Christiba
Member
- May 27, 2020
- 24
- 32
Kipindi ambacho mtoto ujifunza KUWA sauti/neno analolisikia mara kwa mara kutoka kwa wazazi wake ni jina lake, mtoto uanza kujilinganisha yeye na neno hilo, ambalo huja kuwa wazo kwenye fikra zake kuwa yeye ni hilo neno nakuwa neno hilo linamuwakilisha 100% hakika. kipindi hicho ndipo binadamu upata utambuzi feki kuwa wao ni kina nani hapa binadamu ujitambua kwa jina lake na kuwa jina hilo ni yeye 100%, kwa kuwa mtoto huwa bado ajapotea moja kwa moja kwenye utu wa jina au neno hilo kuna kesi za watoto kutumia majina yao au neno analoitwa sana kwa kuliweka kwenye mfumo wa nafsi ya tatu kujimaanisha yeye mwenyewe mfano kama jina lake ni James atasema, " James ananjaa" au mtoto ananjaa. Hii inaonesha kwamba anaemuongelea James ni utu mkubwa ulio ndani ya mtoto na James ni utu mdogo wa nje wenye mahitaji ya kimwili. Hapa jina James utumiwa na mtoto kuelezea hali, matakwa na uhitaji unaohusu utu wake wa nje mdogo ambao sio yeye halisi.
Baadaye mtoto ujifunza neno moja la ajabu sana ambalo awali linaanza kama neno masikioni mwake kisha uingia kwenye mchakato wa ubongo kama wazo ambalo matunda yake hubadili fikra za mtoto na utu wake kiujumla, kisha uanza kulitumia neno hilo kujiwakilisha au kuurejelea utu wake neno hilo ni " nina". Neno hilo ulitumia kwa ulinganifu wa jina lake mfano; James ambalo awali alilinganisha Jina hilo na yeye mwenyewe. Hapa mtoto uacha kutumia jina kuurejelea utu wake wa nje na uanza kutumia neno "nina", kwenye fikra zake akidhani yeye ni "nina", mfano hapa ataanza kusema "ninanjaa". Neno "nina" hubadilisha taswira nzima ya fikra ya mtoto na kwa haraka udhoofisha ule utu mkubwa wa ndani na uupa utu mdogo wenye mahitaji ya kimwili nguvu na utawala wa hisia ya kujitambua kwake. Neno mbalo mtoto alielewa kimakosa kuwa ndio yeye halisi linakuja kuchepua maneno mengine kama yangu, changu na vyangu ambayo yanakuja kuwa sehemu ya "nina". Maneno hayo yanakuja kuwakilisha vitu ambavyo moja kwa moja vitakuwa sehemu ya "nina" au sehemu ya utu wa kimakosa, utu huo unaanza kujitambulisha na vitu, usishangae mtoto akiwa analia akisema "nimepoteza mdoli ^wangu^", inamaana kapoteza sehemu ya utu wake ndio maana analia.
Mpaka unaona neno nina linajitanua na kujitambulisha kuwa yeye ndie mtu halisi, ukubwani linakuja kuzaa utambulisho mbali mbali kama; Taifa langu, dini yangu, ninapenda hiki, sikipendi kile, stori yangu, mali zangu na watoto wangu. Kumbuka nina lilianza kama neno ambalo likaja kuwa wazo kwenye fikra ya mtu, nina ni wazo tu wala sio wewe halisi mtoto mara anapozaliwa si ni mtu sio? Mtoto huanza kuzaliwa kabla ya nina kwahiyo ni wazi mtu anaanza kabla ya neno "nina".
"Nina" ni mental construct imetengenezwa na ubongo tu ni wazo lako tu sio Mungu aliekuumba uje kuwa "nina", "yangu", "changu", "vyangu" na "wangu". Yesu alijua hilo aliposema ukitaka kuona kunifuata ujikane nafsi ("nina") yako yaani kuacha kuishi kwenye maisha yasio halisi maisha ya starehe "yangu", mali "zangu" na gari langu na kumfuata. Yesu aliposema ni vigumu tajiri kuuona ufalme wa Mungu alimaanisha matajiri wamezama kwenye utambulisho huu fake wa utu na ni vigumu wao kuishi maisha yao halisi ambayo hayana maneno yangu na changu, langu na vyangu ambayo msingi wake ni neno "nina"ni vigumu kwa wao kuishi maisha yao ya ndani ambayo hayana muunganiko na umiliki wa vitu, utu usio na muunganiko na mali ambao huo uonesha utukufu wa Mungu ndani yetu.
Wewe sio neno nina, wewe sio huyu wa nje, wewe sio hizo mali, wewe sio hiyo furaha feki ya nje, wewe sio hiyo huzuni ya utu nina, wewe umefichwa na neno nina, wewe upo ndani sana nyuma ya huu utu wa nina.
Kwa kumalizia.
• Tunaona unapouhusianisha neno au wazo kwenye ubongo na utu wake ndivyo unavyokimbia uhalisia, ubongo umeonganisha utu na neno "nina" matokeo yake umeleta ubinafsi na kutokujitambua sisi ni akina nani.
• Neno nina limebadilisha maana halisi ya upendo, furaha, na huzuni kwa kuwa tunaishi kwenye utu fake basi hata furaha na upendo baina yetu ni fake, kwa mfano, kama nyumba zinavunjwa kwenye mtaa wako bahati nzuri yako isipovunjwa utafurahi si ndio? Utasema nashukuru Mungu nyumba "yangu" haikuvunjwa. Jiulize ulipaswa ufurahie jambo hilo?
• Je sisi si zaidi ya lile neno "nina" ambalo ndio chanzo cha yangu, vyangu na changu. Maneno yanaundwa na irabu tano tu a, e, i, o na u, je sisi si zaidi ya a, e, i, o na u? Tujitafute leo sisi ni kina nani na inabidi tuishije hapa duniani.