Jina libakie kuwa Jiji la Dar es Salaam ila lichukue maeneo ya kijografia ya Ilala

Laptop01

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,365
796
Nakubaliana kimsingi kwamba kuwepo kwa Halmashauri ya Jiji la DSM (DSM City Council-DCC) katika OR-TAMISEMI na mipaka ya nchi kwa ujumla kwa maana ya Uongozi na mipaka yake ya Kijiografia hauna tija kabisa katika uchumi na maendeleo ya nchi.

DCC is a mere consumptive administrative organisation. Hawana kitu chochote cha maendeleo wanachoweza kujivunia kwamba ndicho wanachokifanya. Hawana maeneo yoyote ya ardhi wanayoweza kujivunia na kuyaendeleza. Hata hivyo, Jina la DCC siyo rahisi kulipoteza kwani ni Nembo inayobeba mambo mengi katika historia, uchumi, siasa ukuaji wa miji hapa nchini na Mambo mengine mbalimbali ktk jamii ya WaTz.

Ikiwezekana: (a) DCC iongezewe maeneo ya kijografia kwa kutwaa maeneo yaliyopo kati ambayo kwa sasa yapo chini ya Manispaa ya Ilala ili Manispaa ya Ilala ikaanzie Tabata au Kinyerezi kuelekea Kisarawe. (b) DCC ichukue Manispaa ya Ilala yote. Ingawa wazo (b) litaleta changamoto ktk uendeshaji kwani kijografia na kiutawala DCC itakuwa so huge and complex to plan for it and govern.
 
Ilala ndiyo imekuwa Jiji ,sasa maana yake Jiji la Dar es salaam linakufa rasmi.kwa hiyo tutakuwa na mkoa wa Dar es salaam na Jiji la Ilala.
Lililotakiwa kuondolewa lilikuwa linawezekana bila kubadiri majina.
 
Kwahiyo sasa hivi tukizungumzia mikoani na Daslama imo!

Kuna watu walituvimbia sana humu, eti sie ni wa mikoani. Sasa rasmi daslam ni mkoa kama ilivyo Mara, Katavi, Kigoma, nk. Na Ilala ndiyo JIJI.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Tanzania uelewa mdogo ndo maana CCM inatawala na itaendelea tawala.
 
Ilala ndiyo imekuwa Jiji ,sasa maana yake Jiji la Dar es salaam linakufa rasmi.kwa hiyo tutakuwa na mkoa wa Dar es salaam na Jiji la Ilala.
Siyo kitu kipya mkuu sema tu Dar ina eneo dogo ndio maana inaonekana issue mfano manispaa ya ilemela na Nyamagana ndio zinazotengeza jiji la mwanza hivyo, ukiwa mbali na hayo maeneo haupo jijini mwanza ila upo mkoa wa Mwanza.
 
Unapozungumzia Jiji la Dar es Salaam unazungumzia manispaa za Ilala,Temeke,Kigamboni,Kinondoni na Ubungo. Hizo ni mbwembwe na kutaka attention! Kwa maana nyingine Dar ea salaam itaendelea kuwa na hadhi ya Jiji regardless mgawanyo wa kimamlaka wa kiserikali za mitaa

Kiutawala itasomeka hivyo na kuleta ukakasi manispaa ya ilala kuitwa Jiji la Dar es salaam.

Kiutendaji halmashauri ya Jiji (DCC) iliyovunjwa haikuwa na kazi! Kwa kuwa manispaa zilikuwa zinajitegemea na zilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi ya bajeti zake za ndani. Rais alitakiwa avunje Mamlaka iliyoitwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (Dar city council). Hili ndio aliopaswa ashauriwe.

Halmashauri ya Jiji ni ngazi ya juu kabisa katika Mamlaka za serikali za mitaa ikifuatiwa na Manispaa,(Municipal Councils), halmashauri za miji (Town Councils) na halmashauri za wilaya (District councils). Mgawanyo huu unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na uwezo kimapato,uwepo wa shughuli za Kiuchumi k.v viwanda,uwepo wa huduma za Kijamii k.v vyuo n.k
 
sio kitu kipya mkuu sema tu Dar ina eneo dogo ndio maana inaonekana issue mfano manispaa ya ilemela na Nyamagana ndio zinazotengeza jiji la mwanza hivyo, ukiwa mbali na hayo maeneo haupo jijini mwanza ila upo mkoa wa Mwanza
Kwani ilishindikana nini Jiji a Dar kuundwa na manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke?
 
kwani ilishindikana nini Jiji a Dar kuundwa na manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke?

Nilielezea kuelewesha watu kwa yaliyofanyika kutokana na uelewa wangu kwa kuona si kitu kipya maana hata dar yenyewe ilitengenezwa kuwa jiji kutoka katika mkoa wa pwani. Kuhusu uzuri au ubaya wa hii movement, siwezi kusemea unless nipate ufahamu zaidi.
 
Back
Top Bottom