Jinamizi / Nightmare

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,273
KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANA YAKE? NA
NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI

KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANA YAKE?

Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu wengi sana.

Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping Paralysis)

Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.

Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.

Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa hofu kwa muda fulani.

Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi,

Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata “ugonjwa wa Kupooza”.

Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumbani kwako, wengine wanaona kama wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine wanahisi wanabakwa, wengine wanaona wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbali mbali ya kutisha.

Kukabwa na Jinamizi kama tunavyoiita kunatokana na sababu nyingi, ya kwanza kabisa ni jinsi wewe mwenyewe ulivyolala, mara nyingi unapolala chali mambo hayo yanakutokea, au ukiwa na jambo linalokusumbua kimaisha ambalo huwezi kulitatua linaweza kukuletea kukabwa na Jinamizi.

Sababu nyingine ni mazingira unayoishi au eneo ulilopo kama kuna makelele, au chumba kisicho na hewa ya kutosha au kuwa na mawazo kuhusu jambo fulani, au kulala na njaa au ukiwa umelala umekasirika au ndoto unazoota.

Njia ya kwanza ya kupambana na tatizo hili ni kujaribu sana lisikutokee, unatakiwa ujaribu kujua kitu gani kinakusababashia wewe kupata matatizo hayo, mfano ukijua kwamba kila ukilala chali unakabwa basi badilisha ulalaji wako, lala upande au lalia tumbo.

Ikiwa unakabwa ukiwa umelala usiku sana, au umefanya kazi ngumu, Jaribu kubadili muda wako wa kulala au punguza kufanya kazi mpaka ukachoka.

Njia nyingine ni kuhakikisha unapata muda mrefu wa kulala na umepunzika kabla ya usingizi haujakuja.

NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI

1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.

2.Jiepushe kulala chali.

3.Punguza mawazo mengi.

4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka 10.

5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.

6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.

7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii inatisha lakini haina hatari yoyote.

8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali ya kukabwa itakwisha.

9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini kwa dakika 5 halafu lala tena.
 
Joseverest unaliona Fala hili, badala ya kula mzigo, eti limekaa juu yake.

John_Henry_Fuseli_-_The_Nightmare.JPG
 
Majinamizi huwezi kuyatofautisha na ulimwengu wa mapepo machafu wanaozurura usiku.

Hakuna cha mawazo wala kulala vibaya, ni mapepo machafu yanayoamua kutesa watu ila kwa kiaso flani hayana madhara isipokuwa ni kukusumbua usiku.
 
Asee hii story unaletaa mida hii yaKulala kweli mbona hujatutendea haki bwana
 
Majinamizi huwezi kuyatofautisha na ulimwengu wa mapepo machafu wanaozurura usiku.

Hakuna cha mawazo wala kulala vibaya, ni mapepo machafu yanayoamua kutesa watu ila kwa kiaso flani hayana madhara isipokuwa ni kukusumbua usiku.
Kweli mkuu haya ni mapepo.ukikabwa na ukakemea kwa jina la yesu linakuachia.me nilitembelea mkoa flan unasifika kwa walozi.aiseee ilikua kama mchezo.nikakemea wee yakianza vurugu au nikihisi vurugu basi hayakugusi.unasema tu ktk jina la yesu mapepo toka.!!!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom