Jinsi CCM Itakavyomtumia Zitto Kushinda Urais 2015

Status
Not open for further replies.

Kaldinali

JF-Expert Member
May 25, 2012
263
144
Wakuu

Nadhani wote tunajua kuwa CCM inapanga kutumia kila mbinu on earth ili kuendelea kutawala mwaka 2015 kihalali au kwa zuluma. Sasa hivi, Chama Hiki (ambacho kwa sasa ni marehemu) kiko kwenye mikakati mikubwa na madhubuti ya kuhakikisha kitaendelea kutawala hata kama hakitapata kura za kutosha mwaka 2015. Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na:

Kumteua Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa makubaliano maalumu kuwa atapewa ulaji huo only if atakubali kuitangaza CCM kuwa mshindi wa Urais 2015 hata kama itapata asilimai 10 tu ya Kura (Lubuva Ameshakubali na atafanya hivyo)

Kuruhusu matokeo ya Urais kupelekwa mahakami ili kuja kumnyang'anya Slaa urais kupitia mahakani in case things fall apart and somehow someway CCM looses. So Lubuva Akishindwa kazi Othman Chande atafanya kazi ya kutangaza CCM kuwa mshindi no matter what.(Chande ameshakubali na atafanya hivyo)

Kupanga ugomvi wa CHADEMA na polisi ili watu wauliwe na hivyo kuwatisha watu kuwa CHADEMA ni wagomvi na ikiwezekana kuifuta CHADEMA kupitia kwa jaji Mutungi. (Mutungi amekubali na yuko tayari kufanya hivyo ikibidi)

Na kama haya yote yakishindwa (Yaani Lubuva, Othman na Mutungi) then karata kubwa ya Mwisho ni Zitto Zuberi Kabwe.
Sijui kama yeye anajua hili ila CCM watakuja watamshawishi Zitto Kabwe agombee urais kama mgombea binafsi. Ushawishi huu utafanywa directly na CCM yenyewe na indirectly kwa CCM kuwapa hela rafiki zake Zitto wajerumani ili wajidai wanampsonsor ili agombee Urais kama Mgombea binafsi.

Lengo kuu la CCM katika hili ni kugawanya kura za CHADEMA ili kuishinda. Wanachotaka CCM ni hiki - Zitto akigombea basi Slaa anaweza kupata asilimia 37 za wapiga kura wote Tanzania na Zitto akapata kama asilimia 25 huku CCM ikiambulia kama asilimia 38. Mpaka hapo (Japokuwa CHADEMA itakuwa na asilimia 62) Mgombea wa CCM atakuwa ameshinda (ukichukulia watachakachua kura pia). Hii ni trick ya kudivide kura za CHADEMA na kuwafanya wagombea wote wa CDM wasipate kura za kutosha ilihali angegombea Slaa peke yake angepata asilimia 62. Kama hili litafanikiwa Zitto atakuwa ametumiwa kumnyang'anya Slaa kura huku akiipa CCM ushindi thru this divide and continue to rule trick. Tricky hii huwa inatumiwa sana Marekani na ndio kete ya mwisho ya CCM kuiangusha CDM thru Zitto Zuberi Kabwe.

CHADEMA PLEASE BEWARE OF THIS POWER MONGER YOUNG BOY ZZK! Anatamaa sana mpaka zinam-blind. Haoni chochote anaona sifa binafsi tu. I hope siku moja atakuja ataamka.
 
Kile kiwanda kinaendelea kuzalisha bidhaa zake,sasa nadhani mko vizuri sana kwa kuzalisha bidhaa zenu za uwongo,yaani unatuandikia habari ya kufikirika halafu unataka kutuaminisha? Subiri labda misukule waje wakuamini maana wengine huwa hawachuji habari mradi umewataja na umemtaja adui yao watakusapoti tu
 
Wewe mbona unaharara na zito unazingua kweli yaani mpaka sayo.
 
Kwanza nani kakwambia dr slaa atagombea chadema?kaa usubili uongozi wa chadema ufanye uteuzi wa nani agombe kiti cha urahisi acha porojao,lazima ccm waondoke madarakani
 
Pumba tupu!

Tafadhali naomba unilipe kwa muda wangu niliopoteza hapa ofisini kusoma hili bandiko lako la pumba!
 
Sasa nimeamini Zitto Kabwe sio tishio tu kwa CCM Bali kwa vyama vyote ikiwamo CHADEMA yenyewe, nguvu kubwa inayotumika kumchafua na kumjadili inadhihirisha bila Shaka yeyote kuwa kijana Huyo ni mahiri, kwa kiasi naanza kuiona nguvu ya Zitto Kama Raila Amolo Odinga.

By. Phd safarini Palestine, Gaza on the Western Bank
 
we uliesoma za kimataifa mbona wazidi ingiza tifa hasara kwa mikataba feki

Tifa....? au taifa? Mzee unatukia PC ya shemeji nini ? Mimi sina muda wakupoteza kushughulika na wana siasa akili yangu nimeweka kwenye family yangu na kazi yangu'
 
ana uhuru wa kugombea binafsi au chamani.
Wapiga kura kwani hatuna akili??

Mnampa uzito mkubwa mno, let him play his game na sie wapiga kura tutacheza game yetu.
 
Mbinu ya kumpata mgombea binafsi kwaajili ya kupunguza kura za mgombea wa CHADEMA ni dhahiri kuwa ni jambo ambalo CCM watapenda na kufurahia, lakini si lazima awe Zitto, na hakuna ushahidi wowote kuwa Zitto au atakubali kutumika kwa namna hiyo au Zitto mwenyewe kuwa na wazo hilo. Hapa zaidi umeelezea hisia kuliko ukweli, lakini ukumbuke kuwa kuziweka hisia kwenye ukumbi huu, hisia zinazomwathiri mtu mwingine kwa nanma yeyeote ile siyo uungwana. Ujumbe mkubwa tulioupata toka kwako ni kuwa humwamini Zitto.

Kile kiwanda kinaendelea kuzalisha bidhaa zake,sasa nadhani mko vizuri sana kwa kuzalisha bidhaa zenu za uwongo,yaani unatuandikia habari ya kufikirika halafu unataka kutuaminisha? Subiri labda misukule waje wakuamini maana wengine huwa hawachuji habari mradi umewataja na umemtaja adui yao watakusapoti tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom