Jinsi DC Sabaya alivyomnasa Afisa Ugani na mtandao wa kitapeli wa Q NET alivyochota mamilioni ya watu

Kila kitu serikali serikali..pumbaf

Tumezidi kuwa wajinga..na dunia ya leo ukiwa mjinga wewe ni mtaji kwa watu.

Mtu ni mwalimu mwenye degree,lakini bado anadandia project fake za kitapeli bila hata kushtuka..hapo na serikali ni ya kuiita jameni?

Na mahakamani hapo kesi kimsingi hamna kwa uelewa wangu mdogo wa sheria..labda mambo yafanyike kibabe maana hawa watu wanachukua hela za watu kirahisi sana
Huyo waziri na katibu mkuu wa wizara waliokata utepe kufungua ofisi za matapeli Hawa wawekwe kundi gani ??
 
Watu washapigwa sana na hii Qnet mimi nilitegemea kwa serikali makini wangeshawafurusha nchini muda sana. Mpaka huwa najiuliza wanakula nao?
 
HAI, KILIMANJARO

Mkuu wa wilaya ya HAI, Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya amemsweka ndani mtumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Dominica Mwapombe kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa kitapeli na kufanikiwa kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu kwa njia ya udanganyifu.

Aidha ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru wilayani humo, kufanya uchunguzi wa kina juu tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria.

Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya kupokea malalamiko ya watu mbalimbali wakiweno walimu waliofika ofisini kwake wakidai kutapeliwa na Mwapombe

Kupitia taasisi ya biashara ya Qnet Marketing ambapo yeye ni mwakilishi wake.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, Mwapombe ambaye ni afisa ugavi wa halmashauri hiyo amefanikiwa kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu na wafanyabiashara (majina yamehifadhiwa) waliopo katika wilaya hiyo baada ya kuwashawishi na kufanikiwa kuwaunganisha na mtandao wa kibiashara wa Qnet.

Walimu wanne na mfanyabiashara mmoja waliohojiwa na mkuu huyo wa wilaya katika mkutano wa walimu uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, walidai kumpatia mtuhumiwa mamilioni ya fedha kwa makubaliano kwamba watapokea kiasi cha dola 200 kila mwezi na kwamba ili upate kiasi hicho lazima ulete mwanachama wawili ama watatu wa kujiunga na mtandao huo.

"Kuna walimu na wafanyabiashara wamefika ofisini kwangu kulalamika kutapeliwa na taasisi ya Qnet kupitia Mwampombe na wenzake kuna mwalimu amelipa kiingilio cha Sh. milioni 4.2, kuna aliyetoa Sh. milioni 4.3, mwingine amelipa Sh. million 3.5 na mwingine ametoa Sh. milion 1.6 "

"Hawa wote waliahidiwa kupokea sh, laki NNE kwa mwezi lakini tangu wametoa fedha hizo kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu hawajawali kupokea chochote kwa sababu hawajaleta wanachama, sasa huu ni utapeli kama matapeli wengine" alisema Sabaya.

Aliongeza kuwa mtandao huo wa Qnet haujasajiriwa kupitia wakala wa usajiri wa makampuni (BRELA), hii ni baada ya kupiga simu kwa mkurugenzi wa Brela, David Nyaisa ambaye kupitia simu ya mkuu huyo wa wilaya iliyokuwa imewekwa sauti alithibitisha kuwa kampuni hiyo haina usajiri.

Mmoja ya walimu hao(Jina limehifadhiwa) akiongea katika mkutano huo,alisema alishawishiwa na rafiki yake kujiunga na mtandao huo na kutoa kiasi cha sh milioni 4.3 kwa mtuhumiwa ,akiahidiwa kupokea dola 200 kila mwezi baada ya kuwa ameleta wanachama wengine huku akipewa zawadi ya saa na cheni.

"Tangu nimetoa hii hela tarehe 5mwezi wa kwanza mwaka huu sijaona hela yoyote nimeingiziwa kwenye akaunti yangu na kila nikiwafuata kuwaomba hata lisiti wanadai nitaingiziwa kwenye mtandao ,nakuomba mheshimiwa unisaidie maana ndoa yangu ipo mashakani" Alisema mmoja ya wahanga wa tukio hilo.

Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni mwakilishi wa Qnet alisema kuwa kampuni hiyo ni ya kibiashara na imesajiriwa kwa ajili ya kufanya biashara kwenye mtandao.

"Kwanza Mimi sio mwajiriwa wa Qnet ni mwakilishi huru na hii biashara niyakwenye mtandao hata kwenye ilani ya 61 ya ccm inaeleza mkakati wa kuimarisha biashara ya kwenye mtandao" alisema Mwapombe.

Ends...

Picha 1 ,DC Sabaya
Picha 2,Mtuhumiwa wa utapeli wakati akihojiwa.
Picha 3,Mhanga wa utapeli akielezea jinsi alivyotapeliwa.

View attachment 1646957View attachment 1646958View attachment 1646961
Za mwizi....
 
Kila siku tunapiga kelele jamani matapeli wamezidi mitandaoni lakini bado walimu wamelala usingizi wa Pono hivi inawezenaje receipt isubiriwe kutoka malasia huku tayari umetoa hela? Haocwalimu wanajidhalilisha tu.
 
Wanamtandao wote mapapa waliofungua kabisa ofisi zao ndio wakamatwe...wasishughulike na hao wadogo ambao wameshadhulumiwa nao walikua wanatafta wanyonge wenzao wa kuwadhulumu
 
Hii ni ishara tu ya matokeo ya kuua "curiosity" na kutengeneza "obedience", kuua "questioning" na kuhimiza "compliance", kuua "logic and reasoning" na kupandikiza "indifference", kuua "independent thought" na kutengeneza "bandwagon-minds"...yaani tangu utotoni na kupitia elimu zetu.

Ni ishara ndogo sana kupitia kundi dogo sana, ila bado ni ishara.
You can say that again and again and again.
Every thing should be reason, questioned and explored including religion.
 
Kundi la waalimu limejaa watu wajinga sn sijui ni kwanini?
Kumbuka ndio walikufanya unabwabwaja hapa nilikwambia wewe akili zako ndogo sana . Taasisi gani haitapeliwi tuanzie hapo
 
Kule ndio kitovu cha mambo hayo wanasema hatoki mtu akiingia kwenye kumi na nane zao.

Hela ya vikoba watu wamepeleka huko huku buza si watakufa na wewe Honey.
Morning my Business partner/hubby, hivi makumbusho na posta ndiyo centre za mambo ya network marketing?, nakumbuka kuna mtu alinipeleka "Forever living " makumbusho huko huko waliongeaa wakaongea nikawa nawasikiliza ila inakuja inakataa yani + nilikua broke vibaya at the end nikawaambia sina mtaji na bidhaa zao ni ghali mno dawa ya meno 40,000/= sijui 25,000/= hivi Buza kwetu huko ningemuuzia nani jamani watu tunanunua whitedent letu kubwaa 2500/= tu
 
Polisi mkoani Kilimanjaro wanamshikilia mtumishi wa serikali, Dominic Mwapombe anayedaiwa ni afisa wa Kampuni ya Qnet inayodaiwa kuwaibia watumishi wa serikali mamilioni ya fedha. Mwapombe na wenzake wanashukiwa kukusanya TZS milioni 4.3 kwa watu mbalimbali kama ada ya kujisajili.



Nilipowaona tu hawa Jamaa (Qnet) kuwa Hamnazo Kichwani (Akili za Kipa Katoka) ni pale tu Salamu yao muda wote ikiwa ni 'Good Morning' tu.
 
Jamaa wana ushawishi, ukiishiwa misimamo shurti wakutendeee, kweli wajinga mjini hawaishi...na watu husahau haraka sana toka enzi za deci...

Pia pana hawa crowd1 nao hushawishi saana, wakaniunga kwa whatsapp group lao so nimebaki kutazama tu chat zao baada ya mkasa wa qnet naona maswali yakawa mengi kwa members wametoa pesa zao na rewards waliambiwa baada ya miezi mitatu, ila ishapita miezi sita hakuna kitu baada ya maswali kuzidii admin akaanza leftisha wauliza maswali baadae kapiga ban members kupost.
 
Back
Top Bottom