Jinsi gani teamwork inaweza saidia kupunguza makali ya ukata wa ajira kwa wasomi wetu

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
400
1,000
Mimi ni muumini wa msemo usemao Tanzania kazi ni nyingi sana ila ushirikiano ndio mdogo sana.

Kuna watu wanajua sana kuandaa proposal mpaka wakapewa kazi fulani ila ile kazi hawaiwezi. Kuna wale wanaojua kazi mwanzo mwisho ila kuandaa proposal yenye ushawishi hawawezi.

Changamoto kubwa kuwaunganisha hawa watu wawili. Kila mmoja anapambania upande wake. Nina hakika kama Watanzania wangekuwa na teamwork kama Wachina basi kuna mambo mengi yangepata ufumbuzi na suala la ukata wa ajira lingepungua makali.

Hata asilimia kubwa ya kampuni nyingi changa za teknolojia nchini China na India zimeasisiwa na umoja wa vijana kadhaa walioamua kuunganisha nguvu zao na uwezo wao katika kukabiliana na changamoto ya ukata wa ajira.
 

Bf Tulinagwe

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
211
500
Aaah watz bhn kuwaunganisha pa1 ni mtihani... most ov us hatuna uaminifu.. kutapeliana ndo fashen kwe2,, tutafanya vp kaz pa1 kila mmoja anawaza kumpiga mwenzake,,??
 

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
400
1,000
Wenye ngozi nyeupe ndo wapigaji zaidi. Umesahau walitutageuza makoloni ili wapige maliasili zetu? Unasahau wanachimba madini mpaka sasa kinyemela nyemela katika mataifa ya watu weusi? Kikubwa ni kuwa makini usiruhusu kupigwa.

Utapeli wa mtu mmoja mmoja upo dunia nzima. Nadhani cha msingi ni kujenga ari ya umoja bila kuogopa changamoto zitakazojitokeza.

Aaah watz bhn kuwaunganisha pa1 ni mtihani... most ov us hatuna uaminifu.. kutapeliana ndo fashen kwe2,, tutafanya vp kaz pa1 kila mmoja anawaza kumpiga mwenzake,,??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom