Jinamizi la Mradi wa Dege Eco Village na mustakabali wa nchi yetu

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,608
2,000
Habari za wakati huu,

Mradi wa DEGE ECO VILLAGE ulioko Kigamboni umekwama kwa muda sasa. Sababu zipo ingawa bado ni suala linalohitaji mjadala.

Kwa kuzingatia gharama za mradi huu ambazo ni TZS 2 Tril kwa bei za sasa, je siyo wakati sasa kwa Serikali kuamua kuuchukua huu mradi, kuukamilisha na kisha kuwapa watu waishi kwa kuwauzia katika mfumo wa mkopo?

Sioni sababu ya mradi huu kuendelea kuwa magofu wakati pesa nyingi sana za Mifuko ya hifadhi zimekaa pale.

Ni maoni yangu tu maana nafikiri ukikamilika unaweza kutupa picha ya namna ambavyo tunaweza shughulikia tatizo la makazi holela Mijini

Naomba kuwasilisha
 

CANIMITO

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,385
2,000
Huu mradi watu walishapiga pesa kupitia 'UPEMBUZI YAKINIFU'. Labda kwa kuwa MTOTO WA MFALME anakaa Kigamboni, mradi unaweza kufufuka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom