Jinsi baba alivyoharibu maisha ya mwanawe kwa kisingizio cha kumlinda

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
69,274
136,390
Inauma saana kuna jamaa yangu alianza kazi baada ya kama 6 yrs akapata mafanikio sana majumba biashara magari akaamua kuacha kazi ili asimamie vizuri biashara zake na maambo yalikuwa bam bam ghafla akashangaa moja haikai mbili haisimami akafilisika akaanza kuuza kila kitu akawa ombaomba na kwa kuwa kila hatua ya maisha alimhusisha baba yake ndipo siku moja jamaa akamwambia baba yake kwamba mbona mambo yameharibika ghafla, hivyo anataka kwenda kwa mganga kuchunguza dingi akamkatalia na akawa anampeleka kwa waganga marafiki zake ambao waliongea vitu visivyo na kichwa wala miguu lakini siku moja akaamua kuchunguza kivyake akagundua kuwa baba yake mzazi ndiye anaehusika na baadaye baba akagundua kuwa amegundulika alienda kwa mganga aliyemzindua kijana na kuanza kumfokea kwamba kwanini amemwambia mambo yote.

Ndipo mzee akamfungukia mganga na kwa bahati mganga akarekodi kila kitu, akasema nimemfunga mwanangu aanze kupata mafanikio angalau akifikisha miaka 55 kwani akipata mali nyingi chini ya umri huo atakufa mapema kwasababu bado miiko na taratibu za dunia hazijui, kwani aweza tembea na wake za watu akauawa au aweza kuwa na dhararu hasa kwa wazee wakamchukua msukule etc.

Akaongeza kuwa nimemfunga mwanangu asioe mapema kwani wanawake wanamikosi wengine wachawi hivyo akiwajua wanawake kabla hajapevuka akili (40 yrs) wanawake watamuua mapema nimkose kijana wangu nami ndiye ninae tegemea, akaongea na mengine mengi sana akaongeza kuwa mganga huyo aachane na kijana wake mara moja kwani hayo ni mambo ya kifamilia.

Mganga akamwambia kijana mambo yote na kumsikilizisha ile rekodi yule jamaa alilia sana tena kwa uchungu mkubwa akaanza kulalalama kwamba nimeteseka usiku na mchana kuhakikisha baba namjengea nikafanikiwa, nasomesha wadogo zangu nimemnunulia mashamba lakini ananitenda hivi? Ndipo mganga akamwambia haya yote alosema baba yako ni kweli na kwa sasa anadaiwa nyama na wachawi wenzie na wanakutaka wewe na ili afanikiwe ni lazima akushushe chini uwe masikini wa kutupwa kisha mzee wako ndo linakuwa kimbilio lako mwisho anakutungua kwa urahisi ili kuwaridhisha wenzie kwani kesha kula nyingi za wenzie na hana namna.

Akaendelea kuambiwa kuwa alikuwa ktk hatua za awali za kumalizwa akamwambia cha kufanya ili awe salama, huyu jamaa yangu hadi hapa alikuwa ana 39 yrs hajawahi kuwa na mahusiano na demu yeyote na kwamba alikuwa hawataki kumbe alikuwa kapigwa kifungo na dingi yake ili asiwe nao karibu.

Mwisho, kama umezaliwa ktk familia isiyokuwa na mambo haya mshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa neema na rehema hiyo kiukweli kuna watu wanataabika sana pia kuna watu huwa hawaamini haya mambo wamwombe sana Mungu awaepushie ni hatari kuliko neneo lenyewe.
 

Ruble

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
245
329
Alaf mtoto wako ndio kiongozi wao. Unashangaa familia nzima had wazazi wako wanamnyenyekea mtoto wako unazania ni deko la bibi na mjukuu kumbe ndio boss wao😂😂😂
Kuna mzee nahangaika naye wanataabika kishenzi kumbe upande wa umamani ni wachawi haswa. Ni wahaya wa kiziba. Shenzi kabisa wachawi, mbwa kabisa wanatesa sana watu. Mchawi unakata panga kabisa unaua.
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom