Jinsi ambavyo tunaweza kuondoa kama sio kupunguza tatizo la Rushwa

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Rushwa ni tatizo tena tatizo kubwa.

Rushwa tunaikuza na kuifanya itamalaki wenyewe kwa udhaifu wa sheria zetu. Sheria haiwezi kusema kuwa anayepokea ama kutoa rushwa wana makosa,swali la kujiuliza,nani atamripoti mwenzie kuhusu rushwa? Jibu,ni hakuna. Sheria lazima imuonee mmojawapo na kumpa haki mmoja wapo kwa mujibu wa mazingira ya mtoa ama mpokea rushwa.

Pendekezo: ili kuondoa rushwa,lazima mtumishi wa umma aonewe na sheria. Kufanya hivyo kunampa mtoa rushwa haki ya kuripoti mbele ya mamlaka husika. Kwa sababu gani,mosi,mtoa rushwa atweza kuripoti kwenye mamlaka husika bila hofu ya kutiwa hatiani,pili,mara nyingi wanaotoa rushwa ni watu wasiowatumishi wa serikali kwa mfano askari wa barabarani wanavyopokea rushwa kutoka kwa madereva nk.

Kufanya hivyo kutamfanya mtoa rushwa kutoa taarifa. Kwa nini,kwa sababu,hakuna mtu anayependa kutoa rushwa ila wakati mwingine tunalazimishwa ili kuhalalisha uovu na/au kupata huduma. Na itakapoinika kapokea rushwa adhabu kali itolewe dhidi ya mpokea rushwa.

Angalizo: mazingira ya kutoa na kupokea rushwa yaangaliwe kati ya mtoa rushwa na mpokea rushwa.
 
Kuangalia mazingira kati ya mtoa na mpokea rushwa kutasaidia sana kumtia hatiani muhusika kwa haki (hii itafaa pale ambapo tendo limeshafanyika na kugundulika) lakini sidhani kama kuangalia mazingira kunaweza kuwa suluhu ya hili tatizo. Naamini suluhu ni kwa kujikomiti tu, mtoaji na mpokeaji wote wanuie kuacha,

Ukiombwa rushwa kataa na chukua hatua ya kumripoti muhusika, nawe muombaji acha hiyo tabia, sema tatizo linakuja pale watu wanamatatizo na mahitaji mengi sana hivyo rushwa kinaonekana kitu muhimu zaidi. Pia tabia ya ubinafsi ndugu yangu ni tatizo, kwa hali hii sijui kama rushwa itakoma without real individual commitment.
 
Mkipata rais anayechukia Rushwa kwa dhati kabisa kabisa. Rushwa itapungua sana kiasi cha kuanza kusahaulika.
 
Back
Top Bottom