Jinsi biashara nyingi Bongo zinavyoanguka ghafla

Midnight

JF-Expert Member
Apr 24, 2021
229
673
Kuna kitu nimekiona miongoni mwetu sisi waswahili, ambacho sio salama kabisa katika kuendesha miradi yetu ya kibiashara. Hii unaweza kuwa ndio sababu kubwa sana ya biashara nyingi kufa kifo cha mende hasa pale zinapoanza kuchangamka tu.

Jana nilipita mahali kupata lunch majira ya mchana,palikuwa ni kihoteli fulani hivi cha hadhi ya kawaida kiasi, basi nikavuta kiti nikakaa hapo,wahudumu nawaona.... Wananiona nawatazama, wananitazama Lakini nika kaa na kukaa zaidi bila kuulizwa wala kufuatwa. Nilipoona sihudumiwi nikajiongeza nikasema labda hapa ni mgahawa wa Magereza nipo recreation (Kama sijakosea kuandika)🙃 baada ya kusogea counter ya vyakula pale jitu unaliuliza vipi naweza kupata huduma, lipo kimya ndo kwanza linaendelea na hamsini zake. Bila hiyana wala matusi nikageuka nyuma nakusonga mbele kwa mbele kutafuta sehemu nyingine ya kupata lunch.

Kwenye ma -bar, unaweza kukaa ukisubilia waiters zaidi ya nusu saa, au either uwaite kwa miluzi Kama mfuga mbwa. Au manager awe Karibu na ulipo ndio upate huduma kwa haraka,

UZI WENYEWE SASA.

Nimetoa mifano miwili tu kati ya mifano milioni moja.
Napenda kuwashauri wamiliki wa biashara mbali mbali. Jitahidini sana kuwepo ninyi mara nyingi iwezekanavyo kwenye biashara zenu mlizo waajiri watu, maana hao mliowaajiri ndio maadui wa kwanza kuua hizo biashara.

Ikumbukwe mbongo ni mvivu, mbinafsi, ana wivu na roho ya kwanini wewe uendelee kupitia yeye ili hali yeye hana biashara kama wewe. Hivyo hapa kazini kwake ambapo ndio office yako atapafanya genge la mastory mbadala wa kazi, majivuno na majibu mabaya kwa wateja kutokana na stress zake za wivu wa maendeleo ya biashara yako.

Kuna bar zina wahudumu wale wale miaka nenda rudi, na biashara zinaenda vyema kabisa hii Ni kutokana na usimamizi mzuri na costomer care nzuri.
Sasa unakuta muhudumu wa tigo pesa unamuuliza kutoa elfu 70000 nakata kiasi gani? Yeye anakujibu hiyo sio kazi yangu, wewe toa pesa nikupe pesa yako.
Biashara nyingi kubwa lakini hazina wateja, badirisha mbwa hao watakuulia biashara yako.

Pia nyie wenye biashara msitegemee kulelewa watoto wenu na ma- house girl vizuri ikiwa na nyinyi hamuendi nao sawa hao wafanya kazi wenu. Sisi wateja Ni watoto wenu hatutopatiwa huduma bora na wajakazi wenu Kama hamtawawekea mazingira bora.

Note: Jifunzeni kwa wahindi, ukifika kwenye eneo lake la biashara hata ukiwa chizi atakuondoa kwa kukuita Boss wangu njoo baadae ehhh Boss
 
Kweli kabisa apa wengi Sana tumejisahau mwanzo tulikua tuna fanya vizuri na kufatilia vizuri lakini Sasa hivi tunachukulia kawaida Asantee kwa kutukumbusha
 
Mkuu upo sahihi mnoo mimi nimeshafanya biashara ya mgahawa na biashara nikaipa wese (hela) kila kitu fully equiped na workers ujira wao nawalipa on time.......on a daily basis kila kitu na kuhakikisha wanakua comfortable na kazi yao.

Huwezi amini ile biashara ilikufa (upumba.vu wa hawa hawa wafanyakazi) nikafunga nikarudisha vyombo vyangu home na vinjwaji na beer zingine nikawapa wageni wakanywa home wakija.....

Trust me unajua ndio maana mkoloni alimtumikisha mtu mweusi kwa mijeledi....yani sisi watu weusi bila mijeledi na viboko hatuendi mkuu. Kuna workers wapu.mbav.u sana mkuu. Amini. Nikaja nikafungua biashara ya butchery hivyo hivyo jamaa ananiibia na nikamkamata live. Nikaja shikwa na hasira kodi ilivyoisha nikatemana nayo.

Biashara fanya unayoi control mwenyewe kwa 85% na hakikisha upo jikoni hata ikitokea siku mfanyakazi kazengua kazi inaendelea...

Nimeamua kuwa muwekezaji sasa..na trading business kiasi flani ambayo najua my stock and revenues first hand.
 
Wahudumu wa bar,mahotel na huduma nyingine zinazofanana na hizo wakiona huna dalili ya kuwatongoza watakuahamisha kwa madharau watakayokuwa wanakufanyia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom