Jinamizi la Malori ya Mizigo Kuvamia Nyumba za Watu Kimara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinamizi la Malori ya Mizigo Kuvamia Nyumba za Watu Kimara

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mabaki ya nyumba iliyobomolewa na lori la mizigo Friday, September 11, 2009 6:59 AM
  Jinamizi la malori makubwa ya mizigo kuvamia nyumba za watu kwenye maeneo ya Kimara Mwisho limezidi kupoteza maisha ya wakazi wa eneo hilo safari hii lori kubwa lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara lilivamia nyumba usiku na kuua mtu mmoja aliyekuwa amelala. Picha za ajali hiyo mwisho wa habari hii. Lori lenye namba za usajili T934 ASM lilokuwa na trela namba T885 ASM liliokuwa limeegeshwa katika eneo la Kimara mwisho usiku wa kuamkia jana liliporomoka na kuvunja nyumba iliyokuwa jirani na kuua mtu mmoja na kumjeruhi mwingine.

  Aliyefariki alifahamika kwa jina la Salumu Mussa Ndete na majeruhi wa ajali hiyo alikuwa ni Hamis Salumu (28).

  Gari hilo lilikuwa limeegeshwa usiku kwenye eneo hilo na dereva ambaye aliondoka zake kwenda kulala sehemu nyingine lakini cha kushangaza majira ya saa kumi na moja alfajiri gari hilo lilijiendesha lenyewe na kuvamia nyumba hiyo.

  "Nilisikia mlio kama wa mabomu ya mbagala, nilipoamka na kwenda kungalia nini kilichotokea nilikuta gari kubwa limevamia nyumba yangu" alisema jirani wa nyumba zilizoathirika .

  Hata hivyo matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika eneo hili.

  "Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka huu hivyo sisi wananchi wa eneo hili tunajiuliza kuna nini" alisema mkazi wa eneo hilo, Hamisi Juma.

  Wakati ajali hiyo inatokea, marehemu Salum alikuwa peke yake chumbani kwake amelala huku jirani yake Salumu naye akiwa amelala chumbani chumba cha jirani kwenye nyumba hiyo ya kupanga.

  Hata hivyo waswahili wanasema mungu mkubwa, Mke wa marehemu Salum na mwanae jioni ya tukio walikuwa wamekwenda kwenye msiba wa mama yake sehemu nyingine na hivyo kunusurika maisha yao.

  Ajali kama hii ni ya tano katika eneo hilo katika kipindi cha muda wa miaka 5.

  Wakazi wanaoishi karibu na eneo hilo la barabara ya Morogoro wameanza kujiuliza maswali mengi bila majibu.

  "Sijui kuna nini maeneo haya labda kuna mashetani" alisema mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la John.

  Mwili wa marehemu Salum umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. GONGA HAPA KWA PICHA ZA AJALI HIYO

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3056846&&Cat=1http://www.nhttp://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3056846&&Cat=1ifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3056846&&Cat=1
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wabongo hata kama gari hukufunga breki sawa ikaserereka na kugonga nyumba watakwambia kuna mashetani.
   
 3. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 3,173
  Trophy Points: 280
  Hakuna mashetani ni ubovu wa miundo mbinu na uzembe wa madereva
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Magari mabovu ni mengi sana barabarani hapa bongo. Inabidi yakaguliwe na kupewa MOT kama kule UK.
   
Loading...