Jinsi Freeman Mbowe alivyofanyiwa umafia ndani ya nchi yake

Mbowe kasema aliwakuongea na Jpm kuhusu hilo la kukwapuliwa pesa na kubambikiziwa kodi with all in vain.

Itoshe tu kusema mzee baba alikuwa anafurahia wenzake wakiteseka.
Halafu kila jumapili unakwenda kanisani kumuomba Mungu huku unawanyanyasa wenzako kisa ni kutofautiana ki itikadi za siasa.
 
December 2018 Freeman Mbowe na Ester Matiko walikamatwa kwa madai ya kuruka dhamana kwenye kesi ya uchaguzi iliyokua inawakabili. Walidaiwa hawajahudhiria mahakamani mara 3 hivyo wakafutiwa dhamana.

Mbowe alikua Afrika Kusini kwa matibabu. Hata hivyo mara zote aliwakilishwa mahakamani na mawakili wake. Kisheria hakuruka dhamana kwa sababu dhamana yake haikumzuia kusafiri nje ya nchi.

Aliporejea aliwasilisha barua ya ruhusa ya Spika. Hakimu akapuuza barua hiyo na kumfutia dhamana. Hapa mahakama iliingilia uhuru wa mhimili mwingine (Bunge). Hata alipojitetea kuwa mara zote mawakili wake walimuwakilisha mahakamani, utetezi wake haukusikilizwa. Akatupwa gerezani Segerea.

Akiwa huko TRA wakamwandikia barua ya kumweleza kwamba hoteli yake ya Aishi Protea inadaiwa kodi ya 2Bil. TRA wakatuma barua kwenye email binafsi ya Mbowe huku wakijua Mbowe hana access ya email gerezani. TRA wakiwa na nia ovu hawakutuma barua hiyo kwenye email ya hoteli wala hawakumcopy Manager wa hoteli husika. Walituma kwenye personal email ya Mbowe, wakijua hataiona.

Baada ya siku 30 wakamwandikia barua nyingine wakimpa nafasi ya kujitetea kama anakubaliana na kodi hiyo au ana malalamiko apunguziwe. TRA wakatuma barua kwenye email ya Mbowe na hawakucopy management ya Hotel. Mbowe hakuiona kwa sababu bado alikua gerezani.

Baadae wakatuma barua nyingine kumjulisha kwa kuwa amekaa kimya, means anakubaliana na kodi hiyo. Kwahiyo anatakiwa aanze kulipa. TRA walifanya hayo wakijua Mbowe hapati barua zao kwa kuwa yupo gerezani. Na ktk kuonesha nia ovu hawakucopy mangement ya hoteli.

Baadae wakamuandikia barua nyingine ya kumpiga penalt TZS 600M kwa kuchelewesha kulipa kodi hiyo. Mbowe alipotoka gerezani (bada ya miezi minne) akakuta hoteli yake inadaiwa 2.6Bil. Alipouliza akaambiwa ni malimbikizo ya kodi pamoja na penalt kwa kuchelewa kulipa.

Akaendaa TRA kuuliza mbona hajapewa notification ya maandishi? TRA wakamwambia walimtumia barua kwenye email yake. Akaingia na kukuta TRA walimtumia barua 3 akiwa gerezani. Akawauliza kwanini wamtumie barua wakijua yupo gerezani na hataziona? Kwanini hawakutuma kwa management ya hoteli

TRA hawakumjibu, badala yake wakafunga (freeze) akaunti ya hoteli, akaunti za makampuni mengine ya Mbowe na akaunti yake binafsi. TRA walijua wanafanya makosa lakini hawakujali.

Mbowe akahoji uhalali wa kodi ya 2Bil. Kampuni inayoweza kulipa kodi ya 2Bil ni inayotengeneza faida ya 12Bil kwa mwaka. Na ili kampuni itengeneze faida ya 12Bil inahitaji kufanya mauzo ya angalau 60Bil.

Yani ukifanya mauzo ya 60Bil, unaweza kupata faida ya 12Bil, hivyo utalipa kodi ya 2Bil. Sasa jiulize ni hoteli gani inaweza kufanya mauzo ya 60Bil? Yani milioni elfu 60?? Hoteli kubwa kama Serena haiwezi kufanya mauzo hayo, sembuse Aishi Protea iliyopo Machame?

Halafu kila mwaka hoteli hiyo imekua ikilipa kodi na kupewa Tax clearence, kuonesha hawadaiwi. Sasa hilo deni la 2Bil na penalt ya 600M vimetoka wapi? TRA hawakua na majibu zaidi ya kumlazimisha alipe.

Kwa miaka mitatu Mbowe hana access na akaunti zake. Hawezi kutoa fedha wala kufanya transaction yoyote. Kampuni zake nazo zinachechemea maana akaunti za kampuni zimefungwa, hata mishahara ya watumishi ni tabu. Amelazimika kupunguza wafanyakazi kwa sababu ya USHETANI wa TRA.

Rais Samia aliagiza waliofungiwa akaunti na TRA wafunguliwe. Jumanne 06 April 2021, TRA wakafungua akaunti zote za Mbowe, lakini hazina kitu. Kwenye akunti yake binafsi wamekomba zaidi ya 528M ambazo ni malimbikizo ya mshahara na kiinua mgongo chake cha ubunge. TRA wamekomba pia mamilioni ya shilingi kwenye akaunti za kampuni zake.

Tayari Mbowe amemjulisha Mhe.Rais Samia kuhusu uharamia huo wa TRA, kwamba wamemfungulia akaunti lakini wamekomba fedha zote. Tunaamini atahakikisha haki inatendeka maana MAMA ni mtu wa haki.

Hivi ndivyo mtakatifu mwendazake alivyotumia mkono wa chuma kuwanyoosha wale waliopishana nae mawazo. Lakini kila mara alijinyeyekeza Kanisani, akasahau Mungu hadhihakiwi.

Wapo wanaodai "si vizuri kumsema marehemu". Lakini napenda kuwajibu kuwa huwezi kuzuia watu kukusema ukifa. Either utasemwa kwa mazuri au mabaya. Idd Amin, Mobutu, Hittler wanasemwa kwa mabaya kwa kuwa waliacha historia mbaya. Kwahiyo jitahidi uache historia nzuri ili usemwe kwa mazuri siku ukiondoka hapa duniani (Ufunuo 14:13).!

Credit: Malisa Godlisten
Duuh.. kumbe jiwe alikuwa mtumishi kamili wa sheitwani.

Na hapo bado shuhuda za mauaji
 
Huu ni upande wa Mbowe,

Hatujasikia upande wa TRA wala Magufuli anayetuhumiwa hapa.
 
Unaamini vip maneno ya Mbowe pekee bila kuwahoji TRA? hivi mnafanya kila mtu ni mfuasi wa Mbowe ataamini tu anachosema? ebu acheni utoto, lazima tupate maoni ya TRA ndio unaweza kusema chochote
mimi nimetoa ya Mbowe,wewe toa ya TRA
 
Ebu Soma Tena acha ujinga usijione unaakili kumbe ni mjinga wa kutupa
Acha utoto, Mbowe kaeleza wazi baada ya kuona account zinafungwa, akaona isiwe kesi naweza kwenda kufanya biashara ata Dubai, swali langu alipokuwa huko nje kwanini hakusema aliyoyasema baada ya JPM kufa? usijifanye unielewi, wakina Ansbert Gulumo tulikuwa tunawasikia sana ata JPM alipokuwa hai
 
Maoni gani mbona wamefungua account baada ya Reis Samila kusema wafungue si wangesema account sina makosa kisheria. TRA wametumika sana hata kwa askofu Kakobe kila mtu anafahamu. Waliohusika watajuwana na Mungu wao maana malipo ni hapa hapa kama walikubali kutenda dhambi itawarudia wao na familia zao.
Sasa ulitaka wamgomee Rais Samia lazima wafungue ata kama Mbowe analo kosa au hana, lakini huwezi kuamini upande wa Mbowe tu bila TRA kusema na wao
 
Aende zake huko, Nchi yake Nchi gani? Mtu alizoea kukwepa kodi, ujanja ujanja, "mission town" kibao
 
Back
Top Bottom