Jinsi elimu ya tanzania inavyofuta ujinga bila kuongeza maarifa

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
230
583
Kalamu ya Baba Askofu Bagonza (PhD) .

ELIMU YETU
Inafuta Ujinga, Haiongezi Maarifa

Duh!! Tanzania yetu inaumwa. Pole sana. Habari mbaya kila wakati. Taifa linaumwa sana.

Tuliona Samunge. Walikwenda madaktari, Maaskofu, Mitume, Wanajimu, Maprofesa, na wengine wasiotajwa kirahisi. Mzee wa kikombe ni mzalendo kweli. Kama mabeberu wangemtumia, tungekosa majeneza ya kuzikia. Tatizo hapo si ugonjwa. Ni kukosa maarifa. Kikombe kutibu magonjwa yote!!??

Tumeona Morogoro, Mbeya na kwingineko. Lori la mafuta linaanguka. Wenyeji wanaona Mungu kawakumbuka! Wanaiba mpaka betri ya gari. Mafuta yale na betri vina wateja mitaani. Eti serikali ipige marufuku!? Itapiga marufuku malori kuanguka? Elimu haijaongeza maarifa. Tunataka miujiza, tuibe katikati ya moto wa petroli bila kuungua.

Sasa umekuja upako. Mafuta, chumvi, maji, juice, vitambaa, na hata mikate. Si bure, kuna mtu anapata fedha. Sasa badala ya kukanyaga mafuta, tumekanyagana kwenye mishipa ya fahamu. Upako umetutoa roho. Eti serikali ihakiki vyeti vya Mitume na manabii? Subutu!! Wahakiki vyeti ndio wateja wa upako. Polisi anaenda kuwasaka mitume akiacha kidumu cha upako uvunguni mwa kitanda!! Ujinga umeondoka, maarifa hayajaripoti.
Kupenda vya bure, kupenda mafanikio bila kazi, ni donda ndugu.

Tuwe wapole, tujadili kwa nini:

- Watu wapewe chandarua halafu wanavulia dagaa,

- Watu wanakufa kwa mafuriko mabondeni, wengine wanajenga msingi siku hiyo hiyo bondeni,

- Serikali inafukuza watu mabondeni, huku inapokea kodi ya ardhi ya walio mabondeni,

- Manabii wa upako wapate vibali vya mikutano bila ulinzi wa polisi lakini Asasi zikose vibali hata kwa mikutano ya ndani!

- Serikali haijawapa maji safi wananchi, lakini wanaojichimbia kwa gharama, inawatoza kodi au kufungia visima vyao,

-Serikali inatangaza elimu bure. Inafuta karo ya elfu 70 lakini inakalia kimya michango inayofikia laki 6!

Duh! Kuna mtu kakanyaga mrija wa Oksijeni. Mgonjwa wetu atakata roho.

Leteni kodi ya ujinga, upako utakosa wateja. Tunavyopenda kukwepa kodi, tutajielimisha ili tusilipe kodi ya ujinga.

Poleni wafiwa, poleni watanzania.
Mnaopenda kutukana, msijisumbue. Ni heri kutukanwa kuliko kutukana. *Unayo Ole ukitukana, ninayo Heri nikitukanwa.*
 
Elimu yetu bado haiondoi ujinga wapo wasoni wengi lakini bado wajinga “ignorant”.
 
Halafu bado kuna watu hujisifu kwa kuwa na elimu na kuwaambia wenzao kuwa hawana elimu!
 
"Serikali haijawapa maji safi wananchi, lakini wanaojichimbia kwa gharama, inawatoza kodi au kufungia visima vyao"


Hichi kitu kinaniuma sana rohoni.. Kwanini nitozwe kodi kubwa kila mwezi kwa kisima nilichokichimba kwa gharama zangu mwenyewe?


Kama sio roho mbaya ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom