Rais Magufuli: Uwekezaji wa NSSF wa Dege Eco Village(Kigamboni) haufai

Nasikia pale nssf kilikua kiwanda cha kuwaongezea nguvu waislamu sasa jiwe kaingia anaendeleza mfumo katoliki ndo maaana hadi foxy unaisoma namba ah ah
Rais Magufuli ameshindwa kabisa kuielewa biashara ya real estate. Ameshindwa pia kuelewa kuwa Kigamboni ndiyo city mpya. Pia ameshindwa kuelewa uwekezaji wa dege na daraja jipya ulikuwa na uhusiano upi kibiashara.

Nadhani kuna hila kama aliyaelewa yote hayo.

Mradi wa dege ungeachwa umalizike, ni mradi mzuri sana na wenye faida endelevu kwa hesabu zozote zile.

Cha mwisho alichojitetea ni kusema ule mradi unafaa "private".

Makemikali na biashara wapi na wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais anapaswa kubadilisha mshauri wake wa Masuala ya Biashara Na Uchumi

Kwenye Uchumi wa Soko huria Kuwa Na mshauri Mwenye mlengo wa Kijamaa sio sahihi

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pesa inazokusanya lazima iwekeze Kwenye Miradi ambayo ni ya longterm ambayo risk yake ni ndogo Sana Na kawaida Biashara yoyote ambayo level of risk is very minimal lazima return yake iwe ndogo Pia japo inadumu Kwa Muda mrefu, Miradi ya Majengo Ni Moja ya hizo investment

Sasa hivi NSSF imeshauriwa Na imeanza kuwekeza Kwenye zao la Pamba

Biashara ya Mazao hasa ya Biashara ni Biashara ya Muda mfupi ( seasonal ) Na Pia ni very risk Kwa Kuwa determinants zake ni nyingi Sana mfano haki ya hewa Na Soko la Kimataifa ambapo vyote hivyo ni uncontorable factors

Mradi wa Dege Beach ulikuwa Mradi Mzuri Sana Kwa Mwenye kuwaza Kwenye Falsafa ya kibiashara.
Rais hataki pension fund wawekeze Kwenye Majengo ila hasemi wawekeze wapi ambapo ni risk free
Imagine umewekeza Kwenye Soko la hisa Halafu linatikisika within 24 hrs unakuja kuwaeleza vipi wastaafu?

Fedha Za Pension Pia ni Za kuweka Kwenye Biashara ili zizalishe sio kuweka Kwenye Kibubu kusubiri Mtu astaafu!

Serikal kuu haikupaswa kuwekeza Kwenye Majengo, kazi hiyo ingefanywa Na Pension fund Halafu wao wakawa wakodishaji kuepuka gharama kubwa Za maintenance Na zinginezo

Ukiwaza Na kujitia Sana Hofu ya kuogopa kuibiwa Na Wafanyakazi wako usifanye Biashara tafuta shughuli nyingine
👍👍👍👍👍👍
 
Rais yupo sahihi, hiyo miradi imeanzishwa kiwizi wizi kwa watu kupiga 10% na kupelekea gharama za mradi kuwa kubwa mno. Hii itahitaji hizo nyumba zinunuliwe kwa bei kubwa sana tena cash au zilipiwe ndani ya muda mfupi ili mfuko uweze kurudisha mapato. Sababu nssf ni mfuko unaochangiwa na wafanyakazi ambao kwa kiasi kikubwa wana challenge za makazi, uwekezaji huo ulitakiwa kulenga kwa kiasi kikubwa wafanyakazi kwa kuwakopesha hizo nyumba kwa gharama ambazo wanaweza kumudu kulipa kidogo kidogo ndani ya muda wao wa utumishi. Hii nchi either kuna mamtu hayana akili au yamejaa ubinafsi
 
Kama hujui alikuwa wapi we syo mtanzania na sina haja ya kukujibia, hata nikikujibia hope hutaelewa maana huna uwezo wa kuelewa.
Ni kweli siwezi kuwaelewa watu wa ccm wenye ndimi mbili, hamueleweki mnasimamia nini
 
Rais anapaswa kubadilisha mshauri wake wa Masuala ya Biashara Na Uchumi

Kwenye Uchumi wa Soko huria Kuwa Na mshauri Mwenye mlengo wa Kijamaa sio sahihi

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pesa inazokusanya lazima iwekeze Kwenye Miradi ambayo ni ya longterm ambayo risk yake ni ndogo Sana Na kawaida Biashara yoyote ambayo level of risk is very minimal lazima return yake iwe ndogo Pia japo inadumu Kwa Muda mrefu, Miradi ya Majengo Ni Moja ya hizo investment

Sasa hivi NSSF imeshauriwa Na imeanza kuwekeza Kwenye zao la Pamba

Biashara ya Mazao hasa ya Biashara ni Biashara ya Muda mfupi ( seasonal ) Na Pia ni very risk Kwa Kuwa determinants zake ni nyingi Sana mfano haki ya hewa Na Soko la Kimataifa ambapo vyote hivyo ni uncontorable factors

Mradi wa Dege Beach ulikuwa Mradi Mzuri Sana Kwa Mwenye kuwaza Kwenye Falsafa ya kibiashara.
Rais hataki pension fund wawekeze Kwenye Majengo ila hasemi wawekeze wapi ambapo ni risk free
Imagine umewekeza Kwenye Soko la hisa Halafu linatikisika within 24 hrs unakuja kuwaeleza vipi wastaafu?

Fedha Za Pension Pia ni Za kuweka Kwenye Biashara ili zizalishe sio kuweka Kwenye Kibubu kusubiri Mtu astaafu!

Serikal kuu haikupaswa kuwekeza Kwenye Majengo, kazi hiyo ingefanywa Na Pension fund Halafu wao wakawa wakodishaji kuepuka gharama kubwa Za maintenance Na zinginezo

Ukiwaza Na kujitia Sana Hofu ya kuogopa kuibiwa Na Wafanyakazi wako usifanye Biashara tafuta shughuli nyingine
Tena nadhani hizi pension funds zina guidelines kabisa investment za aina gani wafanye na za aina gani wasifanye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna ishu ya mgawanyo wa share, nssf walikuwa na share 45% na akbar 55% na nssf walishatoa zaidi ya 200+b na akbar only 12b.ukakasi uko hapo kwenye share na hapo ndiko Dau alikopiga.
Hivi kuna tatizo gani kwa Akbar alishatoa 20% ambayo ilikuwa based kwenye value ya Land
Then 35% alikuwa akopeshwe na hao hao NSSF, wee unafikiri NSSF walikuwa wajinga kutaka wamkopeshe ni wazi waliona credit worthiness yake wakaona kwa nini aende kwingine. Hivi Akbar angesema aende AfDB angekosa kukopeshwa pesa hiyo ???
Watanzania wengi bado tunakasumba kuwa tajiri lazima uwe na ma cash mengi.
NSSF Walishaona mbali saana ule mradi ulikuwa na double impact kwanza wange invest hiyo 45% ambayo baadaye wangepata dividend
Pili wangevuna interest ya ile 35% ambayo wanamkopesha Akbar
Halafu angalia kitu kingine huu mkopo risk yake ilikuwa very minimal kwa sababu huyu jamaa tayari ana ardhi ambayo thamani yake ni 20% ya project, kwa hiyo amount ambayo inaweza ikawa kwenye risk ni 35%-20%= 15% Ambazo nadhani ana Sufficient Collateral==> Saa nyingine unakuta hana tangible collateral kuna international financial institution ina mdhamini kwa Nssf basi mambo yanakwenda
Halafu hii ya Tshs 800m per acre hapa naona kwa sababu partner na yeye alikuwa anahusika kukuza thamani ya eneo kwa 55% hivyo basi valuation method ililenga kuchukua thamani ya eneo likiwa tayari LIMESHAENDELEZWA sio bonde la mpunga kama mwanzo, hebu jaribu kuangalia thamani ya ardhi Mlimani City kabla na baada ya kujengwa kwa lile Mall

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asema bila kujali ulianzishwa na nani na kwa malengo gani ni uwekezaji usio na tija. Ungefanywa na kampuni binafsi ingeeleweka

Asisitiza, tena kwa sasa ndo haufai kabisa kufuatia Serikali kuhamia Dodoma.

Amewataka NSSF kujitafakari juu ya uwekezaji huu.

Amesema kama SSRA wangekuwa makini miradi kama hii isingekuwepo.

Soma pia:
Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Kigamboni ulioanzishwa na NSSF (Dege Eco Village) unapigwa mnada - JamiiForums

Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani? - JamiiForums
Waliofisadi huo mradi wamechuliwa hatua gani za kisheria zaidi ya kusimamishwa kazi? Mahakama ya mafisadi mbona haina wateja?
 
Hivi kuna tatizo gani kwa Akbar alishatoa 20% ambayo ilikuwa based kwenye value ya Land
Then 35% alikuwa akopeshwe na hao hao NSSF, wee unafikiri NSSF walikuwa wajinga kutaka wamkopeshe ni wazi waliona credit worthiness yake wakaona kwa nini aende kwingine. Hivi Akbar angesema aende AfDB angekosa kukopeshwa pesa hiyo ???
Watanzania wengi bado tunakasumba kuwa tajiri lazima uwe na ma cash mengi.
NSSF Walishaona mbali saana ule mradi ulikuwa na double impact kwanza wange invest hiyo 45% ambayo baadaye wangepata dividend
Pili wangevuna interest ya ile 35% ambayo wanamkopesha Akbar
Halafu angalia kitu kingine huu mkopo risk yake ilikuwa very minimal kwa sababu huyu jamaa tayari ana ardhi ambayo thamani yake ni 20% ya project, kwa hiyo amount ambayo inaweza ikawa kwenye risk ni 35%-20%= 15% Ambazo nadhani ana Sufficient Collateral==> Saa nyingine unakuta hana tangible collateral kuna international financial institution ina mdhamini kwa Nssf basi mambo yanakwenda
Halafu hii ya Tshs 800m per acre hapa naona kwa sababu partner na yeye alikuwa anahusika kukuza thamani ya eneo kwa 55% hivyo basi valuation method ililenga kuchukua thamani ya eneo likiwa tayari LIMESHAENDELEZWA sio bonde la mpunga kama mwanzo, hebu jaribu kuangalia thamani ya ardhi Mlimani City kabla na baada ya kujengwa kwa lile Mall

Sent using Jamii Forums mobile app

Waliona mbali ila wamekuja wenye kuona mbali zaidi yao ndo wakagundua Dau alifanya dili kupitia mradi huo, kwanini akbar alikimbia immediately dau alipotolewa?????kwanini dau alikataa ku invest kwenye short terms(treasury bond nk) akakimbilia kwenye majengo ambayo hadi sasa mengi hayana wakaaji.

Ni juha pekee ataelewa hiyo mambo.
 
Hayo maneno ya Akbar kukimbia ni maneno ya vijiwe vya kahawa
Hebu nikuulize Akbar kuna legal grounds zozote za kumtia hatiani mpaka akimbie, hivi tunaishi generation ya Primitive Society tuanze kukimbiana kama Kima ???
Dunia ya sasa haiko hivyo una matatizo na Company yangu leta legal grounds zako nipeleke hata hiyo mahakama ya Mafisadi

Kuhusu suala la Short term investments. Nilishagusia hapo mwanzo kwamba hii mifuko ina guidelines ktk ku invest kama ingekuwa ni rahisi kama unavyodhani Mifuko yote ingetupia hela zao huko na wala kusingekuwa na shida hizi. Kingine lazima ujue hizo Treasury Bills & Bonds haziko wakati wote katika market, BoT huwa inazitoa kwa nyakati fulani fulani kulingana na Liquidity Requirements na interests nazo huwa zinatofautiana. Ule mkopo wa Akbar ni longterm loan ambayo nssf ilikuwa inajihakikishia lets 10 years to come nitakuwa na uhakika wa interest kiasi kadhaa every year ukijumlisha na dividend inayotokana na 45% shares Uko wapi
Ni rahisi sana kumkosoa coach/mchezaji ukiwa nje ya pitch lakini ingia ndani uone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jinsi Dar ilivo over populated Dege Eco Village ingekua ni moja ya solution ya makazi. Kwa mwenye maono mazuri na serikali kiujumla wawekeze kwenye mradi huo ni mzuri kwa ajili ya maisha ya baadae ya Dar haijalishi serikali imehama au la.
 
Habari za wakati huu,

Mradi wa DEGE ECO VILLAGE ulioko Kigamboni umekwama kwa muda sasa. Sababu zipo ingawa bado ni suala linalohitaji mjadala.

Kwa kuzingatia gharama za mradi huu ambazo ni TZS 2 Tril kwa bei za sasa, je siyo wakati sasa kwa Serikali kuamua kuuchukua huu mradi, kuukamilisha na kisha kuwapa watu waishi kwa kuwauzia katika mfumo wa mkopo?

Sioni sababu ya mradi huu kuendelea kuwa magofu wakati pesa nyingi sana za Mifuko ya hifadhi zimekaa pale.

Ni maoni yangu tu maana nafikiri ukikamilika unaweza kutupa picha ya namna ambavyo tunaweza shughulikia tatizo la makazi holela Mijini

Naomba kuwasilisha
 
Huu mradi watu walishapiga pesa kupitia 'UPEMBUZI YAKINIFU'. Labda kwa kuwa MTOTO WA MFALME anakaa Kigamboni, mradi unaweza kufufuka.
 
Wadau kwema jamvini?

Admin naomba hii post usiiunganishe Na zile zilizopita.
Leo katika pita pita zangu nilipita ulipo mradi wa pili kwa ukubwa Africa wa DEGE ECO VILLAGE unaosimamiwa na NSSF pamoja Na kampuni ya AZIMIO HOUSING LTD ambao umetelekezwa Kwa zaidi ya miaka 7 sasa. Kwakweli roho imeniuma hasa ukizingatia zile ni hela zetu wanachama wa NSSF. Kila kitu kimeibwa, majenereta yameng’olewa kila kitu, karakana imeibiwa karibu kila kitu Na majumba yakizidi kuharibika huku yakiwa ni magofu.

Namuomba Rais wetu aingilie Kati kuokoa mradi huu.

Angalia kwa clip yangu hapo chini utaelewa Namaanisha nini.

Back
Top Bottom