Jinamizi ni nini? Naomba msaada wenu

Kaka kwaio hao sio wachawi Kumbe ni hali ya kawaida katika ubongo.?
Kichawi liko hivi
19399370_1346869158681885_8247704969629167972_n.jpg
 
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.

Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.
Hatua hiyo sasa tunaiweka kwenye Astral projection? au Lucid dreaming? maana hata Mimi huwa inanitokea sana nakuwa sijuw nini nifanye.
 
Majinamizi ni roho za watu na mapepo ambao hayana mwili.
Kwahiyo yanakuvagaa wew kidogo yaonje raha ya kua na mwili.
Na yanavyokukaba haliwi moja yanakua mengi mengi ili yakuzidi nguvu vizur, yani hufurukuti hata kidogo.
 
Nakumbuka nyumba ya mwisho niliyohama usiku mmoja mwenye nyumba alisikia kuku wake wanapiga kelele usiku binafsi pia niliwasikia ila kW mbali na sikutilia mkazo, ila wao walitoka nje kuangalia ni nini. Katika kutafuta wakapita dirishani kwngu huku wanazungumza jamaa anamuambia mkewe... Ila ni muda huu na nna uhakika hajatoka nje" ikabidi niwaulize kupitia dirishani sababu nilikuwa nawasikia VP! Mmefanikiwa kuona chochote? Hapana... Na wakarudi ndani yani kile kitendo wanamaliza kufunga mlango nikaanza kusikia vishindo vinaelekea kutoka nje kupitia geti dgo si ndio nikataka niinuke nichungulie dirishani kwani niliweza kuinuka sasa! Nilikandamizwa mpka vishindo vilipotokomea ndo nikaweza kuinuka yaani ule mkandamizo ni dizaini hii ya jinamizi kiasi hta kuongea nilishindwa
 
Jini, mapepo na mizimu ni kitu kimoja. Mizimu ni majini/mapepo yenye nguvu katika familia, ukoo au jamii fulani. Mashetani ni malaika walioasi na wapo katika daraja la juu na wana nguvu zaidi ya mapepo/majini/mizimu.

Jinamizi kusababishwa na majini yapendayo kumwingia mtu akia usingizini na kuchukua hatamu ya sehemu muhimu katika ubongo wa mwanadamu ili kuweza kufanya watakavyo. Mchawi aliye katika roho anaweza pia akamwingia mtu kama jinamizi. Hawawezi kuchukua hatamu ya roho yako kwani roho yako ina nguvu ya ajabu ya kimungu, hivyo huchukua hatamu ya mwili wako tu.

Wanapenda pia kuchukua hatamu ya uwezo wa mtu wa kutamka ili mtu asiweze kupata msaada kwa wenzake au kwa Mungu (Yesu Kristo).

Cha kufanya unapopata jinamizi ni kujitahidi kuita Jina la Yesu. Kama huwezi basi fikiri au leta picha ya Yesu kichwani na mara moja jinamizi hutoweka.

Ili usipate jinamizi dawa yake ni kuwa mtu wa Yesu Kristo, yaani mtu aliyekombolewa kwa Damu ya Yesu Kristo na kuishi maisha safi. Pia usikubali hata siku moja kulala bila kusali na kujiweka chini ya ulinzi wa Yesu Kristo. Ukifanya hivyo majinamizi utasikia tu hadithi zake kwa wengine.
Asante umenitoa sehemu. Unarikiwe
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom