Jinsi gani nitapata namba ya NIDA?

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,955
6,885
Habari za muda huu ndugu, Kaka,Dada na wengineo wengi mliomo humu JF.

Ni jinsi gani naweza kupata namba ya NIDA au kitambulisho Cha taifa ikiwa wazazi wangu hawajajiandikisha NIDA Wala hawana vitambulisho Wala vyeti vya kuzaliwa na hawatilii maanani.

Kwa mnaojua utaratibu Ni lazima niwe na copy ya vitambulisho vyao

Naombeni ushauri maana namba ya NIDA Ina umuhimu mkubwa kwangu.
 
Kama we mtanzania wa kuzaliwa utapata tu

Mbona watoto wa sahvi mnashindwa kujiongeza

Kwenye mambo wa wakadhawakadha

Ova
 
Kwanza wao walijiandikisha?

Unafahamu majina yao halisi yote matatu pamoja na majina ya babu zako?

Inawezekana kupata namba zao za NIDA bila kuwaomba wao.

Karibu
 
Maelezo kibao halafu pointless
Sasa mkuu kwani nimetaka kutoa point au kutafuta utatuzi? Sipendi shobo ujue Kama we hujui jinsi ya kushauri mtu tafadhali acha kuropoka kwa sababu unajua kuandika ...Nimeuliza nikujua huku watu mnajitambua sijategemea kupata comment ya kipuuzi Kama yako shame on you
 
Kwanza wao walijiandikisha?

Unafahamu majina yao halisi yote matatu pamoja na majina ya babu zako?

Inawezekana kupata namba zao za NIDA bila kuwaomba wao.

Karibu
Hawajajisali
 
Sasa mkuu kwani nimetaka kutoa point au kutafuta utatuzi? Sipendi shobo ujue Kama we hujui jinsi ya kushauri mtu tafadhali acha kuropoka kwa sababu unajua kuandika ...Nimeuliza nikujua huku watu mnajitambua sijategemea kupata comment ya kipuuzi Kama yako shame on you
Sawa boss
 
Kama we mtanzania wa kuzaliwa utapata tu

Mbona watoto wa sahvi mnashindwa kujiongeza

Kwenye mambo wa wakadhawakadha

Ova
Napataje mkuu??? Nishaenda Office zao Mara 3 Ila bila kitambulisho Cha mzazi Cha NIDA au cheti Cha kuzaliwa wananiambia haiwezekani, Mimi cheti changu ninacho
 
Napataje mkuu??? Nishaenda Office zao Mara 3 Ila bila kitambulisho Cha mzazi Cha NIDA au cheti Cha kuzaliwa wananiambia haiwezekani, Mimi cheti changu ninacho
Kama we cheti cha kuzaliwa unacho
Na wazazi wapo na ni watanzania kwanini
Usiwatengeneze avidavity,ukipata hizo document uwapeleke uanze taratibu

Ova
 
Kama we cheti cha kuzaliwa unacho
Na wazazi wapo na ni watanzania kwanini
Usiwatengeneze avidavity,ukipata hizo document uwapeleke uanze taratibu

Ova
Sijaelewa avidavity Nini mkuu, Naomba nieleweshe
 
Hati ya kiapo
Wazazi wako si hawana vyeti vya kuzaliwa
Kuonesha kma wamezaliwa tz

Ova
Kipindi najiandikisha sikutoa vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wala cha kwangu. Na wazazi hawakuwahi kuwa na kitambulisho kipindi hicho...nilijaza tu details zilizohitajika .
Utaratibu ulikuja kubadilika?
 
Kipindi najiandikisha sikutoa vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wala cha kwangu. Na wazazi hawakuwahi na kitambulisho kipindi hicho...nilijaza tu details zilizohitajika .
Utaratibu ulikuja kubadili?
Zoezi likiwa mwanzoni ukifanya kuna kuwaga hakuna miyeyusho....

Ova
 
Back
Top Bottom