Jinsi gani ''magulio'' yanavyoweza kutatua tatizo la wamachinga.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi gani ''magulio'' yanavyoweza kutatua tatizo la wamachinga....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by paesulta, Mar 9, 2011.

 1. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Magulio pia yangeweza kutumika kuondoa tatizo la wamachinga.Kila manispaa/halmashauri,ingeweza kupanga ratiba yake kwa wiki,ambapo itatenga maeneo mbalimbali ndani ya manispaa/halmashauri mabapo wamachinga pamoja na wafanyabiashara wengine wadogowadogo,wanakutana katika eneo lilotengwa katika neighborhood fulani,sema Kimara,Manzese,Mwenge,Ubungo n.k,n.k,ambapo kila neighborhood watakutana katika siku maalum yqa wiki,sema j/tatu wanakuwa Ubungo,j/nne Manzese n.k,na hii inakuwa ni ratiba ya kudumu hivyo wananchi wanajua kuwa leo j/tatu gulio litakuwa hapa,na j/nne litakuwa pale,n.k.Kwa namna hii unafanikiwa kuwaorganise wamachinga pamoja na wafanya biashara wengine wadogo wadogo,na inawezekana kwa Manispaa/Halamashauri,kukusnya mapato kwa njia ya ushuru.

  Hili litapunguza tatizo la wamachinga kuzagaa mijini,machinga wanapata soko la kuaminika na vilevile daladala zinapata kazi kuwapeleka na kuwarudisha wafanyabiashara na biadhazao,na pia wateja,bial kusahau kuwa eneo ambalo litakuwa linafanyika gulio hili,kuatakuwa na improvment,kwani watu wenye maduka nao wataweza kufaidika kwa kuuza bidhaa zao kama soda,mikate n.k ili kuwahudumia wamachinga pamoja na ateja watakaofika hapo.

  Maeneo ambayo yanapendekezwa ni maeneo ya wazi,na kama haya hakuna,basi katika baranara fulani moja,inachaguliwa ili itumike,na inafungwa kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa nane/tisa mchana.

  Kinachohitajika ni organisation tu,na yote yanawezekana.Tunaweza kutatua matatizo fulani fulani kwa solution za kirahisi kabisa....
  Naomba kuwakilisha....
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nitarudi kumalizia kusoma badae!!

  ila jitahidi uwekepo japo vi-paragraph vidogo vidogo!!
   
 3. n

  ntobistan Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good boy good idea.But u're based on the same place Dar es salaam only so what about another reginal such az Moro,Dom,Sind,Tang,Mza.Wao kwao si mhimu kwa hawa wamaching kuw na magulio?
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Wazo zuri. Lakini kuna ugumu wa kuwakusanya wamachinga wote (na wafanyabiashara wengine) wa Dar kwenye eneo moja. Ni wengi mno. Pili unahitaji kuwekeza kwenye miundombinu kwanza, i.e. vyoo, shelters, huduma ya kwanza, maegesho ya magari, n.k. Pia kuna wakati wa mvua na jua kali. Wafanyabiashara na wateja wao wote watapata shida. Ni mojawapo ya majawabu lakini si jawabu pekee.
   
 5. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nadhani swala si kuwakusnya wamachinga wote wa Dar,sema.Idea ni kuwa kila manispaa itakuwa na ratiba yake tofauti,kwa maana kwamba kwa mfano Kinondoni wanakuwa na ratiba kuanzia J/tatu mpk J/pili,na wakati huo huo manispaa nyingine pia inakuwa na ratiba kama hiyo.Kwa mtindo huu,si kwamba wamachinga wote watakuja kwenye gulio la kinondoni,bali wengine watakwenda Ilaa au Temeke,maana yatakuwa yanafanyika kwa wakati mmojaq,hivyo unaepuka kuwakusnya wote mahali pamoja.

  Kuhusu swala la miundo mbinu,kwa sababu gulio hili si lakudumu,basi vitu kama vyoo,vinaweza kutumika vile mobile chemical toilets.Kumbuka kwamba idea ni kuwa gulio halitafanyika katika sehemu moja,bali litakuwa lina-rotate.Kwa mfano katika ratiba ya Manispaa ya Kinondoni,J/tatu litakuwa Ubungo J/ne Kimara,J/tano Mwenge nk.Hivyo hivyo itakuwa pia katika ratiba ya manispaa nyingine.Siku ambazo maeneo hayo hayana ratiba ya gulio,basi shughuli za kila siku ambazo zilikuwa zikifanyika katika mamaeneo hayo,zinaendelea kama kawaida.

  Nimechukulia mfano wa Dar kwani ndipo ambapo nadhani naweza kuonyesha kwa mifano,lakini hili linaweza kutekelezwa katika miji mingine pia kama Mwanza,Arusha<Tanga n.k......
   
 6. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sorry Mkuu,natumia mobile ndo maana imenitatiza kidogo kuweka paragrafs.....hope msg imepatikana though....?
   
Loading...