Jinsi ajali ya Mv Bukoba ilivyozama na hazina ya mashairi ya Nazitaka Mbichi Hizi ya Mwanasheria Audax

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
See the source image

Kuna mengi katika historia ya ushairi na maisha ya washairi ndani ya Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa haijukani na wengi wala kuhuifadhiwa katika kumbukumbu nzuri za kihistoria kwa sababu ambazo ni ngumu kuziweka wazi hasa katika kutazama tamaduni na mila za lugha ya Kiswahili,labda kwa sababu ya ukisasa ambao unaweza kuwa ni sababu ya kuuficha utamaduni halisi wa mila ya lugha ya Kiswahili.

Audax Khendaguza Vedasto mmoja kati ya wanasheria na wasomi wa fani ya sharia nchini kupitia kitabu chake ama diwani yake ya CHOPIKWA KIKAPIKA ya mwaka 2010 anaelezea ,mkasa mzito a kupoteza tungo zake nyingi ambazo alizitunga akiwa katika umri mdogo na baadae tungo hizo kupotea na mpaka wa leo hakuna matumaini kama atakuja kuzipata au zitakuja kupatikana.
Tarehe 21 Mei 1996 katika katika ya ziwa Victoria ajali mbaya ya meli ya Mv Bukoba ilizima na mamia ya watu kupoteza maisha akiwemo Mwalimu Dominick Alimanya.
Domonick Alimanya alifariki dunia katika jail ya meli ya ya Mv Bukoba akiwa na hazina ya mashairi yaliyoandikwa na Audax Kahendaguza na mashairi hayo kupotelea majini.
Shairi muhimu kabisa ni shairi lake la kwanza kutunga ambalo alikuwa akijibu shairi la SIZITAKI MBICHI HIZI huku yeye akijibu nazitaka mbichi lakini bahati mbaya shairi hilo pamoja mashairi mengine yaliweza kupotelea majini na kushindwa kupatikana kwa sababu hasa katika zama hizo tungo nyingi zilikuwa zikihifadhiwa katika madaftari.

mawasiliano-iddyallyninga@gmail.com
 
Sidhani kama ilishawahi tokea ajali kama hiyo nchini.

Watu zaidi ya 1000?
 
kwahiyo hakumbuki hata sentensi chache aweze kuunga unga na kwenye meli hilo daftari lilikuwa linatoka Bukoba analipeleka Mwanza ili kuchapishwa au ? Na sidhani kama ni busara kumpa mtu your only copy ya kazi yako ya maisha yako hata kama anaenda kuisomea chumbani let alone kutoka nayo mji mmoja kwenda mwingine
 
kwahio hakumbuki hata sentensi chache aweze kuunga unga na kwenye meli hilo daftari lilikuwa linatoka Bukoba analipeleka Mwanza ili kuchapishwa au ? Na sidhani kama ni busara kumpa mtu your only copy ya kazi yako ya maisha yako hata kama anaenda kuisomea chumbani let alone kutoka nayo mji mmoja kwenda mwingine
Kipindi hicho yeye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam na Mwalimu Dominuick alikuwa akisafari kutpoka Bukoba ili kuyapeleka mashairi hayo kwa Audax.
Ingelikuwa na wakati wa teknolojia kama sasa basi hakuna ambacho kingepotea.
Subiri utaona mengi ikiwemo hata Shaaban Robert mwenyewe jinsi tungo zake zilivyotoweka.
 
DAAH ENZI HIZO UMETUKUMBUSHA MBALI..WASHAIRI KUMBE NAO WALIKUWA VIZURI
Historia kubwa na kwa kiasi kikubwa imefichwa sehemu ila machache yataanza kusikika sasa,kuna historia tokea miaka ya 1830,mwaka 1936 kwa Shaabani Robert,kuna historia hadi za kisiasa na harakati za uhuru wa Afrfika ya mashariki.
 
Kipindi hicho yeye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam na Mwalimu Dominuick alikuwa akisafari kutpoka Bukoba ili kuyapeleka mashairi hayo kwa Audax.
Ingelikuwa na wakati wa teknolojia kama sasa basi hakuna ambacho kingepotea.
Subiri utaona mengi ikiwemo hata Shaaban Robert mwenyewe jinsi tungo zake zilivyotoweka.
Anyway kwa kizazi cha sasa hayo mashairi hata yangekuwepo yangekuwa maktaba yanapigwa vumbi kwa kumshauri yeye na hao washairi wengine wateneneze mashairi ambayo yanaweza kulika kwa kizazi cha sasa.., Kuliko hawa vijana kuimba mihogo ya jangombe kila siku wawatungie mashairi yatakayoishi milele...
 
Historia kubwa na kwa kiasi kikubwa imefichwa sehemu ila machache yataanza kusikika sasa,kuna historia tokea miaka ya 1830,mwaka 1936 kwa Shaabani Robert,kuna historia hadi za kisiasa na harakati za uhuru wa Afrfika ya mashariki.
TUNASUBIRI MKUU
 
Anyway kwa kizazi cha sasa hayo mashairi hata yangekuwepo yangekuwa maktaba yanapigwa vumbi kwa kumshauri yeye na hao washairi wengine wateneneze mashairi ambayo yanaweza kulika kwa kizazi cha sasa.., Kuliko hawa vijana kuimba mihogo ya jangombe kila siku wawatungie mashairi yatakayoishi milele...
Hapana viojana wa sasa tunayatafuta vibaya mno tena kwa nguvu na tunatumia gharama kubwa mno kupata mashairi haya ya zamani kwa sababu:
Ni sehemu ya elimu inayotolewa hadi vyuo vikuu kama utakua unafanya utafiti wowote wa kifasihi.
Pili,katika harakati za kuchunguza historia ya nchi yetu.
Tatu,ni sanaa inayohitaji vitu vingi mno ambavyo wasanii wengine hawawezi,ikiwemo kujibidiisha katika kusoma vitabu jambo ambalo ni ngumu sana sana tena sana kwa mtu mweusi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom