Jinsi ArchAngel Raphael alivyo tumia MANJANO na MDALASINI kunitapisha uchawi niliolishwa kwenye ndoto

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,402
2,000
It was sometime in 2013, nikiwa nimelala nilijiwa na ndoto ambayo karibu kila mtu amewahi kukutana nayo. Niliota nikiwa nalishwa kitu kimefungwa kwenye kitambaa.

Kustuka ilikua saa kumi alfajiri. Kwa mnao fahamu habari za ndoto mnajua ukiota ndoto around saa kumi Hadi saa kumi na mbili alfajiri Basi ndoto hiyo ina ukweli kwa asilimia nyingi Sana.

Kama kawaida nilimuomba Mwenyezi Mungu aibatilishe ndoto hiyo.

Siku ishia hapo, nikamuomba ArchAngel Raphael anionyeshe dawa ambayo itaondoa huo uchawi nilio lishwa.

( For those who don't know Raphael means " God is the healer" na ArchAngel Raphael ndio malaika.wa Mungu anae husika na.mambo yote ya tiba na uponyaji kuanzia magonjwa ya kawaida Hadi magonjwa ya kisheitwani .And in addition to that ArchAngel Raphael is always there, willing to save and he answers very quickly. )


Baada ya kufanya maombi yangu nikarejea kulala tena.

Nikiwa nimelala Tena niliota ndoto nyingine nipo kwenye sherehe na marafiki halafu ukawa unapigwa wimbo wa BETTY MASIKINI yule.mcongo ambao ndani yake Kuna maneno anasema " MANJANO NA MDALASINI".


Kustuka tayari ilikuwa imefika saa kumi na mbili na nusu na.kilicho nistusha ni sauti kubwa ya muziki kutoka kwa jirani yangu and surprising enough wimbo uliokuwa unachezwa NI huo huo wa Betty MASIKINI ( MANJANO na MDALASINI )

Nikaungajisha dot kwamba huenda nilikuwa naota wimbo wa MANJANO na MDALASINI ( Najua hili sio halisi la wimbo wenyewe) kwa sababu ulikuwa unapigwa kwa sauti ya juu na jirani yangu na kwamba pengine haikuwa ndoto halisi.

Nikaoga na kujiandaa kwenda kwenye shughuli zangu. Nikiwa naoga nikasikia simu inaita . Iliita Mara tatu . So nilipomaliza kuoga nachek namba mpya.

Kupiga simu ili nijue ni Nani simu ikawa inaita. Surprising enough mlio wa simu hiyo ulikuwa NI wimbo huo huo wa MANJANO na MDALASINI.

Hilo halikujishangaza, lililo nishangaza zaidi NI mtu alie nipigia simu.

NI mjukuu wa shangazi yangu ambae Mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa mwaka 94.Wakati huo jamaa ( mjukuu) alikuwa Bado kinda, std 3 student ambae by that time shule ilikuwa inaelekea kumshinda kwa sababu alikuwa amebobea kwenye madrasa courtesy of the said shangazi.

Huyo shangazi yangu NI " Ninja" ( Mchawi anae paa usiku) na yeye ndio kamuingiza kwenye " industry" huyo mjukuu wake.

If that is not enough huyu jamaa alisema kuwa namba zangu za simu alipewa na ndugu yangu mmoja ambae anaitwa ABDALLAH YASIN ( Kwa msio fahamu jina MDALASINI Lina uhusiano mkubwa Sana na jina ABDALLAH YASSIN but this will be a topic for another day)

Huyo ABDALLAH YASEEN ni shabiki wa kutupwa wa DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS . Huyu ABDALLAH YASEEN nyumbani kwake Hadi vikombe NI rangi ya njano.

Hakuongea lolote la maana.but kwa kuwa naijua vizuri saikolojia na mode operandi ya wachawi tukio la jamaa huyo kunipigia Simu nililitafsiri kwamba jamaa alikuwa anapeleleza ili kujua maendeleo ya uchawi alio nitupia yeye na Bibi yake.

Nikiwa naenda kwenye mishe zangu nikiwa ndani ya gari ukapigwa wimbo wa MANJANO NA MDALASINI hapo ndo nikakata shauri kwamba hii ni sauti ya ARCHANGEL RAPHAEL ananielekeza dawa ya kutibu tatizo langu.

Wala sikuchelewa mzee nikaenda zangu straight Hadi sokoni nikachukua MDALASINI na MANJANO nikamix na maji nikamshukuru MUNGU na.ARCH.ANGEL RAPHAEL Kisha nikapigilia.

Usiku wa siku hiyo niliota nikiwa natapika.mataka taka . Na nilipostuka nikawa najisikia mwepesi kabisa na amani tele moyoni.

LESSONS:

1. Ukimshirikisha Mungu katika Vita yako na wachawi, wachawi hawataweza kukuroga na Kama wakikuroga Basi wao wenyewe ndio watakao kujulisha dawa ya kukuopoa bila wao kujua Kama ilivyo nitokea Mimi. Jamaa kapiga simu ili kutuatilia maendeleo ya uchawi alio nifanyia halafu mwisho wa siku mlio alio uweka kwenye simu yake ndio dawa ya kunitapisha uchawi wake.


2. Kama una maradhi yoyote Yale ya kawaida au ya kichawi, kuwa na.imani jaribu kufanya kama.nilivyo fanya Mimi, muombe Archangel Raphael akuonyeshe suluhisho la tatizo lako and am telling you atakuonyesha kikubwa uwe na Imani.


3. ANGALIZO: Wanasheria wanasema ' every case has to be treated according to its own merits, hata katika ulimwengu wa kiroho NI vivyo hivyo, every spiritual issue has to be treated on its own.

What am I saying here is that usiende kutumia MANJANO na MDALASINI ili kujitibu maradhi ya kichawi uliyo nayo. Inawezekana tiba ya suluhisho lako ikawa NI kitu kingine kabisa kulingana na Mungu atakavyo kufunulia kwa kupitia ARCHANGEL RAPHAEL

MUOMBE ARCHANGEL RAPHAEL ATAKUELEKEZA SULUHISHO LITAKALO ENDANA NA TATIZO LAKO.

MUNGU AKUFANYIE WEPESI
 

Majan

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
860
1,000
Duh sasa huyo Archangel Raphael anaombwaje /kwa staili gani mkuu, na hiyo Manjano ni nini?
 

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,402
2,000
Duh sasa huyo Archangel Raphael anaombwaje /kwa staili gani mkuu, na hiyo Manjano ni nini?

Unamuomba kawaida tu hakuna complication yoyote. Like ArchAngel Raphael naomba uni onyeshe suluhisho la tatizo langu la kiafya. Kama NI Mkristo unaweza kusindikiza na jina la YAH'SHUA ( YESU) na Kama ni Muislamu unaweza sema Ewe Mwenyezi Mungu(Taja jina.lake) nakuomba umuamuru au umtume malaika wako RAPHAIL anionyeshe suluhisho la maradhi yanayo nisumbua. Unaweza sindikiza na Suratul Yasin au Suratul Al Rahman.au zote kwa pamoja .

It works alot mkuu

# MANJANO ni Binzari.
 

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,402
2,000
Anayeombwa ni Mungu tu, kuomba asiye Mungu hata kama ni malaika unakuwa unakosea sana
Mungu NI mfalme...Ame delegate some of his powers to his servants. Ndio maana hata wakati ana mpelekea taarifa Bikira Maria Alimtumia messenger wake Djibril/Gabriel
 

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,769
2,000
Aina nyingine ya UZUMARIDI hii, kumuomba Mungu ni kupitia jina la YESU tu na si vinginevyo

Yohana 14:13
Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,677
2,000
Hapana Anayestahili kuombwa Ni Mungu na sio Malaika!
Ha ha ha /Omba hekima ya kujuzwa malaika rafael hawa ndio wasaidizi wa mungu kitu ambacho hawawezi kukifanya ni kimoja tu nacho ni KUSAMEHE DHAMBI.
Lakini katika maisha yako ya kila siku wapo!.
Gabriel frue-istreel hoihme deshaahie..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom