Jinsi Fedha inavyotengenezwa..Doubts!!.

Jiraniyetu

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
350
333
Salam zenu wakuu,
Naombeni tu nijuzwe maswali kadhaa tu yaliyoniacha njia panda

Nimejaribu kufatilia interview moja kutoka kwa millardAyo kuhusu pesa za tanzania zinavyotengenezwa,aliyekuwa anaeleza utendaji kazi wa B.O.T alieleza kuwa pesa huwa zinatengenezwa na B.O.T lakini B.O.T hakuna kiwanda cha kutengeneza pesa,

Kwa maana hiyo basi B.O.T hutoa tenda kwa makampuni makubwa ya nche ili itengenezewe pesa lakini vigezo vyote vya utengenezaji huo hutolewa na banki kuu ya Tanzania, Benki kuu ndiyo Taasisi kuu ya fedha Hapa Tanzania na Inafanya kazi na serikali..

Maswali yangu ni kwamba,
1: Kama benki kuu inaweza kutoa tenda kwa kampuni itengenezwe pesa sasa kuna haja gani ya serikali kuweka kodi kwa wananchi wanaotumia pesa ya Tanzania badala ya kufyatua zingine huko..

2: Je pesa ikizalishwa B.O.T inawezaje kufika kwa wananchi wa kawaida mbali na wafanyakazi wa serikali..

3: Je,pesa ni nani anayepanga thamani ya pesa kati ya nchi na nchi..
Ni hayo tu wadau,nahitaji nijue..

Karibuni!!..
 
Jibu la 2 ni hivi,b.o.t wanakopesha benki ndogo ndogo na pia ni bank ya benki hizi kama nbc etc hivo ,benki za kawaida hupewa hela na kutunziwa na B.O.T
 
2. pesa inaingizwa kwnye mabenk na kwenye mifumo mingi ya kibihashara...
3. inategemeana.....lkn sana ni soko ndo huwa linaamua thamani ya fedha ipande au ishuke
 
1. BoT haiwezi kutoa tu tenda ya kutengeneza hela ili iache kutoza wananchi kodi kwa sababu,lazima kuwepo uwiano kati ya MAHITAJI ya hela dhini ya USAMBAZWAJI. Ikitokea hela ikatengenezwa zaidi ya inavyohitajika hela itakuwa nyingi alafu thamani yake itashuka(thamani ya hela inaongezeka zaidi inapokuwa adimu) Pia vitu vitapanda bei hivyo bado itakuwa shida. Kwa upande mwingine endapo hela ikiwa adimu zaidi inaweza sababisha watu kurudi kwenye biashara ya vitu na vitu.
2. Pesa ikishatengenezwa huingizwa kwenye mfumo kwa njia tofauti tofauti,sana sana kwa njia ya mabenk..benk za biashara hukopesha na BoT alafu benk hizo hukopesha watu,pia serikali inaweza kununua hisa zake hivyo kutoa hela kwenye mzunguko.
3. Thamani ya pesa ya nchi husika dhini ya pesa ya nchi zingine inaweza kupangwa na benk kuu au ikajipanga yenyewe kutokana na soko kupitia nguvu ya uhitaji na utoaji wa pesa husika. Kama pesa yetu (Tsh) itahitajika zaidi na nchi zingine( tunapouza zaidi bidhaa au huduma zetu nje) basi pesa yetu itapanda zaidi thamani. Lakin kama pesa yetu haiitajiki au tunahitaji zaid pesa za nchi nyingne(pale ambapo hatuuzi sana bidhaa na huduma zetu nje au tunapoagiza zaidi vitu nje) pesa yetu itashuka thamani.

Povu/marekebisho/nyongeza ruksa.....bado tunajifunza.
 
Namba tatu nimekuelewa sana mkuu
 
1.Kwa ufupi tu bank ikifanya hivyo kutatokea kitu kinaitwa inflation yaani thamani ya shilingi itapungua na utahitaji pesa nyingi kununua kitu kidogo tu yaani unaenda kununua nyanya sokoni na toroli lililojaa pesa
 
Mambo ya Zambia kipindi hiyo..
 
Salam zenu wakuu,
Naombeni tu nijuzwe maswali kadhaa tu yaliyoniacha njia panda

Nimejaribu kufatilia interview moja kutoka kwa millardAyo kuhusu pesa za tanzania zinavyotengenezwa,aliyekuwa anaeleza utendaji kazi wa B.O.T alieleza kuwa pesa huwa zinatengenezwa na B.O.T lakini B.O.T hakuna kiwanda cha kutengeneza pesa,

Kwa maana hiyo basi B.O.T hutoa tenda kwa makampuni makubwa ya nche ili itengenezewe pesa lakini vigezo vyote vya utengenezaji huo hutolewa na banki kuu ya Tanzania, Benki kuu ndiyo Taasisi kuu ya fedha Hapa Tanzania na Inafanya kazi na serikali..

Maswali yangu ni kwamba,
1: Kama benki kuu inaweza kutoa tenda kwa kampuni itengenezwe pesa sasa kuna haja gani ya serikali kuweka kodi kwa wananchi wanaotumia pesa ya Tanzania badala ya kufyatua zingine huko..

2: Je pesa ikizalishwa B.O.T inawezaje kufika kwa wananchi wa kawaida mbali na wafanyakazi wa serikali..

3: Je,pesa ni nani anayepanga thamani ya pesa kati ya nchi na nchi..
Ni hayo tu wadau,nahitaji nijue..

Karibuni!!..
Inaonekana umeishia fight fo food fo fo years wew
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom