Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253

Sultani Abdulrauf Songea Mbano
Kibao kimeandika jina lake kama ''Lwafu'' Nduna Mbano

Kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano

Kwa miaka mingi sana na hadi leo jina la Sultani wa Wangoni Abdulrauf Songea Mbano Jemedari wa Wangoni katika Vita ya Majimaji, jina lake la ‘’Abdulrauf’’ moja ya sifa za Allah ikiwa na maana ‘’Mwenye Huruma,’’ lilikuwa halifahamiki kwa wengi na wanahistoria kwa sababu zao hawakutaka kulisema lijulikane kama vile wengi hawajui kuwa Sultani Mkwawa jina lake ni ''Abdallah.''

Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''

Kaburi la Kleist Sykes

Tunaweza tukasema kuwa haya yote ni matatizo ya ukoloni. Lakini swali linakuja iweje hata baada ya ukoloni kutoweka ikabakia historia yetu hatuiweki sawa?

Leo gazeti la ''Habari Leo,'' (28 Februari, 2018) ukurasa wa mbele imetoka picha ya kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano jina linalosomeka katika kaburi hilo ambalo ni la Kiislam ni ‘’Songea Mbano,’’ na jina lake halisi ''Abdulrauf,'' halipo.

Laiti kama Sultani Abdulrauf asingezikwa katika kaburi la Kiislam mengi katika historia ya Majimaji yasingelipata ushahidi madhubuti ukizingatia kuwa katika wale majemedari walionyongwa na Wajerumani, majina yao ya Kiislam yalifutwa yakawekwa mengine.

Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hii aingie hapo chini:
  1. Mohamed Said: SULTAN ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?
  2. Mohamed Said: KUTOKA JF: MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI - SULTAN SONGEA BIN RAUF NA SHEIKH SULTAN MATAKA BIN HAMIS MASSANINGA
  3. Mohamed Said: KUTOKA JF: UCHAKACHUAJI WA MAJINA YA KIISLAM KATIKA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI
  4. Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI
 
ndio anaona.cha muhim sana kurithisha watoto. mkuu watu dizain hii wala usihangaike nao maana ndivyo alivyo ni nature yao.
Kitalii,
Publishers wakubwa duniani kama Oxford University Press wamechapa
kazi zangu si kwa lingine ila kwa kuwa nimechangia katika elimu mpya
ambayo kabla ilikuwa haifahamiki.

Unaweza ukanitafuta katika Dictionary of African Biography (DAB),
Oxford University Press, New York.
 
Unajua mambo mengine bwana. Hakuna muhehe yoyote ambaye alimfahamu Mkwawa kama sijui nani unayemsema wewe. Kama alipewa hilo jina sikatai maana ni kweli alikuwa na urafiki na waarabu. Lakini waarabu walimkuta Mkwawa ni mtu mzima na tayari kashakuwa mtwa. Ndiyo jina la cheo chake kwa kihehe na si sultan kama unavyomuita wewe.

Kwa hiyo kwa umri huo na cheo chake hakuna sehemu alipowatangazia wananchi zake kwamba kabadili jina maana kubadili jina kwa muhehe wakati ule ilikuwa lazima ufanye tukio la kishujaa ndipo upewe ruhusa ya kujipa jina au kupewa jina.

Hata hilo jina la Mkwawa alipewa akiwa kijana si la kuzaliwa nalo.. Hilo jina ni kifupisho cha jina Mkwavinyika, yaani mtwaa nchi. Hali kadhalika kwa Songea Mbano wanaandika jina lenye asili ya Songea na kabila lake hayo ya kiarabu nayo pia ni matokeo ya ukoloni. Ila ukoloni huo kwasababu ni wa kiarabu wewe huoni kwa sababu umepigwa upofu wa iman

Binafsi naona wako sawa kwa sababu wameenziwa kwa majina yao haswa na si majina ya kigeni, wangekuwa waliitwa majina ya kizungu hapo ningekusaidia kulaumu
 
Unajua mambo mengine bwana.....hakuna muhehe yoyote ambaye alimfahamu mkwawa kama sijui nani unayemsema wewe....kama alipewa hilo jina sikatai maana ni kweli alikuwa na urafiki na waarabu...lakini waarab walimkuta mkwawa ni mtu mzima na tayari kashakuwa mtwa...ndiyo jina la cheo chake kwa kihehe na si sultan kama unavyomuita wewe....kwahiyo kwa umri huo na cheo chake hakuna sehemu alipowatangazia wananchi zake kwamba kabadili jina..maana kubadili jina kwa muhehe wakati ule ilikuwa lazima ufanye tukio la kishujaa ndipo upewe ruhusa ya kujipa jina au kupewa jina....hata hilo jina la mkwawa alipewa akiwa kijana si la kuzaliwa nalo...hilo jina ni kifupisho cha jina mkwavinyika..yaani mtwaa nchi...hali kafhalika kwa songea mbano wanaandika jina lenye asili ya songea na kabila lake hayo ya kiarabu nayo pia ni matokeo ya ukoloni....ila ukoloni huo kwasababu ni wa kiarabu wewe huuoni kwasababu umepigwa upofu wa iman.....binafsi naona wako sawa kwasababu wameenziwa kwa majina yao haswa na si majina ya kigeni...wangekuwa waliitwa majina ya kizungu hapo ningekusaidia kulaumu
Mwinyikungu,
Ahsante kwa maelezo yako.

Mimi nimeeleza ukweli katika historia kuwa Mkwawa alikuwa na jina lingine nalo ni Abdallah na alikuwa kaijua kuandika na kusoma kwa irabu za Kiarabu na alikuwa na urafiki mkubwa na Rumaliza.

Rumaliza jina lake halisi ni Muhammad bin Khalfan bin Khamis al-Barwani.

Nnilijaliwa kukutana na kitukuu cha Rumaliza, Mohamed Said Dubai mwaka wa 1999 na anajua mengi katika historia ya babu yake mkuu na Mkwawa.

Vitabu vinamwandika kama ''Chief,'' na chief tafasiri yake ni sultani lakini iwe iwavyo hayo ni majina na vyeo, ukweli wa historia kuhusu maisha yake ndiyo muhimu.

Tusitishike na historia hizi ambazo wako ambao kwa sababu zao hawakupenda zijulikane.
 
Unajua mambo mengine bwana.....hakuna muhehe yoyote ambaye alimfahamu mkwawa kama sijui nani unayemsema wewe....kama alipewa hilo jina sikatai maana ni kweli alikuwa na urafiki na waarabu...lakini waarab walimkuta mkwawa ni mtu mzima na tayari kashakuwa mtwa...ndiyo jina la cheo chake kwa kihehe na si sultan kama unavyomuita wewe....kwahiyo kwa umri huo na cheo chake hakuna sehemu alipowatangazia wananchi zake kwamba kabadili jina..maana kubadili jina kwa muhehe wakati ule ilikuwa lazima ufanye tukio la kishujaa ndipo upewe ruhusa ya kujipa jina au kupewa jina....hata hilo jina la mkwawa alipewa akiwa kijana si la kuzaliwa nalo...hilo jina ni kifupisho cha jina mkwavinyika..yaani mtwaa nchi...hali kafhalika kwa songea mbano wanaandika jina lenye asili ya songea na kabila lake hayo ya kiarabu nayo pia ni matokeo ya ukoloni....ila ukoloni huo kwasababu ni wa kiarabu wewe huuoni kwasababu umepigwa upofu wa iman.....binafsi naona wako sawa kwasababu wameenziwa kwa majina yao haswa na si majina ya kigeni...wangekuwa waliitwa majina ya kizungu hapo ningekusaidia kulaumu
Umemaliza maneno niliyotaka kuzungumza hapa.
Watu walimfahamuje muhusika?
Hilo jina la Kiarabu au kizungu alipewa lini?
Nafikiri Historia ya Afrika iachwe iwe ya Afrika.
 
Mohamed Said,
Mimi sikukatalii kuwa wanaweza wakawa na majina hayo lakini hoja yangu mimi ni kwamba mfano Mkwawa jina lake halisi ni Mkwavinyika hilo ndilo anatambulika na watu wake na ni jina la heshima kwake, yawezekana kweli alijua kuandika kiarabu na akawa muislamu lakini bado haikubadilisha lolote juu ya kujulikana kwake kama Mkwavinyika

Hata hao walioandika hayo majina ya asili ndio walikuwa sahihi kuliko uavyotaka wewe. Leo hii unataka mkwawa ajulikane kama sijui Abdala, abdala ni nani katika uhehe? Zunguka uhehe yote mfano uliza nani alikuwa Mtwa wenu watakuambia ni Mkwawa hivyo ndivyo alijulikana.

Pia Mtwa mkwawa hakuwa chief ama Sultan kama ulivyosema. Mkwawa tafsiri halisi ya cheo chake ni mfalme ndio alikuwa ni Mfalme wa wahehe
 
Umemaliza maneno niliyotaka kuzungumza hapa.
Watu walimfahamuje muhusika?
Hilo jina la Kiarabu au kizungu alipewa lini?
Nafikiri Historia ya Afrika iachwe iwe ya Afrika.
Ndo hapo ambapo nimemshangaa waalabu wamemkuta mkwawa akiwa mtu mzima sana, toka udogo wake mpaka anajiuwa watu wake walimfahamu kwa jina la mkwava...hilo la kiarabu walipeana wenyewe labda na wakaitana wenyewe lakini halikuwa official name...sasa mkwawa na Songea wanapoenziwa kwa majina yao halisi mtu analeta nongwa
 
mnyikungu, Historia hujaijua vyema, mimi ni mfuatiliaji wa maandiko tofauti. Upo ushahidi hadi Iringa, mmoja wa watu wa ukoo wa Mkwawa alishathibitisha hilo na kuna kitabu kiliandikwa. Hao waarabu wapo Tanganyika Mkwawa tangu karne ya 17, uje kusema kawajua ukubwani.

Hebu usiongee usichokijua, hata historia hii ya mashuleni iliyofichwa mengi inaeleza
 
Mengi yamejificha hayajulikani, hadi hii leo watu hawajui kama lile fuvu si la Mkwawa. Watafiti wenyewe waliweka shaka, ila walificha tu kwani aibu kwao kueleza wamezidiwa ujanja na mtu mweusi. Lile fuvu wajerumani walikata kichwa kwa kumkuta mtu aliyeangukia kwenye moto baada ya wao kusikia mlio wa risasi, sura haikujulikana maana iliharibika na moto.

Mkwawa alikuwa ni kichwa haswa kimbinu na kila namna, haitosahaulika alivyochukua bunduki ya mjerumani akaifumua na kuunda vifaa vinavyofanana kisha akafunga na kupata bunduki nyingine.

Yule aliyechukuliwa fuvu lake ni mlinzi wake na ndiye aliyekuwa naye mahali ambapo kulisikika mlio wa bunduki kwa mujibu wa kitabu kimoja, aliwachezea akili wajerumani. Eneo hilo hakuwa peke yake walikuwa watatu unaweza kuamini walinzi waliruhusu ajiue, au mlinzi mmoja alitoroka na kumwacha ajiue?
Eneo hilo miili ilikutwa miwili mmoja ndo uso uliangukia kwenye moto, mwingine ulijulikana wazi ni wa mlinzi mmojawapo naye hakuuawa na wajerumani sasa nani kamuua huyo mlinzi mwingine?

Hapo ndiyo utabaini wazungu walichezewa akili, wakaamua kuficha hii aibu
 
Sasa mkwawa alienda wapi?
 
Back
Top Bottom