tumia mouth wash ikibidi. Kuna kitu kama nyuzi maalumu kinaitwa dental floss hiki ni kizuri sana kwani kinapenya kati ya meno ambapo mswaki hauwezi kuingia. Kama utafanikiwa kupata(bei rahisi tu) tumia kila mara kuondoa vyakula kati ya meno.

Angalia aina ya mswaki unaotumia kama ni hard brush au soft. Hard inaweza kuwa inaumiza ufizi na soft yaweza kuwa haifanyi kazi kama inavyotarajiwa. Kwa mantiki hii ni mganga wa meno anaweza kukupa jibu sahihi la tatizo lako.

Wakati ukisubiri kumuona unaweza kutumia buble gum(zisizo na sukari) kuondoa harufu hiyo.

Hata hivyo ni muhimu sana umuone daktari wa meno kwani anaweza kujua undani na ukubwa wa tatizo.
 
mwambie atumie quality toothbrush na toothpaste, asukutue meno in a circular motions,asugue ulimi haswa kwani ndo huwa chanzo cha harufu. Pia narecomend atumie listerine mouthwash twice a day after brushing.

Hope it will help. Ani update akiona changes au la ili nimpe mbinu zingine.
Mkuu wengine ni mataizo ya meno kuoza au machafu zaidi ya mswaki, mfumo wa chakula au wa hewa pamoja mswaki, si vibaya pia kumuona dentist.
 
Asali inatibu Maradhi mengi sana.

Kinywa kutoa harufu mbaya Mdomo Mtu mwenye huo Ugonjwa atachukuwa Asali Safi ya nyuki iliyo mbichi haijapikwa, Asali vijiko 2 aikoroge katika maji.

na ayachemshe katika moto mdogo mpaka yatoe moshi na avute puani moshi huo mdomoni kupitia kwenye paipu ya (bomba) iliyofungwa vizuri juu ya chombo.

Tiba hii atakuwa akiendelea nayo pamoja na kutafuna nta ya asali. Harufu mbaya ya Mdomoni itaondoka kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom