Jinsi DC Sabaya alivyomnasa Afisa Ugani na mtandao wa kitapeli wa Q NET alivyochota mamilioni ya watu

Monster20

Senior Member
Nov 30, 2020
160
250

HAI, KILIMANJARO

Mkuu wa wilaya ya HAI, Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya amemsweka ndani mtumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Dominica Mwapombe kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa kitapeli na kufanikiwa kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu kwa njia ya udanganyifu.

Aidha ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru wilayani humo, kufanya uchunguzi wa kina juu tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria.

Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya kupokea malalamiko ya watu mbalimbali wakiweno walimu waliofika ofisini kwake wakidai kutapeliwa na Mwapombe

Kupitia taasisi ya biashara ya Qnet Marketing ambapo yeye ni mwakilishi wake.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, Mwapombe ambaye ni afisa ugavi wa halmashauri hiyo amefanikiwa kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu na wafanyabiashara (majina yamehifadhiwa) waliopo katika wilaya hiyo baada ya kuwashawishi na kufanikiwa kuwaunganisha na mtandao wa kibiashara wa Qnet.

Walimu wanne na mfanyabiashara mmoja waliohojiwa na mkuu huyo wa wilaya katika mkutano wa walimu uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, walidai kumpatia mtuhumiwa mamilioni ya fedha kwa makubaliano kwamba watapokea kiasi cha dola 200 kila mwezi na kwamba ili upate kiasi hicho lazima ulete mwanachama wawili ama watatu wa kujiunga na mtandao huo.

"Kuna walimu na wafanyabiashara wamefika ofisini kwangu kulalamika kutapeliwa na taasisi ya Qnet kupitia Mwampombe na wenzake kuna mwalimu amelipa kiingilio cha Sh. milioni 4.2, kuna aliyetoa Sh. milioni 4.3, mwingine amelipa Sh. million 3.5 na mwingine ametoa Sh. milion 1.6 "

"Hawa wote waliahidiwa kupokea sh, laki NNE kwa mwezi lakini tangu wametoa fedha hizo kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu hawajawali kupokea chochote kwa sababu hawajaleta wanachama, sasa huu ni utapeli kama matapeli wengine" alisema Sabaya.

Aliongeza kuwa mtandao huo wa Qnet haujasajiriwa kupitia wakala wa usajiri wa makampuni (BRELA), hii ni baada ya kupiga simu kwa mkurugenzi wa Brela, David Nyaisa ambaye kupitia simu ya mkuu huyo wa wilaya iliyokuwa imewekwa sauti alithibitisha kuwa kampuni hiyo haina usajiri.

Mmoja ya walimu hao(Jina limehifadhiwa) akiongea katika mkutano huo,alisema alishawishiwa na rafiki yake kujiunga na mtandao huo na kutoa kiasi cha sh milioni 4.3 kwa mtuhumiwa ,akiahidiwa kupokea dola 200 kila mwezi baada ya kuwa ameleta wanachama wengine huku akipewa zawadi ya saa na cheni.

"Tangu nimetoa hii hela tarehe 5mwezi wa kwanza mwaka huu sijaona hela yoyote nimeingiziwa kwenye akaunti yangu na kila nikiwafuata kuwaomba hata lisiti wanadai nitaingiziwa kwenye mtandao ,nakuomba mheshimiwa unisaidie maana ndoa yangu ipo mashakani" Alisema mmoja ya wahanga wa tukio hilo.

Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni mwakilishi wa Qnet alisema kuwa kampuni hiyo ni ya kibiashara na imesajiriwa kwa ajili ya kufanya biashara kwenye mtandao.

"Kwanza Mimi sio mwajiriwa wa Qnet ni mwakilishi huru na hii biashara niyakwenye mtandao hata kwenye ilani ya 61 ya ccm inaeleza mkakati wa kuimarisha biashara ya kwenye mtandao" alisema Mwapombe.

Ends...

Picha 1 ,DC Sabaya
Picha 2,Mtuhumiwa wa utapeli wakati akihojiwa.
Picha 3,Mhanga wa utapeli akielezea jinsi alivyotapeliwa.
Nimependa hapo kwenye Ilani ya 61 ya CCM, Lumumba hebu tusaidieni..... mmemtuma?.
 
Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
13,302
2,000
Kabisa aisee, mpaka unamwonea huruma. Kuna mwalimu mwez wa nane aliamua kuacha kazi kimya kimya ili asishauliwe chochote. Amepigiwa simu pamoja na kufuatwa nyumbani mara nyingi kumsihi arudi kazini, akasema wamwache na maamuzi yake.
Baadae wakaja wakaguzi wakaambiwa kuhusu huyo mwalimu, wakampa wiki awe amerudi kazini. Lakini hakurudi.
Baadae ndio katika kutafuta watu wengine wa kujiunga na Qnet ndio siri ikafichuka. Maama alianza kuwashawishi walimu wenzake wajiunge na hiyo network.
In short mwalimu kapauka sana. Anatamani apigiwe simu tena arudi kazini.
Walimu Mungu awasaidie sana. Maana pamoja na malalamiko haya, bado kunawatyu wanaendelea kujiunga. Manaigana sana. Mwalimu mmoja akikopa woote wanaenda kukopa hata kama huna project yoyote. Ngoja waendelee kupigwa tu
Kwa kweli MUNGU awape utambuzi wa mapema

Unajua watu wengi wamejikuta wanatafuta njia ya mkato hapo ndio wanapo pigwa kama hawa
 
This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
2,601
2,000
Kumbuka ndio walikufanya unabwabwaja hapa nilikwambia wewe akili zako ndogo sana . Taasisi gani haitapeliwi tuanzie hapo
Wingi wa walimu na status walio nayo ktk jamii,na namna rahis ya kuwapata km kundi inachangia wao kuonekana sana.Lkn si kweli kwamba wao ndio waliotapeliwa tu.Qnet imetapeli wengi sana,kuanzia wajasiria mali,wafanyabiashara wa kati na hata machinga watu wamenyooshwa sawa sawa.Ila kikubwa watu hawajifunzi na hata ukiwaambia hueleweki kisa hela za chapchap.

Kwa jinsi pyramid schemes zilivyo watu wa mwanzo wachache huwa wanafaidika lkn kundi likishakuwa kubwa sir rshisi kujiendesha tena.Na Ndio wakat wa wale wajanja wachache kupiga hela za kutosha.
 
This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
2,601
2,000
Mimi kuna Mdada Mmoja wa Ofisi zao Kinondoni karibu na Club ASET ( Twanga Pepeta ) aliniita huko na kuanza 'Kunishawishi' na kwakuwa tayari 'Kisaikolojia' nilishamsoma 'Udhaifu' wake japo 'alijimwambafai' Kwangu kuwa ana Masters Degree na bonge la 'exposure' duniani nami nikamwonyesha kuwa Mimi ni Mtoto wa Mjini ambapo 'nikamtongoza' kwa 'Mbinu' kali mno na akajaa 'Mkenge' Mwanamume 'nikamkojolea' na nilipomaliza pale pale Kitandani nikamwambia 'Good Morning' na tusijuane tena.
Hahahaaaaa......gud morning to you! Nmecheka sana 🤣🤣🤣
 
emperor

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
211
250
Mimi kuna Mdada Mmoja wa Ofisi zao Kinondoni karibu na Club ASET ( Twanga Pepeta ) aliniita huko na kuanza 'Kunishawishi' na kwakuwa tayari 'Kisaikolojia' nilishamsoma 'Udhaifu' wake japo 'alijimwambafai' Kwangu kuwa ana Masters Degree na bonge la 'exposure' duniani nami nikamwonyesha kuwa Mimi ni Mtoto wa Mjini ambapo 'nikamtongoza' kwa 'Mbinu' kali mno na akajaa 'Mkenge' Mwanamume 'nikamkojolea' na nilipomaliza pale pale Kitandani nikamwambia 'Good Morning' na tusijuane tena.
Lazima ni Caty huyu.. keupe kembamba kalinunua BMW anadanganya sana watu.. kana Masters mwalimu wa UDSM na kaliacha kazi.. kashenzi sana. Bora umekatia
 
demulikuy

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,047
2,000
Hii ni ishara tu ya matokeo ya kuua "curiosity" na kutengeneza "obedience", kuua "questioning" na kuhimiza "compliance", kuua "logic and reasoning" na kupandikiza "indifference", kuua "independent thought" na kutengeneza "bandwagon-minds"...yaani tangu utotoni na kupitia elimu zetu.

Ni ishara ndogo sana kupitia kundi dogo sana, ila bado ni ishara.
Best inference! Mkuu itafutie hati miliki! Awesome!
 
radicals

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
4,417
2,000
Mimi kuna Mdada Mmoja wa Ofisi zao Kinondoni karibu na Club ASET ( Twanga Pepeta ) aliniita huko na kuanza 'Kunishawishi' na kwakuwa tayari 'Kisaikolojia' nilishamsoma 'Udhaifu' wake japo 'alijimwambafai' Kwangu kuwa ana Masters Degree na bonge la 'exposure' duniani nami nikamwonyesha kuwa Mimi ni Mtoto wa Mjini ambapo 'nikamtongoza' kwa 'Mbinu' kali mno na akajaa 'Mkenge' Mwanamume 'nikamkojolea' na nilipomaliza pale pale Kitandani nikamwambia 'Good Morning' na tusijuane tena.
We jamaa huwa sikuamini, sijui ni kwa nini
 
radicals

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
4,417
2,000
Q net ni biashara mtandaoni. Na ipo huru
Kweli ipo huru kuwalaghai na kuwatapeli watu kwa ahadi ya kuwa mamilionea.

NB. Huwezi kutajirika kwa kuchangishana pesa, bali utatajirika kwa kuuza bidhaa/huduma sahihi kwa wakati sahihi
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
2,419
2,000

HAI, KILIMANJARO

Mkuu wa wilaya ya HAI, Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya amemsweka ndani mtumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Dominica Mwapombe kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa kitapeli na kufanikiwa kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu kwa njia ya udanganyifu.

Aidha ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru wilayani humo, kufanya uchunguzi wa kina juu tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria.

Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya kupokea malalamiko ya watu mbalimbali wakiweno walimu waliofika ofisini kwake wakidai kutapeliwa na Mwapombe

Kupitia taasisi ya biashara ya Qnet Marketing ambapo yeye ni mwakilishi wake.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, Mwapombe ambaye ni afisa ugavi wa halmashauri hiyo amefanikiwa kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu na wafanyabiashara (majina yamehifadhiwa) waliopo katika wilaya hiyo baada ya kuwashawishi na kufanikiwa kuwaunganisha na mtandao wa kibiashara wa Qnet.

Walimu wanne na mfanyabiashara mmoja waliohojiwa na mkuu huyo wa wilaya katika mkutano wa walimu uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, walidai kumpatia mtuhumiwa mamilioni ya fedha kwa makubaliano kwamba watapokea kiasi cha dola 200 kila mwezi na kwamba ili upate kiasi hicho lazima ulete mwanachama wawili ama watatu wa kujiunga na mtandao huo.

"Kuna walimu na wafanyabiashara wamefika ofisini kwangu kulalamika kutapeliwa na taasisi ya Qnet kupitia Mwampombe na wenzake kuna mwalimu amelipa kiingilio cha Sh. milioni 4.2, kuna aliyetoa Sh. milioni 4.3, mwingine amelipa Sh. million 3.5 na mwingine ametoa Sh. milion 1.6 "

"Hawa wote waliahidiwa kupokea sh, laki NNE kwa mwezi lakini tangu wametoa fedha hizo kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu hawajawali kupokea chochote kwa sababu hawajaleta wanachama, sasa huu ni utapeli kama matapeli wengine" alisema Sabaya.

Aliongeza kuwa mtandao huo wa Qnet haujasajiriwa kupitia wakala wa usajiri wa makampuni (BRELA), hii ni baada ya kupiga simu kwa mkurugenzi wa Brela, David Nyaisa ambaye kupitia simu ya mkuu huyo wa wilaya iliyokuwa imewekwa sauti alithibitisha kuwa kampuni hiyo haina usajiri.

Mmoja ya walimu hao(Jina limehifadhiwa) akiongea katika mkutano huo,alisema alishawishiwa na rafiki yake kujiunga na mtandao huo na kutoa kiasi cha sh milioni 4.3 kwa mtuhumiwa ,akiahidiwa kupokea dola 200 kila mwezi baada ya kuwa ameleta wanachama wengine huku akipewa zawadi ya saa na cheni.

"Tangu nimetoa hii hela tarehe 5mwezi wa kwanza mwaka huu sijaona hela yoyote nimeingiziwa kwenye akaunti yangu na kila nikiwafuata kuwaomba hata lisiti wanadai nitaingiziwa kwenye mtandao ,nakuomba mheshimiwa unisaidie maana ndoa yangu ipo mashakani" Alisema mmoja ya wahanga wa tukio hilo.

Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni mwakilishi wa Qnet alisema kuwa kampuni hiyo ni ya kibiashara na imesajiriwa kwa ajili ya kufanya biashara kwenye mtandao.

"Kwanza Mimi sio mwajiriwa wa Qnet ni mwakilishi huru na hii biashara niyakwenye mtandao hata kwenye ilani ya 61 ya ccm inaeleza mkakati wa kuimarisha biashara ya kwenye mtandao" alisema Mwapombe.

Ends...

Picha 1 ,DC Sabaya
Picha 2,Mtuhumiwa wa utapeli wakati akihojiwa.
Picha 3,Mhanga wa utapeli akielezea jinsi alivyotapeliwa.

View attachment 1646957 View attachment 1646958 View attachment 1646961
Kuna manesi pia wamepigwa sana,namkumbuka nesi mmoja pale mnazi mmoja hospital ndiyo alikiwaga dalali wao.alikuwa anaimbisha manesi wa kike ili wawe conected. anaye shitukia deal na kuchomoa kabbla hawajampiga alikuwa ana mchukia balaa.
sema pia nadhani walikuwaga conected na loan oficers.sababu inasemekana walikuwa wanakuunganishia mkopo NMB unaupata ndani ya mda mfupi sana,ilimradi wewe ni mtumishi wa umma na umekubali kujiunga nao.

Serikali ifanye uchunguzi wa kina itapata mengi humo
 
kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
6,040
2,000
Hawa ndio walimu wanaofundisha ujinga mashuleni.

FaizaFoxy
Hao nao ni walimu?
Screenshot_20201212-131759.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom