SoC03 Jinsi Fursa nchini Burundi zinazoweza kubadili maisha na kuongeza kipato chako

Stories of Change - 2023 Competition

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
UTANGULIZI

Habari za muda huu wanajamvi,Kila mtu anahistoria yake katika safari ya utafutaji wa riziki,Wapo wenye historia za kusikitisha,kufurahisha na kuelimisha.

Mwaka 2019 wakati dunia imekumbwa na mlipuko wa uviko 19,Na kupelekea kazi,Masomo na Shughuli mbalimbali kusimama.Nilipata bahati ya kutembelea Nchini Burundi kwa gari ya mizigo 'Semi' ambayo moja ya gari hizo ilikua ikiendeshwa na Kaka yangu ambae ndio alinishawishi kuungana nae kwenye safari hiyo.

Njiani tulikutana na changamoto kama ambavyo safari zilivyo,hasa pale mpakani kwakuwa mimi nilikua sina passport rasmi nilikatiwa 'Emergency getpass' Na hata waliokuwa na passport walisumbuliwa kwani inabidi ioneshe vipimo vya Cholera,Typhoid na Covid-19 vyote viwe negative.Tulikaa zaidi ya masaa 9 mpakani ndipo walituruhusu kupita na Safari ikaendelea.

Tuliingia Burundi nchi iliyojaa miinuko na mabonde mpaka kufikia mkoa mmoja unaitwa Rumonge.Wakati wote wa Safari nilikua naumiza kichwa kuangalia fursa zinazopatikana nchini humo,Baadae tulikutana na mwenyeji wetu katika kumuuliza maswali ya kiudadisi ndio akanieleza Fursa mbalimbali zinazopatikana nchini humo.

Baada ya kuchambua Fursa mbalimbali.Niliangukia kwenye Parachichi maarufu kama 'Avoca' huko kwao ambapo lengo ni kununua huko na kuzileta/kuziuzai Tanzania.kama nilivyoshauriwa na mwenyeji.Niliongea na Kaka ambae ndio dereva nikamueleza akaniahidi kuniunga mkono.(picha na peasantfarm.en)
20230510_231135.png

Basi nilitafuta namna nikakopa mtaji nikapata kama Milioni 1.5 Tsh Ambayo ukibadili kwa faranga ni kama Milioni 2.9franc,Tukapelekwa kwenye Shamba la miti kuna aina mbalimbali ya matunda.Tukapewa maelezo muhimu na wakulima namna ya kutunza parachichi kwa muda mrefu na mambo mengine muhimu.
20230510_231112.jpg

Safari ya kurudi TZ ikaanza rrasmi wakati huo njiani nilikuwa na mashaka kama tutapata wateja pia sijawahi kufanya biashara ya namna yoyote.Na Licha ya hayo,Najua maeneo kama Moshi,Kagera,Mbeya parachichi zinauzwa bei rahisi sana,nikapiga moyo konde.Tulivyofika TZ tuliuza mzigo Sokoni maeneo mbalimbali nchini kuanzia Kahama,Mwanza,Tabora,Dodoma,Morogoro na Dar.Mwisho wa siku tulijikuta tumeingiza kama Milioni 8.Baada ya kulipa madeni ya Fuso za usafirishaji niliambulia kama 3M ambayo nayo iliishia kulipa madeni na Ada chuoni.(Picha na skyfarm.sn)
20230510_231109.jpg

Nilitamani kurudi lakini ilishindikana hasa wazazi awakuwa tayari kukubali niache masomo hivyo nilijikuta kwenye mgogoro mzito mwisho nikakubali kuendelea na masomo.Lakini baadae nilirudi Burundi kwa project nyingine tofauti na hii.

Sasa katika Fursa nilizoziona,nimejaribu kuchambua zile Top 10 zinazopatikanq nchini humo ambazo kama kijana uko tayari unaweza kufata utaratibu kupata passport na kuingia nchini humo kutafuta Ajira/Fursa mbalimbali.


Fursa zilizopo ni pamoja na:
1.MBAO

kama nilivyotangulia kusema vitu ni bei rahisi na nchi inamisitu mingi hivyo mbao zipo nyingi na bei chee unaweza kutoa huko kuleta TZ na kuuza au kutumia

2.GESI YA KUPIKIA
Bado sana biashara ya gesi ni changa mno kama utaweza kuwaletea mitungi ya orxy utapiga sana pesa

3.GEREJI
Licha ya kuwa magari ni mengi lakini gereji sio nyingi kama TZ ambapovmtaa mmoja hatua saba gereji,Hii inachangiwa na gharama za spea kuwa juu zaidi

4.VITENGE&BATIKI
Hapa wakongo wanapiga sana pesa mjini kwa kuuza vitenge na batiki

5.KUFUNDISHA ENGLISH
Lugha kuu ni kirundi na French ila mwaka jana serikali yao imesisitiza English ifundishwe mashuleni hivyo kupelekea uhaba mkubwa wa walimu wa English kama uko vizuri na kadegree kako ingia fasta ujaribu

6.KUFUNDISHA KISWAHILI.
Shule za burundi zinahitaji sana walimu wa kiswaili kwakuwa ni lugha inayofundishwa shuleni(Somo).

7.NGUO
Kuna uhaba wa nguo kali za kike hasa zilizo on chart kwenye fashion.Ukipata uwezo wa kutoa nguo TZ nzuri kuleta huku hasa bujumbura utapiga pesa

8.MAZAO YA CHAKULA.
Pamoja na kwamba nchini Burundi wanategemea kilimo,Lakini kilimo nao kinawapa mgongo kwakuwa nchi inamiinuko,Mazao na chakula kama mchele,Unga wanahitaji sana na wanategemea kutoka TZ,Kilo ya mchele kule ni 6500/= franc.Kwa walima mpunga kama unaweza safirisha mazao yako lazima utauza tu.

9.UUZAJI CD ZA KUTAFSIRIWA.
Hapa nimeona hii ni fursa kwasababu warundi wengi wanaangalia CD za kina DJ mafia na dj Mark,Katika uchunguzi niliofanya nikauliza wachoma CD walidai changamoto ni kwamba zinachelewa kuwafikia tu ila zinapendwa na zinauzika sana tu.

10.MASHUKA NA PAZIA
Kwasababu wanapenda sana Shuka hivyo kama utaweza kuwapelekea shuka na pazia utakua umefanya jambo la maana vilevile pazia.

Hizi ni fursa chache katika nyingi zilizopo nchini humo,Nashauri kama kijana tenga bajeti ndogo tu utembelee nchi hii ya Burundi,Ni nchi inayoendelea lakini ipo nyuma kimaendeleo.Kama utachanga karata zako vizuri uwezi kukosa Fursa hasa Walimu wa Kiswahili wanahitajika sana watanzania na mpaja vyuoni kinafundishwa kozi zote hata MD,Law,Engineer wanafundishwa somo la Kiswahili.

Kingereza pia,hapa wakenya wameteka soko,Vyuo na Shule nyingi nchini Burundi zimeajiri wakenya kama Walimu wa Kiingereza.

Mambo Niliyojifunza
~Elimu ni kitu muhimu sana.

Nilipofika Nchini humo haikuchukua muda kukumbuka Ramani ya geography inayoonesha lilipopita Bonde la Ufa(Rift Valley) Na pia haikuchukua muda kukumbuka historia ya nchini humo,Wakoloni,Vita vya kikabila vya wenyewe kwa wenyewe(Civil warz) na mambo mengi tuliyosoma huko nyuma.

~Muhimu sana kuwa na Jicho la tatu.
Jicho la kuona fursa,Haijalishi unapitia changamoto gani,au una kilema,Angalia kila kitu kama Fursa tu uwezi kukosa kitu cha kufanya.

~TEMBEA/SAFARI
Usikae idle nyumbani wanasema "An Idle mind is a devil's workshop" ukikaa mpweke akili haichangamki,Jichanganye mtaani,Hata nchi jirani hizi za EAC na SADC ni rahisi kuingia ukiwa na passport safi kabisa,unaingia na kutafta fursa.(Mtembea bure si sawa na mkaa burs) wahenga walisema.

Natanguliza Shukran.

NB
:Nimekuwa najitahidi kujibu PM ila naomba kama unajambo au swali lolote uliza hapahapa public nipo mstari wa mbele kutoa support na kujibu chochote na kwa mnaoomba namba tusameheane kidogo sitatoa namba ila Uliza chochote hapahapa natoa ushirikiano kwa asilimia zote 100%

Baada ya kusoma bandiko hili naomba upige kura kwa kubofya kitufe kilichoandikwa vote.


AHSANTE
,
 
Aloo hongera dogo hizi ndo nyuzi sasa naomba kujua baadhi ya mambo
1.Ilikuchukua mda gani kukamilisha mzigo
2.Wanaongea luga gani huko
3.Lazima niwe na passport au visa?
4.Vipi usalama wa mali na mazingira
5.Vipi bei ya makazi,Malazi na Chakula
6.Hakuna magonjwa ya mlipuko kama Ebola huko mkuu
Natanguliza shukrani
 
Aloo hongera dogo hizi ndo nyuzi sasa naomba kujua baadhi ya mambo
1.Ilikuchukua mda gani kukamilisha mzigo
2.Wanaongea luga gani huko
3.Lazima niwe na passport au visa?
4.Vipi usalama wa mali na mazingira
5.Vipi bei ya makazi,Malazi na Chakula
6.Hakuna magonjwa ya mlipuko kama Ebola huko mkuu
Natanguliza shukrani
Asante Kwa kulizia swala la passport na visa
 
Vipi kuhusi Visa hawasumbui?

Huo mzigo wa Avoca ulisafirisha kwa bei gani hadi kufika sokoni?
2/2
Nilijikuta ninafuraha ya ajabu ambayo sidhani kama inaweza kuelezeka mbali na hilo baada ya Vyuo kufunguliwa nilijikuta nipo kwenye vita vikali sana na wazazi na Akili yangu kwani oneside inanambia niachane na Elimu nijikite kwenye hii biashara the other side ya akili inanambia niendelee kusoma,hii ikipewa support zote na wazazi kwani waligoma kuelewa kabisaa suala la mimi kuacha chuo.

Ilikua ni wakati mgumu sana hasa kwa Mzee haikumuingia akilini kila nilipojaribu kumuelewesha hakuelewa Na hakutaka kuelewa kauli yake kubwa ilikua "Yaani uache chuo ukawe muuza parachichi sokoni?Unakichaa sio bure" wakati mwingine alihisi nimerogwa au pengine nimeanza kutumia 'mjani'.. Asee ulikuwa wakati mgumu mno baada ya kumshirikisha Bro akanambia nayeye kabadilishiwa kituo kwasasa atapeleka mzigo nchini Zambia ila Akanipa moyo kama ntakua tayari kuacha chuo nikomae na hiyo biashara inawezekana vizuri tu.penye nia pana njia na njia imeshapatikana.

Baada ya kuchanganua na kupambana na fikra nikachukua maamuzi ya kurudi chuo kishingo upande kabsa kwani nilikua nimebakiza miaka miwili kumaliza na kuamua kuachana na biashara ile ya parachichi .

Siku hazikuganda nikamaliza mambo ya chuo bila kufikiria mara mbili january tu nikarudi nchini burundi kuanza upyaa na project nyingine ambazo nitaweka jamvini panapo majaliwa siku za usoni.Sasa Kwenye ule Uzi wengi wameuliza Fursa zinazoweza kupatikana nchini burundi...Nami kwa muda nilioishi hapa burundi naweza kutaja baadhi ya Fursa nilizoziona nchini humu.

Fursa nilizoziona
1.MBAO

kama nilivyotangulia kusema vitu ni bei rahisi na nchi inamisitu mingi hivyo mbao zipo nyingi na bei chee unaweza kutoa huko kuleta TZ na kuuza au kutumia

2.GESI YA KUPIKIA
Bado sana biashara ya gesi ni changa mno kama utaweza kuwaletea mitungi ya orxy utapiga sana pesa

3.GEREJI
Licha ya kuwa magari ni mengi lakini gereji sio nyingi kama TZ ambapovmtaa mmoja hatua saba gereji,Hii inachangiwa na gharama za spea kuwa juu zaidi

4.VITENGE&BATIKI
Hapa wakongo wanapiga sana pesa mjini kwa kuuza vitenge na batiki

5.KUFUNDISHA ENGLISH
Lugha kuu ni kirundi na French ila mwaka jana serikali yao imesisitiza English ifundishwe mashuleni hivyo kupelekea uhaba mkubwa wa walimu wa English kama uko vizuri na kadegree kako ingia fasta ujaribu

6.KUFUNDISHA KISWAHILI.
Shule za burundi zinahitaji sana walimu wa kiswaili kwakuwa ni lugha inayofundishwa shuleni(Somo).

7.NGUO(Hasa za kike)
Kuna uhaba wa nguo kali za kike hasa zilizo on chart kwenye fashion.Ukipata uwezo wa kutoa nguo TZ nzuri kuleta huku hasa bujumbura utapiga pesa


8.NA KADHARIKA
Zipo nyingi tu wakuu izo ni chache ambazo kwa research yangu na vetting niliofanya hizo ndo zinaongoza...

NB
:Nimekuwa najitahidi kujibu PM ila naomba kama unajambo au swali lolote uliza hapahapa public nipo mstari wa mbele kutoa support na kujibu chochote na kwa mnaoomba # za whatsApp tusameheane kidogo sitatoa namba ila Uliza chochote hapahapa natoa ushirikiano kwa asilimia zote 100%

NAWASILISHA:
NAOMBA KURA YAKO KUINUA UZI HUU KWENYE (STORY OF CHANGE)

AHSANTE,
 
Aloo hongera dogo hizi ndo nyuzi sasa naomba kujua baadhi ya mambo
1.Ilikuchukua mda gani kukamilisha mzigo
2.Wanaongea luga gani huko
3.Lazima niwe na passport au visa?
4.Vipi usalama wa mali na mazingira
5.Vipi bei ya makazi,Malazi na Chakula
6.Hakuna magonjwa ya mlipuko kama Ebola huko mkuu
Natanguliza shukrani

Shukran Mkuu
1.Ilituchukua mda wa mwezi mzima hii inatokana na mwendo wa gari ni slow siunajua Semi zinaenda mwendo wa kobe
2.Huku ni waswahili watupu wengi wanaongea kiswazi though lugha yao ni kifaransa na kirundi
3.Ndio passport ni lazima ila unaweza kuomba Emergence Getpass kwa 20K TZ ukifika pale boda wanakupigia mhuri chap wanakuruhusu.
4.Makazi ni kawaida hotel kubwa zinajaa na hata guest zinajaa ila bei ni zilezile kutokana na quality 30k,40k mpKa 100k franc
5Case za Ebola hakuna though kuna idadi kubwa ya Cholera hasa kwa watoto
 
Shukran Mkuu
1.Ilituchukua mda wa mwezi mzima hii inatokana na mwendo wa gari ni slow siunajua Semi zinaenda mwendo wa kobe
2.Huku ni waswahili watupu wengi wanaongea kiswazi though lugha yao ni kifaransa na kirundi
3.Ndio passport ni lazima ila unaweza kuomba Emergence Getpass kwa 20K TZ ukifika pale boda wanakupigia mhuri chap wanakuruhusu.
4.Makazi ni kawaida hotel kubwa zinajaa na hata guest zinajaa ila bei ni zilezile kutokana na quality 30k,40k mpKa 100k franc
5Case za Ebola hakuna though kuna idadi kubwa ya Cholera hasa kwa watoto
Mkuu unakaa hotelini au umepanga mtaani!!?
 
Back
Top Bottom