Jinamizi la umri lawatesa vijana wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinamizi la umri lawatesa vijana wa CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280  *katibu mkuu atangaza mpango kabambe kudhibiti wanaoghushi

  Hakimu Mwafongo, Iringa na Ramadhan Semtawa, Dar

  KUBAINIKA kwa Hamad Yusuph Masauni kwamba ameghushi umri wa kuzaliwa kumeanza kuwashtua vigogo wengine wa Umoja wa Vijana (UVCM) baada ya Katibu Mkuu wake Martin Shigela, kutangaza kwamba umoja huo utaweka mipango madhubuti kuhakikisha udanganyifu wa namna hiyo haujitokezi tena.

  Hii ni kauli ya kwanza kwa uongozi wa juu wa UVCCM kukiri hadharani udhaifu katika mfumo wa kupata viongozi wake, tangu Masauni kujiuzulu katika sakata ambalo tuhuma zake zilianza kusambazwa kupitia waraka maalum uliosambazwa mitaani.

  Tangu kujizulu Masauni, tayari kumeanza kuibuka taarifa mpya zaidi ambazo zimeibua hofu zikitaja baadhi ya vigogo wakiwemo wa makao makuu na mikoa takriban 20 kwamba, umri wao ni wa kughushi na tatizo hilo ni kubwa halikuwa kwa mwenyekiti huyo aliyejiuzulu pekee.

  Lakini, Shigela aliweka bayana:, "“Tutaweka mkakati huu kwenye kamati itakayokuwa inasimamia shughuli za uchaguzi ndani ya UVCCM, ili kuweza
  kuiepushia jumuiya na matatizo yanayoweza kujitokeza hapo baadaye.”

  Kwa mujibu wa mtendaji mkuu huyo, ili kuepusha matatizo kama yaliyotokea kwa
  kujiuzulu kwa Masauni aliyetuhumiwa kugushi umri, wataweza
  kudhibiti kwa kuwa makini wakati wa uchaguzi.

  Masauni alijiuzulu kwa tuhuma za kughushi umri ambao ulionyesha wakati akiomba kuchaguliwa UVCCM alisema alizaliwa mwaka 1979 lakini kwa mujibu wa Rais Kikwete, uchunguzi ulipofanyika alibainika alizaliwa mwaka 1973 na mwaka huo wa awali aliotaja alikuwa darasa la kwanza.

  " Kilichomponza Masauni ni kutokuwa mkweli kuhusu umri wake...Alikuwa na tuhuma za kughushi umri uliomwezesha kushinda uchaguzi mwaka 2008."

  "Tulipochunguza ilibainika ni kweli alighushi, wakati wa uchaguzi alisema alizaliwa mwaka 1979 lakini ukweli alizaliwa mwaka 1973 na alianza darasa la kwanza mwaka 1979."

  Shigela akizungumzia jinamizi hilo, alisema pamoja na hilo vijana wa kike watakaotaka kuwania nafasi 10 kupitia UVCCM saba kutoka Bara na watatu
  kutoka Zanzibar, watatakiwa kuwa na umri usiozidi miaka 30
  ili kipindi kimoja kinapoisha wawe na miaka 35.

  Mtendaji huyo mkuu wa vijana CCM, alisema baada ya Malisa kushika wadhifa wa
  uenyekiti kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM Ibara ya 97 (a) aliendesha kikao na kufikia maazimio mbalimbali, likiwemo la kupitisha mkakati wa ushindi ikiwa ni pamoja na kuwataka vijana wagombee nafasi mbalimbali za uongozi kwa wingi.

  Katika hatua nyingine, aliwapongeza wawekezaji wa uendelezaji wa kiwanja No.
  1081/2/1 kwa hatua kubwa waliyofikia katika ujenzi wa maghorofa pacha yenye urefu wa ghorofa 26. Mradi huo uliibua mvutano mkubwa baada ya kijana machachari Nape Nnauye, kumtuhumu Mwenyekiti wa Baraza la Udhamini Edward Lowassa, kwamba mchakato wa mradi huo uligubikwa na utata.

  Hata hivyo, duru zaidi za kisiasa kutoka ndani ya UVCCM ziliweka bayana kwamba kuna baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu wa umoja huo wameghushi umri huku wenyeviti wa mikoa 20 nao wakikalia kuti kavu.

  "Nani msafi UVCCM, ukiangalia orodha ya watu utaona kuna baadhi ya viongozi wa juu makao makuu (majina tunayo) nao wameghushi umri, yaani kwa mikoa kati ya wenyeviti 26 ni sita tu ndiyo wanaweza kuwa salama wengine 20 wamekalia kuti kavu," kilisema chanzo kimoja kutoka UVCCM.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, suala la umri mkubwa kwa UVCCM halikwepi kwani umoja huo umeacha utaratibu wa kuandaa chipukizi wa kweli kuanzia ngazi za chini hadi taifa, ambao walikuwa wakiingia kuchukua nafasi za uongozi wa umoja.

  "Zamani kulikuwa na chipukizi wa CCM kuanzia mashuleni, vilipokuja vyama vingi hakukuwa na utaratibu mbadala wa kupata vijana wapya, kwa hiyo hawa waliopo ni wakubwa kwani hakuna wengine wanaondaliwa," kiliongeza chanzo hicho.

  "Hata ukiwaangalia kwa macho unajua kabisa wamedanganya umri, halafu hata rekodi zao walizosoma zinapingana na hali halisi na taarifa wanazoandika, hakukuwa na mtu msafi wa kumrushia jiwe Masauni labda hao wenyeviti sita na wachache tu."

  Kwa mujibu wa duru zaidi za kisiasa, hata onyo la mwenyekiti wao Rais Kikwete kwamba wakiumbuana watajiangamiza lilikuwa na mantiki pana kwamba inawezekana hakuna aliye msafi zaidi.

  Naye mjumbe Baraza Kuu UVCCM, Hussein Bashe, aliweka bayana msimamo wake akisema Zanzibar bado inapaswa kupewa tena nafasi ya kutoa mwenyekiti wa umoja huo baada ya kujiuzulu Yusuph Hamad Masauni.

  Kauli hiyo inakuja kipindi ambacho kujiuzulu kwa Masauni kumeanza kuhusishwa na nafasi ya Zanzibar katika muungano, huku baadhi wakijaribu kugusa kero hiyo wakisema ni dhahiri visiwa hivyo vinamezwa na bara.

  Hata hivyo, Bashe pamoja na kutaka Zanzibar ipewe tena nafasi hiyo alipingana na hoja inayojaribu kuhusisha kujiuzulu kwa Masauni na matatizo ya muungano.

  Akizungumzia hilo jijini Dar es Salaam juzi, Bashe alisema: "Nafikiri huu ni wakati wa watu kuwa kitu kimoja, Zanzibar ilipewa nafasi hiyo na mwenyekiti ambaye ni mheshimiwa Rais, naamini pia bado inapaswa kupewa tena nafasi hiyo."

  Kuhusu tuhuma za Ridhiwan Kikwete kuhusika kumfanya Masauni ajiuzulu, alisema haamini na si kweli kwamba kijana huyo alishiriki kwani tukio lenyewe liko wazi.

  "Halafu haya mambo ya kusema sijui Ridhiwan (mtoto wa Rais Jakaya Kikwete) kahusika kumfanya Masauni ajiuzulu, hebu tuachane nayo hayana ukweli wowote, ni uongo na kuongeza chuki miongoni mwa vijana," alisema na kuongeza:,

  "Kilichotokea watu wote tumekisikia, tunachopaswa vijana sasa hivi ni kuwa kitu kimoja tuangalie yajayo, Masauni bado ni mjumbe mwezetu tutaendelea kupokea ushauri wake."

  Alisema Masauni ni kijana mpole, mchapakazi na ambaye hekima na busara zake bado zitahitajika ndani ya UVCCM na chama katika siku zilizopo na zijazo.

  UVCM katika kipindi cha wiki mbili ilijikuta ikiingia katika kipindi kigumu baada ya vigogo wake wawili, Masauni na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Nassor Moyo, kutangaza kujiuzulu kwa maslahi ya umoja na chama.Jinamizi la umri lawatesa vijana wa CCM
   
 2. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni upuuzi mtupu kusema unatangaza vita dhidi ya waliozidisha umri wakati umejaza watu waliofoji vyeti vya elimu na umekaa kimya.....umri nini bwana?
  Huwezi kujifanya eti unaumia na unahaha sana na mafua ya MMOJA WA FAMILIA YAKO wakati HUMJALI WALA HUMTHAMINI mgonjwa wa Ukimwi au kansa ALIYEKO KWENYE FAMILIA YAKO huo unafiki, Kama huna mapungufu ya akili basi nitasema kuwa umeamua kwa makusudi kumpendelea huyu na kumnyanyasa huyu au kwa sababu unadhani magonjwa ya vyeti vya elimu hayana dawa maana yanafanywa na waliokuteuwa basi umekata tamaaa! unadhani kupambana na umri inawezekana kwa sababu haiwahusu vigogo ila kupambana na vyeti vya shule ni ngumu na ni ugonjwa usiotibika! kwa ufupi HUU MKAKATI HAUNA TIJA NI UZUSHI NA AIBU KUUTANGAZA BAADA YA UTAFITI WA MSEMAKWELI KUTOKUKANUSHWA KISAYANSI JUU YA WANACHAMA HAO HAO WA CCM WALIOFOJI VYETI....tena wenye dhanama kubwa kabisa serikalini
  'changanya na za kwako'
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :angry:
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  forgery ni sehemu ya itikadi za sisis M mnashangaa nini?
  Subiri muone watakavyoghushi matokeo ya uchaguzi ndio mtajua mzizi wa shida uko wapi.
   
Loading...