Jinsi Elimu ya SUA ilivypoteza dira kwenye labour market, TCU imulikeni kwa macho mawili

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
5,040
Habari wakuu.

Labda niende straight:

Katika vyuo jipu nchini kimojawapo ni SUA.

Kinatoa kozi ambazo kiuhalisia kwenye labor market ufanisi wake ni mdogo sana, Mitaala na Programmes za SUA kwa ujumla zinachangia kuongeza idadi ya majobless nchini kwa kutoa taaluma zisizoendana na mazingira yetu.

Mitaala na programmes za SUA ni copy & paste kutoka nchi za mashariki ya kati, ambapo haziendani na mazimgira halisi ya kitanzania na Africa.

Nina jamaa zangu wengi waliomalizia SUA kozi za kilimo kama Agribusiness, misitu, sayansi ya nzige, Usimamizi wa Asali etc sahivi ni mabank tellers kwa malipo ya kusikitisha hadi laki 2 , hii imepelekea hadi graduates wa SUA kupewa jina la "Cheap labors" na hii imekuwa common wajiri wengi wakitaka kuajiri mtu wa kumyonya huvuta vijana wa SUA, sasa hawana added skills.

Heslb wanatumia mabilion ya fedha kutoa mikopo kwenye vyuo ambavyo havipo relevant na uhalsia wa nje.

Vijana wengi wa PCB/PCM/CBG ambao walikuwa ndoto ya kusoma udaktari na uengeneer, wanapofeli Form 6 na kupata division 3 chafu na div 4 wote hukimbilia SUA, hivyo husomea vitu ambavyo hawakuwah kuwaza kuvisoma.

Hongera kwa UDSM, Mzumbe na Mhimbiri kwa kuendelea kutoa elimu inayongeza ufanisi kwenye jamii, SUA wanatakiwa wajifunze kutoka kwenu.
 
Elimu ya USA?.

Ndugu, Advocate. Kuzungumzia mfumo wa Elimu nchini ni lazima kwanza uwe umeshiba sawa-sawa. Au labda pengine una mkate pembeni.

Naomba nikuulize, unachokipenda toka rohoni ndicho umesomea?. Kama ndiyo, ni wangapi wapo kama wewe?, kama siyo tunakwenda wapi?.

Ni suala la kawaida kumkuta mwanafunzi (sipendi kuita mwanachuo) anasomea U-handisi wakati moyo wake upo kwenye U-alimu. Vise-versa, mwanafunzi anasomea U-alimu wakati mapenzi yake ya dhati yapo kwenye U-handisi.

Hao TCU, NACTE ndiyo majipu haswa. Mwanafunzi anaomba ualimu, wao wanampangia HR. Unaomba uanasheria, wanakupangia Uhandisi. Unategemea nini?.

Wao ndiyo huamua hatima ya wanafunzi. Wao ndiyo hutaka usome kipi, na usisome nini. I'ts un-fair to call them ni "Wapanga" taasubi za kusomea.

Siyo SUA pekee, ni vyuo Taifa zima.
 
Ni kweli mkuu! Lakini SUA ni jipu zaidi, mtu anasomea sayansi ya udongo na nzige alafu field anaenda kupiga NHIF na supervisor anampa max tu.
Kinachotokea baada ya kugraduates ndio wanakuja kuwa ma cheap labors sababu ya kukomaa kwenye fani zisizo zao.
 
Kabla hatujachangia sana
Jaribu kuangalia ni sector ipi ina wataalam wengi sana hapa nchini wenye viwango vya juu vya kimataifa waliochangia zaidi ukuaji na ustawi wa nchi

Pia angalia ni sector zipi hapa Tanzania zimepiga hatua kuliko sector zingine.

Linganisha maendeleo ya Tanzania kwenye kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda, afya, uchumi, fedha na haki na sheria

Halafu uje utuambie ni sector ipi iko juu ya zingine hapa Tanzania kuwa na skilled labor force pamoja na technology ya juu.
 
Unazochuki binafsi tu. Lkn elimu inayotolewa SUA ni pana na ndio maana mwanafunzi anayesomea sayansi ya nzige na bado anaajiriwa NHIF maana yake katika mtaala alioutumia zipo basic kozi zinazohusiana na nafasi za kazi wanazozifanya ambazo zipo kinyume na kozi kuu walizosomea. Usiwe mjinga hata fact ndogo kama hizo. Kama data unazotoa ni sahihi kwanini kwa mfano wasiajiriwe wanafunzi wasio na ajira toka vyuo vingine ambao wamejazana mtaani? Na vitu vingine ulivyoandika ni ujinga wa kitokujua taratibu. Mfano shirika kama NHIF wana salary scale zao na mshahara sometimes kwenye sekta binafsi inategemea bargaining capacity ulokuwa nayo
 
Ngoja movie iendeleee kesho mapema narud nione kinachoendelea
 
Tuwe waangalifu na hili. SUA "imebobea" kwenye program za kilimo (kilimo, misitu, veterinary, science education, uhandisi kilimo, rural development etc). Hakuna chuo kingine hadi sasa kimetoa vijana wenye itaalamu huo. Hivyo kuwaona wanafanya kazi amazo umeziita cheap labour haina maana ya kuwa elimu ya SUA imepoteza dira na ya vyuo vingine ndo iko sawa. Swala ni je kuna kazi gani za kuwaajiri au wao wenyewe kujiajiri? Nchi inamipango gani kuwawezesha kuji ajiri na je kilimo kwa mukutadha wa sasa kinalipa? Tujiulize je tatizo lilisemwa hapo juu ni kubwa kiasi gani au ni hisia tu.

Mitaala na programmes za SUA ni copy & paste kutoka nchi za mashariki ya kati, ambapo haziendani na mazimgira halisi ya kitanzania na Africa.

Hii ni mpya kuwa SUA ina cut na ku paste programs za mashariki ya kati. Nakuchallenge uthibitishe hili.

Vijana wengi wa PCB/PCM/CBG ambao walikuwa ndoto ya kusoma udaktari na uengeneer, wanapofeli Form 6 na kupata division 3 chafu na div 4 wote hukimbilia SUA, hivyo husomea vitu ambavyo hawakuwah kuwaza kuvisoma.

Mkuu hapa unatulisha matango pori. Kuna vijana wengi wenye ufaulu mzuri tu ambao huweka SUA kama choice yao ya kwanza hata enzi ya CAS. Pili kama wamefeli watapataje SUA? SUA inachukua watu wenye ufaulu unaokubalika na TCU. Sijasikia Division 4 kuingia chuo kikuu degree. Usiniambie SUA imeshuka kiasi hicho. Tafadhali thibitisha.

SUA inaweza kuwa na matatizo yake ambayo yanatokana na jinsi serikali inavyo gharamia elimu ya juu Tanzania as such utayakuta pia vyuo vingine.
 
Ni kweli mkuu! Lakini SUA ni jipu zaidi, mtu anasomea sayansi ya udongo na nzige alafu field anaenda kupiga NHIF na supervisor anampa max tu.
Kinachotokea baada ya kugraduates ndio wanakuja kuwa ma cheap labors sababu ya kukomaa kwenye fani zisizo zao.
Musikariri chuo kwakua ni cha kilimo kumbuka chuoni kuna kozi nyingi sana na ndio sababu unawezapata ajira uka-deal na ishu ndogo tu ambayo ni moja ya kozi ulizosomea huku ukiambatanisha kwa uchache sana na knowledge za kozi nyingine. Kukuta mhitimu wa SUA huko NHIF ni wazi kua wahitimu wa hiki chuo wanafit maeneo zaidi ya kile unachokiamini wewe.

Nadhani pia Agriculture haijulikani sana kwa watu ambao hawajihusishi nayo kwanza wanajua ukifanya ukulima hauhitaji kusoma sana, pili wanaona wakulima wengi ni wa hali ya chini au watu wakawaida tu wasio na elimu ya chuo kikuu. Hii inafanya kilimo kujuliwa upana wake na waliokwisha jiingiza humo TU na kilimo ni kipana kuliko watu wanavyofikiria.
 
Ni kweli mkuu! Lakini SUA ni jipu zaidi, mtu anasomea sayansi ya udongo na nzige alafu field anaenda kupiga NHIF na supervisor anampa max tu.
Kinachotokea baada ya kugraduates ndio wanakuja kuwa ma cheap labors sababu ya kukomaa kwenye fani zisizo zao.
Mkuu unaposema wenye division four na three chafu wanaenda SUA una maanisha nini?? Naomba majibu tafadhali!!
 
Ni kweli mkuu! Lakini SUA ni jipu zaidi, mtu anasomea sayansi ya udongo na nzige alafu field anaenda kupiga NHIF na supervisor anampa max tu.
Kinachotokea baada ya kugraduates ndio wanakuja kuwa ma cheap labors sababu ya kukomaa kwenye fani zisizo zao.
Alafu hiyo kozi ya sayansi ya udongo na nzige mbona sijawahi iona sua??

Au una unaongelea sua ipi mkuu??
 
Ni kweli mkuu! Lakini SUA ni jipu zaidi, mtu anasomea sayansi ya udongo na nzige alafu field anaenda kupiga NHIF na supervisor anampa max tu.
Kinachotokea baada ya kugraduates ndio wanakuja kuwa ma cheap labors sababu ya kukomaa kwenye fani zisizo zao.
Alafu graduate wa sua kufanya kazi bank ni kosa la SUA kweli? Sua kazi yao ni kufundisha na sio kumpangia wapi graduate akafanye kazi!!

Nnachoona hapa ni kwamba una chuki binafsi na sua, na kuna uwezekano MLIENDA KWENYE INTERVIEW YA KAZI NA KIJANA WA SUA AKAWAGARAGAZA!!

Alafu hujui agribusiness wanasoma uchumi na finance? Sasa kwann washindwe kufanya kazi bank??

Kama kichwan wewe ni kilaza basi jua vijana wa sua watakupelekesha sana!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom