Jinsi gani uliweza kukabiliana na Tapeli aliyekudhulumu fedha au mali zako na ukafanikiwa kuzirudisha?

Nashukuru mkuu,
Imekuwa ni kama jambo la kawaida watu wanatutapeli nakupotea na pesa zetu,

Kwenda polisi na muda wa kufiatilia ni mdogo,

Unampigiq mtu simu kwa ujeuri hapokei kabisa au anaamuwa kuku block kabisa

Wakati mwingjne kinachouma sio deni ila ni dharau kutoka kwa tapeli anakuona kama zoba mjinga fulani hivi
Aisee pole
 
Nilikodisha eneo la chama cha mapinduzi mtaa wa mjini, kuja kutahamaki miezi3 tayari na sijaruhusiwa kufanya biashara. Jamaa kila siku wananipa kalenda mara mwenyekiti kasafiri kafiwa anaumwa kumbe lile eneo tumekodishwa watu wengi tu wazee wanakula hela. Nilichokifanya nilimtumia sms nyepesi tu mwenyekiti kwamba in 3days jambo langu litakua kwa Mange kimambi.
Nililipwa kesho yake
...Kumbe ndio Wanavyofanya! Kweli CCM Ina wenyewe?
 
Kwanini usisamehe tu maisha yaendelee?

Kama mazingira ya kumshughulikia huyo tapeli kisheria hayaruhusu, move on! Wakati mwingine, kuwa makini ili kutojiingiza katika mazingira ya kutapeliwa tena.

Unataka kulipa kisasi?

OK! "Kabla hujalipa kisasi, kwanza hakikisha unachimba makaburi mawili!"
Umeongea vyema sana.
Kujitahidi kusamehe ni jambo zuri.

Kulipa kisasi ni kuhamishia deni la kudumu moyoni mwako.

Moyo ma nafsi vitakushtaki na kukusumbua daima.

Mimi kwangu kisasi hapana.
 
Back
Top Bottom